Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Sunday, 27 May 2018
FAINALI UEFA, MADRID AMERUDISHA HESHIMA ALIYOTAKA KUIPOTEZA
HAYAWI HAYAWI HATIMAYE YAMEKUA: Uefa FAINALI usiku wa kuamkia Leo, Ni Madrid tena amenyakua ndoo hiyo ya UEFA na kumfanya kuwa (UN-STOPABLE) Kwenye Michuano hiyo mikubwa Barani Ulaya.
Lengo la kurudi kuandika hapa sio kufurahia Liverpool kutolewa kwa kufungwa mabao 3-1, wala sio kwa kitendo cha Mo-Salaa kulazimishwa kutoka nje ya uwanja kwa maumivu ya kuumia Mkono, kitendo kilichomfanya abubujikwe na machozi.
Ila naandika Makala haya tena kukumbushia Makala yangu iliyopita wakati timu takribani nne (4) zilipofuzu kuingia hatua ya Nusu fainali na Nikasemaa:
MADRID ANASTAHILI HESHIMA JAPO KIDOGO, NA HII NI MARA BAADA YA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI KWA UTATA KIDOGO KUTOKANA NA PENATI YA BAO LA USHINDI KUWAVUSHA:
Rudia Hapa Mwenyewe: Mbabe Uefa-2018
NITOE TU KONGOLE KWA MADRID NA MASHABIKI WAKE WOTE DUNIANI KWA KUENDELEA KUITAWALA MICHUANO HIYO YA UEFA:
Labels:
MAKALA / UCHAMBUZI,
MICHEZO
Friday, 20 April 2018
KUELEKEA NUSU FAINALI YA UEFA, TUANGAZIE REKODI MUHIMU ZA SOKA AMBAZO HAZIJAVUNJWA!
REKODI AMBAZO MPAKA SASA HAZIJAWAHI KUVUNJWA KATIKA SOKA NI PAMOJA NA:
Idadi
KUBWA ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani:
Mechi
iliyowahi kufungwa magoli mengi zaidi: Rekodi hii iliwekwa
October 31, Mwaka2002 katika mchezo ngazi ya vilabu kati ya AS Adema
dhidi ya SO l’Emyrne
uliyochezwa Madagascar; Mchezo
ulimalizika kwa AS Adema kuibuka
na ushindi wa Magoli
149 – 0 magoli ambayo SO l’Emyrne walijifunga kwa makusudi
baada ya mchezo uliyopita kutoridhishwa na maamuzi ya refa na kuwafanya wakose matumaini
ya kutwaa Ubingwa. ONA HAPA
Baada ya mechi kocha wa SO l’Emyrne alifungiwa miaka mitatu na wachezaji wanne walifungiwa
hadi mwisho wa msimu.
Licha
ya kuwa Pele ndio anatajwa kuwa
mchezaji aliyecheza mechi nyingi 1375 kwa kila mechi, ila idadi ya mechi zake
rasmi za mashindano zinatajwa kuwa 1115, Golikipa Rogerio
Ceni ndio mchezaji ambaye anatajwa kuwa amecheza mechi nyingi
zaidi rasmi kuliko mchezaji yoyote, amecheza jumla ya mechi 1141.
Ceni alikuwa akiichezea Sao Polo ya Brazil toka mwaka 1992, Rekodi ambayo inatajwa kaiweka akiwa na
klabu moja na jumla ya mechi zake chache alizocheza timu ya taifa.
Rekodi mpya iliyowekwa mwaka huu2018,
ni rekodi ya Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ya
nchini Uingereza na Mchezaji wa timu ya Misri (Mohamed Salah), huyu ameweka rekodi ya
Mchezaji wa kwanza mwenye aslili ya kiafrika na anayetokea Afrika katika ligi
ya uingereza (EPL) kufunga magoli mengi (30) ndani ya msimu mmoja hadi hii sasa, na kuwa mchezaji wa 4 katika historia ya klabu hiyo
kufikisha magoli-40 ndani ya msimu mmoja
kwenye mashindano tofauti, idadi ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote
kutoka bara la Afrika.
Klabu
ya Real Madrid ya Hispania
ndio inatajwa kuwa na rekodi ya kuchukua Kombe la klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mara tano mfululizo, imewahi kufanya hivyo mwaka 1955 na 1960, Licha ya kuwa Barcelona ya Guardiola na FC Bayern
Munich ya Heynckes
kutajwa kuwa bora haijawahi kutwaa taji hilo hata mara mbili mfululizo.
FAHAMU MAAJABU HAYA-10 KUHUSU MICHUANO YA
UEFA
Arsenal
wanashikilia rekodi ya kuwa timu pekee kucheza mechi ya UEFA ikiwa na wachezaji
11 wa mataifa 11 tofauti, Yaani kila mchezaji alikuwa na taifa lake!Real Madrid inashikilia rekodi ya kuchukua kombe la UEFA mara nyingi zaidi ikiwa imechukua mara 11, Pia ikiwa timu pekee hadi sasa iliyochukua kombe hilo mara5 mfululizo (wakati likiitwa “European cup”) kuanzia mwaka 1956 mpaka 1960.
Barcelona inashikilia rekodi ya kufika nusu fainali sita mfululizo kwenye michuano hii mikubwa duniani.
Ni wachezaji wawili tu waliowahi kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa fainali ya UEFA Jens Lehmann (Arsenal) katika fainali ya 2006 na Didier Drogba aliyekuwa (Chelsea), Timu zao zilipoteza michezo hiyo baada ya kadi hizo.
Klabu za Hispania ndio zinaongoza kuchukua kikombe cha UEFA mara 14 (real madrid na barcelona pekee), Wakifuatiwa na vilabu vya England (Liverpool mara5) na Italia mara 12,
Benifica inashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi zaidi katika mechi mbili za hatua ya mtoano ilishinda jumla ya mabao 18-0 dhidi ya Dudelange. Mechi ya kwanza benifica ilishinda 8-0 na mechi ya pili 10-0
Atletico Madrid imefika fainali ya uefa mara mbili tu, ya kwanza ikiwa mwaka 1974 dhidi ya Bayern munich ambapo mechi iliisha kwa sare ya moja kwa moja na kuamuliwa irudiwe siku mbili baadae na Bayern kushinda 4-0. Ya pili ilikuwa ya mwaka 2014 ambapo walicheza dhidi ya r.madrid na real kushinda mabao 4-1.
Mchezaji mkubwa zaidi kucheza UEFA ni Marco Ballotta wa lazio akiwa na miaka 43 huku mchezaji mdogo zaidi kucheza uefa akiwa ni muafrika Celestine Babayaro akiwa na miaka 16!
Mwaka 1967 Celtic ilibeba kombe ikiwa na wachezaji wote wazaliwa wa eneo moja la kilometa 50 kuzunga uwanja wao wa nyumbani.
Goli la mapema zaidi kufungwa lilikuwa la mchezaji wa Bayern muchen Roy Makaay, sekunde 10 tu baada ya mchezo kuanza!
REAL MADRID akiwa ndiye mtawala zaidi wa michuano hii, kidogo anastahili heshima yake pamoja na kutizamwa kwa jicho tofauti zaidi (Kama Mshindi na Sio Mshindwa), hii ni baada ya kuingia nusu fainali kwa tabu dakika za mwisho msimu huu baada ya kupewa penati kwenye dakika za nyongeza katika mchezo waliokuwa nyumbani wakicheza na kibibi kizee cha Turin (Juventus ya Italia.)
Katika mchezo huo kwa matokeo ya awali walioongoza 3-0 ugenini’ wakarudi nyumbani Bernabeu na Juve kupindua matokeo hayo kwa kuandikisha ushindi sawa na huo wa 3-0, kabla ya Madrid kuzawadiwa penati na Mashabiki wengi wa soka wakawa wanalijadili hilo kuwa haikustahili wao kupewa penati, bali refarii aliamua kuwabeba.
HEBU LEO TUANGAZIE HISTORIA FUPI YA REAL MADRID (KWA UFUPI) KATIKA UNYAKUWAJI WA MAKOMBE TOFAUTI TOKEA KUANZISHWA KWAKE.
Uwanja wa Nyumbani: Estadio Santiago Bernabeu
HISTORIA
Ilianzishwa Mwaka: 1902
MATAJI:
European Cup Winners (Sasa UEFA) Mara-11:
European Cup Winners (Sasa UEFA) Mara-11:
1956,
1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016
Kuondolewa Fainali UEFA
1971, na 1983
UEFA Cup
Winners: 1985, na 1986
Spanish Champions (La Liga-32): 1932, 1933, 1954, 1955, 1957, 1958, 1961,
1962, 1963, 1964, 1965, 1967, 1968, 1969, 1972, 1975, 1976, 1978, 1979, 1980, 1986,
1987, 1988, 1989, 1990, 1995, 1997, 2001, 2003, 2007, 2008, 2012
21ST CENTURY EUROPEAN SEASONS:
2000 - Champions League Winners
2001 - Champions League Semi-Final
2002 - Champions League Winners
2003 - Champions League Semi-Final
2004 - Champions League Quarter-Final
21ST CENTURY EUROPEAN SEASONS:
2000 - Champions League Winners
2001 - Champions League Semi-Final
2002 - Champions League Winners
2003 - Champions League Semi-Final
2004 - Champions League Quarter-Final
2005 – 2010 Champions League 2nd Round
2011 – 2013 Champions League Semi-Final
2011 – 2013 Champions League Semi-Final
2014 - Champions League Winners
2015 - Champions League Semi-Final
2016 – 2017 Champions League Winners
2018 …………???????????
2016 – 2017 Champions League Winners
2018 …………???????????
Season
Labels:
MAKALA / UCHAMBUZI,
MICHEZO
Friday, 10 November 2017
KUTANA NA ISABELA, BILIONEA NAMBA MOJA BARANI AFRIKA ALIYEAMUA KUWEKEZA KWENYE SOKA
Nguvu ya uwekezaji katika soka la kileo, huwa na matokeo
chanya haswaa Akihusishwa Mwanamke (kama tunavyokubaliana Palipo mafanikio ya
Mwanaume bhasi nyuma yake kuna mwanamke)
HAKUNA ubishi kuwa hapa nyumbani Tanzania, na duniani kote mchezo
maarufu zaidi ni soka, Ambapo soka ndiyo mchezo wenye mashabiki wengi zaidi
tena kwa kiwango kikubwa cha asilimia (88/100) nyingi.Hapa Tanzania, Wafanyabiashara watatu wakubwa ndiyo wameamua kuwekeza katika mchezo wa soka na mabadiliko yamekuwa yakionekana hata kama si sehemu zote.
Said Bakhresa, yeye ameamua kuanzisha timu yake ya Azam FC. Imekuwa na mafanikio makubwa kwa muda mfupi ingawa haijaweza kuwashawishi mashabiki sana kama ilivyo kwa wakongwe, Yanga na Simba.
Yusuf Manji, bilionea ambaye amekuwa hataki kuonekana au
kujitangaza sana kwa maana ya utajiri, yeye alikuwa tayari kuwekeza Yanga kwa
njia ya kukodisha lakini inaonekana kumekuwa na figisu, jambo linaloonekana
kuikwamisha Yanga na kuifanya iingie katika mwendo wa kusuasua.
Wakati Yanga bado hawajajua kipi ndiyo au hapana, Simba wapo
kwenye mchakato wa kukubali Sh bilioni 20, ofa kutoka kwa bilionea kijana zaidi
barani Afrika Mohammed Dewji ambaye utajiri wake unafikia dola bilioni 1.4
(zaidi ya Sh trilioni tatu).
Mo Dewji anataka kununua hisa za Simba kwa asilimia 51 ili
kuanza kuiendesha kwa nafasi na kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko.
Nadhani umeon nguvu ya uwekezaji?
Wakati mabilionea hao wa Tanzania wameingia katika soka,
upande wa Angola, mwanamama tajiri zaidi nchini humo na tajiri zaidi kuliko
wanawake wote barani Afrika, Isabela dos Santos, yeye amechaguliwa kuwa rais wa
klabu kongwe ya Petro Luanda, hali ambayo inaonyesha wazi sasa ameamua kuingia
kwenye mchezo huo wa soka.
![]() |
| Moja ya nyumba ya kifahari inayomilikiwa na Mwanamama Isabela. |
Utajiri wa Isabela ni dola bilioni 3.3 (zaidi ya Sh trilioni
7). Kumbuka mwanamama huyu mwenye watoto watatu ni mtoto wa Rais Jose Eduardo
dos Santos aliyewahi kuitawala nchi ya Angola.
Lakini ni mke wa Sindika Dokolo, bilionea kutoka DR Congo,
pia ni mtoto wa bilionea wa miaka nenda rudi wa nchini humo. Wawili hao
walikutana wakiwa shule barani Ulaya ambako walianzisha uhusiano wa kimapenzi.
Klabu ya Petro de Luanda ilianzishwa mwaka 1980 na kupata
mafanikio makubwa baadaye. Lakini miaka ya kuanzia 2000, ilianza kudorora na
sasa Isabela anakuwa kama mkombozi. Ushindi wake wa cheo cha rais, bila shaka
ni kama ukombozi kwa mashabiki wa klabu hiyo kwa kuwa wanajua Isabela ni
mwanamama wa chuma ambaye hatakubali kuendesha kitu kinachodorora.
Isabela ni injinia kitaaluma. Lakini amekuwa mfanyabiashara
aliyejijenga katika mafuta, madini hasa almasi lakini barani Ulaya hasa Ureno
na Hispania amewekeza katika makampuni makubwa ya simu ambako anaingiza kiwango
kikubwa cha fedha.
Lakini hivi karibuni kajiingiza kwenye biashara ya saruji na
ameanza umiliki wa mabenki, hasa nchini Ureno.
Baadhi ya wananchi au wanasiasa wapinzani wamekuwa wakipinga
kwamba anapendelewa sana kwa kuwa ni binti wa kwanza wa rais dos Santos, akiwa
ni mtoto wa kwanza wa mkewe wa kwanza.
Mwanamama huyo ambaye pia ni Rais wa Shirika la Msalaba
Mwekundu nchini Angola, anasifika kwa kuwa na tabia ya kutaka ushindi au
mafanikio makubwa kwa kila anachokiongoza.
Kabla aliwahi kuwekeza nchini Marekani katika mpira wa magongo.
Lakini baada ya kushinda katika uchaguzi na kuwa Rais wa Petro de Luanda,
alisisitiza anataka kuona timu hiyo inakuwa kubwa zaidi barani Afrika.
Isabela anasema fedha ni suala linalotokana na ubunifu na
uwezo wa uamuzi hasa katika uchapaji kazi., lakini tatizo ni kuwa Wanawake
wenyewe hawakubaliani katika maswala ya kimaendeleo, lakini zaidi hawapendi
maendeleo ya wanawake wenyewe wao kwa wao, amkeni wanawake.
Amesisitiza Isabela, kama Waangola na hasa watu wa Klabu ya
Petro de Luanda wanaamua kwa kushirikiana naye bega kwa bega, basi hakuna
anayeweza kuizuia klabu hiyo kurudisha sifa yake na kuwa kubwa sana.
![]() |
| Baba wa Isabela na Rais mstaafu wa Angola, aliyelitawala taifa hilo kwa miaka takribani 38 kabla ya kustaafu. |
Kwa mashabiki wa Petro de Luanda ni faraja upya, lakini hofu
kubwa ni kwa mashabiki wa timu nyingine. Kwamba fedha za Isabela na kwa kuwa
ndiye binti kipenzi wa Rais wa Angola ambaye amekaa madarakani tokea mwishoni
mwa miaka ya 1980, mashabiki wengi huamini kuwa huenda upendeleo unaweza kuwa
wazi. Jambo ambalo ni mtizamo hasi.
Wengi wanaamini hata waamuzi, viongozi wa Shirikisho la Soka
la Angola, watakuwa waoga na kuipa nafasi Petro de Luanda kufanya vizuri hata
isipostahili.
Utaona, kuingia kwa bilionea huyo namba moja kwa upande wa
wanawake Angola na Afrika nzima, kumewagawanya wengi. Wapo walio na faraja kuu
na wengine hofu hasa ya haki Kutendeka, ndio imetawala.
Isabela kasisitiza kwamba mafanikio ndani ya Angola ni namba
moja lakini anachotaka yeye ni Petro de Luanda kuwa klabu kubwa zaidi Afrika na
angependa kuona inazipa shida kubwa timu kubwa kutoka Afrika Kaskazini,
Magharibi na ikiwezekana zile za Afrika Kusini huku akiitaja Mamelodi Sundowns
ambayo pia iliwahi kuwa na rais mwanamama.
Wanawake mnaweza, narudia tena Mnaweza, hii ni changamoto
kwenu kuchangamkia fursa hata katika michezo, nitafurahi zaidi mkuu wa TFF, awe
mwanamke, Kwenye klabu zote za soka Tz bara kuwe na uwekezaji wa mwanamke, ndio
nini kinashindikana! Mnaweza! Kama ilivyo kwa isabela.
Isabela anaishi kwenye nyumba ya kifahari ambayo inaaminika
ni ghali zaidi kuliko Ikulu ya Angola ambayo inaongozwa na baba yake mzazi.
Lakini si rahisi kuipiga picha kutokana na ulinzi mkali.
Anamiliki boti ya kisasa, ndege mbili kwa ajili yake na
magari zaidi ya 12 ya kifahari likiwemo aina ya Maybach Exelero lenye thamani
ya dola 250,000 (zaidi ya Sh milioni 544) ambalo wengi waliamini ni la kisela
na si kwa mtu kama yeye.
Kwa kuwa ana umri wa miaka 43, Isabela amekuwa haoni shida
‘kujiachia’ na msisitizo wake ni kwamba yeye ni mama kijana anayehitaji kuishi
anavyoamini kwake ni sahihi.
Lakini amekuwa akisisitiza pia kuwa, sasa furaha yake ni
soka na anaamini uwekezaji wake katika mchezo huo utakuwa sawa na ilivyo
kuwekeza katika madini au zaidi.
Hakuna aliyepinga kuingia kwake katika uwekezaji. Wengi
wanajua si mpenzi sana wa soka au haujui vizuri. Lakini wanaamini kwa kuwa ni
mfanyabiashara, atasaidia kupatikana kwa mabadiliko kwa kuwa anajua ili kufanya
biashara vizuri katika soka, basi lazima timu inayotaka kufanya vizuri ishinde
na kupata makombe.
Isabela anataka makombe yamsaidie kupata biashara. Hivyo
lazima atahakikisha Petro de Luanda inaamka na kuwa bora zaidi ya sasa na
kumsaidia kupata na kufanya biashara ya uhakika.
VIPI KWA SIMBA NA YANGA? ENDELEENI KUGAWA HIZO HISA ZENU BHANA
ILI KUKUZA SOKA LETU TANZANIA:
MAELEZO ZAIDI KUHUSU ISABELA NA MZOZO ULIOPO KATI YA BABA YAKE
(Dos santos - Rais aliyetawala Angola kwa miaka38) na Rais wa sasa wa Angola (João Lourenço) Bofya Hapa:Makala NA: Stewart Meena+Mtandao
Labels:
MAKALA / UCHAMBUZI,
MICHEZO
Subscribe to:
Posts (Atom)







