Wednesday, 25 November 2015

Semina Na Makongamano Yote Ya Serikali Kufanyika Online Kwa Tele-conferencing......... Hakuna Tena Posho Za Vikao Wala Viburudishaji


SERIKALI kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA).

Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.

“Tulianzisha mfumo huo ili kupunguza gharama zisizo na ulazima ambapo awali ilitakiwa kila kunapokuwa na kikao lazma watumishi wasafili kuja Dar es Salaam kwaajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia Video Conference iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. Tumeokoa gharama za nauli, mafuta, chakula na malazi,” amesema Temba.

Temba ameeleza kuwa, hatua za utekelezaji wa teknolojia hiyo ulianza kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2013 hadi sasa ambapo umekamilika na kufanyiwa majaribio yaliyofauli kwa kufanya mikutano kumi ambayo iliunganisha mikoa yote kasoro mitatu ambayo ni mipya ambayo ni, Njombe, Geita na Simiyu.

Kuhusu miondombinu ya mawasiliano amewatoa hofu watumishi kwa kusema: “Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.”
SOURCE: Mpekuzi blog

Barca wazima AS Roma, Arsenal wang'aa

Kikosi cha timu ya Arsenal wakishangilia ushindi wao wa jana dhidi ya Bate Borizov

Barcelona wakiwa nyumbani wamechomoza na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya AS Roma katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Bayern Munich wakiichapa Olympiakos mabao 4-0, Maccabi Tel Aviv wakilala hoi kwa Chelsea kwa kichapo cha mabao 4-0.
Arsenal walijiwekea hai matumaini ya kufuzu kwa hatua ya makundi kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Dinamo Zagreb.

BATE Borisov wakifungana bao 1-1 na Bayer Laverkusen, FC Porto wakilala 2-0 dhidi ya Dynamo Kiev, Zenit St P wakiichapa Valencia 2–0 na Lyon wakilala mbele ya KAA Gent bao 2-1.

Michuano hiyo inatarajia kuendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa.
Miongoni mwa mechi hizo ni Man United dhdi ya PSV Eindhoven, Atletico Madrid na Galatasaray, Juventus dhidi ya Man City na Shakhtar Donetsk watawaalika Real Madrid.

Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa ni kama ifuatavyo:
  • Barcelona 6 - 1 AS Roma
  • Arsenal 3 - 0 Dinamo Zagreb
  • Bayern Munich 4 - 0 Olympiakos
  • Maccabi Tel-Aviv 0 - 4 Chelsea
  • BATE Borisov 1 - 1 Bayer Leverkusen
  • FC Porto 0 - 2 Dynamo Kiev
  • Zenit St Petersburg 2 - 0 Valencia
  • Lyon 1 - 2 KAA Gent