Wednesday, 10 February 2016

FAHAMU MAAJABU YA MANYOYA YA PENGWINI ANAYEITWA EMPEROR.



PENGWINI  “EMPEROR”

Pengwini anayeitwa Emperor akiwa katika Maji akitafuta Mawindo yake. Picha na Mtandao.






Penguin #Emperor anaweza kuogelea kwa haraka sana majini kuliko hata #samaki, kuruka juu ya barafu kwa kasi ya ajabu. #Swali_ni_Kuwa Je!
Pengwini #Emperor Anawezaje kuyafanya hayo.?




#FIKIRIA_HILI: Pengwini huyo hubana hewa katika manyoya yake. Kwa Kufanya hivyo hakuzuii asipigwe na baridi tu bali pia kunamwezesha asonge mbele kwa kasi mara2 au 3 zaidi kwa kadiri anavyotaka na vile ambavyo angesonga.



#JINSI_GANI; Wataalamu wanaochunguza viumbe wa baharini wamesema kwamba huenda anafanya hivyo kwa #Kuachilia _Viputo Vidogo-Vidogo sana vya hewa (pichani) kutoka kwenye manyoya yake.



#Viputo_hivyo_Vinapoachiliwa, vinasaidia kupunguza msuguano uliopo kati ya maji na manyoya yake na hivyo kumwezesha kuongeza mwendo.

Penwini huwa na kawaida ya kukaa kwa Makundi makubwa (Cologne) na Muda wa Asubuhi na Jioni mara nyingi utawakutabwakiwa pamoja kwa Makundi.
Kwa kupendeza, #Mainjinia wamekuwa wakijifunza njia za kufanya #Meli_Zisonge kasi zaidi kwa kutumia Viputo vya hewa ili kupunguza msuguano uliopo kati ya maji na Meli.



Hata hivyo, watafiti wanakiri kwamba si rahisi kufanya uchunguzi huo kwa kuwa “ni vigumu sana kuiga #Manyoya_tata ya Pengwini ili kubuni vifaa vinavyofanana na Manyoya hayo”



SOURCE; Penguin: Paul Nicklen/National Geographic stock & Discovery uk.



LINKI:
NA:

No comments:

Post a Comment