MIONGONI
MWA VIWANJA VYA SOKA VYENYE THAMANI KUBWA ZAIDI BARANI AFRIKA.....
10- Chini Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam huu
ulijengwa kwa dola milioni 53 na nusu ya hela za ujenzi huo zilitolewa msaada
na serikali ya China. ulifunguliwa mwaka 2007 na unauwezo wa kuchukua mashabiki
60000.
9- Chini: Stade Olympique de Radès
huu ni uwanja uliopo Tunisia mji wa Rades, uwezo wake wa kuchukua mashabiki ni
sawa na uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, ila gharama yake inatajwa kufikia
dola milioni 110, ulijengwa mwaka 2001.
|
8-Mbombela Stadium ni moja kati ya
viwanja vilivyotumika katika fainali za michuano ya Kombe la Dunia 2010 nchini
Afrika ya Kusini, kina thamani ya dola milioni 140, kina uwezo wa kuchukua
mashabiki 40,929. | | |
|
7- Estádio 11 de Novembro upo Angola lakini
ulitumika kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2010, umejengwa kwa dola
milioni 227 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.
|
|
5-Nelson Mandela Bay
Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270 upo katika mji
wa Port Elizabeth na unauwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake
limetoka na Rais wa kwanza wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela. |
|
3-FNB
Stadium ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 440, ulichezewa fainali za
Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini. FNB Stadium jina lake lilizoeleka na
wengi ni Soccer City. Huu ndio uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi
zaidi barani Afrika, unauwezo wa kubeba watu 94,736. |
|
2- Moses Mabhida
Stadium ulijengwa kwa dola milioni 450 ,
uwanja huu upo Durban Afrika Kusini na ulitumika kwa baadhi ya mechi za fainali
ya Kombe la Dunia 2010, ulikuwa na uwezo wa kuingia mashabiki 62,760
lakini wakati wa fainali za Kombe la Dunia ulipunguzwa na kuwa na uwezo wa
kuchukua mashabiki 54000.
|
|
1-Cape Town Stadium huu ndio uwanja wenye thamani
kuliko vyote barani Afrika, kwani zimetumika dola milioni 600, unauwezo wa
kuingia mashabiki 64,100.
|
|
4-Abuja
Stadium hiki ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa kwa gharama zaidi barani
Afrika, dola milioni 360 ndio zilitumika kujenga uwanja huu wenye uwezo wa
kuchukua mashabiki 60,491 upo mji mkuu wa Nigeria Abuja. | |
|
6- Peter Mokaba Stadium huu ni uwanja ambao ulijengwa
kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini, ulijengwa kwa dola
milioni 150 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 41,733, kwa sasa unatumiwa
na klabu ya Black Leopards FC kama uwanja wa nyumbani.
|
No comments:
Post a Comment