Jumatano, 14 Oktoba 2026

KUMBUKIZI: Miaka 27, Mwl Julius K. Nyerere – MATUKIO MUHIMU TANZANIA



Leo Tunaadhimisha kumbukizi ya miaka 27 tangu Rais wa kwanza wa Tanzania na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotutoka tarehe (14 Oktoba 1999) akiwa Hospitali ya St. Thomas, Jijini London, Uingereza.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI:

Mwalimu: JK. Nyerere, Alizaliwa: 13 Aprili 1922, Butiama, mkoani Mara, yalipojengwa makumbusho yake kwasasa, ambapo Elimu: alihitiku katika chuo kikuu cha Makerere University Uganda, kisha University of Edinburgh Scotland akichukua (Shahada ya Uzamili).

Siasa: Katika harakati za siasa, Mwalimu Nyerere Alianzisha TANU mwaka, 1954 na kuiongoza Tanganyika kupata Uhuru wake mnamo tarehe 9 Dec 1961, chini ya mkataba uliokuwa wa uangalizi wa nchi ya Uingereza na bila ya kumwaga damu.

Muungano:

Ilipotimu mwaka 1964, April 06" Rais nyerere na Rais wa Zanzibar A.A Karume" aliunganisha Tanganyika na Zanzibar na kisha kuzaliwa taifa moja (Tanzania) tokea hapo ule mshikamano kama taifa, siasa ya ujamaa na kujitegemea vilichukua hatamu, na maendeleo yakaanza kuonekana katika wigo wa Elimu, kilimo kwa chakula na biashara.

Wakati huo taifa likipambana na adui mkubwa "Umasikini, Maradhi na Ujinga'".

Miaka2 baadae: Mwaka 1967 Jijini Arusha, ndipo lilipozaliwa  'Azimio la Arusha', likiwa na falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambapo Rais, mwalimu Nyerere alikua mstari wa mbele kupambana na maadui hao wa3 wa taifa.

UKOMO WA UONGOZI:

Mwaka 1985 Rais. Nyerere aliamua kustaafu kabisa na kwa hiari yake kujihusisha na siasa, hapo ndipo alimkabidhi Ali Hassan Mwinyi hatamu ya uongozi akichaguliwa kuwa Rais wa pili wa Tanzania (1985-1995) akafuatia H. Rais, Benjamini W. Mkapa (1995-2005) Rais wa3 wa Tanzania.

Ndani ya awamu hii ya3 ya uongozi wa Rais Mkapa: Taifa lilipata Pengo na simanzi kubwa ambayo huwenda pengine hadi wa hivi leo 'pengo lake bado halijazibika'

Ilikuwa,"Siku ya Alhamisi,

Tarehe14, mwezi10 , mwaka1999 kutokea (st. Thomas) -nchini Uingereza Mwalimu Nyerere alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya moyo, ndipo taarifa ilipolifikia taifa kuwa Rais wa kwanza, Mwalimu na Baba wa taifa "hatunaye tena" yaani ameiaga Dunia.

Nyimbo za maombolezo ziliimbwa, taifa likiomboleza, rambirambi kutoka kwingi duniani zilitumwa: Kuonyesha hakika H. Mwl Nyerere alikua kipenzi cha Dunia, Mkombozi wa Afrika na mfano mwema wa kuiga kwa Kila kiongozi anayewajali watu wake, maendeleo na kuweka mbele uzalendo wa taifa kwanza.

Mengine: Mwalimu ataendelea kukumbukwa kwa uadilifu, Elimu kwa wote, Kiswahili kutumika na kutambulikana rasi kuwa ni ligha rasmi ya taifa, na mshikamano wa Afrika, na Tanzania, nk.  Mpaka leo hii tukiadhimisha mika27, kumbukizi yake: Baba wa Taifa: Tunajifunza:

"Elimu si namna ya kupata cheti tu pekee, bali ni hali ya kujifunza namna ya kuiishi Elimu hiyo, na kuitumia kuleta maendeleo chanya kwa taifa na mtu binafsi."

 


MATUKIO MAKUBWA MUHIMU YA KUKUMBUKWA TANZANIA TOKA MWAKA 2000

Tokea Mwalimu, na Rais Nyerere (Late) ametutoka, Tanzania imepitia matukio mengi makubwa tangu kuingia kwa Milenia mpya mwaka 2000, hadi 2026: Na haya hapa ni miongoni mwa matukio hayo muhimu na yenye kukumbukwa zaidi:

MWAKA 2000:

Chini ya Rais wa awamu ya tatu. Late-Benjamin W. Mkapa: EAC 9east Africa Community ilifufuka tokea kuvunjika mwaka 1977) na kufurahisha zaidi yeye ndiye alichaguliwa kwa muhula wa pili (kwa 72% ya kura) kuiongoza jumuiya hii ya Muungano wa nchi za Afrika ya mashariki.

JANUARI 2001: Dosari Uchaguzi Zanzibar:

Ni mwaka huu wa 2001, katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar “Waandamanaji wa CUF walijitokeza kwa maandamano yenye vurugu kupinga matokeo ya jumla ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka-2000, ambapo mapambano yaliibuka kati ya waandamanaji na polisi, na hiyo ikapelekea vifo ya watu zaidi ya20, Pemba na Unguja’ ni Tukio hili lilitikisa demokrasia ya Tanzania kama nchi ya Amani na Zanzibar kwa ujumla.

JUNI 24, 2002: Ajali Ya Treni Igandu - Dodoma

Ni tukio baya zaidi la usafiri. Treni ya abiria kutoka Dar kwenda Dodoma ilishindwa kupanda mlima Igandu na kurudi nyuma kwa kasi na kugongana na treni ya mizigo, ambapo ilipelekea Zaidi ya watu makumi kufa katika ajali hiyo, na Taifa likaomboleza.

14 Disemba 2005:

Tanzania ilifanya uchaguzi wake mkuu, Uchaguzi ambao uliwezesha kumpata Rais wa awamu ya 4 (Jakaya Mrisho Kikwete) ambaye  alishinda kwa kishindo (80.28% ya kura zote zilizopigwa) akija na kauli mbiu iliyosema "Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya".

Februari 2008:

Kuliibuka Sakata la kampuni hewa ya umeme (Richmond) iliyolipwa mabilioni ya pesa bila kuzalisha umeme; Ambapo ripoti ya Bunge ilimtaja Waziri Mkuu wakati huo (Mh. Edward Lowassa) na kupelekea yeye na mawaziri 2 kujiuzulu nafasi zao, kisha Rais, Jk. akavunja Baraza lote la Mawaziri.

Oktoba 2015:

Ilitamatisha awamu ya4 ya Urais wa Tanzania, kwa taifa kushuhudia Rais mwingine wa awamu ya5 (L. JP. Magufuli) Kushinda uchaguzi huo mkuu kwa (58%) dhidi ya mpinzani wake aliyetoka CCM na kuhamia CHADEMA” H. Edward Lowassa, aliyechuana naye vikali na kukaribiana kwa kura zilizopigwa kwa asilimia chache kupishana. Akija na kauli mbiu iliyosema “Hapa Kazi Tu” na mengi yalitokea ikiwemo, mafisadi kukalia kuti kavu.

MACHI 17, 2021:

Simanzi kwa Taifa: Ni Mwaka huu - Rais John Magufuli alifariki ghafla kwa matatizo ya moyo, na Siku 2 baadaye, aliyekuwa Makamu wake (Mh. Samia Suluhu Hassan) aliapishwa kuwa Rais wa6, na taifa likaandikisha historia mpya ya kumpata Rais wa kwanza (Mwanamke) katika historia ya Tanzania tokea enzi na enzi.

2022-2024: ENZI YA MIRADI MIKUBWA

SGR: Treni ya kisasa ya umeme Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma - Mwanza yaanza.

Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP): Bwawa kubwa zaidi Afrika Mashariki lenye kuzalisha MegaWatts-2115, likikamilika kwenye viunga vya Mto Rufiji.

Daraja la Kigongo - Busisi: Daraja refu zaidi Afrika Mashariki (Lenye urefu wa: 3.2km) ndani ya Ziwa Victoria lilikamilishwa.

Matukio Mengine Ingia hapa: Facebook

Jumatano, 7 Oktoba 2026

HEKIMA YA NDOA: SIRI YA MWANAMKE / MKE KULINDA KINYWA CHAKE!

 


#Na Stewart Meena

Ukichunguza Mwanamke 'Mke' akifundishwa kulinda kinywa chake ndani ya ndoa: NDOA inakua ni sehemu ya UPENDO na AMANI pamoja na kuwa salama sana ya kuishi, kinyume chake itakuwa uwanja wa mapambano!"

Hii ni hekima ambayo wazee wetu wamekuwa wakiifundisha kwa vizazi na vizazi. Katika dunia ya leo ambapo kila mtu anataka kuongea na kusikilizwa, wanawake wengi wamesahau nguvu iliyopo katika kunyamaza.

Kinywa Ndicho Kinachojenga Au Kubomoa Ndoa

  • Biblia inasema, "Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe." Kubomoa huku mara nyingi hakutokei kwa mapanga, bali kwa maneno.
  • Maneno makali, lawama za kila siku, kulinganisha mume wako na wanaume wengine, na kumjibu mume mbele za watoto au wageni - hivi vyote vinaua heshima na upendo taratibu.

Kulinda Kinywa Si Unyonge, Ni Hekima

  • Watu wengi hudhani mwanamke akilinda kinywa chake ni mnyonge au hana msimamo. La! Hasi!
  • Kulinda kinywa ni: Kujua Lini Kuongea: Kuna muda wa kuzungumza na muda wa kunyamaza. Mume akiwa na hasira, huo si wakati wa kujibizana.
  • Kujua JINSI ya Kuongea: Sio kila ukweli unasemwa kwa ukali. Ukweli unaweza kusemwa kwa upendo.
  • Kutunza Siri za Ndoa: Nini kinaendelea chumbani mwenu kisitoke nje. Rafiki yako si baraza la ndoa.
  • Mwanamke anayejua haya, mumewe humuona kama malkia na mahali pa kupata amani baada ya shida za nje.

Matokeo yake: Ndoa Inakuwa Peponi Duniani

Mwanamke anapolinda kinywa chake:

  • Nyumba inakuwa na (UPENDO) - kwa sababu hakuna maneno yanayochoma moyo kila siku.
  • Nyumba inakuwa na (AMANI) - watoto wanakua katika mazingira ya utulivu, si kelele za ugomvi.
  • Nyumba inakuwa (SALAMA) - mume harudi nyumbani kama anarudi vitani, bali anarudi kupumzika.

Kinyume chake?

Mwanamke asiyelinda kinywa chake, nyumba inageuka kuwa (UWANJA WA MAPAMBANO). Kila siku ni vita, kila neno ni risasi. Mwanaume huanza kupendelea kuwa nje kuliko ndani, na hatimaye ndoa hufa kifo cha taratibu.

ZINGATIA: 

Dada zangu, ukitaka ndoa yako idumu, anza leo, na ujfunze kusikiliza zaidi kuliko kuongea" kwenye kusikiliza kuna hekima ndani yake.

Pia: Jifunze kusema "asante" "samahani" na "nakupenda". Maneno haya matatu yana nguvu kuliko kelele, unazoshindania kuonyesha nafasi yako kama mke au mama wa familia.

Siri ya ndoa imara kwa wanandoa haipo kwenye pesa nyingi, ipo kwenye kutambua nafasi ya kila mmoja, kujali na kuthaminiana zaidi ya unavyoweza kujithamini mwenyewe.

Je, Unakubaliana na Hii? Tuandikie Maoni Yako Hapo Chini!

#SirMeena (Facebook: #HistoryAndAmazingThings #Special4fans)

#HekimaYaNdoa #Mapenzi

#MEENA NEWS BLOG

Facebook: http://www.facebook.com/stewart.meena

WhatsApp: 0778 291 375

Jumapili, 27 Septemba 2026

MZALIA CHINI: MAAJABU YAKE KATIKA KUTIBU FIGO NA INI

CHANCA PIEDRA - (Phyllanthus niruri)



Na. #Stewart Meena

Ukiwa na asili ya Misitu ya Amazon (South of America) kutoka mataifa ya Brazil, Colombia, na Peru “Chanca Piedra” Kwa Kiswahili ukiitwa “Mvunja Mawe’; Jina lililotoholewa kutoka lugha ya Kihispania, na likiwa na maana hiyohiyo "Mvunja Mawe".

Pengine mmea huu ni Baraka tuliyobarikiwa na mazingira asilia (Nature) yanayotuzunguka, ambapo kimsingi sio wote tunaoifahamu lulu iliyopo kwenye matumizi ya mmea huu.

Mmea huu kwa sasa umesambaa karibu ulimwenguni kote haswa kwenye maeneo yenye joto la kitropiki (Tropical) na maeneo yenye jua kali majira ya mchana na baridi nyakati za usiku, hivyo sio nadra kuuona upo na unapatikana kwa wingi maeneo yaliyokuzunguka.

Maeneo unakopatikana kwa Tanzania ni kama mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Iringa, Dodoma, Rukwa, Kigoma, Mwanza, Mara, Geita na kwingineko barani Afrika na afrika mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Burundi nk.

Kwa lugha ya kibantu unaitwa ‘Mwana mwani’ na kwa ‘Wasambaa wa Lushoto, Tanga’ wanauita: ‘Mshasha / Kishanamiti au Mwana wa ngongo’ kutokana na namna unavyozalia matunda yake kwa chini ya majani yake.

Unawezaje Kuutambua?

Ni mmea mdogo usio refuka zaidi ya cm30-50, una Majani madogo madogo kama ya mshita na chini ya kila jani kuna mbegu ndogo ndogo, ambazo hizo ndio utambulisho wake na alama yake kubwa, huku ukiota kwa wingi kandokando ya barabara, maeneo ya nyumba maji yanapotiririka na mashambani sehemu zisizokuwa na kivuli kwa kuwa unapendelea zaidi kupata mwanga wa jua wa moja kwa moja.

 


HIZI HAPA FAIDA ZAKE KUBWA: Katika tiba asilia;

  1. Husaidia kuondoa Mawe ya Figo na Kibofu (Kidney Stones)
  2. Hii ndio kazi yake iliyo kubwa, Unasemekana kusaidia kuyeyusha na kutoa mawe ya figo na kuzuia yasitengenezwe tena, ndio maana unaitwa Mvunja Mawe.
  3. Huondoa sumu kwenye Ini na Homa ya Ini (Hepatitis), Husafisha ini, pia husaidia kupambana na homa ya ini (aina B) lakini pia huondoa mafuta yaliyozunguka na kuleta madharakwenye ini.
  4. Husaidia kupambana na Kisukari: Ambapo chai ya mmea huu baadhi ya tafiti zilionyesha unauwezo pia kwa kushusha sukari kidogo kwa wenye kisukari aina ya 2.
  5. Vidonda vya Tumbo na Presha: Husaidia kupunguza acid tumboni na wengine hutumia kwa presha na malaria
  6. UTI na kibofu ‘Mkojo’ Kuungua au kuwaka moto: Ikiwa ukienda haja ndogo unasikia maumivu kama ya kuungua ‘kuwaka moto’ kwa ndani haja inapotokea basi, mmea huu tafiti hueleza unasafisha njia hiyo vizuri, na pia kuponya walewenye UTI inayojirudia.

KUMB: UTI haiambukizwi kwa njia ya kujamiana (Mwanaume na mwanamke), huambukizwa kwa bacteria wanaozaliana kwa kuvaa nguo za unyevunyevu na zisizokauka, kukaa na haja ndogo muda mrefu, pia huzaliwa kwa kujisaidia mazingira ya uchafu haswa wenye vimelea vya haja kubwa au kwa kushiriki mapenzi kinyume na maumbile HIVYO: ‘Unashauriwa kusaficha vyoo vizuri, kumwaga maji mengi kabla ya kutumia na pia kuepuka


JINSI YA KUTUMIA (Kwa Elimu Tu)

Watu wengi hukaushia majani na shina kivulini, kisha hupika chai - kijiko kimoja cha majani makavu kwenye kikombe kimoja cha maji moto. (Kunywa mara 1-2 kwa siku)

Tahadhari: Usitumie ukiwa mjamzito, unanyonyesha, au una sukari ya chini sana. Kama una mawe makubwa ya figo, nenda hospitali kwanza, usicheze na figo. Mmea huu ni msaada tu, sio mbadala wa daktari.

 English Version:



Here is a simple guide for *Chanca Piedra (Phyllanthus niruri) - The Stone Breaker* as used in traditional herbal medicine.

This is for educational purposes only. Talk to a healthcare professional before use, especially if you have kidney stones, liver disease, or diabetes.

What Part to Use

The whole aerial part - leaves, stems, and small seed pods under the leaves. The roots are also used but leaves are most common.

How to Prepare It

A) Tea / Infusion (Most Common Method

Harvest fresh plant, wash well.

  • Dry it in shade for 3-5 days to keep its power. Don't dry in direct sun.
  • Crush the dried leaves into small pieces.
  • General traditional method: 1 tablespoon of dried herb in 2 cups of hot water. Steep for 10-15 minutes, then strain.
  • People traditionally drink it warm, 1 cup in the morning and 1 in the evening for a few days.

B) Fresh Juice

  • Take a handful of fresh, clean leaves and stems.
  • Pound or blend with a little water, then squeeze and filter the juice.
  • Traditionally a small amount is diluted with water.

C) Powder

  • After drying completely, grind into fine powder. It can be stored in a clean glass jar for months.
  • Traditionally 1/2 teaspoon mixed with warm water.

Traditional Uses

For Kidney Stones & UTI: The tea is taken for 1-2 weeks to help flush the urinary tract. It is believed to help relax the ureter and prevent calcium oxalate stones from forming.

For Liver Support: Taken as a light tea for a few days to help cleanse the liver.

For Digestion: Used in small amounts after meals.

 

Important Safety Warnings

DO NOT use* if pregnant, breastfeeding, or trying to conceive - it may cause issues, as It can lower blood sugar and blood pressure, so if you are on diabetes or pressure medicine, be very careful.

It increases urination, so drink plenty of water, and If you have large kidney stones, severe pain, blood in urine, or fever - *go to hospital immediately.

Lastly: This herb does not replace surgery or hospital treatment; and when consuming don't use it for more than 2-3 weeks continuously without a break.

Jumatatu, 21 Septemba 2026

FAHAMU MMEA WA KONGWA / JONGWA 'Commelina benghalensis' NA FAIDA ZAKE 10 KWA AFYA YAKO!


 

Watu wengi huweza kuuchukulia kama magugu-shamba tu na mimea sumbufu inayotambaa kumbe ni lulu kwenye baadhi ya tamaduni mbalimbali afrika, Asia, Ulaya na Amerika.

Na.

Stewart Meena.

Ni mmea wa porini unaoota sana Tanzania hasa mashambani, kando ya mito na sehemu zenye unyevunyevu, ambapo watu wengi huuona kama majani yanayotambaa na yaliyo masumbufu kwa rutuba ya mazao mengine katika shamba au bustani, kama ilivyo tu kwa mimea ya magugu kwani huota kwa kusambaa kama ilivyo kwa ukoka.

Mmea huu una majina mengi, ikilinganishwa na unakopatikana kwani una asili ya bara Asia, Afrika na ulaya na Amerika kusini, ambapo majina hayo ni kama vile: (Wandering Jew, Tropical Spiderwort, Matangawizi pori, Ndele, Kongwa na kule uchagani wakiuuta: ‘Ishongwe’ au ‘Iriria’ ) kitaalamu ukiitwa: Commelina benghalensis.

Je! Unawezaje kuutambua: Utambulisho Wake ‘Kama ilivyo pichani’ ina Shina laini, lenye maji au utomvu mweupe usio na rangi ya maziwa kama mimea ningine kwa ndani, ambapo huota kwa wingi kama ukoka na ikiwa kwakutambaa chini.

Majani yake ni ya kijani iliyopauka, umbo la yai nan cha katikati kwa mbele, huku Maua yake ni madogo ya yenye rangi ya bluu iliyokolea, na huweza kuonekana kwa wepesi zaidi ikiwa imechanua asubuhi tu, ikilinganishwa na mchana. Pia Huzaa juu na hata chini ya ardhi.

Image: Mr. Meena

Katika tiba asilia mmea huu una maajabu yake: na umekuwa ukitumika kwa miongo mingi kwenye baadhi ya tamaduni na kuleta matokeo katika tiba asilia ya mimea (Natural Herbs) ambazo nitakwenda kuziangazia hapa chini;

Sehemu Zinazotumika kama Dawa:

Majani, shina changa na mizizi yake; Ambapo mara nyingi hupondwa maji yake yakitoka au hukaushwa kivulini ‘usitumie yakiwa mabichi’

Matumizi Yake Kwenye Dawa Za Asili:

Haya ni matumizi yanayojulikana kwa tiba asili, kulingana na tafiti zilizofanyika kwenye baadhi ya tamaduni (Afrika na Asia) na tafiti hizo ni kwa tiba za mimea asilia pekee na sio kwa kwa utabibu mahospitalini au kwa ushauri wa daktari. (Zingatia: Kama una ugonjwa sugu muone mtaalamu wa afya).

Vidonda na Michubuko: Majani yake freshi hupondwa na kuwekwa kwenye kidonda. Unasemekana kusaidia kukausha kidonda haraka na kuzuia usaha kwa sababu una uwezo wa kupambana na bakteria.

Kuvimba na Maumivu ya viungo: Majani hupashwa moto kidogo kisha hubandikwa sehemu inayovimba. Wazee husema hupunguza maumivu.

Macho kuwasha na macho mekundu: Kwa baadhi ya jamii, maji ya majani yake yaliyochemshwa na kuchujwa vizuri hutumika kuosha macho” Hii inahitaji usafi mkubwa sana, usijaribu bila ushauri wa mtaalamu au mtabibu aliyewahi kujaribu kuyatumia.

Homa na Mafua: Chai ya majani yake hupikwa na kunywa kwa ajili ya kupunguza joto na kikohozi.

Matatizo ya njia ya haja ndogo ‘Mkojo’ na Figo: Mizizi yake kwa tiba ya Kihindi (Ayurveda) hutumika kutengeneza dawa ya kusafisha njia ya mkojo.


NB: Sehemu zingine kwa baadhi ya makabila hapa Tanzania, majani yake hupikwa na kutumiwa kama mboga ya kulia ugali kama ilivyo tu kwa ‘mchicha pori’ ikielezwa pia ni chanzo kikubwa cha vitamin mwilini.

JINSI INAVYOANDALIWA

Chukua majani yake freshi, kisha yaoshwe vizuri kwa maji safi, kisha yapondeponde hadi upate uji laini, kisha tumia kuyagandisha kwa nje au juu ya kidonda na ulipopata majeraha.

Au pia waweza kuyachemsha baada ya kuyachuma na kuyaosha kwa maji safi, kisha yakamue kwa chujio au kitambaa safi kisicho na nyuzinyuzi ili kupata juisi au ‘maji yake’ na tumia kama chai kutwa mara mbili.

TAHADHARI MUHIMU: Usitumie kwa kunywa ikiwa mabichi na hujayachemsha kwani huweza kukuletea ‘mzio’ (allergy) na usiyameze majani yake kwa usalama wa tumbo.

Pia: Kwa Wanawake wajawazito na watoto wadogo hawashauriwi kuitumia bila ushauri wa mganga au mtabibu wa dawa asili, Na kama kidonda ni kikubwa au kimevimba sana, nenda hospitali kwanza.

ASANTE KWA KUTUFUATILIA HADI MWISHO: Endelea kutembelea page hii ili kusoma pia Makala nyinginezo kwa ujuzi na maarifa zaidi. “Tuachie maoni yako, sehemu ya comment hapo chini’

Alhamisi, 17 Septemba 2026

UCHAWI, UHUSIANO - ELIMU KUHUSU VIUMBE WASIOONEKANA!



Elimu kuhusu uchawi na majini ni mada pana inayochukua nafasi kubwa katika imani za kijamii, kitamaduni, na kidini (hususan katika dini kuu zilizopo (Mfano: Ile ya Kiislamu na Kikristo), katika mabara yote saba katika sayari hii ya tatu (Dunia) katika mzunguko wa sayari zote kulizunguka jua.

Afrika na zaidi ikiwemo Afrika Mashariki, Pengine uchawi na elimu kuhusu viumbe wasionekana kwa macho ya kibinadamu (Majini) hutumika tofauti sana na ustaarabu wa maeneo mengine duniani, mfano barani Ulaya, America, na Asia – hutumia elimu hii kwa maswala ya utajiri na mali, teknolojia na maswala ya ki-injinia nk. Tofauti na Afrika hutumika kulogana na kutiana uchizi, kuchuma kwa kuiba mali za wengine (Chuma ulete nk.)

Uchawi kwa bara letu la Afrika, huhusishwa na kuwanga ‘Yaani kuzunguka katika majumba ya watu usiku  na kuwatia zongo nanuksi kwa kuwanenea maneno ya kichawi, na kwa mila na Imani zao yale waliyoyanenea hutukia kwa walengwa waliowakusudia.

MAJINI:

(Mitazamo Ya Kidini Na Kijamii (Ukristo na Uislamu)

By Nancystodd - Icon-religion.svg-Wikipedia


UISLAMU: Kuhusu Majini (Majinn)

Katika mafundisho ya kidini (hasa ile ya Kiislamu), majini ni viumbe halisi walioumbwa na Allah; Ikiwa ni tofauti na binadamu walioumbwa kwa asili ya UDONGO (Adamu na Hawa) na Malaika walioumbwa kwa NURU, Majini waliumbwa kwa MOTO usio na moshi (moto wa upepo mkali).

UKRISTO: Kuhusu Majini (Mapepo/Demons)

'bofya kiungo kwenyemaneno yaliyopigiwa mstari'

Katika mafundisho ya uKristo, yamejikita zaidi kuelezea namna binadamu wa kwanza alivyoumbwa, kisha baadae mwanamke (Adam na Eva), na baadhi ya vitabu kama (Kitabu cha HENOKO ‘Enoch’) Kikiwa kimechambua kuhusu uchawi, majini nk. Kikiondolewa na kutotumika kabisa kwa madhehebu yaliyo mengi ndani ya ukristo, Zaidi kikibakia kutumiwa na Kanisa na ambalo pekee linalokitambua kitabu hicho kama sehemu ya maandiko yao matakatifu ni Kanisa la Kiorthodoksi la Tewahedo la nchini Ethiopia.

Kitabu cha Henoko (kwa Kiingereza: The Book of Enoch) ni mkusanyo wa maandishi ya kale ya kidini ya Kiyahudi yanayonasibishwa na Henoko, babu mkuu wa Nuhu; Ingawa kilitungwa kati ya karne ya 3 na ya 2 K.K, kitabu hiki hakimo katika kanoni rasmi ya Biblia inayotumiwa na Wayahudi na madhehebu mengi ya Kikristo Duniani.



SIFA ZA MAJINI:

Uhuru wa Kuchagua: Imeelezwa kwenye uislamu, kama walivyo wanadamu, majini wana uhuru wa kuchagua kuwa wema (waumini) au wabaya (makafiri); ambapo Jini mbaya au kafiri mara nyingi huitwa Shaytani (Shetani) au Ibilisi.

Maisha Yao: Imeelezwa (Kwenye simulizi za Imam-Shafii) kuwa: wanaishi, wanakula, wanazaa, wanasafiri, na wanakufa kama ilivyo kwa wanadamu, na upekee mkubwa walionao ni kuwa wao wanauwezo wa kutuona wanadamu, lakini wanadamu/binadamu hawezi kuwaona katika umbo lao la asili.

AINA ZA MAJINI NA MAKAZI:

Kwa mujibu wa maandiko mbalimbali, wamegawanyika katika makundi makuu matatu: Wenye mbawa na wanaoruka angani; Wanaotambaa au kuchukua maumbo ya wanyama (kama nyoka Paka au hata mbwa weusi) na wengine: ni wale wanaoishi maeneo maalum na kutembea kama binadamu.

MAKAZI YAO: Wanapendelea kuishi maeneo yaliyotengwa kama vile mapango, bahari, majalala, nyika, na nyumba zilizoachwa tupu kwa muda mrefu ‘maghofu’.

JINSI JINI ANAVYOWEZA KUMDHURU AU KUINGIA KWENYE MWILI WA BINADAMU:

Wanachuoni wengi wanakubali kuwa jini anaweza kuingia au kuathiri mwili wa binadamu kutokana na sababu kadhaa:

Kisasi: Binadamu anapomdhuru jini bila kujua (mfano: kumwaga maji ya moto pasipo kutaja jina la Mungu).

Mapenzi: Jini wa kiume kumpenda mwanamke wa kibinadamu (au jini mwanamke kumpenda mwanamume), maarufu kama Jini Mahaba.

Kutumiwa kupitia Uchawi: Jini anapotumwa na mchawi kwenda kufanya uharibifu, au kumdhuru mtu aliyelengwa ‘kunuwiwa’ katika uchuwi huo.

Hali za Ghafla: Jini anaweza kuingia mtu anapokuwa na hofu kubwa iliyopitiliza, hasira kali sana, au kughafilika kiimani, Lakini wengine huenda mbali zaidi na kusema haswa kwa WANAWAKE ‘wakiwa wachafu kama wanamilikiwa na viumbe hawa basi watawapanda kwa kuwa hawapendi seemu iliyo chafu. (Dhahiri: Kwenye baadhi ya shule za mabinti pekee, sio nadra kusikia Fulani kapandisha ‘mapepo’)

 


ELIMU KUHUSU UCHAWI

Uchawi ni vitendo vinavyofanywa na binadamu kwa kushirikisha nguvu za giza (Kutumika kwa majini wabaya au mashetani kama nlivyoeleza hapo juu) ili kubadilisha uhalisia wa mambo au kusababisha madhara kwa mtu mwingine.

KIJAMII: Aina za Uchawi Zinazozungumzwa ni zile za, Kurithishwa / Asili, Kununua, na kwa kujifunza, ambapo “Kiasili – Siri za uchawi zinarithiwa ndani ya familia au ukoo tangu utotoni kizazi na kizazi ‘generation to generation’.

·       Uchawi wa Kujifunza: Mtu anapoenda kwa waganga au wachawi wakubwa ili kufundishwa mbinu na miiko ya uchawi.

·       Uchawi wa Kutupiwa (Vifungo na Magonjwa): Kutumia majini au madawa ya kigiza kumfunga mtu kimaisha, kumfanya mgonjwa, au kuharibu ndoa na biashara yake.

Dalili Zinazohusishwa na Uchawi au Kusumbuliwa na Majini:

Kulingana na matatibu wa tiba asilia na za kidini, mtu aliyeathiriwa na uchawi au majini wabaya anaweza kuonyesha dalili mbalimbali kama vile:

·       Maumivu ya mwili yasiyoonekana kwenye vipimo vya hospitali (kama kifua kubana au moyo kwenda mbio).

·       Kuota ndoto za kutisha mara kwa mara (kama kufukuzwa na wanyama wakali, kuanguka kutoka sehemu ndefu, au kufanya tendo la ndoa ndotoni).

·       Kuchukia ghafla mambo ya ibada au kuhisi uzito mkubwa unapotaka kusali au kusoma vitabu vitakatifu.

·       Mabadiliko ya tabia ya ghafla, mfano: mke kumchukia mume au mume kumchukia mke bila sababu ya msingi.

·       Kuhisi ganzi, joto kali, au baridi isiyo ya kawaida kwenye viungo vya mwili.

 


KINGA NA TIBA DHIDI YA UCHAWI NA MAJINI

Katika mifumo yote ya imani, suluhisho kubwa la kujikinga na nguvu hizi hutegemea kumkaribia Mwenyezi Mungu na kufanya ibada ‘Dua’ kwa kumcha yeye pekee, na kwa waKristo (Kufanya Maombi) kwa kuliita na kulitaja jina la YESU inatosha kukuepushia na maswahibu yote hayo.

·       Nguvu ya Jina la Yesu: Wakristo huamini kuwa mapepo (majini wabaya) na nguvu za uchawi hushindwa kupitia maombi ya damu na jina la Yesu Kristo.

·       Kufunga na Kuomba: Kutenga muda wa maombi maalum ya kuvunja vifungo vya kigiza.

·       Kuishi Maisha ya Utakatifu: Kujiepusha na dhambi ili kuzuia shetani kupata mlango wa kuingia kwenye maisha yako.

Mbali na hilo kwa upande mwingine wa UISLAMU tiba imeelezwa ni kufanya (Tiba ya Ruqya), Kusoma Quran: Kutumia aya za Quran na dua zilizofundishwa na Mtume Muhammad (S.A.W), wakitumia Surah maarufu kwa kinga iitwayo (Ayat al-Kursi, Surah Al-Ikhlas, Surah Al-Falaq, na Surah An-Nas)

·       Dua za Asubuhi na Jioni (Adhkar): Kinga kulinda mwili na nyumba dhidi ya mashetani.

Kujiepusha na Ushirikina: Inashauriwa na ni marufuku kwenda kwa waganga wa kienyeji wanaotumia majini kutoa tiba, kwani kufanya hivyo ni kumuasi Mwenyezi Mungu na kuongeza matatizo kwenye maisha ya muhusika atakayefanya shirki ‘Ushirikina’.

Tahadhari ya Kiteknolojia na Kijamii:

Katika ulimwengu wa sasa, kuna kurasa nyingi za mitandao ya kijamii na tovuti zinazodai kufundisha namna ya kuwamiliki au kuwatumia majini kwa ajili ya utajiri, Kununua pete, na vito mbalimbali ili kupata nguvu hizo za kichawi, zaidi sana zinazotumiwa na waganga.

Viongozi wengi wa dini wanaonya vikali dhidi ya kutembelea au kusoma maudhui haya, kwani yanatajwa kuwa ni mitego inayoweza kumuingiza mtu kwenye matatizo makubwa ya kisaikolojia na kiroho, kwa kuamini kile asichokiamini; – Maana imeelezwa kuwa ‘Imani huumba’

EPUKA KUAMINI, NA ISHI KWA KUMTEGEMEA MUNGU PEKEE KATIKA MAJARIBU NA MASWAHIBU UNAYOKUTANA NAYO, MAANA YEYE NDIE MUHUKUMU WA MWISHO, KWENYE MAISHA HAYA NA BAADA YA MAISHA HAYA.

Tufuatilie hapa tafadhali (bofya kiungo chini kwenda facebook Page):

#SirMeena: Waweza kuniandikia maoni yako na tukajadili pamoja....

Je! Kuna uhusiano kati ya Imani hizi na Fremason? Hili nalo ni fumbo jingine! Tuishie hapa kwa Leo. ASANTE!

Alhamisi, 10 Septemba 2026

KIVUMBASI: Mmea asilia wa Maajabu katika Tiba

Image right: Earth Living

Mmmea uonao pichani unaitwa Mvumbashi au "Kivumbasi" kiswahili, Kihehe-lwenyi, ormanyunyukwai (kiMasai) Mzumbasha kwa wasambaa na wambugu (Lushoto Tanga), Wengine huyaita: Luvumbampuku, Kivumbani, Mrumbavasi-Upareni, nk. Lakini kwa lugha ya kisayansi (Scientific name) huitwa Tusli 'holy Basil' ukiwa na asili kutoka bara asia nchini India.

Mmea huu uotao kwa mrudikano wa kama kichaka (shrubs) kwa miaka kadhaa imekuwa ikitumika katika tiba asilia, na wengine wakitumia kama kiungo cha chai kwenye unywaji wao wa kila siku, na umetajwa kuleta maajabu makubwa katika kinga na kutibu maradhi mbalimbali katika mwili wa mwanadamu kwenye mazingira yao ya kila siku.

Tuangazie namna unavyotumika katika Tiba asilia:

Hutumika kama kinga ya kufukuza mmbu na nzi katika mazingira yetu na hivyo kutibu Malaria, lakini pia ukinywa juisi yake huelezwa kutibu degedege, ngiri, pia hukata ulevi kwa wanywaji pombe, pia hutibu maumivu makali ya tumbo (Tumbo la kukata/kunyonga) nk.

Kwa degedege la watoto: Unayaweka kwenye maji unayomuogeshea pekee, wengine humnusishia harufu ya majani haya ya Mumbashi:

Mvumbashi huwa na harufu (scent) flani hivi ambapo huponyesha kwa kuivuta tu, ila wengine huichemsha kwenye chai kama kiungo kwa harufu yake nzuri huongeza ladha ya chai.
Lakini pia ukichemsha yenyewe kwa kuchanganya na vifuatavyo hutibu maradhi kama:
 
1)-Kikohozi kwa watoto/mtu mzima.
Chukua majani yake yatwangwe changanya na maji ya vugu vugu kunywa kwa dozi ya 1*2.

2)-Homa ya Malaria
Majani haya yana antipyretic ambayo inaweza kutuliza homa kabisa na kuponesha malaria, Kama ni mpenzi wa chai chukua majani yake yasage kisha changanya na maji ya moto + asali kunywa kama chai.

3)-Kuhara na magonjwa ya tumbo
Majani hayo yana uwezo wa calming mfumo wa utumbo kwa kiwango kikubwa Sana.

4)-Kushusha sukari ya damu
Majani haya yanakinga ya saratani na cholesterol  na kwa watu wenye kisukari hasa wasiotegemea insulin (NID) majani haya yanauwezo mkubwa wa kushusha sukari na kuilinda pancreas inayozalisha insulin kutoharibika.

5)-Kiungulia cha moyo.
Majani ya Scent yamekuwa yakitumika katika kutibu kabisa tatizo la kiungulia, kikohozi, kuhisi mwili vibaya, maumivu ya hedhi, homa, malaria, shida ya kupumua, ukosaji choo, kukosa hamu ya kula, Kichefuchefu na kuboost moyo tiba hii unaweza iyaanda na kuitumia kwa njia ya kunywa kama chai.

6)-Kuongeza maziwa kwa mjamzito.
Chukua majani hayo zaidi ya 20 yatafune na mboga zingine za majani  yatasisimua mfumo wa utokaji wa maziwa kwa kiwango kikubwa

7)-Hufukuza mbali nzi na umbu, hii ni kwa kuyachoma majani yake, ule moshi wake mbu hulewa na kufa.

8)-Hupunguza nicotine inayopatikana kwenye sigara.
Kila baada ya kutumia sigara unachukua matawi kadha unatafuna ili kupunguza kiwango cha nicotine uliyovuta kwenye sigara.
Majani haya yanauwezo wa kupunguza mawazo Yani msongo wa mawazo, mawe kwenye figo.

9)-Hupunguza maumivu ya tumbo.
Majani haya ni zaidi ya vidonge vya aspirin au Panadol kutokana kuwa majani haya hayana side effects maana ni mimea asili.
Pia ni tiba ya kinywa na macho kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin A.

10)-Tiba ya kuwahi kukojoa na shahawa zisizo na afya ya kuzalisha.

11)-Tiba ya fugus 

Chanzo: 
Dr. William Mtanzania (Usa America) Kwa maoni ya wadau.
TAHADHARI: Matumizi yoyote waone wataalamu wakusaidie, vinginevyo ukiitumia ni kwa hatari yako mwenyewe na sisi hatutahusika kwayo. (It's for your own risk)
🙏 tafadhali like, share pia: comment kama unayafahamu na yanavyotumika ili wengine nao wapate maarifa uliyonayo. (Africa tuna kila kitu basi tu hatujikubali)