Tuesday, 24 May 2016

BAADA YA UBINGWA FA VAN GAAL SASA IMEKWISHA



 
Meneja wa Man U aliyemaliza muda wake, Lois Van Gaal akisalimiana na meneja mpya Jose Mourinho.
Meneja wa timu ya Manchester United ya Nchini Uingereza Louis van Gaal amenukuliwa akisema sasa imekwisha wakati akitarajiwa kumaliza kandarasi yake ya miaka miwili ya kuifundisha klabu hiyo.

Kuondoka kwa LVG kunafungua fursa ya kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye sasa tayari ameshafunga mkataba wa kuinoa klabu hiyo ya Man united ambayo haijafanya vizuri tokea kustaafu kwa kocha wake wa muda mrefu (Ferguson) ambaye alikabidhi kandarasi kwa David Moyes kabla ya kutimulliwa na timu kukabidhiwa kwa Van gaal.

Mourinho amekubali kutia saini ya miaka mitatu ya kuinoa Man United na anatarajiwa kutangazwa mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii, ingawa kumekuwa na minongono kutoka kwa wachezaji wa zamani kuwa meneja huyo mpya hawezi kuipatia timu hiyo mafanikio yaliyokosekana kwa muda mrefu.

Van Gaal aliyechaguliwa kuinoa Man united tokea msimu wa 2014 ameiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja pekee la FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace mabao 2-1 fainali wikendi ya jana jumamosi, na amefanikiwa kumaliza nafasi ya tano msimu huu na hivyo timu hiyo ya Manchester itakosa kushiriki UEFA lakini  itashiriki michuano ya Uropa msimu huu unaofuata.

Mourinho, kocha mpya wa Manchester United alifukuzwa kutoka klabu ya Chelsea mwezi desemba mwaka jana baada ya mwenendo mbovu wa uchezaji wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment