#Na Stewart Meena
Ukichunguza Mwanamke 'Mke'
akifundishwa kulinda kinywa chake ndani ya ndoa: NDOA inakua ni sehemu ya
UPENDO na AMANI pamoja na kuwa salama sana ya kuishi, kinyume chake itakuwa
uwanja wa mapambano!"
Hii ni hekima ambayo wazee wetu wamekuwa wakiifundisha kwa vizazi na vizazi. Katika dunia ya leo ambapo kila mtu anataka kuongea na kusikilizwa, wanawake wengi wamesahau nguvu iliyopo katika kunyamaza.
Kinywa Ndicho Kinachojenga Au Kubomoa Ndoa
- Biblia inasema, "Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe." Kubomoa huku mara nyingi hakutokei kwa mapanga, bali kwa maneno.
- Maneno makali, lawama za kila siku, kulinganisha mume wako na wanaume wengine, na kumjibu mume mbele za watoto au wageni - hivi vyote vinaua heshima na upendo taratibu.
Kulinda Kinywa Si Unyonge, Ni Hekima
- Watu wengi hudhani mwanamke akilinda kinywa chake ni mnyonge au hana msimamo. La! Hasi!
- Kulinda kinywa ni: Kujua Lini Kuongea: Kuna muda wa kuzungumza na muda wa kunyamaza. Mume akiwa na hasira, huo si wakati wa kujibizana.
- Kujua JINSI ya Kuongea: Sio kila ukweli unasemwa kwa ukali. Ukweli unaweza kusemwa kwa upendo.
- Kutunza Siri za Ndoa: Nini kinaendelea chumbani mwenu kisitoke nje. Rafiki yako si baraza la ndoa.
- Mwanamke anayejua haya, mumewe humuona kama malkia na mahali pa kupata amani baada ya shida za nje.
Matokeo yake: Ndoa
Inakuwa Peponi Duniani
Mwanamke anapolinda kinywa
chake:
- Nyumba inakuwa na (UPENDO) - kwa sababu hakuna maneno yanayochoma moyo kila siku.
- Nyumba inakuwa na (AMANI) - watoto wanakua katika mazingira ya utulivu, si kelele za ugomvi.
- Nyumba inakuwa (SALAMA) - mume harudi nyumbani kama anarudi vitani, bali anarudi kupumzika.
Kinyume chake?
Mwanamke asiyelinda kinywa
chake, nyumba inageuka kuwa (UWANJA WA MAPAMBANO). Kila siku ni vita, kila neno
ni risasi. Mwanaume huanza kupendelea kuwa nje kuliko ndani, na hatimaye ndoa
hufa kifo cha taratibu.
ZINGATIA:
Dada zangu, ukitaka ndoa
yako idumu, anza leo, na ujfunze kusikiliza zaidi kuliko kuongea" kwenye
kusikiliza kuna hekima ndani yake.
Pia: Jifunze kusema
"asante" "samahani" na "nakupenda". Maneno haya
matatu yana nguvu kuliko kelele, unazoshindania kuonyesha nafasi yako kama mke
au mama wa familia.
Siri ya ndoa imara kwa
wanandoa haipo kwenye pesa nyingi, ipo kwenye kutambua nafasi ya kila mmoja,
kujali na kuthaminiana zaidi ya unavyoweza kujithamini mwenyewe.
Je, Unakubaliana na Hii?
Tuandikie Maoni Yako Hapo Chini!
#SirMeena (Facebook: #HistoryAndAmazingThings #Special4fans)
#HekimaYaNdoa #Mapenzi
#MEENA NEWS BLOG
Facebook: http://www.facebook.com/
