Moja ya miti iliyopandwa na Binadamu kwa ajili ya kurejesha halimisitu iliyopotea katika eneo hili. Picha Na Stewart Meena |
Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. lakini pia ipo misitu mingine ya Kupandikizwa na binadamu katika mazingira yaliyomzunguka na kwa muundo anaoutaka yeye mwenyewe (Artificial)
https://sw.wikipedia.org/wiki/Msitu
Kila mwaka ifikapo Tarehe 21/03 ni siku ya Misitu duniani ambapo sambamba na maadhimisho hayo pia elimu hutolewa kuhusiana na utunzaji wa misitu asilia pamoja na ile ya kupandwa na Binadamu ili kurejesha Muingiliano mzuri kati ya binadamu na Mimea (Frora & Fauna)
Mtiririko wa Maji katika chemchem zitokazo ardhini kwenye misitu ya asilia. Na Stewart Meena |
Pasipo mimea hakuna mvua, kutokana na mzunguko mzima wa kuvukiza Maji kwenda angani, na kisha tena kurejea Ardhini, hutegemea sana misitu hii kuvuta mvua hiyo.
Kuanza kufunga kwa mawingu ikiwa kama ishara ya kutaka kunyesha kwa Mvua. Na Stewart Meena |
TUNZA MISITU IKUTUNZE