Showing posts with label MAKALA / UCHAMBUZI. Show all posts
Showing posts with label MAKALA / UCHAMBUZI. Show all posts

Thursday, 17 September 2026

UCHAWI, UHUSIANO - ELIMU KUHUSU VIUMBE WASIOONEKANA!



Elimu kuhusu uchawi na majini ni mada pana inayochukua nafasi kubwa katika imani za kijamii, kitamaduni, na kidini (hususan katika dini kuu zilizopo (Mfano: Ile ya Kiislamu na Kikristo), katika mabara yote saba katika sayari hii ya tatu (Dunia) katika mzunguko wa sayari zote kulizunguka jua.

Afrika na zaidi ikiwemo Afrika Mashariki, Pengine uchawi na elimu kuhusu viumbe wasionekana kwa macho ya kibinadamu (Majini) hutumika tofauti sana na ustaarabu wa maeneo mengine duniani, mfano barani Ulaya, America, na Asia – hutumia elimu hii kwa maswala ya utajiri na mali, teknolojia na maswala ya ki-injinia nk. Tofauti na Afrika hutumika kulogana na kutiana uchizi, kuchuma kwa kuiba mali za wengine (Chuma ulete nk.)

Uchawi kwa bara letu la Afrika, huhusishwa na kuwanga ‘Yaani kuzunguka katika majumba ya watu usiku  na kuwatia zongo nanuksi kwa kuwanenea maneno ya kichawi, na kwa mila na Imani zao yale waliyoyanenea hutukia kwa walengwa waliowakusudia.

MAJINI:

(Mitazamo Ya Kidini Na Kijamii (Ukristo na Uislamu)

By Nancystodd - Icon-religion.svg-Wikipedia


UISLAMU: Kuhusu Majini (Majinn)

Katika mafundisho ya kidini (hasa ile ya Kiislamu), majini ni viumbe halisi walioumbwa na Allah; Ikiwa ni tofauti na binadamu walioumbwa kwa asili ya UDONGO (Adamu na Hawa) na Malaika walioumbwa kwa NURU, Majini waliumbwa kwa MOTO usio na moshi (moto wa upepo mkali).

UKRISTO: Kuhusu Majini (Mapepo/Demons)

'bofya kiungo kwenyemaneno yaliyopigiwa mstari'

Katika mafundisho ya uKristo, yamejikita zaidi kuelezea namna binadamu wa kwanza alivyoumbwa, kisha baadae mwanamke (Adam na Eva), na baadhi ya vitabu kama (Kitabu cha HENOKO ‘Enoch’) Kikiwa kimechambua kuhusu uchawi, majini nk. Kikiondolewa na kutotumika kabisa kwa madhehebu yaliyo mengi ndani ya ukristo, Zaidi kikibakia kutumiwa na Kanisa na ambalo pekee linalokitambua kitabu hicho kama sehemu ya maandiko yao matakatifu ni Kanisa la Kiorthodoksi la Tewahedo la nchini Ethiopia.

Kitabu cha Henoko (kwa Kiingereza: The Book of Enoch) ni mkusanyo wa maandishi ya kale ya kidini ya Kiyahudi yanayonasibishwa na Henoko, babu mkuu wa Nuhu; Ingawa kilitungwa kati ya karne ya 3 na ya 2 K.K, kitabu hiki hakimo katika kanoni rasmi ya Biblia inayotumiwa na Wayahudi na madhehebu mengi ya Kikristo Duniani.



SIFA ZA MAJINI:

Uhuru wa Kuchagua: Imeelezwa kwenye uislamu, kama walivyo wanadamu, majini wana uhuru wa kuchagua kuwa wema (waumini) au wabaya (makafiri); ambapo Jini mbaya au kafiri mara nyingi huitwa Shaytani (Shetani) au Ibilisi.

Maisha Yao: Imeelezwa (Kwenye simulizi za Imam-Shafii) kuwa: wanaishi, wanakula, wanazaa, wanasafiri, na wanakufa kama ilivyo kwa wanadamu, na upekee mkubwa walionao ni kuwa wao wanauwezo wa kutuona wanadamu, lakini wanadamu/binadamu hawezi kuwaona katika umbo lao la asili.

AINA ZA MAJINI NA MAKAZI:

Kwa mujibu wa maandiko mbalimbali, wamegawanyika katika makundi makuu matatu: Wenye mbawa na wanaoruka angani; Wanaotambaa au kuchukua maumbo ya wanyama (kama nyoka Paka au hata mbwa weusi) na wengine: ni wale wanaoishi maeneo maalum na kutembea kama binadamu.

MAKAZI YAO: Wanapendelea kuishi maeneo yaliyotengwa kama vile mapango, bahari, majalala, nyika, na nyumba zilizoachwa tupu kwa muda mrefu ‘maghofu’.

JINSI JINI ANAVYOWEZA KUMDHURU AU KUINGIA KWENYE MWILI WA BINADAMU:

Wanachuoni wengi wanakubali kuwa jini anaweza kuingia au kuathiri mwili wa binadamu kutokana na sababu kadhaa:

Kisasi: Binadamu anapomdhuru jini bila kujua (mfano: kumwaga maji ya moto pasipo kutaja jina la Mungu).

Mapenzi: Jini wa kiume kumpenda mwanamke wa kibinadamu (au jini mwanamke kumpenda mwanamume), maarufu kama Jini Mahaba.

Kutumiwa kupitia Uchawi: Jini anapotumwa na mchawi kwenda kufanya uharibifu, au kumdhuru mtu aliyelengwa ‘kunuwiwa’ katika uchuwi huo.

Hali za Ghafla: Jini anaweza kuingia mtu anapokuwa na hofu kubwa iliyopitiliza, hasira kali sana, au kughafilika kiimani, Lakini wengine huenda mbali zaidi na kusema haswa kwa WANAWAKE ‘wakiwa wachafu kama wanamilikiwa na viumbe hawa basi watawapanda kwa kuwa hawapendi seemu iliyo chafu. (Dhahiri: Kwenye baadhi ya shule za mabinti pekee, sio nadra kusikia Fulani kapandisha ‘mapepo’)

 


ELIMU KUHUSU UCHAWI

Uchawi ni vitendo vinavyofanywa na binadamu kwa kushirikisha nguvu za giza (Kutumika kwa majini wabaya au mashetani kama nlivyoeleza hapo juu) ili kubadilisha uhalisia wa mambo au kusababisha madhara kwa mtu mwingine.

KIJAMII: Aina za Uchawi Zinazozungumzwa ni zile za, Kurithishwa / Asili, Kununua, na kwa kujifunza, ambapo “Kiasili – Siri za uchawi zinarithiwa ndani ya familia au ukoo tangu utotoni kizazi na kizazi ‘generation to generation’.

·       Uchawi wa Kujifunza: Mtu anapoenda kwa waganga au wachawi wakubwa ili kufundishwa mbinu na miiko ya uchawi.

·       Uchawi wa Kutupiwa (Vifungo na Magonjwa): Kutumia majini au madawa ya kigiza kumfunga mtu kimaisha, kumfanya mgonjwa, au kuharibu ndoa na biashara yake.

Dalili Zinazohusishwa na Uchawi au Kusumbuliwa na Majini:

Kulingana na matatibu wa tiba asilia na za kidini, mtu aliyeathiriwa na uchawi au majini wabaya anaweza kuonyesha dalili mbalimbali kama vile:

·       Maumivu ya mwili yasiyoonekana kwenye vipimo vya hospitali (kama kifua kubana au moyo kwenda mbio).

·       Kuota ndoto za kutisha mara kwa mara (kama kufukuzwa na wanyama wakali, kuanguka kutoka sehemu ndefu, au kufanya tendo la ndoa ndotoni).

·       Kuchukia ghafla mambo ya ibada au kuhisi uzito mkubwa unapotaka kusali au kusoma vitabu vitakatifu.

·       Mabadiliko ya tabia ya ghafla, mfano: mke kumchukia mume au mume kumchukia mke bila sababu ya msingi.

·       Kuhisi ganzi, joto kali, au baridi isiyo ya kawaida kwenye viungo vya mwili.

 


KINGA NA TIBA DHIDI YA UCHAWI NA MAJINI

Katika mifumo yote ya imani, suluhisho kubwa la kujikinga na nguvu hizi hutegemea kumkaribia Mwenyezi Mungu na kufanya ibada ‘Dua’ kwa kumcha yeye pekee, na kwa waKristo (Kufanya Maombi) kwa kuliita na kulitaja jina la YESU inatosha kukuepushia na maswahibu yote hayo.

·       Nguvu ya Jina la Yesu: Wakristo huamini kuwa mapepo (majini wabaya) na nguvu za uchawi hushindwa kupitia maombi ya damu na jina la Yesu Kristo.

·       Kufunga na Kuomba: Kutenga muda wa maombi maalum ya kuvunja vifungo vya kigiza.

·       Kuishi Maisha ya Utakatifu: Kujiepusha na dhambi ili kuzuia shetani kupata mlango wa kuingia kwenye maisha yako.

Mbali na hilo kwa upande mwingine wa UISLAMU tiba imeelezwa ni kufanya (Tiba ya Ruqya), Kusoma Quran: Kutumia aya za Quran na dua zilizofundishwa na Mtume Muhammad (S.A.W), wakitumia Surah maarufu kwa kinga iitwayo (Ayat al-Kursi, Surah Al-Ikhlas, Surah Al-Falaq, na Surah An-Nas)

·       Dua za Asubuhi na Jioni (Adhkar): Kinga kulinda mwili na nyumba dhidi ya mashetani.

Kujiepusha na Ushirikina: Inashauriwa na ni marufuku kwenda kwa waganga wa kienyeji wanaotumia majini kutoa tiba, kwani kufanya hivyo ni kumuasi Mwenyezi Mungu na kuongeza matatizo kwenye maisha ya muhusika atakayefanya shirki ‘Ushirikina’.

Tahadhari ya Kiteknolojia na Kijamii:

Katika ulimwengu wa sasa, kuna kurasa nyingi za mitandao ya kijamii na tovuti zinazodai kufundisha namna ya kuwamiliki au kuwatumia majini kwa ajili ya utajiri, Kununua pete, na vito mbalimbali ili kupata nguvu hizo za kichawi, zaidi sana zinazotumiwa na waganga.

Viongozi wengi wa dini wanaonya vikali dhidi ya kutembelea au kusoma maudhui haya, kwani yanatajwa kuwa ni mitego inayoweza kumuingiza mtu kwenye matatizo makubwa ya kisaikolojia na kiroho, kwa kuamini kile asichokiamini; – Maana imeelezwa kuwa ‘Imani huumba’

EPUKA KUAMINI, NA ISHI KWA KUMTEGEMEA MUNGU PEKEE KATIKA MAJARIBU NA MASWAHIBU UNAYOKUTANA NAYO, MAANA YEYE NDIE MUHUKUMU WA MWISHO, KWENYE MAISHA HAYA NA BAADA YA MAISHA HAYA.

Tufuatilie hapa tafadhali (bofya kiungo chini kwenda facebook Page):

#SirMeena: Waweza kuniandikia maoni yako na tukajadili pamoja....

Je! Kuna uhusiano kati ya Imani hizi na Fremason? Hili nalo ni fumbo jingine! Tuishie hapa kwa Leo. ASANTE!

Friday, 4 September 2026

POPULAR LAKES IN TANZANIA (BEOND THE MYTH RECORDED AND COUNTING)

Lake Nyasa (Pomonda Rocks)

 Na.

Stewart Meena (writer)

There is article state: Tanzania Said to have fewer lakes "49" in common (Great and small pools lakes-than others East African countries) Ranking 3rd:

Beside Tanzania: The article also exaggerate: Uganda ranking 1st with "69" and Kenya 2nd with "64" Lakes, and small pools lakes.

BUT: What is a real and what is a myth!? (Language used: (Swahili & English)

Remember, Lakes are not like a Rivers, Streams, Glaciers, Marshes or mangroves, and Dams (Which altogether looks alike) "Small pools "mentioned" resembles like a lake" but they are different)

About the article's the numbers in Kenya and Uganda also involves (Small pools, mangroves, Marshes, Dams etc) that why i said "exaggerated number) If you deny it, give us the names, or outline those-that found in your country!

Tanzania Should be Ranking: 1st, Uganda 2nd, and Kenya 3rd, because of the geographical nature of those mention countries, also the total size of those countries' Non deserts zones, &  sources of inland streams that made a lake etc.

In my accounting bellow (Regards Tanzanian mainland) I try to #Mention Lakes, and not including Swamps, Dams or mangroves areas) to establish evidence in that number...

Lets dive In Swahili: Tanzania imefanyizwa na mikoa takribani (26 mainland & 5 in Islands (Zanzibar regions)  na ikiwa imepakana na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Congo DRC, ambazo kwa pamoja zinaunda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Malawi na Msumbiji upande wa kusini.

Nchi hii ina utajiri wa mbuga za wanyama nyingi zaidi ya 69, ina Mlima mrefu kuliko wote Afrika na wa pili kwa Dunia (Highest standing mountain) KILIMANJARO, na Ecosystem yenye utajiri wa Mito, Maziwa na bahari.

Ni kwa mantiki hiyo basi tunakusogezea baadhi ya Maziwa (Lakes) yanazopatikana katika nchi hii, (Eneo la Tanzania Bara) kama ifuatavyo:

East-africa-map: Peter Hermes Furian

MAZIWA MAKUU (Common Lakes Are): RelatedSource

  1. Ziwa Victoria (likiunganisha mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera) huku likichepukia pia katika nchi za Uganda na Kenya. Ni ziwa hili ndio chanzo kikuu cha mto Mara unaokatisha Kenya na Tanzania pamoja na ule mto Nile (River Nile) ambao huu umeambaa-ambaa hadi nchini Misri.
  2. Ziwa Tanganyika (Ziwa lililopo magharibi ya Tanzania na likipitiwa na Bonde la ufa "Great rift valley) na kuunganisha nchi ya Tanzania, Burundi, na Congo DR. Huku ziwa hili inasemekana ni mojawapo ya chanzo cha mto zambezi uliopo nchini Zambia. (Kwa Tanzania likiunganisha zaidi mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa na Mbeya.) readMore
  3. Ziwa nyasa (Lake Malawi) hili ni ziwa mashuhuri lililopo Kusini mwa Tanzania likiitwa ziwa nyasa upande wa Tanzania na ziwa Malawi upande wa Nchi ya Malawi. Kwa tanzania likiunganisha zaidi mkoa wa Ruvuma na Njombe. Peruzi

 

Lake Kigoma (Kagongo Village  view) By Halidtz

MAZIWA MENGINE NI PAMOJA NA: (eng: Lake = sw: Ziwa) (Geographical Location – HERE)

Lake Natron (Red lake) ziwa lenye magadi, na Maarufu zaidi kwa ndege aina ya flamengo (Kaskazini mwa Tanzania, Mkoani Arusha) HAPA

Lake Natron (Popular for Migrant bird, Flamengo)


Lake chala (Ziwa hili lipo mkoani Kilimanjaro, mpakani kabisa na nchi ya Kenya) Ramani, Mengine hapa ni: Ziwa Kihurio; na Nyumba ya Mungu (God’s house)

Amboseli lake ikiwa Tanzania mpakani na eneo la (Maasai Mara Iliyoko nchini Kenya, mkoa wa bonde la ufa-loitoktok, kajiadoo, kule kunapatikana Hifadhi ya wanyamapori ya Ambussel) hivyo usichanganye na ziwa hili la Tanzania AngaliaHapa

Lake Duluti (Arumeru-arusha)


Ziwa Lutamba; ziwa Maliwe na ziwa Mkoe (Yote yakiwa, Mkoa wa Lindi)

Lake Eyasi (ngorongoro-arusha)

Lake Tenge, (Dar es salaam)

Ziwa Chada; Ziwa Katabe (yote yakiwa Katavi Tanzania)

Lake Kanvi; Kilanga; Tanga; Musimu; Moye; Masimba; & Lake sagara (yote yakipatikana mkoa wa Kigoma)

Lake Manyara; Lake Burungi ‘ziwa sereri’; Lake Austin; Lake Balangida; Lake Tailiwi ‘Ziwa Babati’; Ambussel; Lake Kwansari (Tlawi); Lake Kimana; & Lake Basotu (All are in Manyara Region) Zaidi

Lake Jipe (Mwanga Kilimanjaro) Jipe

Lake Magadi (Simiyu-Tanzania)

Lake Mdutu au Ndutu (Arusha) SomaZaidi

Lake Magadi-(Ngorongoro-Arusha)

Lake Rukwa etc. Yaone hapa (To watch them here:)

 

Ngozi Lake 'Mbeya Region' (By: Joachim Huber-Switzerland)

LAKES NYENGINE NI: (English-Lake; Swahili: Ziwa)

  • Lake ngwazi (Iringa)
  • Lake Saosa (njombe)
  • Mkoa wa Mtwara: una maziwa ya: (Lake-Tandahimba; Mweru; Mpwapwa; Mambamba; Chidya; Kitere na Ziwa Lipelwe)
  • Mkoa wa Tanga una maziwa ya: (Lake Magoroto, na Lake Manka)
  • Pwani Regions Lakes are (Lake Tagalala; Nzerkera; Siwadu; Mzizima na Utenge; & Mansi)
  • Lake Gombo (in Morogoro Region)
  • Lake Kindai; Lake Singida; Minyere; Mikuyu; Ziwa Kitangiri; Ziwa Chaya; na Ziwa Sulunga; Yote yakipatikana mkoa wa (Singida)
  • Hombolo lake; Serya; Haubi lake & Lake Nzuhe (Dodoma)
  • Lake Ngosi / Ngozi crater (Tukuyu-Mbeya)
  • Elemeti lake (Shinyanga)
  • Liteho lake (Ruvuma)
  • Lake Momela lake in (Arusha)
  • Lake burigi (Chato-Geita) etc.

Source: 

https://traveltriangle.com/blog/lakes-in-tanzania

 

Lake Chala - Kilimanjaro (By: Joachim Huber)

MENGINE NI: ZIWA

  • Gombo, Nziwi, Haubi, Igalula, Mamka, Rutamba, Balangida
  • Lake: (Mansi, Sagara), Lelu (Sekena), Basuto (Minyere)
  • Lake Ilamba; Kingiri & Lake W.Heckmann (Mbeya-Tanzania)
  • Lake Sundu (Rukwa-Tanzania)
  • Lake: Bisongo (= Ngoma) Kajumbura, & Mkoe, (Mujunju (= Rwakajunju) Tlawi, Burungi (Kingili)
  • Ziwa Burigi; Lake Ikimba; Bisongu; Kasinga; Lwelo; Ngembe; Kaburi na Ziwa Ruko (Yote yakipatikana mkoa wa Kagera Tanzania)
  • Ziwa Welu, Empakai (Kitere)

Source: https://www.fao.org/3/t0473e/t0473e09.htm

Sunday, 30 August 2026

MJI MTAKATIFU WA JERUSALEM, MWINGILIANO, CHANZO IMANI ZA DINI TOFAUTI


Na.
Stewart Meena'

Kwa miongo kadhaa sasa, tofauti na zamani kumekuwepo na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina, mmoja kati ya hawa akidai kumiliki eneo hilo moja kwa moja na mwingine akidai uvamizi.

Mji wa Yerusalemu (Jerusalem) umegawanywa katika pande mbili, Jerusalem Mashariki na ile ya Jerusalem Magharibi, ambapo Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu (tokea ilipotangaza hilo 1980 kama mji wake mkuu wa milele), huku Jerusalem Mashariki hutazamwa na Palestina kama mji wao mkuu wa taifa lao.

Eneo lote la Jerusalem, kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya mwaka 1967 taifa hilo lilipojitangaza kuwa dola huru chini ya umoja wa mataifa, ambapo Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa kama ukiukwaji wa haki ya umiliki wa mji huo.

Ingawa inakadiriwa eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000, na kutambuliwa kama eneo halali la waPalestina na Mataifa mengi ya nchi za Kiarabu na zile zenye waislamu wengi duniani.

Je! ni kwa nini mji huu huzozaniwa kwa kiasi hicho na mataifa haya mawili?

Sababu kubwa ni kuwa maeneo haya, hupewa umuhimu wa pekee na imani au "Dini kubwa tatu duniani" (Ukristo, Uislamu na Uyahudi) Ambapo imani zote hizi tatu humuangazia 'Abraham/Ibrahim' kihistoria ambaye anatajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani ulimwenguni kote. Mfano: 'Biblia humuita kama baba wa imani'

Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu, ikiwa ni miongoni mwa mji wa kale zaidi ambao upo hadi sasa duniani.

Kihistoria mji huu uliwahi kutekwa, ukabomolewa na kuharibiwa vibaya sana, kabla ya kuja kujengwa upya tena, kwa kuyarudisha na kuhifadhi yale maeneo muhimu yaliyokuwepo tokea enzi maeneo hayo.

Eneo hili, ukichimbua sehemu ya ardhi yake kwenda chini, hufichua enzi fulani katika historia yake kuonyesha eneo ilo palikuwa na mji uliopotea (Lost city), hivyo ingawa kumekuwa na ubishani au mzozano kati ya dini mbalimbali kuhusu umiliki wa eneo hilo, lakini dini zote huungana kwa pamoja kuungama na kusali katika eneo hilo kwa vipindi na misimu, kwa kuutaja ni mji takatifu.

Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale, ikigawanyika katika pande au maeneo manne makuu, likitofautishwa na upekee wa aina ya majengo yake kuwa na muundo wa tofauti kulingana na tamaduni za wenyeji wa mitaa husika.

Moja ya maeneo hayo manne: Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia, na kila eneo likiwa limezungukwa au kutenganishwa na ukuta mkubwa wa mawe. kama ilivyo kwenye ukuta wa maombolezo (Wailing wall & west bank)

Wakristo wana maeneo mawili, yale madogo ya wakristo wa Kiarmenia, na ya wakristo wengineo, kukiwa kumehifadhiwa kwa vituo vya vya kale zaidi vya wakristo hao hususani utamaduni wa Waarmenia duniani, uliohifadhiwa ndani ya Kanisa la St. James na nyumba kubwa ya utawala.

Nje ya Lango la Damascus, kuna Kanisa kuu Ndani ya mtaa huo wa Wakristo, likiwa na ukumbusho wa mahifadhio ya pango au 'Kaburi lenye historia kuhusu kifo na Ufufuo wa Yesu Kristo kama masihi na muokozi wa wakristo kote duniani. Ni eneo hilo inaelezwa 'Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary na hapo ndipo alipofufuka.

Kanisa takatifu hilo husimamiwa kwa pamoja na kwa ushirika wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo wakihudumu hapo, wale wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia. Pia kuna Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.

Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.



Al Qudus: Mtaa wa Waislamu huu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.

Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf, ambapo Waislamu hao huamini kwamba Mtume wao 'Muhammad' alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote katika viunga vya eneo hilo.

Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe jeusi la msingi, huko Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni. Hadi hivi wa leo Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka ku hiji, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.



Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka eneo lote lililokuwa Hekalu Takatifu, ambapo hapo ndipo eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.

Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa; Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac.

Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Patakatifu.

Ukuta wa Magharibi ndilo eneo la karibu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kufanya maombi yao, wakisimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji wa kiyahudi kutoka kila pembe ya dunia.

Hivyo: Kwa mujibu wa imani zote hizo tulizojadili na kuuchukulia kwao kwa upekee sehemu na baadhi ya mitaa ya eneo hilo, ndio maana kumekua na kuongezeka kwa mzozano wa kiimani na kiitikadi kila mmoja kutaka kudai na kutambuliwa kuwa eneo hilo ni lake, huku wengine wakifika mbali kutaka kufuta kabisa kumbukumbu na historia za imani nyingine ili kusiwepo na muingiliano huo.

Ni maeneo haya hususani nyakati za siku kuu za kidini, umati wa wageni hufurika maeneo haya kwa lengo la kutimiza moja ya nguzo zao kiimani, kama njia ya kuenzi na kuwa karibu zaidi na Mungu muweza aliyeziumba mbingu na dunia.

CHANZO:
BBC Swahili, & Blogsite washirika

Saturday, 22 August 2026

MFAHAMU NDEGE KORONGO AINA YA MARABOU, 'THE UNDERTAKER'

 

Picha: Wikipedia

Na.

Stewart Meena

Kutana na ndege wasio na sauti au "mlio", wenye miguu mirefu na wenye kuweza kuhimili ongezeko kali la joto" ikilinganishwa na ndege wengine warukao, na hiyo ikampatia sifa ya upekee na majina mbalimbali kama: 

"Undertaker, na Marabou storks" Kiswahili wakijulikana kama ‘KORONGO MARABOU

Ndege hawa, ni waviziaji na vyakula vyao vikuu ni pamoja na mabaki ya mizoga ya wanyama tofauti, mabaki ya vyakula vitumiwavyo na wanadamu, samaki pamoja na vyakula vingine kama, mijusi, nyoka, vyura, wadudu, panya na ndege wengine wadogowadogo.

Makazi makuu ya ndege hawa ni maeneo yote karibu na mito, maziwa, milimani ndani ya miamba, na kwenye hifadhi za wanyamapori, tambarare zilizo na miti mirefu, ambapo licha ya urefu na ukubwa wao, wanaweza kuruka katika eneo kubwa la anga na kupaa umbali mrefu.

Kuruka kwao, huweza kuruka hewani umbali wa futi-13,000 (feet) toka usawa wa bahari, na inapokuja swala la mwendokasi katika jamii yao ya ndege, Korongo huwenda hawa wakawa wana kiwango kidogo cha mwendokasi huo.

UKWELI USIOUJUA KUHUSU NDEGE HAWA.

Picha: Rubega Safari

Marabou stork, ni miongoni mwa ndege wasiovutia (ugliest bird on the world) kwa kuwatazama, kwa mwonekano wao (wakiwa na Miguu mirefu, shingo ndefu na eneo kama tumbo la kuhifadhia chakula linaloning’inia karibu na shingo yao likiwa na rangi ya pinki (Eng: a pink gular sac).

Ndege korongo huyu, hutambulikana pia kama ndege muuwaji kwa muonekano wake kwa nyuma ukiwa unamtazama, wazungu wakimuita “Nature’s eyesore / the undertaker bird” na ndiye ndege jamii ya tai mwenye miguu mirefu katika jamii hiyo centimita karibu 50, huku mbawazao zikiwa na urefu wa futi11 na kuwafanya ndege hawa kuwa na upekee tofauti na ndege wengine.

Sambamba na ndege wote kuwa au kutambulikana pia kwa milio yao, ndege hawa hawana milio hiyo, ingawa huweza kuwasikia wakitoa milio Fulani inayotokana na kugongesha midomo yao au mbawa zao.

Hadi kufikia umri wa ukomavu ndege hawa, huchukua karibu miaka mine ‘4’ na kuwafanya miongoni mwa ndegw wanaokua taratibu-taratibu Zaidi ikilinganishwa na ndege wengine wanapoanguliwa kwenye mayai yao.

Korongo hawa wa marabou, hupatikana pekee yake barani Afrika (Ukiacha waliohifadhiwa katika zoo za wanyama) kwenye maeneo ya kitropiki kwenye nchi kama, Senegal, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Tanzania, Kenya, Uganda, Namibia, Congo, Afrika ya Kusini nk.

(Unaweza kusoma pia hapa)

Kwa nchi ya Tanzania: Ndege hawa ni maarufu Zaidi kwenye ukaanda wa ziwa Victoria na Tanganyika, na huweza kuwaona Zaidi kwenye hifadhi ya taifa ya Serengeti, Manyara, Nyerere, Tarangire nk. Ambapo wenyeji wa mikoa ya Manyara, Mara, Mwanza, Geita ndege hawa huingia hadi maeneo ya masoko na mijini.

Picha: Natalie Carberi
Marabou (Korongo) ni ndege anayependa kuchangamana Zaidi na binadamu ndani ya makazi yao na hii ni kwa ajili ya urahisi wa kupata vitoweo vyao, huku wale kwenye hifadhi ya wanayama hupendelea Zaidi kuwa karibu na wanyama wawindaji kama Fisi, Chui, Duma, Simba na Mbweha ikiwa ni sehemu rahisi kwao kuvizia mawindo yao na kuyaiba. (Marabou stork are known to be scavenger bird) Kimsingi ndege hawa korongo sio wawindaji hodari, ila ni waviziaji hodari.

Wanawezaje Kuhimili Joto Kali La Uwanda Wa Savana?



Ili kupunguza ongezeko la joto na jua kali linalowatesa ndege wengi, kwa ndege Korongo ni tofauti kidogo, ambapo miili yao inauwezo wa asili wa kubadili kanijoto mwili wao kuendana na ukali wa jua au joto la maeneo waliyopo, kuficha uso wao ndani ya mabawa na kutanua mfuko wao wa pinki uliopo chini ya shingo huwawezesha kuendana na mabadiliko hayo ya joto.

Na endapo kutakua na baridi kali na wanahitaji joto, basi hutanua mabawa yao (mbawa) na hiyo huwawezesha kurudisha kwa haraka ongezeko lao hilo la joto ndani ya miili yao.

Kimazingira kwenye jamii yao, huwenda hawa ndio ndege wavivu zaidi na wasiopenda kuhangaika kutafuta vitoweo, isipokua kusimama karibu na wanaotafuta (kuwinda) na wakishapata kitoweo chao wao ndio huenda eneo hilo na kuwafurusha kwa ajili ya kuiba kitoweo hicho. Mfano: Kanda ya ziwa huiba samaki zilizovuliwa na wavuvi.

Mazaliano yao hupendelea zaidi majira ja kiangazi wakati kina cha maji maeneo mengi yakiwa yameshuka au kukauka, kwani ndio urahisi zaidi wa wao kupata vitoweo vyao kwa urahisi zaidi.

Ni msimu huu huweza kuwaona ndege hawa wakiwa karibu-karibu zaidi, na madume wakipambana kwa midomo yao ili kuwania haki ya kumiliki korogo jike kwa ajili ya mwanzo wa mazalia yao, ambapo atakayeshinda ndio kuanzia hapo ataambatana na jike husika kwa muda wote wa kujenga kiota, kurutubisha mayai, kutaga na kuyaatamia, kisha watoto watakao anguliwa kushirikiana kuwatafutia chakula kwa pamoja hadi watakapoweza kujitegemea wenyewe.

Angalia

Ndege hawa wakishaungana, huishi hivyo wawili pekee kifamilia hadi mwisho wa maisha yao, na ajabu nyingine ni kuwa hawachanganyi mwenza na ikitokea mmoja kati yao amekufa mwingine huakia hivyo hivyo na huelezwa, sababu ya upweke na yeye hachukui muda mrefu kabla ya kufa, ambapo baadhi ya tafiti husema ndege mwenza aliyesalia huweza kujinyima chakula kama njia ya yeye kufa.

Waweza pia kusoma HAPA

MWISHO: Kwa sababu ya urefu wa miguu yao, mbawa zao na midomo yao hii huwafanya kuwa na uwiano sawa wenye kupungua uzito hivyo kumuwezesha kuruka kwa urahisi zaidi wanapopaa angani, ikilinganishwa na jamii nyingine za ndege walio na urefu na uzito kama wa kwake.

Pia eneo la pinki karibu na shingo yake, hutumia hapo kama akiba ya kuhifadhi chakula chake akiwa ameshiba, kisha kula kwa wakati mwingine hususani anapokuwa ana njaa.

Tafadhali unaposasisha (Kushare taarifa hii), hakikisha unatambulisha chanzo cha taarifa hii kwa kutupa ‘credit’ Asante! StewartMeena

Thursday, 8 November 2018

UKWELI USIOUJUA KUHUSU RADI (THUNDER STORM) NA CHANZO CHAKE (LIGHTNING)



Na Stewart Meena

Radi hutokana na mvutano wa hali ya hewa kinzani katika tabaka la juu la mawingu ambapo ukinzani huo huchagizwa na mabadiliko ya hali ya hewa, mgando wa barafu “kuganda na kuyeyuka” matone ya mvua pamoja na mwendokasi wa mzunguko wadunia “kujizungusha yenyewe kwenye mhimili wake (rotation) na kuzunguka jua (revolution) pamoja na sayari nyingine.
Kimsingi katika dunia yetu ambayo ni sayari ya3, kumegawanyika karibu matabaka 4 ya mawingu, ambapo tabaka la juu kabisa hujulikana kama (stratosphere) na eneo la kwanza la tabaka hilo, hutafsiriwa kama mwisho wa upeo wa macho yetu kwa kuangalia angani, ambapo eneo hilo sio eneo la mawangu halisi.

Eneo unapoona rangi ya bluu na nyeupe hapa ndipo mwanzo wa mzalisho wa mawingu yenye barafu katika tabaka la pili la juu yake ambalo hilo ndilo husababisha mvua kunyesha pindi barafu inapoyeyuka kwa joto kupenya eneo hilo.
Eneo hili la kwanza sio mawingu halisi isipokuwa ni msafirisho wa mvuke na ukungu (fogs) unaozalishwa kwa baridi kuendelea kuzidi kwani kwa kadiri unavyopanda juu kutoka usawa wa bahari ndipo ongezeko la baridi linapotokea kwa wale waliobahatika kupanda mlima kama Kilimanjaro ukiwa karibia kileleni ukiangalia chini huwezi kuona villivyopo chini badala yake utaona ukungu huo mweupe unaotanda eneo hilo, na hii ndio sababu maeneo yote ya uwanda wa juu kaskazini na kusini kwa Tanzania yetu kunakuwa na baridi kali muda wote wa mwaka kutokana na mwinuko wao kutoka usawa wa bahari. Mfano:Iiringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Lushoto-Tanga nk.

Mvutano wa hewa nayozungumzia ni hewa inayopatikana eneo la chini ya tabaka la kwanza la mawingu (sehemu tuliyopo) inayoitwa ‘oxygen’ itolewayo na mimea na ile ya ‘carbon-dioxide’ tuitowayo wanadamu na wanyama wengine, na ile inayopatikana tabaka la juu la mawingu naitrojeni ‘nitrogen’ hizi huweza kuchagiza tabia tofauti ya hali ya hewa katika tabaka hilo la kati na la juu la mawingu na hata eneo tulilopo la ardhi na lile la chini kabisa ya ardhi.
Na hapo ndipo huwa chanzo cha kuzaliwa kwa nishati ya radi, uwepo wa tufani kadhaa duniani kama vile vimbunga na zile za baharini, uwepo wa tetemeko la ardhi ikisababishwa na kusafiri kwa volkaniki (volcano) chini ya ardhi n.k

TUNAPOSEMA RADI NDIO NINI, NA KWANINI HULETA MADHARA DUNIANI?

Radi (thunder) sio muungurumo, kama wengi mnavyodhani ila radi ni mwale wa kama shoti ya umeme unaotokea kabla ya muungurumo na baada ya muungurumo kupita; mwale huo ni nguvu kama nishati ya umeme ambao huu huwa na vipimo-nishati zaidi ya umeme (voltage & watts) ambayo hii huwa na kiasi cha Vol. zaidi ya elfu-10 ukilinganisha na ile ya umeme inayoanzia (vol.110/220-1000)
Kama tulivyoona mwanzo kwanini radi hutukia, lakini bado watu huwa na maswali mengi kwanini mara kadhaa imekuwa ikileta madhara kwa kupiga miti’ nyumba na watu wakati mwingine, hivyo kuhusisha radi hiyo na imani za kishirikina pamoja na kuvaa aina ya mavazi.

KUNA UHUSIANO GANI:
Kitaalamu hakuna uhusiano wa radi na imani za kishirikina isipokuwa kuna mazingira yanayoweza kuifanya radi kupenya kwenye mawingu na kushuka moja kwa moja aridhini na kuleta madhara mahala ilipofikia (gravitation area).
Radi huambatana na mvua na mvutano wa nishati kama ya msumaku, na endapo ikitokea ikawa inasafiri angani na kukawa kunauvutano wowote wa mfumo wa nishati kama ya umeme, umande umande wa barafu na mazingira ya mvua huweza kupiga na kushuka hadi eneo hilo.


Ndio maana nyumba zenye umeme huekewa chuma flani ya rangi ya shaba na kuchimbiwa ardhini ili kuzuia radi hiyo kuwa na uwezekeno mkubwa wa kuipiga nyumba hiyo, na hivyo ni hatari zaidi kutumia umeme wa moja kwa moja pasipo kuweka kizuizi hicho kwasababu nishati ya radi huwa ni mara maelfu zaidi ya umeme wa kawaida

Na inapotokea radi hiyo kupiga basi tambua kuna mvutano uliopo katika eneo hilo, mvutano ambao huivuta nishati ya radi na kuileta hadi aridhini na kisha kuleta madhara kwenye eneo husika palipo na kani mvutano huo (gravitation).


Kuna uhusiano mkubwa sana uliopo kati ya nishati umeme wa radi na umeme wa majumbani, Uvutano wa sumaku, mvukizo wa joto la ardhi haswa maji yanaponyweshwa juu yake; na uwepo maji haswa yale ya mvua pamoja na yale ya bomba na aina ya nyenzo yanayopitia (mipira au chuma) wakati radi ikipiga.
Mabomba yaliyotengenezwa kwa chuma cha zinki, aluminium na shaba, hupitisha umeme na hivyo kwa kuwa maji hupita ndani yake, na ukayatumia wakati radi ikipiga kuna uhatarisho; lakini yale yaliyotengenezwa kwa mipira huwezi kuwepo kwenye uhatarishi ukilinganisha na hizo nlizozitaja.

MAVAZI:
Kuhusu mavazi hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa kupigwa na radi na aina ya mavazi tunayoyavaa (Mfano watu husema ukivaa mavazi mekundu ni rahisi zaidi kupigwa na radi kweli?) Jibu ni kuwa sio kweli.!

Isipokuwa mavazi tunayoyavaa na tabia ya hali ya hewa kwa wakati huo, kwa kushirikiana huweza kuleta uwezekano huo kwa kufuata tabia ya miale ya radi inavyosafiri pekee na eneo ulilopo wakati huo kama ilivyo kwa tabia za vyanzo vya nishati nyingine kama jua na moto.
  • Mfano kivizikia (Physics): Jua hutufikia kwa njia a mnururisho;

  • Umeme au moto husafiri kwa njia ya mpitisho;
Hivyo katika mavazi nayo huwa na tabia yake katika kuakisi na kuvuta miale hiyo ya nguvu za sumaku, nishati ya jua, moto na nguvu nyingine za nishati ya umeme kama ilivyo kwa radi.

Mfano: mavazi meusi husharabu moto, joto au nishati ya jua;
Maazi meupe huakisi hali hiyo apo juu.

Mavazi mengine kama ‘Mekundu, Njano, Zambarau nk’ hayaakisi wala kusharabu nguvu hizo za nishati isipokuwa haya huwa na uwezo wa kutunza joto hilo kwa muda flani, na ndio maana katika uvutano wa sumaku mavazi haya na yale yenye asili ya unailoni au mipira huweza kuzalisha miale mfano wa cheche za moto ambazo hizi hutoa muangaza.
(Fanya zoezi moja: Chukua moja ya mavazi hayo, kasha yavae mwilini au yasugulie kwenye nywele zao kisha yafikiche yenyewe kwa yenyewe gizani usiku utaona yakitoa miale hiyo mfano wa cheche)

NINI KINATOKEA HAPO MTU KUPIGWA NA RADI NA UNAWEZA KUJIKINGAJE!:

Kwa utangulizi nilioueleza katika tafiti na makala yangu hapo juu: Imeelezwa kitaalamu kuwa radi huambatana na nishati nyingine duniani, na kuna uhusiano mkubwa sana kati yake na mvua/maji; uvutano wa sumaku na hali-joto ya mahali haswa ardhi wakati radi inapiga pamoja na mwingiliano wa hewa tofauti inayochagizwa na kujizungusha kwa dunia katika mhimili wake (Rotation) na kulizunguka jua (Revolution).
KUJIEPUSHA: usipende kukaa chini ya miti wakati mvua inanyesha na huku ukiwa umevaa mavazi yoyote yenye uwezo wa kutengeneza Usumaku yanapogusana (rejea kwenye mavazi juu); kuweka kizua radi majumbani unapofunga umeme lakini usipende kusikiliza redio au kutumia internet ukiwa kwenye eneo la mwinuko na penye umande umande au chini ya miti wakati mvua ninanyesha.

Unashauriwa kuepuka kutumia maji kwenye mabomba yasiyo ya mpira wakati radi inasafiri, kuoga wakati huo nk; lakini pia ni vyema ukapunguza matumizi makubwa ya vifaa vinavyotumia umeme wakati huo kama vile kuwasha Tvs, Radio, kutumia pasi na Heater kupikia au kuchemshia maji kuchaji simu kwa wakati mmoja.
MWISHO: radi ni mwale ule unaoonekana kabla ya muungurumo kusikika, na muungurumo huo huzalishwa kutokana na nguvu za radi hiyo (mwale) na mgandamizo wa barafu (Mawingu mazito yaliyoganda na matone ya mvua kugusa eneo hilo kutoka tabaka la juu zaidi la mawingu) msuguano wa hali za hewa kinzani.

Tahadhari: Radi ni kama ilivyo kwa nishati ya umeme, na huweza kuleta maafa kwa kuwakisha moto au kumuunguza muhusika, usikae karibu na nyaya za umeme (haswa unaosafirisha voltage kubwa) wakati mvua zinanyesha au radi kupiga.
JIFUNZE ZAIDI NAMNA GANI EATH-QUAKE NA THUNDER STORM’ HUTOKEA KWA KUBOFYA VISAIDIZI HAPA CHINI NA VILIVYO NA RANGI BLUU JUU:

Radi

Tetemeko la Ardhi

Thursday, 31 May 2018

MAAJABU! ZIFAHAMU NCHI-12 AMBAZO ZINAONGOZA KWA UPUNGUFU WA JINSIA YA KIKE KATIKA NDOA.!




Idadi ya wingi na uwiano wa jinsia ya kiume na jinsia ya kike duniani inazidi kutofautiana sana nah ii ikichagizwa na jeografia na historia ya eneo husika, katika rika zote kwa jinsia hizi mbili.
Leo hii, utofauti wa uwiano huo umeingia hadi katika maswala ya mahusiano, ingawa idadi ya mabinti na vijana walio-wapweke (Yaani-single) ikibakia kufanana isipokuwa kuna baadhi ya nchi nyingine hali ni mbaya sana kutokana na vijana au mabinti wengi waliofikisha rika la kuoa au kuolewa wakikosa watu wa kuwaoa kabisa.
Hiyo inasababishwa na nini?

Kwa tafiti zilizofanyika kwenye baadhi ya nchi hizo imebainisha kuwa, ukatili wa kijinsia kwa Wanawake, matukio ya vita vya wenyewe mara kwa mara, kutafuta nafasi nzuri za kazi na umaskini uliokithiri ndio hupelekea watu hasa Mabinti kuhama-hama au kutafuta makao sehemu nyingine salama zaidi kwao, na hivyo katika maeneo waliyotoka kubakia na Upungufu huo mkubwa wa kupata wachumba wa kufunga nao pingu za maisha (ndoa).

Kwa mfano: Nchini Tanzania, tazizo hili lipo zaidi kwa wanawake (Mabinti) kukosa Wanaume waliotayari kuwachumbia na kufunga nao ndoa, ambapo –
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2016, Tanzania inakadiriwa kuwa na wakaazi zaidi ya milioni 47, ikipanda kutoka milioni 45 kwa mwaka 2005, na kati ya idadi hiyo wanaume ni robo ya wanawake wote Tanzania.
Hii inamaanisha kuwa idadi ya (wanawake) au jinsia ya kike kwa tanzania ya leo imeiizidi idadi ya (wanaume) jinsia ya kiume kwa zaidi ya asilimia 35%, ambapo kwa hesabu za haraka haraka inabidi kila mwanaume awe na wake wa3 ili kufidia (gape) uwazi huo uliopo.

Sasa wakati hapa kwetu Tanzania idadi ya wanaume ndio ndogo kulinganisha na wanawake, kwa nchi za wenzetu mambo ni tofauti kabisa, na idadi ya wanawake ni robo ya wanaume wote kwenye nchi hizo ambapo asilimia 72% ndio wanaume na asilimia 28% ndio wanawake.

Kwa mfano huo, Na kwa sababu hizo basi, tofauti na ilivyo kwa Tanzania mabinti wakikosa wanaume waku-waoa, hii hapa orodha nyingine kabisa ya baadhi ya (Nchi-12) zinazoongoza duniani kwa kuwa na upungufu wa wanawake na sio Wanaume kiasi kwamba pindi mtoto anapozaliwa huwekewa (oder) na wazazi wenye mtoto wa kiume kwa minajili ya kuchukua jiko katika nyumba hiyo kwa siku za baadaye pindi watoto wao watakapokua kwa kuwa Vijana wao wanakabiliwa na tatizo la kukosa au kuwa na wakati mgumu kupata wenzi wao wa maisha.
Qatar




Nchi ya Qatar iliyopo katika nchi za kiarabu ni miongoni wa nchi ambazo kuna upungufu wa mabinti, na kushikilia rekodi hiyo kwa muda mrefu kwa sasa. Sababu kubwa ya upungufu huo ni pamoja na taratibu na sheria ya nchi hiyo inayozingatia maadili ya kiislamu zaidi na hivyo kutopendelewa zaidi na mabinti na raia wengine kuingia nchini humo, ikichagizwa na serikali ya nchi hiyo kutotoa visa kwa (Jinsia ya kike) wa mataifa wengine ispokuwa Uingereza na Canada pekee.

Sababu nyingine kubwa ni uzalianaji duni, tokea pale wanaume (karibu-94%) huihama nchi yao na kwenda kufanya kazi mataifa mengine ya kigeni kiasi ya kwamba serikali ya Qatar kwa sasa ikawalazimu kutoa nafasi za wahamiaji na kuwapatia kibali maalumu (Visa) ili kuziba upungufu huo wa nguvukazi taifa waliohama makwao kwa ajili ya kutaka kuinua uchumi wan chi hiyo.

Uwiano (ratio) kati ya wanaume na wanawake kwa nchi hii iliyo mashariki ya kati na iliyo tajiri kwa uzalishaji wa mafuta ni 3.41 to – 1.54.
United Arab Emirates (UAE)


 

Hadi kufikia karne ya (20th-century), UAE ilikuwa na upungufu wa karibu watu 40,000 kwa raia wazawa, huku wanawake pekee wakiwa 22,000, hiyo ikitokana na raia wake kuhama nchi hiyo na kwenda nchi jirani kutafuta maisha kabla ya kugundulika kwa mafuta, ambapo kidogo kwasasa idadi ya wakazi wake imeongezeka kidogo, huku wengi (85%) wakiwa sio raia wa nchi hiyo bali wapo hapo kula maisha. Wengi mtakubaliana na mimi kwa kufanya utafiti mdogo tu wa wakaazi wa dubai, kwa kuangalia wazawa na wale wasio wazawa.

Lakini katika kuongezeka huko bado uwiano baina ya wanaume na wanawake sio sawa, ambapo kwasasa inawalazimu wanaume wan chi hiyo kwenda nchi nyingine za kiarabu kutafuta wachumba huko.

UAE pato lake kubwa hutokana na Mafuta na Utalii, kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali kwenda nchini humo kula bata.
India


India inashika nafasi ya 3 kuwa na upungufu wa mabinti duniani, ingawa tunaweza kusema inashika nafasi ya3 duniani kwasasa kwakuwa na watu wengi ukiacha China na Marekani, huku idadi ya raia wake ikikisiwa kuzipita China na USA na kushika nafasi ya kwanza ifikapo mwaka2024. lakini wengi wa watu hao bado wanaume ndio wengi.

Kwa muda sasa na kwa mila na desturi za nchi hiyo, Mabinti ndio wamekuwa wakitoa mahari ili kumposa Kijana, hii imekaa vipi? Ndio tuseme unafikiria kuwa wanaume ndio adimu! Hapana.

Uwiano uliopo kwasasa kati ya wanaume na wanawake nchini humo ni asilimia karibu 1.08 ya kila mwanaume kwa mwanamke mmoja, yaani sawa na tuseme kila mwanamke wa india awe na wanaume 5 kuleta uwiano sawa.

Ukilinganisha na nchi za (G-20) na ikiwa miongoni,  India kwasasa inapiga hatua kimaendeleo zaidi duniani ingawa bado kuna changamoto za wanandugu kuendelea kushikamana pamoja, wazee wakiwa wengi kuliko nguvu kazi ambapo ni vijana na hivo wanaume wenye uwezo kidogo kuwasaidia wazazi na ndugu zake wote.

Sababu kubwa ya upungufu huo haijawekwa bayana lakini watafiti wanaamini kuwa Wanaume wa nchi hiyo huwa na bahati sana ya kupata watoto wa kiume kuliko wa kike, hivyo familia moja yenye watoto 7, wakike ni wawili tu pekee.
China


China inashika nafasi ya 4 kwa upungufu wa wanawake kwa hivi sasa licha ya kuwa inaongoza duniani kwa kuwa na watu wengi zaidi, Idadi Wanaume kwa nchi hiyo kwasasa ni karibu (40-million) zaidi ukilinganisha na wanawake robotatu ya hiyo, yaani sawa na tuseme kila Mwanamke atatakiwa awe na wanaume3 ili kuweka uwiano sawia.

Upungufu huo umechagizwa na sheria ya muda mrefu ya nchi hiyo, kuwa shurti wazazi wawe na watoto2 pekee ili kupunguza ongezeko la watu nchini humo, hatua iliyowanya wazazi kuzingatia uzazi wa mpango.
Lakini sasa hasara yake ni kuwa, Wazazi wengi walipendelea  kupata watoto wa kiume zaidi, kw imani kuwa wao ndio watakao kuwa Warithi na hivyo pindi mimba ilipopatikana ya mtoto wa kike ilitolewa.

Hivyo, ubaguzi wa jinsia ya watoto, utoaji wa mimba ya mtoto wa kike na sheria ya serikali ya kuzaa watoto wawili pekee ikizidi wa3 ndio imepunguza idadi ya mabinti nchini humo.
Greece

Nchi ya 5 ni ugiriki, ambapo katika nchi hii nako kuna upungufu wa Wanawake ukilinganisha na nchi nyingine, chanzo kikuu cha kushuka idadi ya wanawake wa eneo hilo hutokana na kuhama kwa mabinti wengi kwenda nchi nyingine za ulaya na huko hukaa muda mrefu na kuanzisha familia zao hukohuko.
Tatizo kubwa linalofanya uhamaji huo ni kutokana na kutokuwepo kwa usawa kati ya ujira na nafasi za kazi baina ya wanaume na wanawake na hivyo wanaume pekee ndio huonekana kupewa kipaumbele zaidi kuanzia ngazi ya familia hadi ya taifa.

Idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo sio wazawa huku karibia robo yao ni wahamiaji ambao nao ni wanaume kutoka mataifa mengine, zaidi ya hapo nchi hii ndio njia kuu na kimbilio zaidi kwa wahamiaji wanaotaka kwenda barani ulaya hasa kwa nchi za uingereza na ufaransa.

Nigeria



Nchi ya Nigeria inashikilia nafasi ya6, kwa kuwa na upungufu wa wanawake ukilinganisha na idadi ya wanaume wa nchi hiyo, Wanaume hukadiriwa kufikia (ratio) 1.04 na Wanawake 1.0 Sababu kubwa ya upungufu huo huchagizwa na mabinti wenyewe kutoroka makwao kutokana na kukithiri na kuendelezwa kwa mila za ukeketaji kwa mabinti (FGM), Mabinti kulazimishwa kuolewa wakiwa katika umri mdogo (Forced marriage) Kurithishana wanawake baada ya mume kufariki, na hivyo mabinti wanaofikia rika la kuvunja ungo, hulazimika kutorokea sehemu nyingine ambapo watapata maisha yaliyosalama zaidi kwao, pamoja na machafuko ya waasi (Boko Haramu) na serikali ya nchi hiyo kuwania eneo lenye utajiri wa mafuta.

Mwaka jana serikali ya Nigeria ilitangaza kuwepo kwa upungufu huo endelefu wa mabinti kupatikana kuolewa, na hivyo kuacha idadi kubwa ya vijana wanaotafuta wake wa kuwaoa kubakia mabachela (Ukapera).
Afghanistan


Nchi hii inashikilia nafasi ya 7 kwa upungufu huo wa mabinti kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miongo kadhaa sasa, lakini pia (Sharia) au sheria kali zinazoelemea maadili ya ki-Islam, kwa kutokuwaruhusu mabinti kuwa na sauti mbele ya wanaume.

Matukio ya ubakaji unaofanywa na wanamgambo waliojitenga na serikali (Al- Quaeda) nao umechagiza eneo hili kutokuwa salama zaidi kwa jinsia ya kike na watoto, na hivyo wengi wa mabinti wa nchi hiyo hutorokea nchi jirani kuanzisha familia zao huko huku wanaume wakisalia kupambana vita vyao wenyewe kwa wenyewe.

Sweden



Inashikilia nafasi ya 8, kwa upungufu huo na hiyo hutokana na uhaba wa makazi kuwatosheleza familia nzima na wananchi wote wa Sweden, tatizo hilo pia limechagizwa na ukaribu uliokuwepo kwa nchi marafiki wa nchi hiyo hasa jumuia ya ulaya kuwa ndio kimbilio la mabinti wa nchi hiyo wanaosifika kuwa na urembo mkubwa.

Karibu kiasi cha watu takribani 35,000 ambao ni wakimbizi kutoka mataifa yanayokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe (war-torn countries) huishi nchini humo na hivyo kupelekea mchangamano wa wazawa na wageni kuzalisha upungufu mpya wa mabinti kuolewa na wenyeji.
Egypt


Misri ikiwa ndio nchi inayoongoza barani Afrika kwa kuwa na wingi wa watu na ikishika nafasi ya nne kwa Duniani, lakini nayo inashikilia nafasi ya9, kwa uhaba wa mabinti ukilinganisha na idadi ya Vijana (kiume) wote katika nchi.


Wastani uliopungufu kwa sasa unakadiriwa kuwa kati ya (1-ratio) wa Wanawake, huku idadi ya wanaume ikiwazidi kwa (1.7-ratio) kiasi ambacho kinapelekea kutokuwa na usawa kwa idadi ya jinsia zote mbili.
Chanzo kikuu cha upungufu huo wa mabinti ni pamoja na, jinsia hiyo kuwa bize zaidi na kazi mbalimbali maofisini kiasi kwamba hujikuta wamepitiliza muda wao wa kuwa na familia stahiki, lakini pia kama hutambui mabinti wengi wa misri ndio wasomi wenye shahada za juu kabisa kuhusu maswala ya sheria, madawa na sheria hivyo hujikuta wakihama au kuhamishwa kwa wingi zaidi kwenda kuhudumu katika vitengo hivyo kwa nchi nyingine zilizoendelea kama Ulaya na Uarabuni.
“A large portion of female Egyptians have advanced degrees and aspire to work in the fields of science, medicine, and law, As a result, a lot of them have been immigrating to more progressive countries, This has left a lot of Egyptian guys with lonely heat”

Libya

Libya inashikilia nafasi ya10 duniani kwa upungufu huo wa mabinti wenye rika la kuolewa ukilinganisha na idadi na mahitajio ya wanaume wa nchi hiyo waliowazidi kwa wastani (ratio) wa0.7; yaani sawa na kusema kila mwanamke mmoja anatakiwa awe na wanaume5 ili kuleta uwiano huo sawa.


Nchi ya Libya imeingia katika nafasi hii kutokana na mapambano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoendelea kwa muda mrefu tokea enzi za Rais Ghaddaf hadi kifo chake, na hivyo wanaume wengi wa nchi hiyo huchukuliwa kama wapambanaji na wengi miongoni mwao walifia vitani, hivyo kupelekea uchache wao na kuwa na idadi kubwa ya wanawake walio wapweke ukilinganisha na idadi ya wanaume.
Iceland


Kisiwa hiki kinashikilia nafasi ya11 Duniani kwa kuwa na upungufu wa kupatikana kwa mabinti wa kuweza kuolewa.


Unapofikiria kuhusu nchi ya Iceland, jambo moja kubwa huja kwenye mawazo yako kwamba ni nchi iliyozungukwa au kutawaliwa na barafu (baridi) katika muda wote wa mwaka (ingawa sivyo), lakini pia ukweli uliopo kwa sasa ni nchi mojawapo yenye idadi kubwa ya wanume ukilinganisha na wanawake waliopo, utofauti wa kiasi cha (1.7%) na hivyo kuwafanya vijana kuwa wapweke wakikosa mabinti wa kuoa, na kulazimika kutoka nje ya nchi yao kutafuta wachumba.
Kuliwahi kuwa na uvumi na tetesi kuwa, serikali ya nchi hiyo ilitoa ofa kwa mabinti wa nchi nyingine waliotayari kuolewa na wanaume wa nchi hiyo kiasi cha dola za kiMarekani ($5,000) kwa usiri mkubwa, ingawa Habari hizo ziliposambaa serekali ya nchi hiyo ikajitokeza na kukanusha vikali tetesi hizo na kusema sio za kweli. (Sawaa, kazi kwenu mabinti wa kitanzania, unaweza kuchangamkia fursa hizi – Hahaha, natania..)

Philippines


Ufilipino ikiwa ni nchi iliyo maskini zaidi kwa nchi za ukanda wa nchi za bahari ya Pasific, inashikilia nafasi ya12 kwa kuwa na Uhaba huo wa wanawake wakuweza kuolewa, kutokana na kuwa
Mabinti wa kiFilipino huihama nchi yao kwa minajili ya kutafuta kazi nje ya nchi yao haswaa maeneo ya Australia, Asia na hadi kwenye nchi za Mashariki ya kati.
Matokeo yake sasa, kuondoka kwao huko hupelekea upungufu wa karibu wastani unaofikia  (1.02% to 1) na kw takwimu za hivi karibuni zinaonyesha idadi ya wenzi kufunga ndoa imekuwa kipungua siku baada ya siku, na kuweka ukweli juu ya upungufu huu kuwa idadi ya wanawake imepungua.

SOURCE: Difficulties2GetWife