Tuesday, 24 May 2016

KUELEKEA FIFA-2016 , TIMU YA TAIFA UJERUMANI YAAHIDIWA DONGE NONO


kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani maarufu kama (Die Mannschaft) watapokea bahashishi ya euro laki-3 kila mchezaji ikiwa watashinda Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016).
 
Shirikisho la kandanda la nchini Ujerumani (DFB) limesema licha ya kinyang'anyiro cha mwaka huu kuwa na timu nyingi, na kuongezwa kwa hatua za mechi za mchujo, viwango vya bahashishi vitakuwa sawa na vya michuano ya Euro-2012 ambapo Ujerumani iliondolewa katika hatua nne za mwisho.

Meneja wa timu hiyo Oliver Bierhoff amesema wamekubaliana na DFB pamoja na wachezaji kuwa “kabla ya kuanza kwa Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ukraine mwezi juni-12 Fedha hizo watakuwanazo mkononi, na endapo watinga hatua ya robo fainali watalipwa euro elfu-50 kila mchezaji, euro laki-1 kwa nusu fainali na Euro laki 1 na kwa kutinga hatua ya fainali.

Ikiwa watashindwa katika hatua ya 16 bora za mwisho, au washindwe kufuzu katika Kundi lao wataambulia patupu, lakini Washindi hao wa Kombe la Dunia mwaka-2014 nchini Brazil, ni miongoni mwa timu 24 zinazopigiwa upatu wa kufanya vyema katika mashindano hayo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu, ambapo Ujerumani ipo katika Kundi C pamoja na timu za Ukraine, Poland na Ireland ya Kaskazini.

Wakati huo huo: Kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Guendogan mwenye umri wa miaka 25 atakosa dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 baada ya kuumia goti wakati akifanya mazoezi na anatarajiwa  kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu.

Habari hii ni pigo kwa kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew na pia bahati mbaya mchezaji huyo aliyekosa tena Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na maumivu ya mgongo yaliyomweka nje kwa miezi 14 kuanzia Agosti 2013.

No comments:

Post a Comment