SERIKALI
kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema
haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake
kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA).
Wahusika
wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa
Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu
wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo
washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo
wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso
kwa uso.
“Tulianzisha
mfumo huo ili kupunguza gharama zisizo na ulazima ambapo awali
ilitakiwa kila kunapokuwa na kikao lazma watumishi wasafili kuja Dar es
Salaam kwaajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia Video Conference
iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. Tumeokoa gharama za nauli,
mafuta, chakula na malazi,” amesema Temba.
Temba
ameeleza kuwa, hatua za utekelezaji wa teknolojia hiyo ulianza
kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2013 hadi sasa ambapo umekamilika na
kufanyiwa majaribio yaliyofauli kwa kufanya mikutano kumi ambayo
iliunganisha mikoa yote kasoro mitatu ambayo ni mipya ambayo ni, Njombe,
Geita na Simiyu.
Kuhusu miondombinu ya mawasiliano amewatoa hofu watumishi kwa kusema: “Mfumo
huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali
ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali
kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa
mawasiliano.”
SOURCE: Mpekuzi blog