Meneja
wa timu ya Manchester United ya Nchini Uingereza Louis van Gaal amenukuliwa
akisema sasa imekwisha wakati akitarajiwa kumaliza kandarasi yake ya miaka
miwili ya kuifundisha klabu hiyo.
Kuondoka
kwa LVG kunafungua fursa ya kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye sasa
tayari ameshafunga mkataba wa kuinoa klabu hiyo ya Man united ambayo haijafanya
vizuri tokea kustaafu kwa kocha wake wa muda mrefu (Ferguson) ambaye alikabidhi
kandarasi kwa David Moyes kabla ya kutimulliwa na timu kukabidhiwa kwa Van
gaal.
Mourinho
amekubali kutia saini ya miaka mitatu ya kuinoa Man United na anatarajiwa
kutangazwa mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii, ingawa kumekuwa na
minongono kutoka kwa wachezaji wa zamani kuwa meneja huyo mpya hawezi kuipatia
timu hiyo mafanikio yaliyokosekana kwa muda mrefu.
Van
Gaal aliyechaguliwa kuinoa Man united tokea msimu wa 2014 ameiwezesha timu hiyo
kutwaa taji moja pekee la FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace mabao 2-1 fainali
wikendi ya jana jumamosi, na amefanikiwa kumaliza nafasi ya tano msimu huu na
hivyo timu hiyo ya Manchester itakosa kushiriki UEFA lakini itashiriki michuano ya Uropa msimu huu
unaofuata.
Mourinho,
kocha mpya wa Manchester United alifukuzwa kutoka klabu ya Chelsea mwezi
desemba mwaka jana baada ya mwenendo mbovu wa uchezaji wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment