Friday, 12 February 2016

TUMJUE MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUSEMA NI YESU



HEBU LEO TUMJUE MUIGIZAJI WA FILAMU
YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU WANAMDHANIA KUWA NDIYE YESU HALISI.
Brian Deacon katika moja ya (Scene) aliyoigiza ndani ya Filamu ya YESU miaka kama-30 iliyopita. Picha na Mtandao.
 Makala na Stewart Meena.

Filamu Ya JESUS:
Ni Filamu iliyogusa maisha ya watu wengi Duniani kiasi kwamba wakasahau kuwa Mwigizaji wa Filamu hiyo hakuwa YESU_halisi, ila ni Muigizaji tu na ni Binadamu wa kawaida kama wengine.
Filamu hii iitwayo “JESUS” Imeigizwa Nchini Israel na Muigizaji kutoka nchini Uingereza (pichani) aitwaye Brian Deacon mnamo Mwaka 1979 ambapo kiuhalisia hakuwa Mkristo lakini Uigizaji huo ulimfanya Aokoke mara baada ya kuitazama filamu hiyo akiwa na miaka-30 na kubadili dini na kuwa Mkristo.

 HISTORIA YA DEACON:
Jina lake kamili Msanii huyu anaitwa Brian Deacon alizaliwa Oxford Nchini Uingereza tarehe 13/02/1949 akiwa ni mtoto wa pili kutoka katika familia ya Deacon, (Baba yake) ambaye alikuwa ni Fundi wa kutengeneza magari (Mechanic) na Mama yake akiwa ni Nesi wa hospitali (Nurse)
Ndoa ya kwanza ya Brian na mkewe Bi. Lenska, ilivunjika ambapo walifanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Lara Deacon, na ndoa yake ya pili alifunga na Natalie Bloch Mnamo mwaka-1998 ambaye yupo naye hadi hivi sasa.
Bwana Brian alipitishwa katika Mchujo wa Waigizaji zaidi ya 1,000 ambao walifanyiwa mahojiano huku-260 wakijaribishwa kuigiza (screen test) na yeye akiwa ni Mwingereza pekee kufaulu mtihani huo na kuchaguliwa kuwa muhusika mkuu (Sterring).
Filamu hii ya (JESUS) imenukuliwa katika maandiko matakatifu ya Kitabu cha LUKA, (luke) ambapo Bw Brian anasema:
“ilinichukua zaidi ya mara-20 kwa wiki3 kusoma kitabu cha Luka Mtakatifu pekee, ambapo kusoma huko ilisaidia kumfahamu vyema Yesu Kristo ni mtu wa aina gani, ikanipa nguvu na Ujasiri wa kuigiza filamu hii” alisema_Bw_Deacon.
Katika uigizaji wa Filamu hii ya JESUS, ulichukua zaidi ya miezi-7 kurekodiwa, kuanzia majira ya alfajiri mpaka kiza kilipozama, na miezi mingine-7 kurekodiwa, na Bw_Brian anasema:
“katika uigizaji huo hakuna aliyechoka kwani Waigizaji wote walikuwa wakipokea nguvu ya ajabu kutoka juu (Mbinguni) na hivyo kuifanya kazi hiyo kuwa nyepesi hadi kukamilika kwake” Alisema.
Baada ya Filamu hiyo ya 'JESUS' Bw. Brian alirudi kuigiza Majukwaani na kwenye runinga ambapo kwa miaka zaidi ya 30 hadi hivi sasa tokea kutoka kwa filamu hiyo, tayari imeshatazamwa na watu zaidi ya milioni-133. (hii ni kwa mujibu takwimu za mwaka-2001) ambapo wote walibadilisha maisha yao na kuokoka mara baada ya kuitazama filamu hiyo.
Brian Deacon ambaye baadhi ya Watu (Wakristo) Humdhania kwamba Ndeye YESU halisi, na kusahau kuwa Yesu alikufa takribani miaka 2,000 iliyopita, na Brian bado yuHai.

Filamu nyingine alizowahi kushiriki Brian Deacon kuigiza ni pamoja na:
(A-Zed, Two Noughts-1985, The Feathered Serpent-1977, na Tamthilia iitwayo LILLIE iliyoigizwa mwaka-1978 akitumia jina la Frank Miles, huyo ndie BRIAN DEACON aiyeigiza “Jesus” mwaka-1979.)

KUJUA ZAIDI KUMUHUSU DEACON NA FILAMU ZAKE NYINGINE ALIOIGIZA, Bonyeza linki hapa:

Wakristo Ulimwenguni kote Huadhimisha Mateso na Kifo cha YESU KRISTO Mwokozi wao Msimu wa (Pasaka) Ambapo Ijumaa kuu ni siku ambayo Wakristo huamini na kuadhimisha kuteswa, hadi kufa kwa Masihi wao YESU KRISTO ambapo wanaamini alitumwa Ulimwenguni kulirudisha Kanisa la Mungu lililopotea, kuwakomboa wenye dhambi, na Kulikusanya Kanisa hilo ambalo lilikuwa limepotea, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Wakristo wnaanza mfungo wao rasmi, ambapo siku ya leo kwa (RC) wanakwenda njia ya msalaba.
(nawatakia Wakristo wote maandalizi mema ya pasaka)

VYANZO VENGINE: 

No comments:

Post a Comment