Friday, 29 December 2017

ULEVI UNAVYOWEZA KULETA MADHARA YA UTEGEMEZI SAWA NA MADAWA YA KULEVYA


 
NA: Stewart Meena
Ikiwa ndio kwanza zimebaki siku2 tunajiandaa kuumaliza mwaka huu wa-2017 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2018 nimeona nivyema tuliongelee swala hili la baadhi ya watu kuendekeza sana matumizi ya vinywaji vigumu (mvinyo) kwa ajili ya kusheherehea sikukuu mbalimbali.
Imekuwa ni kawaida kwa vijana na wazazi kulalamikia swala la kutokuwepo kwa maadili katika Jamii wanamoishi, sio watoto / sio vijana na wala sio Wazee.

“Vilio, majonzi na simanzi zimetawala katika nyumba zetu, matukio ya wizi, ubakaji na mauwaji nayo yakizidi kushika kasi”
Pengine ni utandawazi, ukosefu wa ajira, au ni kujitoa ufahamu kwa wanajamii hao, kwa kile kinachoonekana kama ni ‘akili ya kuongezea’ yaani matumizi ya madawa ya kulevya na vinywaji vigumu (mvinyo) haswa zaidi vile vya bei raisi (kama Viroba, Chang’aa, banana na zile pombe nyingine za kienyeji.)


Pombe ya kienyeji inayotengenezwa na Ulezi na Ndizi Mbivu (aina ya Mbege)

Ulevi, ujulikanao pia kama uraibu wa pombe, ni ulemavu tegemevu wa kudhuru. Dalili zake ni unywaji pombe kupindukia bila udhibiti pombe licha ya madhara yake hasi kwa afya ya mnywaji,, mahusiano na hadhi yake machoni pa jamii. Kama matatizo mengine ya kiafya, ulevi ni mojawapo ya magonjwa yanayoweza kutibika.
Neno " ulevi" limetumika kwa muda mrefu tangu kubuniwa mwaka wa 1849 na Magnus Huss, ila katika nyanja ya utabibu istilahi hii iligeuzwa kuwa "utumiaji pombe vibaya" na " utegemezi pombe" katika miaka ya 1980 DSM III.
Aidha mwaka wa 1979 kamati ya wataalamu ya Shirika la Afya Duniani haikupendelea kutumika kwa neno "ulevi" kama istilali ya kiafya, huku ikipendekeza dalili za "utegemezi pombe".

Katika karne ya 19 na mapema karne ya 20, utegemezi pombe uliitwa dipsomania kabla ya kubatilishwa kuwa ulevi".
Hapana uhakika wa Sababu za kibayolojia zinazochangia ulevi, hata hivyo, hali hii yaweza kutokana na mazingira ya kijamii, mfadhaiko wa ubongo, afya ya akili, maumbile, umri, kabila, na jinsia.

Matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu huleta mabadiliko ya kimwili katika ubongo kama vile uhimili na utegemezi, nah ii haitofautiani sana na atahari za madawa ya kulevya, tokea pale kila kitu kikizidisha mwilini huleta athari flani kwenye mwili.


MADA YA KULEVYA NI NINI:

Kwa fasiri sahihi tu kuhusu madawa ya kulevya, ni kuwa mwili kuzoeshwa kilevya akili kwa muda mrefu na hivyo kuleta utegemezi na endapo Vilevya hivyo vikikosekana basi huleta athari katika mwili kwani hutuma ujumbe katika ubongo na fahamu kuwa kuna kitu kimekosekana muda kama huu ambapo kilevya hicho kilipotumika jana yake.

Mabadiliko ya kemia katika ubongo hudumisha hali ya mlevi kutoweza kuacha kunywa pombe na huweza kusababisha dalili za mtegemea-pombe pale aachapo kunywa, na wengine walioathiriwa zaidi huweza kukosa usingizi, kutetemeka mwili na hata kuwa mgonjwa kabisa.

Pombe huharibu takribani kila kiungo katika mwili, na kwa sababu ya athari hizo kwa kujumuisha ya sumu dhurifu ya utegemezi pombe , mlevi hukumbwa na hatari nyingi za matatizo ya kimagonjwa na kiakili.

Pombe sio mbaya, ila huwa mbaya ukizidisha na ukiizoesha mwili kwa muda mrefu, na hivyo ulevi huo huwa na madhara makubwa kwa jamii iliyowazunguka au watu wanaohusika na maisha yao.

ATHARI HIZO NI ZIPI?

Picha Madhara Ya pombe, nA MFUMO Mzima wa Kiakili na kimwili

Atari hizo ni kama vile, Wanawake kukabiliwa na matatizo ya muda mrefu ya utegemezi pombe kwa haraka zaidi kuliko wanaume. Zaidi ya hayo, wanawake hufa kwa kiwango cha juu zaidi kutokana na ulevi kuliko wanaume.


Mifano ya matatizo ya muda mrefu ni pamoja na uharibifu wa ubongo, moyo, na ini na pia ongezeko la hatari ya saratani ya matiti, Zaidi ya hayo, unywaji mzito wa muda mrefu umegunduliwa kuwa na athari hasi katika uwezo wa uzazi kwa wanawake na wanaume.

Hii husababisha mvurugiko wa uzazi kama vile kutozalisha yai, kupunguka kwakiwango cha molekuli ya ovari matatizo, au kukosa utaratibu wa hedhi, na kufunga uzazi mapema.

Ketoasidisi za pombe zinaweza kutokea kwa watu ambao hutumia pombe vibaya mara nyingi na walio na historia ya hivi majuzi yaulevi kupindukia.

Dalili za akili


Matumizi ya mabaya ya muda mrefu wa pombe unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya afya ya akili, na Matatizo sugu ya ubongo sio nadra, takribani asilimia 10 ya matukio yote ya shida za akili ni huhusiana na matumizi ya pombe, na hivyo kuifanya sababu kuu ya shida ya akili.

Matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha uharibifu wa kazi za ubongo, na afya ya kisaikolojia inaweza kuathirika baada ya muda Fulani, na inapoharibika basi kinachofuatia ni tabia tofauti zilizozoeleka na jamii unamoishi na kupelekea unyanyapaaji.

Kwanini matatizo kama hayo yaliyoorodheshwa hapa yakutokee kwa kujitakia! Wakati unaweza kuepuka?! Tuepuke ulevi jamani haswa mwisho huu wa mwaka na sikukuu nyingine zinazofuatia.

TUNAKUTAKIA MAANDALIZI MEMA YA KUUONA MWAKA MPYA! 2018

No comments:

Post a Comment