Maafisa katika jimbo la Nevada nchini Marekani wameamua kuchukua hatua za dharura ili kukabiliana na uhaba wa bangi ambao unaendelea kuyakumba maeeneo hayo.
Habari kutoka nchini humo,
zinasema Mahitaji ya bangi yamekuwa ya juu tangu bangi ihalalishwe kwa matumizi
ya kujiburudisha tarehe mosi mwezi julai mwaka 2017, na hiyo ikichagizwa na ukosefu
wa wauzaji wa kilevya mwili hicho wa kutosha.
Sheria mpya iliyotungwa nchini
humo iliwapa wauzaji wa pombe ruhusa ya kuuza bangi kama sharti la nyumba za
starehe, lakini wengi hawatimizi mahitajio ya leseni zao na sheria isemavyo kwa
kuweza kuuza bidhaa hizo za bangi.
Idara ya kodi katika jimbo hilo
ilitangaza dharura, inayomaanisha kuwa maafisa watachukua hatua za dharura
kukabiliana na uhaba huo.
Mauzo ya karibu dola milioni 3
yalikadiriwa siku nne za kwanza baada ya matumizi ya bangi kuhalalishwa.
Kama zilivyo nchi nyingine, Nevada
ilipiga kura ya kuhalalisha matumizi ya bangi kama moja wapo ya burudani mwezi
Novemba mwaka jana kufuatia hatua kama hizo katika majimbo mengine kupitishwa.
Matumzi ya bangi kwa matibabu
yameruhusiwa katika majimbo 25 ikiwemo Nevada ambapo imehalalishwa tangu nwaka
2001.
KWA MFANO:
Katika nchi kama vile Uruguay,
bangi imehalalishwa na kushauriwa kutumika mahospitalini na maduka ya dawa kama
moja ya tiba za dharura kwa wagonjwa wengi wa akili mbalimbali.
Uruguay
ilipitisha sheria hiyo ya kuuzwa kwa bangi kwenye maduka ya dawa tokea mwezi
julai mwaka jana.
Nchi hiyo ya Marekani Kusini
itakuwa ya kwanza duniani kuuza Bangi kihalali kwa matumizi ya kujiburudisha
tu, na pia inasemekana Safari hiyo ya kuhalalisha matumizi ya bangi ilianza tokea
mwaka wa 2013 baada ya sheria kadhaa zilizokubali uuzaji na ununuzi wake kupitishwa
bungeni.
Hata hivyo imechukua muda mrefu
kwa sheria hiyo kuanza kutumika nchini humo.
ZAIDI KUHUSU HILO HAPA:
No comments:
Post a Comment