KWELI DUNIANI KUNA MAAJABU YAKE
. JE,
Ulishawahi Kujiuliza KWELI #Ziwa linaweza kuwa la rangi ya waridi?
Ziwa
Retba linanaloiitwa Ziwa la Waridi Ambalo linapatikana Nchini Senegali. Jina hilo lometokana na maji yake yanavyonekana
|
Ziwa
Retba linaitwa Ziwa la Waridi, na kwa kuwa liko kilometa 30 tu kutoka mji mkuu
wa Dakar, Senegal, ambayo ipo Afrika ya
Magharibi,
Wageni
hulitembelea Ziwa Hilo ili kujionea kama kweli lina rangi ya waridi. Lahaula
ni kweli wafikapo hukuta kweli Ziwa Retba lina maji yanayong’aa na kwa kweli
yana rangi ya waridi yenye kupendeza.
Mwangaza
wa jua huathiri vijiumbe vilivyo majini na hivyo kutokeza rangi hiyo ya pekee.
Hata hivyo, kuna mambo mengine yenye kupendeza mbali na rangi ya ziwa hilo.
Ziwa
hilo lisilo na kina kirefu lina sakafu ya chumvi. Maji hayo yana chumvi nyingi
sana hivi kwamba mtu anaweza kuelea kwa urahisi.
Wageni fulani wanachukua
fursa hii kuelea kwenye ziwa hilo.
Mbali
na Utalii Ni wazi kwamba watu wengi nchini Senegal hutegemea Ziwa la Waridi
ili kupata riziki yao ya kila siku na kuyaendesha maisha yao.
Ziwa retba, muonekano wake kwa picha ya (Aerial photo) nyuzi 90. |
UFAHARI
WAKE MWINGINE:
NUKUU KUTOKA: http://m.wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102005686
(1). Kwenye kingo za
ziwa hilo, wafanyakazi wanapakia chumvi kwenye malori. Tunatua kidogo ili
kuwatazama wenyeji wakitoa chumvi kwenye ziwa. Tunawaona wanaume wakiwa wamesimama
kwenye ziwa wakivunja chumvi kwa sururu huku maji yakiwa yamewafika kifuani.
Wanachota
chumvi hiyo kwa kutumia sepetu na kuiweka kwenye vikapu kisha wanaipakia
mashuani. Mmoja wa wafanyakazi hao anatuambia kwamba inachukua saa tatu
kukusanya tani moja ya chumvi. Mashua hizo zimepakiwa chumvi nyingi sana hivi
kwamba inakuwa vigumu kuelea
(2). Zinapofika
ufuoni, wanawake wanapakua chumvi hiyo na kuibeba vichwani wakitumia ndoo,
(3). Wote wanafanya
kazi hiyo kwa upatano.
HAKIKA
DUNIA INA MENGI SANA TEMBEA UONE HAYO MENGI………
SOMA PIA ZAIDI KUHUSU ZIWA HILO PIA HAPA CHINI:
https://en.wikipedia.org/wiki/Lake_Retba
No comments:
Post a Comment