Showing posts with label MAKALA / AFYA NA TAFITI. Show all posts
Showing posts with label MAKALA / AFYA NA TAFITI. Show all posts

Monday, 21 September 2026

FAHAMU MMEA WA KONGWA / JONGWA 'Commelina benghalensis' NA FAIDA ZAKE 10 KWA AFYA YAKO!


 

Watu wengi huweza kuuchukulia kama magugu-shamba tu na mimea sumbufu inayotambaa kumbe ni lulu kwenye baadhi ya tamaduni mbalimbali afrika, Asia, Ulaya na Amerika.

Na.

Stewart Meena.

Ni mmea wa porini unaoota sana Tanzania hasa mashambani, kando ya mito na sehemu zenye unyevunyevu, ambapo watu wengi huuona kama majani yanayotambaa na yaliyo masumbufu kwa rutuba ya mazao mengine katika shamba au bustani, kama ilivyo tu kwa mimea ya magugu kwani huota kwa kusambaa kama ilivyo kwa ukoka.

Mmea huu una majina mengi, ikilinganishwa na unakopatikana kwani una asili ya bara Asia, Afrika na ulaya na Amerika kusini, ambapo majina hayo ni kama vile: (Wandering Jew, Tropical Spiderwort, Matangawizi pori, Ndele, Kongwa na kule uchagani wakiuuta: ‘Ishongwe’ au ‘Iriria’ ) kitaalamu ukiitwa: Commelina benghalensis.

Je! Unawezaje kuutambua: Utambulisho Wake ‘Kama ilivyo pichani’ ina Shina laini, lenye maji au utomvu mweupe usio na rangi ya maziwa kama mimea ningine kwa ndani, ambapo huota kwa wingi kama ukoka na ikiwa kwakutambaa chini.

Majani yake ni ya kijani iliyopauka, umbo la yai nan cha katikati kwa mbele, huku Maua yake ni madogo ya yenye rangi ya bluu iliyokolea, na huweza kuonekana kwa wepesi zaidi ikiwa imechanua asubuhi tu, ikilinganishwa na mchana. Pia Huzaa juu na hata chini ya ardhi.

Image: Mr. Meena

Katika tiba asilia mmea huu una maajabu yake: na umekuwa ukitumika kwa miongo mingi kwenye baadhi ya tamaduni na kuleta matokeo katika tiba asilia ya mimea (Natural Herbs) ambazo nitakwenda kuziangazia hapa chini;

Sehemu Zinazotumika kama Dawa:

Majani, shina changa na mizizi yake; Ambapo mara nyingi hupondwa maji yake yakitoka au hukaushwa kivulini ‘usitumie yakiwa mabichi’

Matumizi Yake Kwenye Dawa Za Asili:

Haya ni matumizi yanayojulikana kwa tiba asili, kulingana na tafiti zilizofanyika kwenye baadhi ya tamaduni (Afrika na Asia) na tafiti hizo ni kwa tiba za mimea asilia pekee na sio kwa kwa utabibu mahospitalini au kwa ushauri wa daktari. (Zingatia: Kama una ugonjwa sugu muone mtaalamu wa afya).

Vidonda na Michubuko: Majani yake freshi hupondwa na kuwekwa kwenye kidonda. Unasemekana kusaidia kukausha kidonda haraka na kuzuia usaha kwa sababu una uwezo wa kupambana na bakteria.

Kuvimba na Maumivu ya viungo: Majani hupashwa moto kidogo kisha hubandikwa sehemu inayovimba. Wazee husema hupunguza maumivu.

Macho kuwasha na macho mekundu: Kwa baadhi ya jamii, maji ya majani yake yaliyochemshwa na kuchujwa vizuri hutumika kuosha macho” Hii inahitaji usafi mkubwa sana, usijaribu bila ushauri wa mtaalamu au mtabibu aliyewahi kujaribu kuyatumia.

Homa na Mafua: Chai ya majani yake hupikwa na kunywa kwa ajili ya kupunguza joto na kikohozi.

Matatizo ya njia ya haja ndogo ‘Mkojo’ na Figo: Mizizi yake kwa tiba ya Kihindi (Ayurveda) hutumika kutengeneza dawa ya kusafisha njia ya mkojo.


NB: Sehemu zingine kwa baadhi ya makabila hapa Tanzania, majani yake hupikwa na kutumiwa kama mboga ya kulia ugali kama ilivyo tu kwa ‘mchicha pori’ ikielezwa pia ni chanzo kikubwa cha vitamin mwilini.

JINSI INAVYOANDALIWA

Chukua majani yake freshi, kisha yaoshwe vizuri kwa maji safi, kisha yapondeponde hadi upate uji laini, kisha tumia kuyagandisha kwa nje au juu ya kidonda na ulipopata majeraha.

Au pia waweza kuyachemsha baada ya kuyachuma na kuyaosha kwa maji safi, kisha yakamue kwa chujio au kitambaa safi kisicho na nyuzinyuzi ili kupata juisi au ‘maji yake’ na tumia kama chai kutwa mara mbili.

TAHADHARI MUHIMU: Usitumie kwa kunywa ikiwa mabichi na hujayachemsha kwani huweza kukuletea ‘mzio’ (allergy) na usiyameze majani yake kwa usalama wa tumbo.

Pia: Kwa Wanawake wajawazito na watoto wadogo hawashauriwi kuitumia bila ushauri wa mganga au mtabibu wa dawa asili, Na kama kidonda ni kikubwa au kimevimba sana, nenda hospitali kwanza.

ASANTE KWA KUTUFUATILIA HADI MWISHO: Endelea kutembelea page hii ili kusoma pia Makala nyinginezo kwa ujuzi na maarifa zaidi. “Tuachie maoni yako, sehemu ya comment hapo chini’

Thursday, 10 September 2026

KIVUMBASI: Mmea asilia wa Maajabu katika Tiba

Image right: Earth Living

Mmmea uonao pichani unaitwa Mvumbashi au "Kivumbasi" kiswahili, Kihehe-lwenyi, ormanyunyukwai (kiMasai) Mzumbasha kwa wasambaa na wambugu (Lushoto Tanga), Wengine huyaita: Luvumbampuku, Kivumbani, Mrumbavasi-Upareni, nk. Lakini kwa lugha ya kisayansi (Scientific name) huitwa Tusli 'holy Basil' ukiwa na asili kutoka bara asia nchini India.

Mmea huu uotao kwa mrudikano wa kama kichaka (shrubs) kwa miaka kadhaa imekuwa ikitumika katika tiba asilia, na wengine wakitumia kama kiungo cha chai kwenye unywaji wao wa kila siku, na umetajwa kuleta maajabu makubwa katika kinga na kutibu maradhi mbalimbali katika mwili wa mwanadamu kwenye mazingira yao ya kila siku.

Tuangazie namna unavyotumika katika Tiba asilia:

Hutumika kama kinga ya kufukuza mmbu na nzi katika mazingira yetu na hivyo kutibu Malaria, lakini pia ukinywa juisi yake huelezwa kutibu degedege, ngiri, pia hukata ulevi kwa wanywaji pombe, pia hutibu maumivu makali ya tumbo (Tumbo la kukata/kunyonga) nk.

Kwa degedege la watoto: Unayaweka kwenye maji unayomuogeshea pekee, wengine humnusishia harufu ya majani haya ya Mumbashi:

Mvumbashi huwa na harufu (scent) flani hivi ambapo huponyesha kwa kuivuta tu, ila wengine huichemsha kwenye chai kama kiungo kwa harufu yake nzuri huongeza ladha ya chai.
Lakini pia ukichemsha yenyewe kwa kuchanganya na vifuatavyo hutibu maradhi kama:
 
1)-Kikohozi kwa watoto/mtu mzima.
Chukua majani yake yatwangwe changanya na maji ya vugu vugu kunywa kwa dozi ya 1*2.

2)-Homa ya Malaria
Majani haya yana antipyretic ambayo inaweza kutuliza homa kabisa na kuponesha malaria, Kama ni mpenzi wa chai chukua majani yake yasage kisha changanya na maji ya moto + asali kunywa kama chai.

3)-Kuhara na magonjwa ya tumbo
Majani hayo yana uwezo wa calming mfumo wa utumbo kwa kiwango kikubwa Sana.

4)-Kushusha sukari ya damu
Majani haya yanakinga ya saratani na cholesterol  na kwa watu wenye kisukari hasa wasiotegemea insulin (NID) majani haya yanauwezo mkubwa wa kushusha sukari na kuilinda pancreas inayozalisha insulin kutoharibika.

5)-Kiungulia cha moyo.
Majani ya Scent yamekuwa yakitumika katika kutibu kabisa tatizo la kiungulia, kikohozi, kuhisi mwili vibaya, maumivu ya hedhi, homa, malaria, shida ya kupumua, ukosaji choo, kukosa hamu ya kula, Kichefuchefu na kuboost moyo tiba hii unaweza iyaanda na kuitumia kwa njia ya kunywa kama chai.

6)-Kuongeza maziwa kwa mjamzito.
Chukua majani hayo zaidi ya 20 yatafune na mboga zingine za majani  yatasisimua mfumo wa utokaji wa maziwa kwa kiwango kikubwa

7)-Hufukuza mbali nzi na umbu, hii ni kwa kuyachoma majani yake, ule moshi wake mbu hulewa na kufa.

8)-Hupunguza nicotine inayopatikana kwenye sigara.
Kila baada ya kutumia sigara unachukua matawi kadha unatafuna ili kupunguza kiwango cha nicotine uliyovuta kwenye sigara.
Majani haya yanauwezo wa kupunguza mawazo Yani msongo wa mawazo, mawe kwenye figo.

9)-Hupunguza maumivu ya tumbo.
Majani haya ni zaidi ya vidonge vya aspirin au Panadol kutokana kuwa majani haya hayana side effects maana ni mimea asili.
Pia ni tiba ya kinywa na macho kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha vitamin A.

10)-Tiba ya kuwahi kukojoa na shahawa zisizo na afya ya kuzalisha.

11)-Tiba ya fugus 

Chanzo: 
Dr. William Mtanzania (Usa America) Kwa maoni ya wadau.
TAHADHARI: Matumizi yoyote waone wataalamu wakusaidie, vinginevyo ukiitumia ni kwa hatari yako mwenyewe na sisi hatutahusika kwayo. (It's for your own risk)
🙏 tafadhali like, share pia: comment kama unayafahamu na yanavyotumika ili wengine nao wapate maarifa uliyonayo. (Africa tuna kila kitu basi tu hatujikubali)

Thursday, 27 August 2026

MWANAMKE: KWANINI TALAKA HAIPASWI KUWA SULUHISHO LA MGOGORO JUU YA USALITI!

 

FIKIRIA: Mwanamke, unamuacha mumeo (Mwanaume wako) kwasababu ya usaliti, alioufanya kuwa na mwanamke mwingine, (Aah!)

Mna familia pamoja, mtoto mmoja" au wawili. (Ok!)

Hivyo, ukaomba talaka na mkatalikiana kwa sababu umeumizwa sana na usaliti wake na huwezi kuuvumilia! Na baada ya mchakato wa talaka kukamilika, ukaondoka na watoto wako! (Ooh!)

Ukaanza kufanya kazi kwa bidii ili ujipatie mahitaji yako na uwalelee watoto wako mweyewe bila kuonyesha kuhitaji msaada wa baba yao na kuzimudu gharama za maisha mwenyewe. (Good)

Ili kuendana na kuongezeka gharama za maisha, unaangukia kwa mwanaume mwengine ‘Labda tajiri) Hujali chochote maana unahitaji kulipa ada za watoto kama mwanamke unayejiamini na unajitegemea unahitaji kuuthibitishia ulimwengu unajiweza mwenyewe kwa yote ndio maana ukakubali kuwa na mwanaume huyo tajiri katika penzi la siri ingawa unafahamu ni mume wa mtu. (Unajikuta umerudia kosa lilelile lililofanya nyie kutengana kwa talaka)

Hatimaye sasa na wewe umekua mchepuko kwa mume wa mtu, tena mwenye familia yake na watoto pia (side chick to cheating situation)

Ndipo unakumbuka na unaanza kufikiria kuhusu mwanamke wa pembeni aliyekua naye mumeo, na kwa nini alikua naye! “Umechelewa’ Nda yako haipo tena!

Ulichofanya, ndicho alichokifanya mwanamke uliyemfuma na mume wako, hukufikiria kuhusu maadili, na unaanza kumuelewa taratibu: Pengine alikuwa na mume wako kwasababu ya ugumu wa maisha, wingi wa majukumu, watoto aliotelekezewa wa kuwalea! Na zaidi tumbo linalohitaji chakula kila siku.

NA SASA: Kama yule tu, unatamani hata kumpigia mwanaume wa sasa uliye naye, lakini huwezi sababu unatambua yupo na mke wake na familia yake nyumbani, na wewe unalinda nafasi yako kwake maana mkewe akigundua hawezi kukimbilia kuachana zaidi wewe ndio utaachika. “Mateso yanarudia tena upya”

Hivyo amekupa masharti yake ambayo utake usitake lazima uyafuate, na unapaswa kuheshimu faragha yao kuwa sasa yupo nyumbani na familia yake na wewe utaendelea kuwa option-tu, Linapokuja swala la Kupunguza mawazo na tamaa zake.


Unafikiria tu kuhusu maumivu yako!

Unafikiria tu kuhusu faraja (Consolation) yako!

Ila walau awali ulikuwa na mume wako pekee yako’ Ndio alikusaliti lakini bado aliendelea kuwa wako!

Hatimaye unajaribu kutafuta tena kufahamu juu ya yanayoendelea kwenye maisha yake baada ya kutalikiana na kila mmoja kushika maisha yake, unang’amua sasa ame ‘move-on’, na tayari anaishi na mwanamke mwingine pengine mdogo kiumri au mrembo kukuliko wewe.

Unakaza roho, kwakua mawasiliano yake bado unayo unaamua kupigia na kumuomba miadi ya kukutana sehemu kuongea kwa kigezo cha watoto wame-mmisi wanataka aje kuwatembelea, kweli anafika na kuwaletea vizawadi watoto na kukuachia pesa kidogo ya matumizi ya watoto, lakini haitoshelezi kama ilivyokuwa zamani. (Mke mpya ameshikilia matumizi yake yote)

Mnapanga kutoka matembezi kidogo, mnakumbushiana wakati mzuri mliokuwa nao zamani na hamadi-bila kutarajia, na ngono mnashiriki! Kwa muda mchache unasahau taabu na dhiki na upweke uliokuwa nao wote!

Punde, mmemaliza kila kitu anakuaga kurudi kwa mkewe anapiga simu, ghafla unagundua sio wako tena na dhiki, taabu na upweke unarudi kama ulivyokuwa siku zote!

NDIPO: Unagundua sasa unahusiana ‘dating’ na wanaume wawili tofauti, ambapo wote wawili wamewasaliti wake zao na wewe ndio sababu!

Ghafla unaikumbuka ndoa yako, uhuru uliokuwa nao ukiwa na mume wako wa ndoa, kisha unagundua ni kama dunia nzima imekugeukia na maisha hayako sawa kwako!


Unaweza kudhani hii ni stori tu, lakini kuna wanawake wanaoiishi kiuhalisia, na ninge’ au ningalijua huja baada ya kuwa tukio lishatokea. Siungi usaliti ndoani, Lakini pia siungi vitendo vya ukatili ndoani" Mninukuu vizuri!

Mbali ya tofauti zetu, familia ni baba na mama na sio mzazi mmoja, licha ya changamoto zilizoko ndani ya familia hizo.

Asilimia kubwa ya ndoa zinawaka moto, na sio salama kwa asilimia mia, (Ni kusameheana na kuvumiliana) Tafakari chukua hatua!

#MwalimuMeena (0778291375) Kwa Maoni, au Unahitaji ushauri wa ndoa nipo hapa kukushauri!

Unaweza kusambaza elimu hii: (Share) iwafikie wengi zaidi, lakini (usi-copy na ku-paste) na kufanya kama ni chanzo cha mawazo na Sanaa yako) ukifanya hivyo nipe credit yangu katika chapisho lako. Asante!

 LINK INTO ENGLISH VERSION: ReadMore

Monday, 24 August 2026

NINI HUTOKEA, MAUMIVU TUMBO LA HEDHI KWA WANAWAKE?

Picha: JohnsHopkin Health Blog


Kuingia hedhi ni jambo la kawaida kwa kila binti/msichana aliyepevuka itoshe kusema "Ni jambo la kujivunia" kwakuwa hedhi ni kipimo sahihi cha kuwa Mwanamke ambaye siku za usoni utatarajia kuitwa mama; na ikiwa binti huioni hedhi yako inapaswa kuwaona madaktari mapema kutibu na kushughulikia tatizo hilo haswa kwa wasichana waliokatika umri wa kuvunja ungo (kupevuka)

Nini hutokea wakati wa hedhi!?: Kibiolojia hedhi hutokea baada ya kupita zile siku za urutubishaji wa yai (Ovulation circle) ambapo hii hutukia wiki ya3 kwa wanawake wengi wenye mzunguko wa siku21, 28 na 31.

Wakati huu, Yai ambalo halijarutubishwa (kwa kukutana na mwanaume) hutolewa kutoka kwenye ovari za mwanamke kwa mfumo maalimu wa mwili (kuflashi) na hapo muhusika huweza kuona uchafuuchafu wa kawaida, na damu kwa muda wa siku2, 3 au 4, huku wengine wakienda mpaka wiki moja (siku7) ambapo hii watabibu wengi huieleza kuwa sio nzuri sana kiafya, ila kikawaida inatakiwa siku4 iwe imekata.

Ni wakati huu wa hedhi: Wanawake wengi hupitia madhila mbalimbali yakiambatana na #maumivu_makali chini ya kitovu, kuumwa na kiuno na mgongo, kichefuchefu, kukosa hamu ya kula na kutapika.

Nikiwanukuu baadhi ya kina dada wanasema:

"Mimi staki kuongea maana nahesabu siku tu nianze kuhangaika daa mungu sijui sababu zake lakini kwakweli ata ukielezea akuna atakaye kuamini";

"Maumivu ya tumbo + kiuno + kichefuchefu + kutema mate kama mjamzito, eee Mungu tusaidie sisi";

LAKINI SULUHISHO AU TIBA YAKE IPOJE?
Hakuna tiba maalumu ya changamoto hii, maana wengine hutumia dawa za asili (mitishamba) na wakapona, wengine hutumia tiba-lishe wakapona, Wengine dawa za hospitali za kutuliza maumivu wakapona.

Nikiwanukuu wadau kadhaa (wanawake) wenyewe husema:
  1. "Tunywe Maji Ya Karafuu, Ikifika Siku Wala Tumbo Haliumi"
  2. "Chai ya moto yenye mchanganyiko wa tangawizi, karafuu, mdalasini, hiliki inanisaidia sana"
  3. "Ikianza tuu day one chemsha mizizi ya mkunde pori kunywa ila hii #kupata_mimba ni nje nje inasaidia na tatizo halijirudii me nshasahau hzo mambo za kuumwa tumbo baada ya kupata ujauzito na kujifungua"
  4.  "Kpindi Cha ubinti wangu nilikuwa naumwa mnoo yaani hadi home walikuwa wanajua, lakini tangu nijifungue mwanangu siumwi tena na chochote yaan"
  5. "Tumbo la P, mdogo wangu alikuwa anaumwa mpaka anazimia... Ila tulijitajidi kumchemshia #mzugwa mara nyingi tuwezavyo sa hivi anaumwa ila cyo km zamani"
Liziki Nambale anasema: "Mimi nimeponea majani ya Mbaazi" Nakama unaumwa siku nyingi inasaidia kukata hedhi kama unaumwa siku kuanzia saba kwenda mbele au hedhi isioleweka yaani kama huna tarehe maalumu chukua hayo majani matatu ya mbaazi, yaoshe utafune mabichi, na kwamanuizi kua: Mfano-nataka kuumwa siku tatu kama aya majani utaumwa ivyoivyo" Maajabu haya ya M'mbaazi.

Wengine hutumia dawa za Hospitali za kuondoa maumivu, huyu anasema: "Unaweza ukatumia piroxicam Mana ni dawa ya maumivu ila dawa nzuli na yenye nguvu ni #hyocine au ibrufen wengine wanatumia ata mifenamic acid au Vivian au hata paracetamol.

KIPI HUSHAURIWA: Wataalamu wa dawa mbalimbali, na watabibu wa afya hushauri kila tiba au dawa inaweza kuwa na side-effect (Madhara) endapo isipotumiwa kwa usahihi, au dawa kukataana na mgonjwa husika.

Mfano: kuna dawa hazishauriwi kwa wanawake ambao wanamzio wa chakula flani, dawa au harufu fulani kama ya pafyum, marashi nk.

Hivyo: kila dawa unayotaka kutumia uwaone wataalamu wakupe njia sahihi za matumizi.

ONYO: Njia yoyote utakayotumia hapa ni kwa hatari yako (risk of your own) hatutahusika kwa madhara.
🙏 Asante kwa kutufuatilia, na tafadhali Like page hii: https://www.facebook.com/stewart.meena na utu - Follow, ili kusoma na kupata habari, na makala nyinginezo za kuvutia kama hizi.

Wednesday, 19 August 2026

ATHARI / MADHARA YA KUKAA NA HAJA NDOGO KWA MUDA MREFU

Image by: Harbin Clinic


Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji-taka mwili, haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili 'kuwa kibofu chake kimejaa.

Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wafanyavyo kimazoea kitu ambacho hakishauriwi kitabibu na kwa afya ya mwili wako.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia katika milo yetu kila wakati, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, unaojitengeneza wakati vyakula vinachaguliwa (Kuchakatwa) na mwili, hivyo mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huyo husika huanza kuhisi hitaji la kwenda haja ndogo (kukojoa).

Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo.

Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.

Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda haja ndogo mara kwa mara husababisha uwezo wa kibofu chake cha mkojo kushindwa kujitawala upotee.

Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake.

Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection), kama vile U.T.I (Urinary Tract Infections), na pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, (bacteremia).

Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.

Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na haja (mkojo), hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya..

Monday, 17 August 2026

ELEWA CHANZO CHA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI (KIDNEY FAILURE)

 

Picha na: Ahli Hospital

FIGO ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu. Wiki iliyopita nilieleza jinsi kiungo hiki kinavyopata mawe na jinsi ya kujikinga na tatizo hili.

Chanzo: Global

Nashukuru wengi wamepiga siku kushukuru kwa elimu ile. Kwa kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu za chini.

Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.

Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.

Kazi nyingine za figo ni kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili, husaidia kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika utengenezaji wa chembe nyekundu za damu, husaidia uzalishaji wa vitamini D na husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).

Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika mwilini.

Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu zifuatazo;

Hatua ya kwanza ni UCHUJAJI.

Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi midogo ya damu iliyojizungusha pamoja.

Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa kwa ajili ya uchujaji zaidi.

Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.

Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo, husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo kama ureta.

Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye mrija wa urethra.

Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na kutengeneza mkojo.

Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.

Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi yafuatayo, Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF), Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency) na tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure).

Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF) Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika damu.

Hali hii huwapata karibu asilimia 5 ya wagonjwa waliolazwa hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa ICU.

SABABU ZAKE

Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu: Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure), matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure), matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/ failure)

Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika figo (Prerenal causes/failure) Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka 70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake  ipasavyo. Mambo yanayoweza kusababisha pre-renal failure ni pamoja na:

Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi, kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia), kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya: Kushuka kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha shinikizo la damu, kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo.

Figo inaweza kufeli pia kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwa shinikizo la damu na ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.

Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.

Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.

Visababishi hivyo ni pamoja na: Magonjwa katika mishipa ya damu, kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo, ajali/ Kuharibika kwa tishu na seli za figo, magonjwa ya mzio katika glomeruli na figo kwa ujumla (glomerulonephritis).

Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi (infection) ya bakteria jamii ya streptococci.

(More: Here Endelea kusoma hapa)

Wednesday, 15 February 2023

BAADHI TABIA HATARISHI ZINAZOFANYA MTU KUTOKUELEWEKA KATIKA UHUSIANO.

Image copyright: fakazanews

 Na. Stewart Meena

Mahusiano siku hizi za karibuni yamekuwa na chagamoto nyingi sana kiasi kwamba Watu wanapoingia katika mahusiano (Uchumba) inakuwa kama kila mmoja ana mashaka na mwenzi wake kuwa je ana malengo ya kufanya maisha pamoja ama yuko kwa sababu ya jambo Fulani na anapita tu baada ya muda hudai kuachana.

Kisaikolojia: Mwanamke hupenda kwanza kasha mengine hufuatia baadae, tofauti na Wanaume wao hutamani kwanza kasha kupenda huja baadae “Yaani kupenda kwao hutokea ndani ya huo uhusiano, alikotamani kwanza” na hapa ndipo bahati mbaya kwa Wanawake huwaona Wanaume zao kama hawaeleweki, lakini pengine Wanawake hawa wameshindwa kuchunguza mambo ambayo Mwanaumeze wake hupende, kasha aishi humo na baadae kueleweka na kupenda kwa Mwanaumehuja tu moja kwa moja (Automatic)

Tabia za mwanaume zinazochagizwa na kuwa na mwanamke kwa kumtamani kwanza ndio hupelekea mwanamke husika amuone mwanaumw wake ‘Haeleweki’ kasha hujikuta amefanya maamuzi ya kumuacha Mwanaume wake, na kwenda sehemu nyingine, mpaka pale atakapopata huyo anayedhani kwake anaeleweka".

Bahati mbaya ni kuwa kwa kutokufahamu kwake, tatizo halipo hapo kwa (Mwanaume wake haeleweki) ila lipo hapa kwenye kufahamu Mwanaume wake nini anapenda kutoka kwake kwenye hayo mahusiano, na ni vipi mwanamke huyo ajiweke vile ambavyo mwanaume wake anavyopenda ili kutengeneza Uhusiano imara na wenye kuzaa matunda ya ndoa na Familia.

Kimsingi: Ulishawahi kusikia Kauli Kama hizi Kwa wanawake, wakisema mwanaume Yule haeleweki, Mpenzi wake haeleweki, au hata wale walio kwenye ndoa utasikia pia wanasema Mume wake haeleweki, mchumba wake haeleweki nk.

Nachotaka kuwakumbusha Wanawake na Wanaume ni kuwa: Mwanaume hutamani kwanza kasha kupenda huja baadae; na Mwanamke hupenda kwanza kasha kutamani kuwa na huyo mwanaume huja baadae, ‘Ndio maana wahanga wakubwa wa hii KUTOKUELEWEKA’ ni wanawake zaidi ya wanaume sababu tayari wameingia sehemu kwa kupenda kwanza, na walicho kitegemea ni tofauti sana na wanaume zao walichokiwaza.

WANAWAKE WASEMAPO ‘Mwanaume haeleweki’ HUMAANISHA HAYA YAFUATAYO:

-    Mwanaume ameshindwa kumfanya ajione yupo pekeake moyoni mwake, na pia hana uhakika yeye ndio utaolewa.

-     Mwanaume kutoa mara kwa mara zisizotimilizika, Wanawake hupenda kuwajaribu wanaume zao kwenye ahadi wawapazo.

-    Mwanaume kuficha chanzo cha kipato chake kwa Mwanamke wake, na hivyo kumfanya Mwanamke wake kushindwa kujua siku Mwanaume wake akiwa na pesa ama asipokuwa na pesa, hivyo anakuwa hana uhakika na huduma atakazozipata pindi atakapoolewa.

-    Mwanaume kuficha shughuli azifanyazo, kuficha ndugu zake, marafiki zake kwa Mwanamke husika kwa kutokutaka mwanamke huyo atambulike kwao,na kumwambia sio wakati sahihi kutambulishwa, kwa kuwa bado ana hofu ya kutambulisha kasha baadae kuachwa solemba hivyo ni kama na yeye anatega-tega hivi.

-    Mwanaume anayepoteza kumbukumbu za matukio muhimu kwa mwanamke wake, hupelekea kutoeleweka na mwanamke husika hushindwa kuelewa wanathaminiwa na kupendwa ama laah. “Wanaume wanaopoteza kumbukumbu hasa zile za muhimu kama birthday zao, Ahadi wazitoazo nk, Mwanamke hufikiri Mwanaume wake hamjali.

Image: ThePrint


HIVYO: Katika mahusiano (Uhusiano) Mwanamke anahitaji kwanza ‘Life Security’ kama ‘Kuthaminiwa, Kupendwa yeye pekeake, kuhudumiwa mahitaji yake mbalimbali, Kutunzwa au kupewa kipaumbele kwanza na (Kudekezwa – Hii ipo kwa wote wawili).

WANAUME: Kadhalika, hupendelea kufanyiwa yale wawafanyiao wenza wao, na wasipofanyiwa huanza kuwa na mashaka na sehemu waliyoko na kukaa nusunusu (Kwa mashaka) na kuwaza kuachana muda mwingi sababu tunaishi kwenye Dunia ambayo kuachana imekuwa ‘Faheni’

WANAUME WASEMAPO ‘Mwanamke haeleweki’ HUMAANISHA HAYA YAFUATAYO:

-    Mwanamke kushindwa kumfanya mwanume ajione yupo pekeake kwako, na hata iweje huwezi kumsaliti kwa wengine sababu unafaa kuaminiwa na ni mwanamke unayejiweka mbali na mambo ya anasa kama Pombe, Starehe, kwenda club nk. Lazima Mwanaume wako asikuelewe sababu mazingira kama hayo kumsaliti ki tendo la dakika1 tu.

-    Mwanamke, kutamani kila jambo zuri ufanyiwe wewe tu, na wewe huna hata siku moja unayotamani kumfanyia mwanaume wako mambo hayo mazuri wewe unayotaka ufanyiwe. Mfano: Kutafutwa kwa simu, wewe ndio utafutwe tu, vijizawadi wewe ndio upewe tu, kusifia wewe ndio usifiwe tu, birthday wewe ndio ikumbukwe tu na ufanyiwe, khaa! Kwani yeye sio mja (Binadamu!?) Lazima mwanaume wako ahisi hufurahii yale ambayo anakufanyia.

-    Mwanamke kufuja fedha, yaani wewe hujui kama kuna kupunguza matumizi yasio ya lazima sana, hujui ‘kuSave’ kwa ajili ya kesho au maisha yenu ya siku zijazo, wewe kila siku ni kuitisha vitu tu vya gharama, badala ya kupika mle nyumbanikila siku unataka mitoko ya hoteli kubwakubwa-, sawa utapewa yote hayo lakini mwisho wa siku mwanaume huyo utamuona haeleweki kwako, punde akishakutumia. ‘Wanaume hupenda na hutulia kwa Wanawake wanaoifikiria kesho yao’

-    Kama ilivyo kwa Wanaume, Mwanamke kuficha kipato chake, kushindwa kumsaidia mwanaume wake hata kwa mambo madogo-madogo, lazima taa nyekundu iwake kichwani kwa Mwanaume husika “Yaani Mwanaume anaweza kukwambia hata kwa kukutega-naumwa, sina hata pesa ya kwenda kupima, na wewe kwa kujitutumua unamwambia ‘Pole utapata, badala ya kumwambia ngoja tufanye maarifa, au nna elfu5 hapa tafuta ya kuongezea, au ngoja nikuletee paracetamol utilize maumivu nk. Mwanaume lazima akuone hueleweki na mwishowe hutafuta huyo atakayeeleweka.

HIVYO: Katika mahusiano (Uhusiano) Mwanaume kamailivyo kwa Mwanamke, naye anahitaji kwanza ‘Love Security’ tofauti na Mwanamke anahitaji kwanza (Life Security), kama ‘Kuthaminiwa, Kuonyeshwa anapendwa pia, kutekelezewa huduma na mahitaji yake mbalimbali ya msingi, Kupewa kipaumbele kwanza kabla ya ndugu zako na marafiki zako, na zaidi kumsikiliza kwa yale anayotaka ufanye na yale asiyoyataka usifanye. (Wanaume hupenda sana kusikilizwa na kupewa nafasi ya kuwa kiongozi wa uhusiano wenu, na sio kupandwa kichwani n.k).

WANAWAKE: Huwaelewa wanaume wanaotimiza ahadi hasahasa ahadi ndogondogo kwani kupitia kutimiza ahadi kunamfanya akuamini na azidi kukupenda, yaani ni Bora usimuahidi jambo lolote kuliko utoe ahadi ambazo utashindwa kuzitimiza, jambo ambalo yeye analichukulia Kama Deni.

Fikiria: Unapenda mwenza wako akufanyie nini, hivyo upendavyo vivyo hivyo Mwanza wako naye hutamani wewe umfanyie hay ohayo “Na ukimfanyia atafurahia vile ambavyo wewe ufurahiavyo”

MWISHO: Wanaume wenye kufikiria kutumia mabavu, Maneno machafu, makali au Kauli za vitisho na Kuhisi mabaya kwa mwanamke wake, “Mfano, kumwambia – Unachepuka eeh, ondoka kwenu, nitakupa talaka, nitaongeza mke mwingine n.k” huwanyong’onyeza wanawake husika na kujiona hawako sehemu sahihi, sababu Wanaume wanachopaswa kufahamu ni kuwa “Wanawake huamini maneno zaidi kuliko hata matendo” yaani Kadiri unavyomtisha mwanamke wako unamtengezea mazingira ya kujihami na kujiandaa Kwa lolote ‘Kuachana, Kuchepuka nk’.

Kama ilivyo kwa Wanawake, Wanaume pia hawapendi kuishi na mtu wasiyemuelewa, kwani kila mmoja hufikiria usalama wake kwenye huo Uhusiano, hufikiria kumpata mtu sahihi wakufanya naye maisha na atakaye mthamini katika wakati wa shida na raha hadi umauti umfike mmojawapo.

Tafadhali, uchukuapo na kunakili makala tambulisha na blog hii: Saysteefeatures.blogspot.com" asante; Share Makala haya na Wengine wapate kuelimika zaidi kuboresha mahusiano yao.

Source: (Msaada wa Mitandao Washirika)

Tufuatilie Mitandao ya Kijamii:

Facebook: www.facebook.com/stewart.meena

Instagram: @ Master The Last

Friday, 2 July 2021

FAHAMU: FAIDA LUKUKI KIAFYA KUWEKA KITUNGUU MAJI KWENYE UNYAYO WA MIGUU

Na: StewartMeena

Wengi tunafafamu kitunguu maji, (pichani) lakini bado wengi wetu hatufahamu faida zake nyingine, ambapo pia kitunguu maji hicho huweza kuwa tiba au dawa vilevile ambayo hukupatia afya bora, kukuondolea uchovu wa mwili, kupambana na kuondoa bakteria mwili pamoja na kupandisha kinga ya mwili.

Kama, tujuavyo: ulaji wa vitunguu maji haswa vikiwa vibichi kwa kachumbari, inashauriwa sana na wataalamu wa Afya walau kutumiwa kwenye kila mlo wako wa siku itakusaidia sana katika kuuzuia mwili wako kushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile, homa, mafua "flu" kifua kubana, kuondoa harufu mbaya mdomoni, kupandisha kinga ya mwili kwa kuzipa nguvu seli nyeupe na nyekundu za mwili kupambana na maradhi hayo.

HEBU LEO TUANGAZIE FAIDA NYINGINE ZA KITUNGUU HICHO ENDAPO KIKIWEKWA KWENYE UNYAYO WA MIGUU NA KUBANWA NA SOKSI KISHA KULALA NACHO USIKU MZIMA MIGUUNI: Msomaji, je! unafahamu chini ya miguu yako kuna neva (mawasiliano) "meridians" nyingi tofauti zinazopeleka mawasiliano kwenye sehemu mbalimbali kwenye kila kiungo cha mwili wako "ndani na nje ya mwili" (zaidi milango6 ya fahamu) viungo vya ndani ya mwili wako, kamavile: figo, maini, ubongo, kibofu cha mkojo, moyo nk!?
ANGALIA KUHUSU: (FootReflexology )

Ndio fahamu hilo, kwasababu chini ya unyayo wako kumefanyizwa mishipa mbalimbali ambayo hupeleka mawasiliano ya moja kwamoja kwenye viungo vya ndani ya mwili wako na nje pia, na ndio maana chini ya unyayo, inaelezwa pia na wataalamu kuwa huwenda ndipo sehemu pekee yenye hisia mchanganyiko kubwa kwa mwanadamu..endapo ikipapaswa au kuminywaminywa na inapaswa kuwekewa uangalifu na umakini mkubwa zaidi.

Mfano mdogo, ikiwa ubongo wako umechoka, unamaumivu ya kichwa "kipandauso" au una unauchovu wa mwili Fanyiwa masaji "massages" maeneo hayo ya miguu kwa kukandwakandwa na barafu au maji ya ubaridi, halafu uone, majibu utayapata kwa mwili wako kusawijika au kuwa sawa na ubongo wako kuwa-active.

Hivyo: sambamba na hayo kitunguu maji pia huweza kutumiwa kuamsha_hisia za viungo tofauti vya mwili stimulation" na kuvifanya vifanye kazi zake kwa ubora na kiwango kilichokusudiwa kiafya.. JE! HII IPOJE!?
Mfano kwa kushusha Homa: OnaHapa Kwanza: FAIDA 

Hivyo: MATUMIZI: Chukua kitunguu maji, kikate vipande mviringo kisha viweke chini ya unyayo wako, lala nacho mpaka asubuhi Majimaji yake yatakusaidia kiafya kurekebisha mfumo wa mwili wako na kupandisha kinga mwili yako kupambana na maradhi mbalimbali, lakini pia kukuondolea harufu mbaya ya miguu.

"Kwa wale wenye miguu inayotoa harufu sababu yamiguu kutoa jasho" Fanya hivyo mara1 au mbili tu kwa wiki:::: kwa msaada zaidi watafute wataalamu wa TibaLishe waulizie manufaa zaidi ya kitunguu maji katika mwili, na matumizi sahihi ni yapi.

TAHADHARI Kila chenye faida kina hasara, uangalifu unapaswa kuchukuliwa; Isipokuwa matunda, viungo au dawa-lishe hizi, hazina madhara sana kwa mtumiaji ukilinganisha na mitishamba.

Hivyo katika matumizi yake, kitunguu hiki hakipaswi kutumiwa zaidi ya mara1, na pia kikishakatwa kilichosalia kisitumiwe sababu kinaweza kutengeneza bakteria sababu ya uchachu-asidi wake.. hivyo vitunguu vizuri ni vile vilivyo-"fresh" tu.

(Kwenye makala zijazo, nitachambua, Maajabu na ni kwavipi mguu unaweza kutumiwa kuamsha hisia za kufurahia tendo ktk mahusiano) Kupata makala kama hizi, tafadhali LIKE PAGE yetu hii (History And Amazing Things) inayopatikana kwenye facebook: Kisha Share ili na wenginge wapate elimu, na maarifa uliyoyapata wewe kupitia kusoma hapa kwenye blog hii.

Monday, 24 August 2020

JE! WAIFAHAMU AFYA YAKO KUPITIA RANGI YA MKOJO (Urine Colour)?

 

Picha kwa hisani ya mtandao (Google search)

Na Stewart Meena

Je unafahamu ya kwamba rangi ya Mkojo wako (Ashakhum sio matusi nitatumia jina lake halisi badala ya kupunguza ukali wa maneno kusema  "haja ndogo" ili tuelewane) inakupa matokeo sahihi kuhusu hali ya afya yako?

Lakini pia wajua maji ndio afya yako! Kwa sababu asilimia kubwa ya ufanyizo wa mwili wako ni maji (Yaani damu+maji) na asilimia 25% ni mjumuisho mwingine kwenye mwili wako, mfn. Nyama za ndani na nje nk.

Kama jibu ni hapana basi "MAKALA HII" inakusu wewe moja kwa moja; Kwani rangi ya mkojo kwa mujibu wa watalamu wa afya kupitia mahojiano mbalimbali niliyoyafanya na madaktari na wataalamu wa tiba za asili, pamoja na tafiti zangu zingine nlizozifanya kwa kuandika, au kusoma vitabu na majarida mbalimbali yahusuyo Afya:

(Nikiwa Fani yangu ni Mwandishi wa Habari)

Nimekuja na majibu kuwa kupitia Rangi ya mkojo wako unauwezekano mkubwa na ndio kipimo sahihi kinachoweza kukupa ukweli wewe juu ya afya yako, kuweza kujua dalili za awali kabla hata ya kwenda kupima maabara au kufanyiwa uchunguzi wa vipimo na daktari.

Ndio ili daktari ajue wewe unaumwa nini, au niugonjwa gani unakusumbua kwa wakati huo "ukiacha scanning na kupigwa picha ya X-rays" Daktari huitaji kupima damu yako kwa matatizo ya nje ya mfumo wa tumbo lako au kupima haja ndogo (mkojo) na (haja kubwa) ili kujua matatizo ya ndani ya mfumo ulioko tumboni mwako.

Asilimia takribani 75% kwa 25% ya mwili wako ni maji, damu na nyenzo mwili nyingine, na vyote hivi hufanya kazi kwa pamoja katika kuendesha maisha ya muhusika na ikiwemo mwili kujitengenezea kinga yake ya kutosha na muhusika kuishi kwa afya bora.

Naposema matatizo ya ndani ya mfumo uliopo tumboni (namaanisha magonjwa ambayo tunayahisi kupitia eneo la tumbo letu) Kama vile, maumivu ya tumbo na yanayoweza kuambatana na vichomi vya mara kwa mara, ambayo haya huweza kusababishwa na maradhi-mwili kadhaa ya mfumo huo kama vile typhoid, amoeba, Vidonda vya tumbo, matatizo ya figo na ini, Safura, kansa ya utumbo, Chango na ngiri nk.

HEBU NA TUJADILI SASA UTAMBUZI WA AFYA YAKO KUPITIA RANGI YA MKOJO.

Maelezo Mengine Kwa kina:

HAPA

Picha kwa hisani ya mtandao (Google search)


Kwa kawaida mkojo tuutowao una rangi mbalimbali (pichani) zenye majina yake kufuatana na rangi au muonekanao wake, Na hiyo huchagizwa na mazoea ya mtu kuijali afya yake au kuipuuza afya yake kwa kujua au kutokujua.

(Ndio mbona uvutaji wa tumbaku au sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako, na imeandikwa hivyo lakini bado watu wanakunywa pombe kupitiliza na kuvuta tumbaku!?).

Sawa, sasa na hebu tuanze  kuzichambua rangi hizo (Pichani) na ZINAVYOASHIRIA KWENYE AFYA YA MWILI WAKO.

No1. (Transparent)

Mweupe kabisa au Mkojo usio na Rangi ya mkojo (Light yellow): Inaashiria Unakunywa maji mengi sana, na sumu iliyoko katika mwili wako inasafishika vyema, Kwani figo yako kwa msaada wa maji mengi mwilini huchuja sumu na taka mwili vyema kwa kutenga virutubisho mwili na taka-mwili.

Kiafya, mkojo wa rangi hiyo (Nyeupe kama maji) sio mzuri sana na huweza kuwa kwenye mwili wako kuna kasoro fulani au mmeng’enyo na huenda uchakataji wa virutubisho na kuondoa sumu mwili haiko sawia kwako (balanced)

KIAFYA: Binadamu anapaswa kunywa walau glasi 8 za maji kwa siku hadi lita mbili, na sio pungufu kwa faida za kiafya, hivyo kunywa maji pia kupitiliza huleta matokeo mengine tofauti kiafya.

Hivyo unashauriwa, utakapoona mkojo wako hauna rangi ya mkojo yani unatoka mweupe kama rangi ya maji hapo Kiafya kuna jambo haliko sawa (balanced) kwa hivyo unatakiwa aidha kupunguza kidogo unywaji mwingi wa maji au kuzingatia ulaji sahihi vya virutubisho mwili (balance-diet)

No2. (Lemonade) Hiyo ni Excellent / great / better / Very good

Manjano isiyokoza (Light yellow) inaashiria  unakunywa maji ya kutosha, afya yako iko vizuri na imara, hauna matatizo yoyote hivyo endelea kufanya unacho kifanya kwa kula vyakula "balanced-diet", kula matunda na kunywa maji mara kwa mara.

KIAFYA: Wewe unashauriwa ushikilie hapo hapo katika utaratibu wako wa maisha ya kila siku "life style" kwani mwili wako unajiendesha vyema.

Ili Kupata matokeo haya: Unapaswa kula vyema vyakula vyenye virutubisho mwili vyote (Wanga+Protini+Vitamini) ikiwemo na matunda kwa kuzingatia ulaji sahihi (Balance diet) pamoja na unywaji wa maji mara kwa mara hata pasipo kuhisi kiu (isipungue glasi 6-10 kwa siku)

No3. (Light like a beer)

Majano isiyokoza (yellow) yaani rangi halisi ya mkojo, inayokaribia kufanania na rangi ya asali na isiyotoa harufu kali, inaashiria afya yako kwa wakati huo haina matatizo yoyote na unazingatia ulaji mzuri wa vyakula na unaupenda mwili wako, #Isipokuwa tatizo lako ni kuwa sio mnywaji mzuri wa maji ya kutosha vyema hivyo mwili wako hauna maji ya kutosha.

KIAFYA:

Ukiona hivyo hupaswi kuwa na wasiwasi, kwani kwa unywaji wako mdogo wa maji bado mwili wako unajitengenezea maji ya kutosha pengine kutokana na aina ya vyakula uvilavyo pia.

Isipokuwa unashauriwa tu kuongeza unywaji wa maji zaidi kwa siku kabla ya kula na baada ya kula unatakiwa usubiri angalau dakika20-30 hata kama hauna kiu ili kurahisishia figo yako ufanisi wake zaidi.

No4 (Amber) that is Bad/Warning

Manjano iliyochanganyika na uKijani kwambaali (Amber) Inaonyesha mwili wako upo upo "kawaida" na una afya ingawa si mnywaji wa maji mengi na unasubiri hadi uhisi kiu ndio unywe tena kidogo ndio maana unapokojoa mkojo hutoka na harufu kali, hauzingatii ulaji wa virutubisho-mwili sahihi (yani wewe hauli balance-diet kwa kuegemea aina ya vyakula fulani pekee na mara kwa mara, haswa vile venye rangi ya uKijani kama mbogamboga na matunda" (mwili unatengeneza vitamini na wanga pekee), ila kwa uchache unywao Mwili wako una maji ya kutosha.

KIAFYA: Ukiona hivyo ni ishara ya tahadhari au onyo mwili wako unakupatia ujumbe kuwa kuna kitu au jambo haliko sawa mwilini mwako hivyo yakupasa ubadili mfumo wako wa maisha mara moja; pia unatakiwa uzingatie unywaji wa maji hata pasipo kuhisi kiu, pamoja na kula kwa kuchanganya vyakula vyenye kuupatia mwili wako madini ya protini kwa wingi na Vitamini-C.

Protini inapatikanaje!?

Hii hupatikana kwa kula vyakula kama Nyama nyekundu (Ng'ombe, mbuzi nk) pamoja na vitu kama Maharagwe, samaki, maziwa nk.

No5 (Very bad / Worse)

Manjano iliyochanganyika na nyekundu au rangi ya udongo (Brown) isiyo na harufu kali ya mkojo na yenye harufu kali au ya wastani, Inaashiria Upo kawaida tu ila mashakani, sababu wewe kwanza si mywaji wa maji, pili hauzingatii ulaji sahihi wa chakula na pengine hauli kwa muda sahihi pia na upo hatarini kupatwa na Vidonda vya tumbo (ulcers) Tatu, kuna aina ya kemikali unazokula au kunywa na kusababisha mwili kukaushwa maji yake kwa wingi zaidi.

KIAFYA:

Kunywa maji ya kutosha kwa siku mbili au tatu, na kama hali ikiendelea hivyo yakupasa umwone daktari upesi kwa vipimo vya mkojo wako kujua kama una UTI, baikteria mwilini waletwao na unywaji wa maji machafu "typhoid" nk.

LABDA NIELEZEE HAPA KIDOGO:

Kuna aina ya vinywaji na vyakula tunavyokula ambavyo huweza kufyonza maji-mwili kwa wingi zaidi au hata kazit unazozifanya kwa kupata mkate wetu wa kila siku.

Mfano kazi za kutumia nguvu sana, kukaa karibu na moto kwa muda mrefu zaidi, kufanya kazi viwandani haswa vile vyenye kutumia nishati ya umeme au moto na makaa ya mawe nk.

Kutembea kila siku umbali mrefu tena juani kwenda na kurudi; kubeba mizigo mizito nk inafyonza sana maji mengi mwilini.

Ukiwa mpasuaji mbao kunywa maji yakutosha, ukiwa unafanya kazi ya upishi hakikisha unakunywa maji ya kutosha tena mara kwa mara, ukiwa fundi ujenzi, makenika, injinia, dereva, mbeba mizigo mizito, mfanyaji mazoezi mara kwa mara, mwana michezo, mchumia juani nk. Hakikisha chupa ya maji haibanduki pembeni yako na unakunywa maji mengi mara kwa mara.

Ndio maana wataalamu wanasema na kushauri: Ikiwa unaishi kwenye ukanda na mikoa yenye joto kali (Dar es  Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro, Dodoma, Mara, Mwanza, Singida, Mtwara, Kilimanjaro "sehemu baadhi" nk) yakupasa unywe maji mengi kwa siku kwa sababu maeneo hayo humfanya muhusika kutokwa na jasho jingi kupita kiasi hata bila kufanya kazi nzito au kufanya mazoezi.

Kutokunywa maji hayo hupelekea mwili kudhoofu, kuharibu mfumo mzuri wa uchujaji wa sumu mwili, chakula kutokusagika na kuchaguliwa vizuri nk. Na ikidumu hivyo kwa muda mrefu ndipo mtu unaweza kupatwa na #magonjwa hatari zaidi kama vile figo kufeli, kupata vidonda vya tumbo, ini kuungua, Kinga za mwili kushambuliwa na magonjwa mengi zaidi na kwa mjumuisho wa hayo yote na pasipo kupata suluhisho la kitabibu kama kumuona Daktari kinachofuatia ni kifo tu hakuna cha ziada.

Muhimu kutambua ni kuwa: Mwili wa Binadamu hutegemea kupata maji yake kupitia pia aina ya vyakula unavyokula kila siku, matunda, vinywaji, maji yenyewe na virutubisho-dawa, ambapo kwa mjumuisho wavyo mtu huweza kuwa na maji ya kutosha mwilini, kuwa na afya njema, kinga za mwili kufanya kazi sawia, na Kupambana na maradhi nyemelezi, mwisho maradhi shambulizi yatakupitia pembeni (utayasikia kwa jirani tu)

Mwili unafanyizwa na seli mbili za damu (nyeupe na nyekundu) ambazo hizi ndio ngao zetu, kinga na ndio huyafanya maisha yetu yasonge.

Ndio maana ukipungukiwa na damu wewe ni wa ICU, ukipungukiwa na maji wewe ni wa ICU pia na uzembeaji kidogo, malaika mtoa roho utamuona akipita pembeni yako mara kwa mara.

(NDUGU ZANGU AFYA NI MALI NA NI UHAI WAKO USIUCHEZEE

Swali la kujiuliza kabla ya kuhitimisha ni kuwa: Je! Unawezaje kuchezea uhai wako na afya yako!?

Binadamu huchezea afya yake na kuhatarisha uhai wake kwa kufanya mambo mbalimbali (mengi unayafahamu) na ndio maana unaweza kumsikia mtu akisema maisha yenyewe mafupi haya!?

Sababu anafanya jambo ingawa anatambua madhara yake, na hii ni kweli kabisa watu wengi walioelimika Wasomi ndio haswa huongoza hapa: ni walevi wa pombe kali, watumiaji wa madawa ta kulevya, hawazingatii ulaji sahihi na kwa wakati hupuuzia taarifa kama hizi (uisomayo) na mwisho wa siku pyuuuuuuu! They disappear forever!

Sio ajabu kizazi chetu cha leo (karne ya 21) kumuona kijana umri mdogo kabisa lakini Kimuonekano kashaZeeka kabisa, ndio si tunawaona mtaani huko!?

Wazee wetu (miaka ya 60, 50, 40, kurudi nyuma) ukiwaona leo hii bado ni imara licha ya changamoto ya maisha na umaskini na huwezi kuwasikia wakiwa na matatizo kwa wingi kama tuliyonayo vijana wa miaka hii (80, 90, 2000 kuja mbele) ambapo magonjwa kama presha, kizukari, miguu kuvimba, utasa, kupoteza nguvu za kiume, yote haya anayo mtu mmoja..

HIYO NDIO KUCHEZA NA AFYA NA UHAI WAKO PIA.

Ndio! Ukipatwa na hayo yote mwisho wa siku unafikiri nini kinafuatia!? Saa nyingine hebu tuache kumbebesha MUNGU lawama na mizigo asiyostahili, amekupa maarifa ya kutambua mema na mabaya yatumie!?

Acha kuwa kichwa_maji (ashakhum sio matusi) Huwezi ukaambiwa unywaji wa pombe kupitiliza ni hatari kwa afya yako bado unakunywa! Tumbaku, bangi, cocaine ni hatari kwa afya yako bado unavuta!?

Kunywa maji mengi bado hunywi!, kula mlo kamili (balance diet) bado huli wakati afrika tumejaaliwa vitu vyote hivyo, ungekuwa unaishi jangwani (deserts) ungesemaje!?

Wewe si mnywaji wa maji, hivyo Endelea kunywa maji ya kutosha walau glasi 4-8 au zaidi kwa siku, ukipata #Stakafeli kula, juisi ya Miwa, ndizi, nanasi, chungwa, limao, tangawizi, karafuu, nazi, mihogo, #maharagwe, viazi "sio vya kukaanga na mafuta" kula.

Embe, limao, nyama, bamia, mboga za majani kulaaa-uwiiiiii! Hahaha! Vingine unavijua! (Muhimu hakikisha mlo wako unajumuisha virutubisho na madini ya  -  Vitamini, wanga na protini)

Makala zinazofuata, ntajaribu kukuorodheshea baadhi ya vyakula na matunda ambavyo huweza kuupatia mwili vitamini, wanga na protini.

KUMBUKA: Rangi ya mkojo inayotoka na “Uwekundu (mfano wa damu) na mkojo unaotoa harufu (Red urine colour) Ndugu yangu hapo kimbilia kituo cha Afya kilichopo karibu na wewe, na sio kuendelea kukaa nyumbani na kutumia muzugwa, dawa za miti shamba (hapo punde tunaweza kukuimbia ule wimbo wa parapanda)

RANGI HIYO KIAFYA: Mwili Upo kawaida (sababu bado unaweza kujihisi una nguvu kiafya) ingawa sumu mwili iliyopo katika damu haichujwi vyema na kusafishika na figo

zako, yaani Ini limekataa kufanya kazi yake, hivyo madhara ya hivi muda mrefu huweza kuzalisha matatizo katika figo zako kufa kabisa, kupata vichomi vya mara kwa mara, tumbo kuuma, mwili kuishiwa nguvu nk.

HEBU SOMA HAPA KUHUSU KUJUA KAMA FIGO ZAKO ZINA HITILAFU:

(Chuchuza Figo)

MKOJO wenye Rangi ya Pinki, damu ya mzee na inayokaribia kuwa kama Nyekundu

(Blood colour). Kama hujala matunda yoyote, chakula, au kinywaji chenye asili ya uwekundu kwa wingi" (juisi ya rangi, ubuyu wa rangi nk)

Au Mwanamke haupo kwenye siku zako za hedhi (ashakhum sio matusi)" basi huwenda una matatizo makubwa kwenye mwili wako, ambapo damu hulazimika kuchanganyika na njia ya mkojo "kwenye kibofu chako cha mkojo".

Ukiona dalili hiyo tambua kuwa Inaweza ikawa sio ishara mbaya kwa mara moja ila ikijirudia kwa muda wa siku zaidi ya 2 au 3 ni tatizo hilo, tena lenye kuhitaji vipimo na matibabu ya kidaktari upesi zaidi.

Muone daktari haraka sana Ufanyiwe Vipimo kujua kama, unakabiliwa na magonjwa yepi.

LABDA NIELEZEE KIDOGO HAPA:

Mara nyingi (sio zote) mkojo kutoka na rangi ya kama damu huwa inachagizwa na kuchanganyika na damu, na hadi ikitokea hivyo zaidi ya mara2 au siku2, (Isipokuwa wanawake wakati wa hedhi) basi kuna jambo ambalo halipo sawa mwilini. "Mwili una dosari fulani)

Na huwenda muhusika anakabiliwa na magonjwa kama vile ya zinaa (mf.Kaswende, pangusa nk); au kinaMama kuwa na tatizo kwenye mlango wa kizazi "mwanamke", kuathirika kwa ini, tatizo katika kibofu chako cha kuhifadhia mkojo, njia ya kupitishia mkojo, au pengine inaweza ikawa ishara ya ugojwa wa Figo, Ini au uvimbe kwenye njia hiyo ya mkojo nk.

PATA USHAURI WA KIDAKTARI NA PIMA AFYA YAKO MAABARA AU KITUO CHA AFYA AU KWA KUJICHUNGUZA MABADILIKO YAKO MARA KWA MARA MWENYEWE HUKU UKIJIPENDA NA KUILINDA AFYA YA MWILI WAKO PIA.

ENDELEA HAPA ZAIDI (Chanzo kingine):

Tafadhali waweza tufuatilia pia Facebook kwa page yetu ya: (FB-Page)