Ni sauti ya ngombe aliaye horini ikiwa ni utambulisho wa kuzaliwa Yesu kristo ambapo Kila mwaka ifikapo tarehe kama ya leo Desemba 25, Wakristo duniani kote huadhimisha sherehe ya kuzaliwa kwa Masiha wao (Yesu Kristo) aliyewaunganisha wanadamu na ufalme wa mbingu tena baada ya wanadamu kumwasi sana Mungu, Bwana Yesu Kristo.
Kiuhalisia, Wapo wanaojua maana halisi ya neno X-Mass kama siku ya kuzaliwa kwake Yesu, Lakini pia wapo baadi yao ambao hawaifahamu vyema siku hii.
JAPO KWA UCHACHE, HAYA HAPA MAELEZO MACHACHE AU TAFSIRI HALISI YA NENO HILI (X-MASS)
Kwa Kuanza Hebu Tujuzane Kwanza, Neno Christimass Limetokana Na Nini.!?
Krismasi inatokana na neno
la Kiingereza
lenye maana ya "Christ`s Mass" yaani misa au ibada ya Kristo Au
kwa Kiswahili christimas ni Noel ambapo Noeli
inatokana na Kiingereza "Noel" (au "Nowell") ambako
imepokewa kutoka lugha
ya Kifaransa
"noël".
Hilo
ni ufupisho wa Kilatini "Natalis (dies)", likimaanisha "(siku
ya) kuzaliwa..Christimass au Noel ni sikukuu ambayo Wakristo wengi
husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Katika
sikukuu hii watu hupenda kupamba nyumba zao kwa miti ya xmass na maua yenye
rangi mbalimbali pamoja na taa za kuwakawaka vivyo hivyo utaratibu huu
ulikuwepo toka zamani ambazo ni
kumbukumbu ya Alama za nyota zilizowapeleka mamajusi hadi Bethlehemu alikozaliwa
Yesu kristo.
Halikadhalika kuna miti ya Krismasi ambayo ni Ni ishara ya Krismasi ambapo zamani mti wa xmass ulipambwa zaidi kwa matunda mbalimbali, siku hizi miti hiyo hupambwa kwa kuzungushiwa taa za vimulimuli, pamoja na maua yadukani (Spesho)
Pamoja
hayo kumekuwa na desturi ya watu kupeana
zawadi ya maua na kadi zenye maneo mazuri ya kutakiana heri ya xmass na jambohili la kadi na kupeana zawadi mbalimbali ambazo
hufunguliwa siku ya pili baada ya xmass
ambayo huitwa boxing day (26/12) yaani siku ya kufungua zawadi ililikuwepo toka zamani.
KWA
MFANO: (Ieleweke
Hapa silengi Wafuasi flani, ila ni kuzidi kuelimishana)
Katika
historia hapo mwanzo tunaelezwa
jambo hili lilianzia kwa kiongozi
mmoja wa dini wa zamani aitwaye - Martin Luther yeye enzi za uhai wake alikuwa na desturi ya
kuwazawadia watoto kwenye siku ya Mtakatifu
Nikolasi tarehe 6 Desemba, wiki 2 kabla ya sikukuu.
Hapo Luther alipendekeza kuhamisha zawadi kwa watoto kwenda siku ya kuzaliwa kwake Yesu ili wamkumbuke zaidi Yesu kuliko mtakatifu huyo na Hapo alikuwa anarejea zawadi zilizopelekwa kwa Yesu na mamajusi kutoka mashariki kwa mujibu wa maandiko.
VIPI
SEHEMU NYINGINE DUNIANI:
Lakini Katika nchi nyingi Duniani ikiwemo na Tanzania mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine, Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na Kadi,miti ya xmass na mapambo ya Krismasi vimekuwa vikiuzwa sana katika maduka mengi.
Lakini yote kwa yote, Wakati huu wa sikukuu ya
Christmas ni wakati ambao familia huungana pamoja kwa shughuli mbali mbali
ikiwemo kula,kunywa na kupeana zawadi hasa kwa watoto,kwa hivyo tusitumie
nafasi hii kwa kufanya mambo yatakayo ziumiza familia zetu kwa namna moja au
nyingine. Nakutakia Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.Lakini Katika nchi nyingi Duniani ikiwemo na Tanzania mwezi wa Desemba umekuwa mwezi wa mapato makubwa kushinda miezi mingine, Hata katika miji mikubwa ya nchi kama Dubai au Japani ambako Wakristo ni wachache desturi ya kupeana zawadi imeenea na Kadi,miti ya xmass na mapambo ya Krismasi vimekuwa vikiuzwa sana katika maduka mengi.
No comments:
Post a Comment