Friday, 5 January 2018

FAHAMU MAMBO KADHAA USIYOYAJUA KUHUSU HALLOWEEN.



Halloween, hujulikana zaidi kama “Mkesha wa sikukuu ya Watakatifu Wote, na Husheherekewa unakoishi”
 
Katika nchi kama Canada na Marekani Halloween ni maharufu sana na husheherekewa kila ifikapo octoba 31 kila mwaka.
Hata hivyo sherehe hizo, zinazofanywa wakati wa Halloween, kwasasa zimeenea katika sehemu tofautitoauti Ulimwenguni pote.
Katika sehemu Fulani, kuna sikukuu ambazo ingawa zimepewa majina tofauti, lakini zina kusudio kama la Halloween:
 
HALLOWEEN NI NINI? “Halloween ni kuwasiliana na Viumbe Wa Roho (Mizuka) iwe ni kupitia roho za Wafu, Wachawi, au hata Ibilisi na Malaika zake waovu.
Mara nyingi Alama inayotumiwa na Wafuasi wa Imani hiyo ni (Pembe tatu-tatu 3/3 pamoja na alama ya meno manne-juu & chini)


Huenda wewe binafsi Usiamini kwamba kuna Viumbe wa Roho wenye Nguvu zisizo za kawaida, na Pia huenda ukawa na Maoni tofauti ya kwamba Kushiriki katika Sherehe ya Halloween na Sherehe nyingine zinazofanana na hizo ni njia ya kujifurahisha tu na ya Kuwafundisha Watoto wako kuwa wabunifu.

Hata hivyo watu wengi wanaona Sikukuu hizo kuwa zenye Madhara kwa sababu zifuatazo:

Kitabu cha Encyclopedia of American Folklore (ensaiklopedia ya Desturi ya Wamarekani) kinasema: “Halloween inahusisha hasa kuwasiliana na Viumbe wa roho ambao wengi wao hutisha au kuogopesha.”
SIKUKUU ZINAZOFANANA NA HALLOWEEN ULIMWENGUNI POTE.
 
Kwa Ujumla Halloween huonwa kuwa sikukuu kwa wa Marekani, Lakini sasa sikukuu hiyo inapendwa sana katika sehemu nyingine ulimwenguni, istoshe kuna sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo kwa maana kwamba Zinasheherekewa kuwapo kwa viumbe wa roho na utendaji wao (Kufanya mila za matambiko).
Zifuatazo ni baadhi ya Sikukuu Maarufu zinazofanana na Halloween ambazo zinapatikana Ulimwenguni pote.
 
Asia – sherehe ya ‘BON’
 
Afrika – dansi ya ‘EGUNGUN
 
Amerika kusini – ‘KAWSASQANCHIS’
 
Amerika kaskazini na Ulaya – ‘SIKU YA WAFU’ na ‘HALLOWEEN’
 
CHANZO CHAKE NI NINI?
 
Zipo baadhi ya imani mbalimbali ambazo zinaelezea Chanzo kuhusu Roho Hawa wenye nguvu na wasioonekana kwa macho ya kawaida, ambapo kila mmoja kwa Tamaduni yake ana Namna anavyoweza kuelezea Viumbe hao wasionekana:
 
Baadhi Huamini kwamba; ni Majini Yanayonyonya Damu za watu, mbweha n.k.
 
Wengine husema Roho hawa huhusiana sna na Wachawi wanaowawangia watu usiku wakiwa wamelala, au kuhusisha na imani za Iluminati (Feemason) ambavyo vyote hivyo hutendekea gizani au kwa uficho na usiri mkubwa.
 
ISHARA ZINAZOTUMIWA:
 

Peremende (pipi):
 
WASELTI wa kale walijaribu Kuwatuliza viumbe waovu kwa kuwapa Peremende, Baadaye Kanisa liliwatia watu moyo waende nyumba kwa nyumba mkesha wa sikukuu ya Watakatifu wote ili kuwaombea wote waliokufa katika Imani, na kupewa chakula kama malipo (matambiko)
 
Mwishowe hiyo ikaja kuwa Desturi ya Halloween, na watu walienda nyumba kwa nyumba wakiomba Peremende na Kuwatisha watu wasiowapa peremende.
 
MAVAZI YANAYOTUMIWA:
 
Waselti walivaa vinyago usoni ili roho waovu wadhani kwamba wao ni miongoni mwao hivyo wasiwadhuru, Kanisa liliingiza desturi za kipagani katika sherehe za sikukuu za wafu na siku ya Watakatifu wote.
 
Baadaye waadhimishaji walienda nyumba kwa nyumba wakiwa wamevalia kama watakatifu, malaika na Mashetani.
 
MABOGA:


Aina flani ya Boga linaloitwa Tanipu lilichongwa na kutiwa mshumaa hutumika katika sherehe hizo ikiaminika husaidia kuwatuliza au kuwafukuza roho waovu.
 
Watu flani huamini na husema kwamba boga na mishumaa hiyo uliwakilisha nafsi zilizokuwa zimezuiliwa toharani, ambapo baadaye watu walianza kutumia Maboga ya kawaida endapo yale ya tanipu yasipopatikana.
 
KUMBUKA: Halloween na sikukuu nyingine nyingi zina asili ya Kipagani na huhusisha sana kuabudu watu waliokufa ambapo hata hivi wa leo, watu wanaoisheherekea katika Nchi zao mbalimbali, idinazidi kuongezeka, na wengi wao Hawatambui baadhi ya ishara na Mapambo ya majumbani wanayotumia Yanahusiana na Wapagani waimani hizi.
 
Maelfu Ya Jamii Ya Kichawi inayoitwa WICCAN, Ambayo hufuata desturi za waselti wa kale bado huiita ‘Halloween’ kwa jina lake la kale, yaani Samhain, nao husema kwamba huo ndio usiku mtakatifu zaidi katika mwaka.
 
Gazeti la USA TODAY likimnukuu mtu aliyejiita Mchawi linasema; “Watu wa imani tofauti hawatambui kuwa Wanasheherekea sikukuu yetu pamoja nasi, Tunafurahia jambo hilo”
 
HISTORIA YA HALLOWEEN


‘Hallow’ ni neno la kale linalomaanisha (mtakatifu) na ‘ween’ ikimaanisha (usiku) ambapo kwa ujumla muunganiko wa neno ‘Halloween’ linamaanisha (Usiku mtakatifu)
 
Karne ya-1 (w.k)
 
Watu wa Roma ya kale waliwashinda waselti na wakaanza kufuata desturi mpya za Samhain zinazohusiana na roho za waovu.
 
Karne ya 5: (k.w.k)
 
Waselti wengi waliadhimisha sherehe ya Samhain mwishoni mwa mwezi Oktoba, mwezi ambao waliamini Mizuka na roho waovu walizurura duniani kuliko wakati mwingine wowote.
 
Karne ya 7: (w.k)
 
Inasemekana kwamba Papa Boniface wa4 aliyeanzisha sherehe ya kila mwaka ya watakatifu wote (kwa wakatoliki) ili kuwakumbuka Wafia_Imani wote.
 
Karne ya-11 (w.k)
Novemba2 inawekwa kuwa siku ya Wafu, yaani siku ya kuwakumbuka wote waliokufa.
Karne-ya 18 (w.k): jina la siku ya ‘Halloween’ linaanza kuonekana katika machapisho.
Karne ya19 (w.k): Maelfu ya watu wa IRELAND wanaohamia Marekani walikuja na desturi zao za Halloween na baada ya muda, desturi hizo zinachanganywa na zile za wahamiaji wengine kutoka Uingereza, Ujerumani, Afrika na sehemu nyingine ulimwenguni.
Karne ya 20 (w.k) Halloween inakuwa sikukuu maarufu zaidi nchini Marekani.
Karne Ya 21: Halloween inakuwa biashara kubwa inayowaingizia Wafanyabiashara mabilioni ya Pesa Ulimwenguni pote kama ilivyo kwa sikukuu nyingine za iddi, au xmass.
NUKUU:
“Kwa sababu ya mambo yote nliyoyazungumza katika makala haya, ni jambo jema na la hekima kulizingatia kwa kujua chanzo cha HALLOWEEN na sikukuu nyingine zinazofanana na hiyo ili kujua mambo kiundani na pia itakusaidia kuepuka kwa kujiunga na watu ambao husheherekea sikukuu kama hizo”

SOURCES:

All saints day: © The Bridgeman Art
University of Michigan Library And Google; customs,
Wikipedia,
Archieves; pope Boniface IV.
 

No comments:

Post a Comment