Thursday, 19 May 2016

AIFF 2016 YOUTH CUP, SERENGETI BOYZ KUNOGA

Kikosi cha Vijana wa timu ya Tanzania (Serengeti Boys) wenye umri chini cha miaka-17 wakiwa katika picha ya pamoja. Heko kwa Vijana hawa kwa kuiwakilisha vyema Tanzania kule nchini India.
Serengeti Boyz mpaka sasa imeshacheza mechi 3 na kuifunga India 3-1 na kutoka sare na USA 1-1 na kisha South Korea 1-1.
Ili kutinga Fainali Serengeti Boys wanapaswa kuifunga Malaysia ambayo nayo katika mchezo wa awali ilitoka sare na India na kubondwa na South Korea 3-0.

Ikiwa Serengeti Boys wataifunga Malaysia basi njia yao itakuwa nyeupe ikiwa pia Jumamosi mechi kati ya Marekani na Korea Kusini itaisha kwa timu moja kushinda.
2016 AIFF Youth Cup ni mashindano yaliyoandaliwa na shirikisho la soka la India, All India Football Federation (AIFF), mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya mashindano ya AFC U-16 na yale ya 2017 FIFA U-17 World Cup.
Mashindano haya yanachezwa kuanzia Mei 15 hadi Mei 25 huko Tilak Maidan Stadium huko Vasco, Goa nchini India,mashindano haya yana hatua mbili za kundi na za mtoano.
Timu 4 za juu za kundi ambalo lina timu 5 zitasonga kuingia mtoano ambapo timu mbili za juu zitacheza fainali.

No comments:

Post a Comment