Friday, 20 April 2018

KUELEKEA NUSU FAINALI YA UEFA, TUANGAZIE REKODI MUHIMU ZA SOKA AMBAZO HAZIJAVUNJWA!



REKODI AMBAZO MPAKA SASA HAZIJAWAHI KUVUNJWA KATIKA SOKA NI PAMOJA NA:
  Idadi KUBWA ya mashabiki wengi wa soka kuingia uwanjani:
Hii ni rekodi iliwekwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 katika mchezo kati ya Brazil dhidi ya Uruguay katika dimba la Maracanazo, mchezo huu wa fainali ulitajwa kuingiza idadi rasmi ya watu Laki moja na sabini na tatu elfu mia nane hamsini (173,850) ila inatajwa huenda kuwa idadi hiyo ilivuka na kufikia hadi watu (2,10.000) pamoja na watazamaji wasiokuwa na tiketi. ONA HAPA

Mechi iliyowahi kufungwa magoli mengi zaidi: Rekodi hii iliwekwa October 31, Mwaka2002 katika mchezo ngazi ya vilabu kati ya AS Adema dhidi ya SO l’Emyrne uliyochezwa Madagascar; Mchezo ulimalizika kwa AS Adema kuibuka na ushindi wa Magoli 149 – 0 magoli ambayo SO l’Emyrne walijifunga kwa makusudi baada ya mchezo uliyopita kutoridhishwa na maamuzi ya refa na kuwafanya wakose matumaini ya kutwaa Ubingwa. ONA HAPA
 
Baada ya mechi kocha wa SO l’Emyrne alifungiwa miaka mitatu na wachezaji wanne walifungiwa hadi mwisho wa msimu.

Licha ya kuwa Pele ndio anatajwa kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi 1375 kwa kila mechi, ila idadi ya mechi zake rasmi za mashindano zinatajwa kuwa 1115, Golikipa Rogerio Ceni ndio mchezaji ambaye anatajwa kuwa amecheza mechi nyingi zaidi rasmi kuliko mchezaji yoyote, amecheza jumla ya mechi 1141.

Ceni alikuwa akiichezea Sao Polo ya Brazil toka mwaka 1992, Rekodi ambayo inatajwa kaiweka akiwa na klabu moja na jumla ya mechi zake chache alizocheza timu ya taifa.

Rekodi mpya iliyowekwa mwaka huu2018, ni rekodi ya Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza na Mchezaji wa timu ya Misri (Mohamed Salah), huyu ameweka rekodi ya Mchezaji wa kwanza mwenye aslili ya kiafrika na anayetokea Afrika katika ligi ya uingereza (EPL) kufunga magoli mengi (30) ndani ya msimu mmoja hadi hii sasa, na kuwa mchezaji wa 4 katika historia ya klabu hiyo kufikisha magoli-40 ndani ya msimu mmoja kwenye mashindano tofauti, idadi ambayo haijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote kutoka bara la Afrika.

 
Klabu ya Real Madrid ya Hispania ndio inatajwa kuwa na rekodi ya kuchukua Kombe la klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mara tano mfululizo, imewahi kufanya hivyo mwaka 1955 na 1960, Licha ya kuwa Barcelona ya Guardiola na FC Bayern Munich ya Heynckes kutajwa kuwa bora haijawahi kutwaa taji hilo hata mara mbili mfululizo.

FAHAMU MAAJABU HAYA-10 KUHUSU MICHUANO YA UEFA
Arsenal wanashikilia rekodi ya kuwa timu pekee kucheza mechi ya UEFA ikiwa na wachezaji 11 wa mataifa 11 tofauti, Yaani kila mchezaji alikuwa na taifa lake!

Real Madrid inashikilia rekodi ya kuchukua kombe la UEFA mara nyingi zaidi ikiwa imechukua mara 11, Pia ikiwa timu pekee hadi sasa iliyochukua kombe hilo mara5 mfululizo (wakati likiitwa “European cup”) kuanzia mwaka 1956 mpaka 1960.

Barcelona inashikilia rekodi ya kufika nusu fainali sita mfululizo kwenye michuano hii mikubwa duniani.

Ni wachezaji wawili tu waliowahi kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa fainali ya UEFA Jens Lehmann (Arsenal) katika fainali ya 2006 na Didier Drogba aliyekuwa (Chelsea), Timu zao zilipoteza michezo hiyo baada ya kadi hizo.
Klabu za Hispania ndio zinaongoza kuchukua kikombe cha UEFA mara 14 (real madrid na barcelona pekee), Wakifuatiwa na vilabu vya England (Liverpool mara5) na Italia mara 12,

Benifica inashikilia rekodi ya kushinda magoli mengi zaidi katika mechi mbili za hatua ya mtoano ilishinda jumla ya mabao 18-0 dhidi ya Dudelange. Mechi ya kwanza benifica ilishinda 8-0 na mechi ya pili 10-0

Atletico Madrid  imefika fainali ya uefa mara mbili tu, ya kwanza ikiwa mwaka 1974 dhidi ya Bayern munich ambapo mechi iliisha kwa sare ya moja kwa moja na kuamuliwa irudiwe siku mbili baadae na Bayern kushinda  4-0. Ya pili ilikuwa ya mwaka 2014 ambapo  walicheza  dhidi ya r.madrid na real kushinda mabao 4-1.

Mchezaji mkubwa zaidi kucheza UEFA ni  Marco Ballotta wa lazio akiwa na miaka 43 huku mchezaji mdogo zaidi kucheza uefa akiwa  ni  muafrika Celestine Babayaro  akiwa na miaka 16!

Mwaka 1967 Celtic ilibeba kombe ikiwa na wachezaji wote wazaliwa wa eneo moja  la kilometa 50 kuzunga uwanja wao wa nyumbani.

Goli la mapema zaidi kufungwa lilikuwa la mchezaji wa Bayern muchen Roy Makaay, sekunde 10 tu baada ya mchezo kuanza!

REAL MADRID akiwa ndiye mtawala zaidi wa michuano hii, kidogo anastahili heshima yake pamoja na kutizamwa kwa jicho tofauti zaidi (Kama Mshindi na Sio Mshindwa), hii ni baada ya kuingia nusu fainali kwa tabu dakika za mwisho msimu huu baada ya kupewa penati kwenye dakika za nyongeza katika mchezo waliokuwa nyumbani wakicheza na kibibi kizee cha Turin (Juventus ya Italia.)

Katika mchezo huo kwa matokeo ya awali walioongoza 3-0 ugenini’ wakarudi nyumbani Bernabeu na Juve kupindua matokeo hayo kwa kuandikisha ushindi sawa na huo wa 3-0, kabla ya Madrid kuzawadiwa penati na Mashabiki wengi wa soka wakawa wanalijadili hilo kuwa haikustahili wao kupewa penati, bali refarii aliamua kuwabeba.

HEBU LEO TUANGAZIE HISTORIA FUPI YA REAL MADRID (KWA UFUPI) KATIKA UNYAKUWAJI WA MAKOMBE TOFAUTI TOKEA KUANZISHWA KWAKE.

Uwanja wa Nyumbani: Estadio Santiago Bernabeu


HISTORIA
Ilianzishwa Mwaka: 1902
MATAJI:
European Cup Winners (Sasa UEFA) Mara-11:
1956, 1957, 1958, 1959, 1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016
Kuondolewa Fainali UEFA 1971, na 1983
UEFA Cup Winners: 1985, na 1986
Spanish Champions (La Liga-32): 1932, 1933, 1954, 1955, 1957, 1958, 1961, 1962, 1963, 1964, 1965, 1967, 1968, 1969, 1972, 1975, 1976, 1978, 1979, 1980, 1986, 1987, 1988, 1989, 1990, 1995, 1997, 2001, 2003, 2007, 2008, 2012

21ST CENTURY EUROPEAN SEASONS:

2000 - Champions League Winners
2001 - Champions League Semi-Final
2002 - Champions League Winners
2003 - Champions League Semi-Final
2004 - Champions League Quarter-Final
2005 – 2010 Champions League 2nd Round
2011 – 2013 Champions League Semi-Final

2014 - Champions League Winners
2015 - Champions League Semi-Final
2016 – 2017 Champions League Winners
2018 …………???????????
 WASHINDI: (Bofya kwenye Mwaka kwenda kwenye taarifa Zaidi)
Season

No comments:

Post a Comment