HEBU LEO TUMJUE MUIGIZAJI WA FILAMU
YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU WANAMDHANIA KUWA NDIYE YESU HALISI.
YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU WANAMDHANIA KUWA NDIYE YESU HALISI.
Brian Deacon katika moja ya (Scene) aliyoigiza ndani ya Filamu ya YESU miaka kama-30 iliyopita. Picha na Mtandao. |
Makala na Stewart Meena.
Filamu Ya JESUS:
Ni
Filamu iliyogusa maisha ya watu wengi Duniani kiasi kwamba wakasahau kuwa
Mwigizaji wa Filamu hiyo hakuwa YESU_halisi, ila ni Muigizaji tu na ni Binadamu
wa kawaida kama wengine.
Filamu
hii iitwayo “JESUS” Imeigizwa Nchini Israel na Muigizaji kutoka nchini Uingereza
(pichani) aitwaye Brian Deacon mnamo Mwaka 1979 ambapo kiuhalisia hakuwa Mkristo
lakini Uigizaji huo ulimfanya Aokoke mara baada ya kuitazama filamu hiyo akiwa
na miaka-30 na kubadili dini na kuwa Mkristo.
HISTORIA YA DEACON:
Jina
lake kamili Msanii huyu anaitwa Brian Deacon alizaliwa Oxford Nchini
Uingereza tarehe 13/02/1949 akiwa ni mtoto wa pili kutoka katika familia ya
Deacon, (Baba yake) ambaye alikuwa ni Fundi wa kutengeneza magari (Mechanic)
na Mama yake akiwa ni Nesi wa hospitali (Nurse)
Ndoa
ya kwanza ya Brian na mkewe Bi. Lenska, ilivunjika ambapo walifanikiwa kupata
mtoto wa kike aitwaye Lara Deacon, na ndoa yake ya pili alifunga na Natalie Bloch
Mnamo mwaka-1998 ambaye yupo naye hadi hivi sasa.
Bwana Brian alipitishwa katika Mchujo wa Waigizaji zaidi
ya 1,000 ambao walifanyiwa mahojiano huku-260 wakijaribishwa kuigiza (screen test) na yeye akiwa ni Mwingereza pekee kufaulu mtihani huo
na kuchaguliwa kuwa muhusika mkuu (Sterring).
Filamu
hii ya (JESUS) imenukuliwa katika maandiko matakatifu ya Kitabu cha LUKA, (luke)
ambapo Bw Brian anasema:
“ilinichukua
zaidi ya mara-20 kwa wiki3 kusoma kitabu cha Luka Mtakatifu pekee, ambapo kusoma
huko ilisaidia kumfahamu vyema Yesu Kristo ni mtu wa aina gani, ikanipa nguvu
na Ujasiri wa kuigiza filamu hii” alisema_Bw_Deacon.
Katika uigizaji
wa Filamu hii ya JESUS, ulichukua zaidi ya miezi-7 kurekodiwa, kuanzia majira
ya alfajiri mpaka kiza kilipozama, na miezi mingine-7 kurekodiwa, na Bw_Brian
anasema:
“katika
uigizaji huo hakuna aliyechoka kwani Waigizaji wote walikuwa wakipokea nguvu ya
ajabu kutoka juu (Mbinguni) na hivyo kuifanya kazi hiyo kuwa nyepesi hadi
kukamilika kwake” Alisema.
Baada
ya Filamu hiyo ya 'JESUS' Bw. Brian alirudi kuigiza Majukwaani na kwenye
runinga ambapo kwa miaka zaidi ya 30 hadi hivi sasa tokea kutoka kwa filamu
hiyo, tayari imeshatazamwa na watu zaidi ya milioni-133. (hii ni kwa mujibu takwimu
za mwaka-2001) ambapo wote walibadilisha maisha yao na kuokoka mara baada ya kuitazama
filamu hiyo.
Brian Deacon ambaye baadhi ya Watu (Wakristo) Humdhania kwamba Ndeye YESU halisi, na kusahau kuwa Yesu alikufa takribani miaka 2,000 iliyopita, na Brian bado yuHai. |
Filamu nyingine
alizowahi kushiriki Brian Deacon kuigiza ni pamoja na:
(A-Zed,
Two Noughts-1985, The Feathered Serpent-1977, na Tamthilia iitwayo LILLIE
iliyoigizwa mwaka-1978 akitumia jina la Frank Miles, huyo ndie BRIAN DEACON
aiyeigiza “Jesus” mwaka-1979.)
KUJUA
ZAIDI KUMUHUSU DEACON NA FILAMU ZAKE NYINGINE ALIOIGIZA, Bonyeza linki hapa:
Wakristo Ulimwenguni
kote Huadhimisha Mateso na Kifo cha YESU KRISTO Mwokozi wao Msimu wa (Pasaka) Ambapo Ijumaa kuu ni siku ambayo Wakristo huamini na kuadhimisha kuteswa, hadi kufa kwa
Masihi wao YESU KRISTO ambapo wanaamini alitumwa Ulimwenguni kulirudisha Kanisa la Mungu lililopotea,
kuwakomboa wenye dhambi, na Kulikusanya Kanisa hilo ambalo lilikuwa limepotea, zaidi
ya miaka 2000 iliyopita.
Wakristo wnaanza mfungo wao rasmi, ambapo siku ya leo kwa (RC) wanakwenda njia ya msalaba.
(nawatakia Wakristo wote maandalizi mema ya pasaka)
Wakristo wnaanza mfungo wao rasmi, ambapo siku ya leo kwa (RC) wanakwenda njia ya msalaba.
(nawatakia Wakristo wote maandalizi mema ya pasaka)
VYANZO VENGINE:
No comments:
Post a Comment