Moja ya Kiwanja cha mpira wa Miguu nchini ufaransa (kati ya Viwanja 10) kitakachotumika kwa michuano ya mataifa ya ulaya (Euro-2016) |
Ikiwa
zimebaki wiki mbili pekee kuanza kwa michuano ya UEFA-Euro 2016, hali ya usalama
nchini Ufaransa Inakofanyika Michuano hiyo bado imeelezwa kuwa tete, ambapo
Wanausalama nchini Ujerumani wameonya kuwa Mtanange huo huenda ukakabiliwa na
mashambulizi ya kigaidi.
Waziri
wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault anasema "Kila kitu
kimefanywa kuimarisha usalama wa raia wa Ufaransa pamoja na wageni wote
wataokuja kushiriki katika Euro 2016”
Mapema
wiki hii Bunge la nchini Ufaransa limeidhinisha mswada wa kurefushwa kwa miezi
miwili zaidi, kutangazwa kwa hali ya hatari ambayo iliyowekwa tangu
mashambulizi ya kigaidi ya Novemba mwaka jana.
UEFA inapanga kuwaajiri maafisa usalama
wa kibinafsi takribani elfu-10, wakati wa kinyang'anyiro hicho na kila uwanja
kati ya viwanja-10 vitakavyotumika kutakuwa na maafisa 900 wa usalama
watakaoweka ulinzi kwa kila mchuano.
No comments:
Post a Comment