Watu wengi huweza kuuchukulia kama magugu-shamba tu na mimea sumbufu inayotambaa kumbe ni lulu kwenye baadhi ya tamaduni mbalimbali afrika, Asia, Ulaya na Amerika.
Na.
Stewart Meena.
Ni mmea wa porini unaoota sana
Tanzania hasa mashambani, kando ya mito na sehemu zenye unyevunyevu, ambapo watu
wengi huuona kama majani yanayotambaa na yaliyo masumbufu kwa rutuba ya mazao
mengine katika shamba au bustani, kama ilivyo tu kwa mimea ya magugu kwani
huota kwa kusambaa kama ilivyo kwa ukoka.
Mmea huu una majina mengi,
ikilinganishwa na unakopatikana kwani una asili ya bara Asia, Afrika na ulaya
na Amerika kusini, ambapo majina hayo ni kama vile: (Wandering Jew, Tropical
Spiderwort, Matangawizi pori, Ndele, Kongwa na kule uchagani wakiuuta: ‘Ishongwe’
au ‘Iriria’ ) kitaalamu ukiitwa: Commelina benghalensis.
Je! Unawezaje kuutambua: Utambulisho
Wake ‘Kama ilivyo pichani’ ina Shina laini, lenye maji au utomvu mweupe usio na
rangi ya maziwa kama mimea ningine kwa ndani, ambapo huota kwa wingi kama ukoka
na ikiwa kwakutambaa chini.
Majani yake ni ya kijani
iliyopauka, umbo la yai nan cha katikati kwa mbele, huku Maua yake ni madogo ya
yenye rangi ya bluu iliyokolea, na huweza kuonekana kwa wepesi zaidi ikiwa imechanua
asubuhi tu, ikilinganishwa na mchana. Pia Huzaa juu na hata chini ya ardhi.
![]() |
| Image: Mr. Meena |
Katika tiba asilia mmea huu una maajabu yake: na umekuwa ukitumika kwa miongo mingi kwenye baadhi ya tamaduni na kuleta matokeo katika tiba asilia ya mimea (Natural Herbs) ambazo nitakwenda kuziangazia hapa chini;
Sehemu Zinazotumika kama Dawa:
Majani, shina changa na mizizi yake; Ambapo mara nyingi hupondwa maji yake yakitoka au hukaushwa kivulini ‘usitumie yakiwa mabichi’
Matumizi Yake Kwenye Dawa Za Asili:
Haya ni matumizi yanayojulikana kwa tiba asili, kulingana na tafiti zilizofanyika kwenye baadhi ya tamaduni (Afrika na Asia) na tafiti hizo ni kwa tiba za mimea asilia pekee na sio kwa kwa utabibu mahospitalini au kwa ushauri wa daktari. (Zingatia: Kama una ugonjwa sugu muone mtaalamu wa afya).
Vidonda na Michubuko: Majani yake freshi hupondwa na kuwekwa kwenye kidonda. Unasemekana kusaidia kukausha kidonda haraka na kuzuia usaha kwa sababu una uwezo wa kupambana na bakteria.
Kuvimba na Maumivu ya viungo: Majani hupashwa moto kidogo kisha hubandikwa sehemu inayovimba. Wazee husema hupunguza maumivu.
Macho kuwasha na macho mekundu: Kwa baadhi ya jamii, maji ya majani yake yaliyochemshwa na kuchujwa vizuri hutumika kuosha macho” Hii inahitaji usafi mkubwa sana, usijaribu bila ushauri wa mtaalamu au mtabibu aliyewahi kujaribu kuyatumia.
Homa na Mafua: Chai ya majani yake hupikwa na kunywa kwa ajili ya kupunguza joto na kikohozi.
Matatizo ya njia ya haja ndogo ‘Mkojo’ na Figo: Mizizi yake kwa tiba ya Kihindi (Ayurveda) hutumika kutengeneza dawa ya kusafisha njia ya mkojo.
JINSI INAVYOANDALIWA
Chukua majani yake freshi, kisha
yaoshwe vizuri kwa maji safi, kisha yapondeponde hadi upate uji laini, kisha
tumia kuyagandisha kwa nje au juu ya kidonda na ulipopata majeraha.
Au pia waweza kuyachemsha baada
ya kuyachuma na kuyaosha kwa maji safi, kisha yakamue kwa chujio au kitambaa
safi kisicho na nyuzinyuzi ili kupata juisi au ‘maji yake’ na tumia kama chai kutwa
mara mbili.
TAHADHARI MUHIMU: Usitumie kwa
kunywa ikiwa mabichi na hujayachemsha kwani huweza kukuletea ‘mzio’ (allergy) na
usiyameze majani yake kwa usalama wa tumbo.
Pia: Kwa Wanawake wajawazito na
watoto wadogo hawashauriwi kuitumia bila ushauri wa mganga au mtabibu wa dawa
asili, Na kama kidonda ni kikubwa au kimevimba sana, nenda hospitali kwanza.
ASANTE KWA KUTUFUATILIA HADI
MWISHO: Endelea kutembelea page hii ili kusoma pia Makala nyinginezo kwa ujuzi
na maarifa zaidi. “Tuachie maoni yako, sehemu ya comment hapo chini’



No comments:
Post a Comment