Friday, 26 January 2018

MASHINDANO YA UREMBO WA NGAMIA SAUDI ARABIA WATUMBUKIA KATIKA KASHFA

 Haki miliki ya picha Reuters Image caption Visitors to the festival in al-Dahna, north of Riyadh, can also watch camel racing
Imezoeleka kuwa na aina ya mambo au vitu vinavyofanyika katika eneo au nchi flani kwa Jeografia yake kulitangaza eneo hilo au nchi husika kimataifa kama vile ilivyo kwa matukio tofauti yanayowahusisha wanadamu kukusanyika eneo flani moja kushuhudia jambo flani.
 
Pengine ni ubunifu, au uwepo wa tafsiri tofauti na baadhi ya mambo ambayo binaadamu tunavutiwa nayo, yatumiwe vyema kutangaza, kuliwaza na kutuliza akili zetu na mawazo yetu kama vile ilivyo muziki mzuri wenye ala zilizopangiliwa vyema kimirindimo.
 
Kubwa nalotaka kuzungumzia leo ni kuwa, tanzania na nchi nyingine za afrika mashariki nao wabuni baadhi ya tukio (Event) muhimu ambayo itawakushanya watu pamoja kama njia ya kupata burudani lakini wakati huohuo wakiitangaza nchi yao na utamaduni wao duniani.
 
HEBU TUANGAZIE HILI LA SAUDI-ARABIA.
 
Ngamia 12 wamepoteza sifa za mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya wamiliki wao kuwachoma sindano ya kubadili maumbile.

Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na kushindanishwa kwa muonekano wa nyuso zao, nundu na maumbile yao.

Lakini majaji waliingia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za fedha.
Vile vile tamasha hilo lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim dola milioni 57.
Mtandao wa habari wa The National imeripoti kuwa Ali Al Mazrouei, mwana wa mfugaji bingwa , alisema dawa ya botox ilitumika kwenye midomo, pua na hata taya.
"Dawa hiyo inavimbisha kichwa kwa hio ukimuona ngamia unadhani ana kichwa,mdomo na pua kubwa" aliezea Mazrouei.
Majaji pia walikuwa wakishindanisha nundu na misuli ya ngamia.
Kabla ya tamasha hilo, vyombo vya habari vya Saudia viliripoti daktari wa wanyama alikamatwa akiwa pasua ngamia hao ili kuwabadilisha ukubwa wa masikio pamoja na kuwachoma sindano ya dawa ya kubadilisha maumbile.
    Haki miliki ya picha Reuters Image caption Shindano lina vigezo vikali vya urembo
Pia unaweza soma yafuatayo§ Binti shujaa mbunifu wa Emoji iliyo na Hijab


Jaji mkuu Fawzan al-Madi amesema kuwa ngamia ni mojawapo wa "nembo ya Saudi Arabia" kimataifa na mashindano hayo ya urembo wa ngamia nchini humo yalianza kufanyika kwa mara ya kwanza tokea mwaka 2000.
SOURCE: bbc Swahili
 

Friday, 19 January 2018

IMEKAA VIPI HII ZA BANGI KURUHUSIWA KIHALALI KATIKA BAADHI YA NCHI ZA MAGHARIBI!


Maafisa katika jimbo la Nevada nchini Marekani wameamua kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana na uhaba wa bangi ambao unaendelea kuyakumba maeeneo hayo.
Habari kutoka nchini humo, zinasema Mahitaji ya bangi yamekuwa ya juu tangu bangi ihalalishwe kwa matumizi ya kujiburudisha tarehe mosi mwezi julai mwaka 2017, na hiyo ikichagizwa na ukosefu wa wauzaji wa kilevya mwili hicho wa kutosha.
Sheria mpya iliyotungwa nchini humo iliwapa wauzaji wa pombe ruhusa ya kuuza bangi kama sharti la nyumba za starehe, lakini wengi hawatimizi mahitajio ya leseni zao na sheria isemavyo kwa kuweza kuuza bidhaa hizo za bangi.
Idara ya kodi katika jimbo hilo ilitangaza dharura, inayomaanisha kuwa maafisa watachukua hatua za dharura kukabiliana na uhaba huo.
Mauzo ya karibu dola milioni 3 yalikadiriwa siku nne za kwanza baada ya matumizi ya bangi kuhalalishwa.
Kama zilivyo nchi nyingine, Nevada ilipiga kura ya kuhalalisha matumizi ya bangi kama moja wapo ya burudani mwezi Novemba mwaka jana kufuatia hatua kama hizo katika majimbo mengine kupitishwa.
Matumzi ya bangi kwa matibabu yameruhusiwa katika majimbo 25 ikiwemo Nevada ambapo imehalalishwa tangu nwaka 2001.
KWA MFANO:
Katika nchi kama vile Uruguay, bangi imehalalishwa na kushauriwa kutumika mahospitalini na maduka ya dawa kama moja ya tiba za dharura kwa wagonjwa wengi wa akili mbalimbali.
Uruguay ilipitisha sheria hiyo ya kuuzwa kwa bangi kwenye maduka ya dawa tokea mwezi julai mwaka jana.
Nchi hiyo ya Marekani Kusini itakuwa ya kwanza duniani kuuza Bangi kihalali kwa matumizi ya kujiburudisha tu, na pia inasemekana Safari hiyo ya kuhalalisha matumizi ya bangi ilianza tokea mwaka wa 2013 baada ya sheria kadhaa zilizokubali uuzaji na ununuzi wake kupitishwa bungeni.
Hata hivyo imechukua muda mrefu kwa sheria hiyo kuanza kutumika nchini humo.
ZAIDI KUHUSU HILO HAPA:
http://www.bbc.com/swahili/habari-39530537
CHANZO:
http://www.bbc.com/swahili/habari-40591100
 

Friday, 5 January 2018

FAHAMU MAMBO KADHAA USIYOYAJUA KUHUSU HALLOWEEN.



Halloween, hujulikana zaidi kama “Mkesha wa sikukuu ya Watakatifu Wote, na Husheherekewa unakoishi”
 
Katika nchi kama Canada na Marekani Halloween ni maharufu sana na husheherekewa kila ifikapo octoba 31 kila mwaka.
Hata hivyo sherehe hizo, zinazofanywa wakati wa Halloween, kwasasa zimeenea katika sehemu tofautitoauti Ulimwenguni pote.
Katika sehemu Fulani, kuna sikukuu ambazo ingawa zimepewa majina tofauti, lakini zina kusudio kama la Halloween:
 
HALLOWEEN NI NINI? “Halloween ni kuwasiliana na Viumbe Wa Roho (Mizuka) iwe ni kupitia roho za Wafu, Wachawi, au hata Ibilisi na Malaika zake waovu.
Mara nyingi Alama inayotumiwa na Wafuasi wa Imani hiyo ni (Pembe tatu-tatu 3/3 pamoja na alama ya meno manne-juu & chini)


Huenda wewe binafsi Usiamini kwamba kuna Viumbe wa Roho wenye Nguvu zisizo za kawaida, na Pia huenda ukawa na Maoni tofauti ya kwamba Kushiriki katika Sherehe ya Halloween na Sherehe nyingine zinazofanana na hizo ni njia ya kujifurahisha tu na ya Kuwafundisha Watoto wako kuwa wabunifu.

Hata hivyo watu wengi wanaona Sikukuu hizo kuwa zenye Madhara kwa sababu zifuatazo:

Kitabu cha Encyclopedia of American Folklore (ensaiklopedia ya Desturi ya Wamarekani) kinasema: “Halloween inahusisha hasa kuwasiliana na Viumbe wa roho ambao wengi wao hutisha au kuogopesha.”
SIKUKUU ZINAZOFANANA NA HALLOWEEN ULIMWENGUNI POTE.
 
Kwa Ujumla Halloween huonwa kuwa sikukuu kwa wa Marekani, Lakini sasa sikukuu hiyo inapendwa sana katika sehemu nyingine ulimwenguni, istoshe kuna sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo kwa maana kwamba Zinasheherekewa kuwapo kwa viumbe wa roho na utendaji wao (Kufanya mila za matambiko).
Zifuatazo ni baadhi ya Sikukuu Maarufu zinazofanana na Halloween ambazo zinapatikana Ulimwenguni pote.
 
Asia – sherehe ya ‘BON’
 
Afrika – dansi ya ‘EGUNGUN
 
Amerika kusini – ‘KAWSASQANCHIS’
 
Amerika kaskazini na Ulaya – ‘SIKU YA WAFU’ na ‘HALLOWEEN’
 
CHANZO CHAKE NI NINI?
 
Zipo baadhi ya imani mbalimbali ambazo zinaelezea Chanzo kuhusu Roho Hawa wenye nguvu na wasioonekana kwa macho ya kawaida, ambapo kila mmoja kwa Tamaduni yake ana Namna anavyoweza kuelezea Viumbe hao wasionekana:
 
Baadhi Huamini kwamba; ni Majini Yanayonyonya Damu za watu, mbweha n.k.
 
Wengine husema Roho hawa huhusiana sna na Wachawi wanaowawangia watu usiku wakiwa wamelala, au kuhusisha na imani za Iluminati (Feemason) ambavyo vyote hivyo hutendekea gizani au kwa uficho na usiri mkubwa.
 
ISHARA ZINAZOTUMIWA:
 

Peremende (pipi):
 
WASELTI wa kale walijaribu Kuwatuliza viumbe waovu kwa kuwapa Peremende, Baadaye Kanisa liliwatia watu moyo waende nyumba kwa nyumba mkesha wa sikukuu ya Watakatifu wote ili kuwaombea wote waliokufa katika Imani, na kupewa chakula kama malipo (matambiko)
 
Mwishowe hiyo ikaja kuwa Desturi ya Halloween, na watu walienda nyumba kwa nyumba wakiomba Peremende na Kuwatisha watu wasiowapa peremende.
 
MAVAZI YANAYOTUMIWA:
 
Waselti walivaa vinyago usoni ili roho waovu wadhani kwamba wao ni miongoni mwao hivyo wasiwadhuru, Kanisa liliingiza desturi za kipagani katika sherehe za sikukuu za wafu na siku ya Watakatifu wote.
 
Baadaye waadhimishaji walienda nyumba kwa nyumba wakiwa wamevalia kama watakatifu, malaika na Mashetani.
 
MABOGA:


Aina flani ya Boga linaloitwa Tanipu lilichongwa na kutiwa mshumaa hutumika katika sherehe hizo ikiaminika husaidia kuwatuliza au kuwafukuza roho waovu.
 
Watu flani huamini na husema kwamba boga na mishumaa hiyo uliwakilisha nafsi zilizokuwa zimezuiliwa toharani, ambapo baadaye watu walianza kutumia Maboga ya kawaida endapo yale ya tanipu yasipopatikana.
 
KUMBUKA: Halloween na sikukuu nyingine nyingi zina asili ya Kipagani na huhusisha sana kuabudu watu waliokufa ambapo hata hivi wa leo, watu wanaoisheherekea katika Nchi zao mbalimbali, idinazidi kuongezeka, na wengi wao Hawatambui baadhi ya ishara na Mapambo ya majumbani wanayotumia Yanahusiana na Wapagani waimani hizi.
 
Maelfu Ya Jamii Ya Kichawi inayoitwa WICCAN, Ambayo hufuata desturi za waselti wa kale bado huiita ‘Halloween’ kwa jina lake la kale, yaani Samhain, nao husema kwamba huo ndio usiku mtakatifu zaidi katika mwaka.
 
Gazeti la USA TODAY likimnukuu mtu aliyejiita Mchawi linasema; “Watu wa imani tofauti hawatambui kuwa Wanasheherekea sikukuu yetu pamoja nasi, Tunafurahia jambo hilo”
 
HISTORIA YA HALLOWEEN


‘Hallow’ ni neno la kale linalomaanisha (mtakatifu) na ‘ween’ ikimaanisha (usiku) ambapo kwa ujumla muunganiko wa neno ‘Halloween’ linamaanisha (Usiku mtakatifu)
 
Karne ya-1 (w.k)
 
Watu wa Roma ya kale waliwashinda waselti na wakaanza kufuata desturi mpya za Samhain zinazohusiana na roho za waovu.
 
Karne ya 5: (k.w.k)
 
Waselti wengi waliadhimisha sherehe ya Samhain mwishoni mwa mwezi Oktoba, mwezi ambao waliamini Mizuka na roho waovu walizurura duniani kuliko wakati mwingine wowote.
 
Karne ya 7: (w.k)
 
Inasemekana kwamba Papa Boniface wa4 aliyeanzisha sherehe ya kila mwaka ya watakatifu wote (kwa wakatoliki) ili kuwakumbuka Wafia_Imani wote.
 
Karne ya-11 (w.k)
Novemba2 inawekwa kuwa siku ya Wafu, yaani siku ya kuwakumbuka wote waliokufa.
Karne-ya 18 (w.k): jina la siku ya ‘Halloween’ linaanza kuonekana katika machapisho.
Karne ya19 (w.k): Maelfu ya watu wa IRELAND wanaohamia Marekani walikuja na desturi zao za Halloween na baada ya muda, desturi hizo zinachanganywa na zile za wahamiaji wengine kutoka Uingereza, Ujerumani, Afrika na sehemu nyingine ulimwenguni.
Karne ya 20 (w.k) Halloween inakuwa sikukuu maarufu zaidi nchini Marekani.
Karne Ya 21: Halloween inakuwa biashara kubwa inayowaingizia Wafanyabiashara mabilioni ya Pesa Ulimwenguni pote kama ilivyo kwa sikukuu nyingine za iddi, au xmass.
NUKUU:
“Kwa sababu ya mambo yote nliyoyazungumza katika makala haya, ni jambo jema na la hekima kulizingatia kwa kujua chanzo cha HALLOWEEN na sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo ili kujua mambo kiundani na pia itakusaidia kuepuka kwa kujiunga na watu ambao husheherekea sikukuu kama hizo”

SOURCES:

All saints day: © The Bridgeman Art
University of Michigan Library And Google; customs,
Wikipedia,
Archieves; pope Boniface IV.