Friday, 29 December 2017

ULEVI UNAVYOWEZA KULETA MADHARA YA UTEGEMEZI SAWA NA MADAWA YA KULEVYA


 
NA: Stewart Meena
Ikiwa ndio kwanza zimebaki siku2 tunajiandaa kuumaliza mwaka huu wa-2017 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 nimeona nivyema tuliongelee swala hili la baadhi ya watu kuendekeza sana matumizi ya vinywaji vigumu (mvinyo) kwa ajili ya kusheherehea sikukuu mbalimbali.
Imekuwa ni kawaida kwa vijana na wazazi kulalamikia swala la kutokuwepo kwa maadili katika Jamii wanamoishi, sio watoto / sio vijana na wala sio Wazee.

“Vilio, majonzi na simanzi zimetawala katika nyumba zetu, matukio ya wizi, ubakaji na mauwaji nayo yakizidi kushika kasi”
Pengine ni utandawazi, ukosefu wa ajira, au ni kujitoa ufahamu kwa wanajamii hao, kwa kile kinachoonekana kama ni ‘akili ya kuongezea’ yaani matumizi ya madawa ya kulevya na vinywaji vigumu (mvinyo) haswa zaidi vile vya bei raisi (kama Viroba, Chang’aa, banana na zile pombe nyingine za kienyeji.)


Pombe ya kienyeji inayotengenezwa na Ulezi na Ndizi Mbivu (aina ya Mbege)

Ulevi, ujulikanao pia kama uraibu wa pombe, ni ulemavu tegemevu wa kudhuru. Dalili zake ni unywaji pombe kupindukia bila udhibiti pombe licha ya madhara yake hasi kwa afya ya mnywaji,, mahusiano na hadhi yake machoni pa jamii. Kama matatizo mengine ya kiafya, ulevi ni mojawapo ya magonjwa yanayoweza kutibika.
Neno " ulevi" limetumika kwa muda mrefu tangu kubuniwa mwaka wa 1849 na Magnus Huss, ila katika nyanja ya utabibu istilahi hii iligeuzwa kuwa "utumiaji pombe vibaya" na " utegemezi pombe" katika miaka ya 1980 DSM III.
Aidha mwaka wa 1979 kamati ya wataalamu ya Shirika la Afya Duniani haikupendelea kutumika kwa neno "ulevi" kama istilali ya kiafya, huku ikipendekeza dalili za "utegemezi pombe".

Katika karne ya 19 na mapema karne ya 20, utegemezi pombe uliitwa dipsomania kabla ya kubatilishwa kuwa ulevi".
Hapana uhakika wa Sababu za kibayolojia zinazochangia ulevi, hata hivyo, hali hii yaweza kutokana na mazingira ya kijamii, mfadhaiko wa ubongo, afya ya akili, maumbile, umri, kabila, na jinsia.

Matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu huleta mabadiliko ya kimwili katika ubongo kama vile uhimili na utegemezi, nah ii haitofautiani sana na atahari za madawa ya kulevya, tokea pale kila kitu kikizidisha mwilini huleta athari flani kwenye mwili.


MADA YA KULEVYA NI NINI:

Kwa fasiri sahihi tu kuhusu madawa ya kulevya, ni kuwa mwili kuzoeshwa kilevya akili kwa muda mrefu na hivyo kuleta utegemezi na endapo Vilevya hivyo vikikosekana basi huleta athari katika mwili kwani hutuma ujumbe katika ubongo na fahamu kuwa kuna kitu kimekosekana muda kama huu ambapo kilevya hicho kilipotumika jana yake.

Mabadiliko ya kemia katika ubongo hudumisha hali ya mlevi kutoweza kuacha kunywa pombe na huweza kusababisha dalili za mtegemea-pombe pale aachapo kunywa, na wengine walioathiriwa zaidi huweza kukosa usingizi, kutetemeka mwili na hata kuwa mgonjwa kabisa.

Pombe huharibu takribani kila kiungo katika mwili, na kwa sababu ya athari hizo kwa kujumuisha ya sumu dhurifu ya utegemezi pombe , mlevi hukumbwa na hatari nyingi za matatizo ya kimagonjwa na kiakili.

Pombe sio mbaya, ila huwa mbaya ukizidisha na ukiizoesha mwili kwa muda mrefu, na hivyo ulevi huo huwa na madhara makubwa kwa jamii iliyowazunguka au watu wanaohusika na maisha yao.

ATHARI HIZO NI ZIPI?

Picha Madhara Ya pombe, nA MFUMO Mzima wa Kiakili na kimwili

Atari hizo ni kama vile, Wanawake kukabiliwa na matatizo ya muda mrefu ya utegemezi pombe kwa haraka zaidi kuliko wanaume. Zaidi ya hayo, wanawake hufa kwa kiwango cha juu zaidi kutokana na ulevi kuliko wanaume.


Mifano ya matatizo ya muda mrefu ni pamoja na uharibifu wa ubongo, moyo, na ini na pia ongezeko la hatari ya saratani ya matiti, Zaidi ya hayo, unywaji mzito wa muda mrefu umegunduliwa kuwa na athari hasi katika uwezo wa uzazi kwa wanawake na wanaume.

Hii husababisha mvurugiko wa uzazi kama vile kutozalisha yai, kupunguka kwakiwango cha molekuli ya ovari matatizo, au kukosa utaratibu wa hedhi, na kufunga uzazi mapema.

Ketoasidisi za pombe zinaweza kutokea kwa watu ambao hutumia pombe vibaya mara nyingi na walio na historia ya hivi majuzi yaulevi kupindukia.

Dalili za akili


Matumizi ya mabaya ya muda mrefu wa pombe unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya afya ya akili, na Matatizo sugu ya ubongo sio nadra, takribani asilimia 10 ya matukio yote ya shida za akili ni huhusiana na matumizi ya pombe, na hivyo kuifanya sababu kuu ya shida ya akili.

Matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha uharibifu wa kazi za ubongo, na afya ya kisaikolojia inaweza kuathirika baada ya muda Fulani, na inapoharibika basi kinachofuatia ni tabia tofauti zilizozoeleka na jamii unamoishi na kupelekea unyanyapaaji.

Kwanini matatizo kama hayo yaliyoorodheshwa hapa yakutokee kwa kujitakia! Wakati unaweza kuepuka?! Tuepuke ulevi jamani haswa mwisho huu wa mwaka na sikukuu nyingine zinazofuatia.

TUNAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA KUUONA MWAKA MPYA! 2018

Monday, 25 December 2017

X-MASS ASILI YAKE NININI? NA JE! LENGO LA KUPEANA ZAWADI LIMEANZIA WAPI!


 
Na: Stewart Meena

Ni sauti ya ngombe  aliaye horini ikiwa ni utambulisho wa kuzaliwa Yesu kristo ambapo Kila mwaka ifikapo tarehe kama ya leo Desemba 25, Wakristo duniani kote huadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Masiha wao (Yesu Kristo) aliyewaunganisha wanadamu na ufalme wa mbingu tena baada ya wanadamu kumwasi sana Mungu, Bwana Yesu Kristo.

Kiuhalisia, Wapo wanaojua maana halisi ya neno X-Mass kama siku ya kuzaliwa kwake Yesu, Lakini pia wapo baadi yao ambao hawaifahamu vyema siku hii.

JAPO KWA UCHACHE, HAYA HAPA MAELEZO MACHACHE AU TAFSIRI HALISI YA NENO HILI (X-MASS)

Kwa Kuanza Hebu Tujuzane Kwanza, Neno Christimass Limetokana Na Nini.!?

Krismasi inatokana na neno la Kiingereza lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo Au kwa Kiswahili christimas ni Noel ambapo  Noeli inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako imepokewa kutoka lugha ya Kifaransa "noël".

Hilo ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", likimaanisha "(siku ya) kuzaliwa..Christimass au Noel ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

 

Katika sikukuu hii watu hupenda kupamba nyumba zao kwa miti ya xmass na maua yenye rangi mbalimbali pamoja na taa za kuwakawaka vivyo hivyo utaratibu huu ulikuwepo toka zamani ambazo ni  kumbukumbu ya Alama za nyota zilizowapeleka mamajusi hadi Bethlehemu alikozaliwa Yesu kristo.

Halikadhalika kuna miti ya Krismasi  ambayo ni Ni ishara ya Krismasi ambapo zamani mti wa xmass  ulipambwa zaidi kwa matunda mbalimbali, siku hizi miti hiyo hupambwa kwa kuzungushiwa taa za vimulimuli, pamoja na maua yadukani (Spesho)

Pamoja hayo kumekuwa na desturi ya  watu kupeana zawadi ya maua na kadi zenye maneo mazuri ya kutakiana heri ya xmass  na jambohili la kadi na  kupeana zawadi mbalimbali  ambazo  hufunguliwa siku ya pili baada ya xmass  ambayo huitwa boxing day (26/12) yaani siku ya kufungua zawadi  ililikuwepo toka zamani.
KWA MFANO: (Ieleweke Hapa silengi Wafuasi flani, ila ni kuzidi kuelimishana)

Katika historia hapo mwanzo tunaelezwa  jambo  hili lilianzia kwa kiongozi mmoja wa dini  wa zamani aitwaye - Martin Luther yeye  enzi za uhai wake alikuwa na desturi ya kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu.



Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo na Hapo alikuwa  anarejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kwa mujibu wa maandiko.
Desturi ya kuwazawadia watoto kwenye sikukuu hii ilienea hadi kuwa desturi ya kupeana zawadi kati ya watu wa kila umri. Katika karne ya 20 desturi ilienea kiasi cha  hata kuwa ni  nafasi muhimu ya biashara.

VIPI SEHEMU NYINGINE DUNIANI:

Lakini Katika nchi nyingi Duniani ikiwemo na Tanzania mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine, Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na Kadi,miti ya xmass na  mapambo ya Krismasi vimekuwa vikiuzwa sana katika maduka mengi.
Lakini yote kwa yote, Wakati huu wa sikukuu ya Christmas ni wakati ambao familia huungana pamoja kwa shughuli mbali mbali ikiwemo kula,kunywa na kupeana zawadi hasa kwa watoto,kwa hivyo tusitumie nafasi hii kwa kufanya mambo yatakayo ziumiza familia zetu kwa namna moja au nyingine. Nakutakia Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.

Wednesday, 20 December 2017

MUZIKI NI KARMA AMBAYO MUNGU AMEIUMBIA MIOYO YETU, TUNAITUMIAJE?


Tokea enzi na enzi, vizazi na vizazi muziki umetumiwa kama sehemu ya utaratibu huu, kwa kuwa tu binadamu walioumbiwa hisia na ufahamu kutambua lipi jema au lipi baya (Lisilofaa kutendwa) wamekutanika pamoja kwa lengo na dhumuni moja.

Tangu tulipozaliwa, inaelekea tumekuwa tukisikia muziki wa ala fulani, ambazo hatukuweza mara moja kuzitambua kutokana na uchanga wetu duniani, lakini kadiri tulivyokuwa ndipo taratibu tukaanza kuzielewa na kuzipenda pia (iwe kwa kufuatisha kuimba au kutikisa vichwa vyetu).

Pengine ,huenda mama yako alikuimbia wimbo flani ili kutubembeleza ulale, na kweli haukupita muda mrefu ulilala, Hivyo ndivyo tunavyoweza kuuelezea muziki ambao hupelekea hisia mbili tofauti kwa mwanadamu kulinganisha na namna mapigo na mirindimo ya ala zake zilivyo vurumishwa.

NAJUA KILA DINI, TAMADUNI WANA MFUMO NA AINA YA UIMBAJI NA MIZIKI WANAYOIPENDELEA, HIVYO MIMI SILENGI DINI FULANI WALA SIBAGUI DINI AU TAMADUNI FLANI;

TUANGAZIE MUZIKI KATIKA BIBLIA:

Chanzo:
Mwandishi wa amkeni! Nchini hispania



MUZIKI una nguvu. Unaweza kutuliwaza, kutusisimua, na kuchochea hisia zetu. Unaweza kuonyesha shangwe na huzuni yetu, Karibu katika tamaduni zote—za kale na za leo—muziki hugusa akili na moyo. Naam, kwa kweli muziki ni zawadi kutoka kwa Mungu.—Mwanzo 4:21.

Tulipokuwa vijana, huenda tulianza kupendezwa na muziki uliosisimua mioyo yetu, Hata tukiwa watu wazima, wengi wetu bado tunapenda kusikiliza muziki unaotutuliza nafsi zetu, pindi tunapoendesha gari au tunapokuwa nyumbani mwishoni mwa juma (wikendi) baada ya kwisha kwa siku zenye shughuli nyingi.

Maneno ya wimbo fulani huenda yakatia ndani mambo kuhusu utamaduni au historia ya nchi, Waisraeli wa kale waliadhimisha pindi za (Majira) fulani ya pekee kwa nyimbo, (Kutoka 15:1-21; Waamuzi 5:1-31)

Nabii Musa alitunga wimbo ambao ulitia ndani historia na mahimizo mazito kwa ajili ya watu aliokuwa akiwaongoza (Kumbukumbu la Torati 32:1-43) Hapana shaka kwamba nyimbo kama hizo zilikuwa njia nzuri kabisa ya kujikumbusha mambo tofauti na kuhimizana kutokukata tamaa mpaka watakapoifikia ile ahadi Musa aliyopewa na Mungu wao.

UNAWEZA KUIMBA!

Huenda ukasema, ‘Siwezi kuimba vizuri.’ Hata hivyo, fikiria kidogo kuhusu sauti yako. Kwa sababu ya ala hiyo yenye matumizi mengi, kwa kadiri fulani karibu kila mtu anaweza kuimba, iwe ana ala nyingine au laah, Unachohitaji tu kufanya ni kufungua kinywa chako na kuimba. Na unapoimba, usihangaikie sana ikiwa utashinda tuzo fulani au kupigiwa makofi kwa sababu ya sauti yako. Ukifanya mazoezi, utaiboresha.

“Sauti inahusiana sana na chanzo cha hisia zetu za ndani, nayo ndiyo ala bora zaidi ya kuonyesha hisia hizo,” lasema gazeti Psychologies la Hispania. “[Kuimba] kunasisimua,” anasema Ainhoa Arteta, mwimbaji wa soprano. “Ningependekeza yeyote anayetaka kufunua hisia zake kwa kuimba afanye hivyo kwa uhuru na kwa hiari.”

Kwa sababu muziki unaweza kuwa na uvutano mkubwa juu ya moyo, tunapaswa kuwa wateuzi wa ala gani haswa zaupendeza moyo wetu, tusiwe na michanganyo kwani hata Mungu hapendi michanganyo.

Kwa mfano, mdundo mtamu unaweza kufunika maneno machafu ambayo yanapunguza uzito au hata kuchochea chuki, ukosefu wa maadili, au jeuri—mambo yasiyoweza kumvutia hata kidogo mtu yeyote anayependa mema kusikiliza aina hiyo ya muziki.

(Waefeso 4:17-19; 5:3, 4) “Linda moyo wako kuliko vitu vingine vyote vinavyopaswa kulindwa,” lasema Neno la Mungu, “kwa maana ndiko zinakotoka chemchemi za uzima.” (Methali 4:23) Ndiyo, kuteua muziki ni suala zito sana.

Muziki Mzuri Unaweza Kuwa Dawa Nzuri


“Mojawapo ya sababu zinazofanya muziki upatikane katika karibu tamaduni zote ni uwezo wake wa kutokeza na kudumisha afya na hali njema ya wanadamu,” chasema kitabu Principles and Practice of Stress Management. Tunapoimba, chasema kitabu kingine, mwili wetu wote unajaa sauti na kutikisika, Na kutikisika huko taratibu kunafanya tishu za mwili zitulie na kupanuka, na hilo linaweza kupunguza maumivu.

Kwa sababu hiyo, madaktari fulani wamewatia moyo wagonjwa walio na mfadhaiko wasikilize muziki unaotuliza, ambao pia unaweza kumchangamsha mtu, hivyo Katika hospitali fulani, muziki huchezwa hata katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Mara nyingi, watoto wanaozaliwa kabla ya wakati na pia wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wanaitikia muziki unaopendeza, Kulingana na kitabu Principles and Practice of Stress Management, uchunguzi unadokeza kwamba kusikiliza muziki unaotuliza “unapunguza sana homoni zinazoleta mfadhaiko wakati wa upasuaji.”

Pia, muziki unaweza kuwafanya wanawake waja-wazito wasiwe na wasiwasi mwingi kwa kuwafanya watulie wanapokuwa na uchungu wa uzazi, pia Nyakati nyingine madaktari wa meno huwachezea wagonjwa walio na wasiwasi muziki wenye kutuliza ili watulie, Lakini muziki na nyimbo zinaweza kuwa na matokeo makubwa zaidi na Zinaweza kutusaidia katika njia ya kiroho.

‘NITAMSIFU MUNGU KWA WIMBO’

Je, ulijua kwamba asilimia kumi ya Biblia ni nyimbo? Mifano iliyo wazi zaidi ni Zaburi, Wimbo wa Sulemani, na Maombolezo. Kwa kufaa, asilimia kubwa ya marejeo mia tatu hivi ya nyimbo yanahusiana na kufanya ibada kwa Mungu.

Kwa kweli, Daudi alipanga wanaume 4,000 wa kabila la Lawi watumike kama wanamuziki na waimbaji huko Yerusalemu. Wanaume 288 kati yao ‘walizoezwa nyimbo kwa Yehova, wote wakiwa wajuzi.’ (1 Mambo ya Nyakati 23:4, 5; 25:7) Hapana shaka kwamba waimbaji hao walifanya mazoezi kwa bidii. Kwa kweli, muziki ulikuwa muhimu sana katika kumwabudu Mungu hivi kwamba waimbaji hawakupewa wajibu mwingine wowote ili wakazie fikira uimbaji.—1 Mambo ya Nyakati 9:33.

Usiku uliotangulia kifo chake Yesu pamoja na mitume wake walimwimbia Mungu sifa, na inaelekea waliimba Zaburi 113 mpaka 118, Kufikia wakati wa Yesu, zaburi hizo—zilizoitwa “Zaburi za Haleli”—ziliimbwa wakati wa sikukuu ya Pasaka.


(Mathayo 26:26-30) Maneno “Zaburi za Haleli” yanarejelea kule kurudiwa kwa neno “Haleluya!” linalomaanisha ufupisho wa kishairi wa jina la Mungu Aliye Juu Zaidi Zaburi 83:18.

Ambapo baadaye Pia uimbaji ulikuja kuwa sehemu ya ibada ya Kikristo, Kitabu The History of Music kinasema: “Wakristo wa mapema walikuwa na zoea la kuimba mbele ya watu na pia katika ibada ya faraghani.

Kwa sababu muziki hutusaidia kufunua karibu kila hisia na kwa sababu unaweza kuwa na uvutano mkubwa juu ya moyo, akili, na mwili wetu, tunapaswa kuheshimu sana hiyo ‘tuzo kamilifu kutoka juu.’ (Yakobo 1:17) Naam, na tuitumie kwa kadiri tuwezavyo na kwa hekima.

Mbali na kukataa nyimbo zinazotukuza chuki, ukosefu wa maadili, na jeuri, wale wanaompenda Mungu na wanadamu wenzao wanakataa pia kusikiliza muziki unaounga mkono ibada ya sanamu, uzalendo, na uwongo wa kidini. —Isaya 2:4; 2 Wakorintho 6:14-18; 1 Yohana 5:21.

SOURCE: https://wol.jw.org/sw/wol/h/r13/lp-sw JARIDA LA AMKENI
KWA KUBOFYA KWENYE MANENO YALIYOPIGIWA MSTARI, UTAONGEZA MAARIFA ZAIDI.

NUKUU: "chakuambiwa ongezea na chako" NAWATAKIA WAKRISTO, NA WASIOKUWA WAKRISTO WOTE MAANDALIZI MEMA YA KUPOKEA X-MASS (Kuzaliwa Kwa Kristo Yesu)

Saturday, 16 December 2017

UTAFITI WAONYESHA KUTIA LITHIUM KWENYE MAJI YA BOMBA KUNAWEZA KUUKINGA UGONJWA WA ALZHEIMER


 
Wanasayansi wa Denmark wamefanya utafiti ukionesha kuwa, kutia Lithium kwenye maji ya bomba kunaweza kuwasaidia watu kukinga ugonjwa wa Alzheimer, ambayo itakuwa njia yenye gharama ya chini zaidi ya kuzuia ugonjwa huo.

Lithium ni aina ya chuma chenye rangi ya fedha, ambayo iko ndani ya njia ya bomba katika maji ya bomba. Utafiti wa awali umeonesha kuwa Lithium inaweza kutumiwa kutuliza hali ya moyo, haswa kwa wale wanaosumbuliwa na presha nk.

 
Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Copenhagen wametoa ripoti ikisema, wamelinganisha kiwango cha ugonjwa wa Alzheimer katika baadhi ya sehemu nchini Denmark na kiwango cha lithium ndani ya maji ya bomba.

Utafiti umeonesha kuwa, kiwango cha juu cha lithium katika njia ya bomba kinaweza kupunguza dhahiri kiwango cha ugonjwa wa Alzheimer.

Watafiti wanaona kuwa kutia lithium kwenye maji kweli kunaweza kuwafanya watu wengi zaidi kuwa mbali na ugonjwa wa Alzheimer, lakini lithium hiyo inatakiwa kuwa katika kiwango mwafaka, kwa kuwa kiwango cha juu au cha chini kinaleta madhara.

Wanasayansi wa Uingereza wamesema, kiwango cha lithium katika maji kina uhusiano wa wazi na ugonjwa wa Alzheimer, lakini hatuwezi kutia lithium ndani ya maji kabla ya kufahamu kiwango mwafaka.

Picha na: Getty Image
SOURCE: Radio China Swh.
TEMBELEA PIA HAPA KWA HISTORIA NA ELIMU ZAIDI: https://www.facebook.com/stewart.meena/
 

Tuesday, 12 December 2017

VIRUTUBISHO AINA 6 (SITA) AMBAYO HUPASWI KUVIWEKA KATIKA FRIJI LAKO


Najua watu wengi sana hupenda kuweka vyakula vyao au baadhi ya matunda kwenye friza (Friji) pasipo kujua madhara ya kuviweka vyakula hivyo au matunda hayo, ambapo lengo kuu la kuhifadhi sehemu hizo ni kwaajili ya kuzuia visiharibike au kuoza mapema kutokana na mazingira yetu ya joto.

Ubaridi upatikanao kwa friji huweza kutunza matunda au baadhi ya vyakula kama nyama kwa siku kadhaa kuanzia 3—6, lakini kiuhalisia ni kuwa kuhifadhi huko hakusaidii kuimarisha virutubisho vyake bali kunafanya kupoteza virutubisho vyote ambavyo huitajika na mwili kujijenga.

Hivyo kwa mujibu wa tafiti zilizokwishafanyika zimeonyesha kuwa, vipo baadhi ya vyakula na matunda ambavyo ukiviweka kwenye friji hubadilisha mfumo wake wa awali, na kutengeneza baadhi ya kemikali ambazo huweza kuleta madhara kwa mwili wa muhusika taratibu.

BAADHI YA MATUNDA HAYO NI KAMA: STRAWBERRIES (Matunda Damu)


Matunda damu haya unapoyaweka kwenye friji, situkuwa hupunguza ladha yake ya asili bali pia haushauriwi kitaalamu kuyaweka kwenye friji zaidi ya siku1 baada ya kuchumwa kutoka mashambani kwani huweza kuyafanya kupoteza virutubisho vyake vya asili ambavyo huzidi kupotea kadiri inavyoendelea kukaa kwenye friji.

Vilevile baada ya kuyachuma, yakupasa uyatumie ndani ya siku zisizozidi 2, zaidi ya hapo haupaswi kuyaweka kwenye eneo lenye joto kali, au lenye jua kwani huweza kuharibika upesi pia, kupoteza virutubisho vyake kwa upesi zaidi kama ilivyokuwa kwenye friza, ANGALIA HAPA: Opt-out of direct sunlight.

Na hautakiwi kuyaosha matunda haya unapoyachuma, labda uyaoshe ndipo uyatumie muda huohuo na kama ni kwa ajili ya matumizi ya baadae usiyaoshe, kwani strawberries hupoteza virutubisho vyake upesi pindi zinapooshwa na kuhifadhiwa.

TOMATOES (Nyanya)


Endapo hutaki nyanya ulizozichuma kwa ajili ya matumizi yako, kwa wakati huo au wa baadaye kuharibika ladha yake na kuwa isiyopendeza, basi yakupasa na unashauriwa pindi unapochuma nyanya zako ambazo bado hazijaiva kutoziweka kwenye friji.

Nyanya zinapoendea kukaa ndivyo zinavyozidi kuiva na kuharibika vilevile, lakini tofauti na matunda mengine kadiri zinavyozidi kuivya ndivyo ladha yake inavyozidi kubadilika badilika na huchukua muda mrefu zaidi kuharibika endapo zitawekwa kwenye chumba chenye joto kiasi na sio ubaridi.

Na kwa sifa hiyo ndio maana nyanya inavyozidi kukaa kwa muda ndivyo hubadilisha ladha yake, na inapofikia wakati huo huifadhiwa na kutengeneza kikolezea vyakula mfano wa viazi au chipsi (chillsource) ambao ni mchanganyiko wa pilipili na nyanya zilizovundikwa.

Nyanya zilizohifadhiwa vyema katika hatua ya mwisho, na mbali ya baridi na joto kali huweza kudumu kwa muda mrefu zaidi ya matunda mengine pasipo kuharibika. Endelea hapa: If you grow your own tomatoes.

POTATOES (Viazi)


Viazi kama ilivyo kwa matunda, navyo pia wataalamu wanashauri visiwekwe kwenye friza kwa minajili ya kuvihifadhi na kutoharibika, kwani pindi unapokuja kuvitumia baadae unapovitoa kwenye friji vinakuwa tayari vimejibadilisha mfumo wake wa awali na kutengeneza ladha ambayo ni ya upekee na ile iliyozoeleka awali ambayo ni kuwa na virutubisho vya protini na wanga (Carbohydrates) vinavyopatikana kwenye viazi hivyo.

Unashauriwa pindi unapovuna viazi vyako shambani kwa matumizi ya baadae, basi viache vikiwa na udongo wake na usivioshe, labda mpaka siku ya matumizi ya wakati huo huo kwani, unapoviosha viazi hivyo na vipapatwa na jua huelezwa kupoteza ladha yake (taste) na kuwa isiyopendeza.

Kama vile tu ilivyo kwenye kuvihifadhi katika friji kulivyo kunaviondolea ladha na virutubisho vyake vya msingi, hivyo epuka kuweka viazi hivi kwenye friza au kuviosha pindi unapovivuna na kuvihifadhi au kuviweka kwa matumizi ya baadae.

ENDELEA KUELIMIKA HAPA: keep root-cellar out of direct sunlight

UNRIPE BANANAS (NDIZI AMBAZO HAZIJAKWIVA VYEMA)

Tunda la ndizi lina faida sana kwa mwanadamu, ikiwemo kuchochea uwezo wa ubongo wa binadamu kutunza kumbukumbu, kupandisha kinga ya mwili na kuondoa harara (vipele) viletwavyo na mafuta yasiohitajika mwilini.

Hivyo kama ilivyo kwa matunda mengine ukiyaweka kwenye friji ni kama umeyazuia kuendelea kuiva vyema, kadhalika ndizi ambazo hazijaiva vyakutosha nazo unashauriwa kutoziweka kwenye friji hilo kwani utapoteza virutubisho vyake vya msingi ambavyo hujitengenezea vyenyewe kadiri tunda hili zinavyozidi kuivya.

ANGALIZO: Ndizi zinazoshauriwa kuliwa ni zile ambazo zimeiva kiasi cha kuwa na (vidotidoti kahawia) na sio zaidi ya hapo kwani, zikiwa za kijani kitupu ni sawa unakula makapi tu, na zikiwa zimezidisha kuiva zaidi na maganda yake kupoteza vidotidoti vyake kahawia na kuwa rojorojo hutoka katika mfumo wake wa asili wa virutubisho na kuzalisha kemikali nyingine ambayo huweza kuelezeka kama ina chembechembe za vilevya mwili (Alcoholic). Ndio, ndio maana pombe kama zile za kienyeji (Mfano-mbege) hutengenezwa kwa kutumia ndizi zilizoiva kupitiliza kisha kupikwa na kuhifadhiwa kwa siku kadhaa nk.

Unaweza ukaweka ndizi zilizoiva vyema kenye Fiji kwa siku kadhaa, lakini hazitafaa kulika tena zikibadilisha rangi kutoka njano na kuwa nyeusi. Nyeusi hiyo hutokana na kuzalishwa kwa kemikali nyingine ndani ya ndizi hizo ilitwayo na ubaridi uliopo kwa wakati huo.

HONEY (Asali)


Asali haushauriwi kitaalamu kuiweka kwenye friji kutokana na kiwango chake kikubwa cha sukari ilichonacho, hivyo tokea zama asali huifadhiwa sehemu ambayo hakuna mionzi ya jua moja kwa moja na pia sehemu isiyo na baridi sana.

Zama hizi, watu huona kwa kuwa wanyao friza basi wanadhani kila kitu ukikiweka kwenye friji kinapedeza kwa kuliwa, ukweli ni kuwa vingine kutokana na baridi, na kadiri vinavyozidi kukaa basi hutengeneza sumu ambayo huleta madhara katika mwili wako badala ya kuleta kinga au kukupatia virutubisho mwili.

Faida za asali katika mwili hakuna asiyezijua, hata wataalamu mbalimbali wa maswala ya tiba asili wamesema hawajawahi kuona mmea au tunda lolote lenye kiwango kikubwa cha virutubisho kama ilivyo kwa asali.

Unashauriwa, kutumia asali walau mara2 au 3 kwa siku, au ikiwezekana tumia kwenye maji ya kunywa au katika chai kama (kikolezeo) badala ya sukari kwani ukifanya hivyo basi miaka100 kwako itakua sio mingi nab ado utakuwa mwenye afya iliyoimara bila kutembelea mkongojo (Fimbo)

Hivyo usiweke asali kwenye friji, bali unaweza kuweka sehemu nyingine: store it on a shelf in your pantry.

UNCUT MELONS (Tikiti maji lisilokatwa)


Kuweka tikiti-maji (watermelon, cantaloupe or honeydew) lisilokatwa licha ya kuwa huchukua nafasi kubwa kwenye friza lako, lakini pia huondosha ladha na virutubisho vya asili endapo ikiwekwa katika friji kwa zaidi ya siku 2.

Hivyo unashauriwa usipendelee sana kuhifadi matikiti kwenye friji, la hasha ikilazimu kwa kuwa umeshayapasua uyaweke lakini yasizidishe siku mbili kuwekwa sehemu hiyo vinginevyo utakapokuja kuyala utakuwa unakula tu ili ujaze tumbo na sio unakula ili kuupa mwili wako virutubisho vya msingi vipatikanavyo kwenye matunda haya.

Sehemu sahihi unayoshauriwa kuyaweka matikiti yako baada ya kuyavuna ni kwenye chumba au sehemu ambayo hakuna joto sana na wala hakuna baridi sana, mfano kwenye sakafu, kwenye vichenje, matenka nk.

If you have leftovers, store them in an airtight container in the fridge for up to three days

ZINGATIO: Vyote hivyo havipaswi kuwekwa kwenye Friji, Na kama ulikuwa ukiviweka vyote hivyo kwenye friji yako awali kwa matumizi ya baadaye, na kwa mazoea basi utakuwa umekosea na unapaswa kutoviweka kuanzia hivi sasa unapoisoma elimu hii.

ZAMBAZA KWA WENGINE NAO WAONE: