MATOKEO YA MECHI ZA UEFA ZILIZOPIGWA SIKU YA JANA
Thursday, 15 September 2016
14/09/2016 UEFA RESULTS
Thursday, 1 September 2016
NAMNA YA KUTATUA MSONGO WA MAWAZO KWA MABINTI
Msongo wa mawazo mara nyingi huwapata mabinti wadogo kuanzia
umri wa miaka 13-22, ambapo wakati huu kwa motto wa kike huwa ni kipindi cha
Kuvunja Ungo (Balehe) na hivyo huanza kushuhudia mabadiliko kadha wa kadha
katika miili yao.
KWA NINI
HILI HUTUKIA
Mabadiliko
ya kimwili. Kukua kwa haraka kunakotokea wakati
wa kubalehe kunaweza kumfanya msichana awe na mkazo sana, hasa ikiwa amechelewa
kukua au amewatangulia wasichana wenzake.
Marry * ambaye
sasa ana umri wa miaka 20 anasema hivi: “Nilikuwa kati ya wasichana wa kwanza
kuvaa sidiria, na niliona haya sana. Nilipojilinganisha na wasichana wengine,
nilijiona kana kwamba nina kasoro fulani.”
Mabadiliko ya kihisia. Jackline, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, anakumbuka hivi:
“Nilichanganyikiwa, sikuelewa kwa nini nilikuwa na furaha mchana na usiku
ulipofika nililia sana. Sikujua nilikuwa na tatizo gani. Nilishindwa kabisa
kudhibiti hisia zangu.”
Kuanza kupata hedhi. Msichana anayeitwa Vivian anasema: “Nilipopata hedhi kwa
mara ya kwanza nilishtuka sana ingawa mama yangu alikuwa ameniambia mengi
kuhusu kipindi hicho. Nilioga mara nyingi kwa siku kwa sababu nilijihisi mchafu
wakati wote. Na pia, kaka zangu watatu walinitania sana bila huruma. Walidhani
kwamba kupata hedhi ni jambo la kuchekesha.”
Kushinikizwa na marafiki. Debora, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, anakumbuka hivi:
“Nilipokuwa na umri wa kati ya miaka 12 na 14, marafiki wangu walinishinikiza
sana. Wanafunzi wenzangu walimchokoza yeyote aliyekuwa tofauti nao.”
MAMBO
UNAYOWEZA KUFANYA
Mtie moyo binti yako azungumzie
mkazo anaokabili. Mwanzoni,
anaweza kusita kuzungumzia jambo hilo. Lakini uwe mvumilivu na ujaribu
kuzungumza naye kwa Upole zaidi naamini atakuelewa na kuweza kuikabili hali
yake mujaraba.
.
Usipuuze mkazo anaopata binti yako. Kumbuka, hana uzoefu kama wewe kwa kuwa hajapitia mikazo
maishani, hivyo hana ujuzi wa kumwezesha kushughulika nayo na pia isitoshe ni
mabadiliko yanayotokea katika mwili wake ghafla tu.
Usimpangie binti yako mambo mengi ya kufanya. Vijana ambao wana mambo mengi sana ya kufanya “mara nyingi
huonyesha dalili za mkazo, kama vile maumivu ya kichwa na tumbo. Na hii hutokea
wakati Familia nyingi za kiAfrika na tamaduni zao humpangia zaidi mtoto wa kike
majukumu mengi kuliko Mtoto wa Kiume.
Hakikisha binti yako anapumzika vya
kutosha. Mara nyingi vijana hawalali vya
kutosha. Binti yako asipolala vya kutosha, uwezo wake wa kufikiri utapungua na
hivyo hataweza kukabiliana na mikazo wake unaomkabili.
Msaidie binti yako ajue jinsi ya
kukabiliana na mkazo. Kwa
wasichana wengi, mazoezi hupunguza mkazo.
Mfano: Wasichana wengi huona kwamba
wanapoandika hisia zao kwenye kitabu, (Diary) huweza kuwiasaidia kukabiliana na mkazo katika
fikra zao. Hivyo nawe Mzazi pia unaweza kumjengea Binti yako utamaduni huu wa
kujitunzia kumbukumbu zake mara kwa mara na hiyo inaweza kumfanya akaifahamu
hali yake vyema na impasavyo.
4HISTORY UP-DATES GO HERE ALSO: www.facebook.com/stewart.meena
Labels:
MAKALA / UCHAMBUZI
FUJO ZAIDI ZAZUKA MARA BAADA YA RAIS BONGO KUTANGAZWA MSHINDI WA UCHAGUZI NCHINI GABON
Fujo zimezuka katika mji mkuu wa Gabon, Libreville baada ya Rais Ali Bongo kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumamosi.
Mgombea wa upinzani Jean Ping amesema watu wawili wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya vikosi vya usalama kuvamia makao makuu ya chama chake.
Serikali imesema inawaandama "wahalifu wenye silaha" ambao awali walikuwa wameteketeza majengo ya bunge
Wakati huohuo:
Kwa upande wake mgombea huyo aliyeshindwa amesema pia vikosi vya usalama vimeshambulia makao yake makuu kwenye mji mkuu Libreville.
Jean Ping aliliambia shirika la habari la ufaransa AFP kuwa vikosi vya ulinzi vimetumia helkopta kushambulia kwa mabomu jengo hilo kabla ya kulivamia.
Amearifu kuwa watu 19 wamejeruhiwa baadhi yao wakipata majeraha mabaya.
Awali, polisi katika mji mkuu wa Gabon, Libreville walitumia mabomu ya kutoa machozi kuweza kuwatawanya wafuasi wa Jean Ping, waliokuwa wamejawa na hasira na ambao wanaamini kuwa matokeo hayo ya uchaguzi yalikuwa ya udanganyifu.
Ni kura chache tu, zilizomuwezesha Bwana Bongo kumshinda mpinzani wake na hatimaye kutangazwa kuwa mshindi, huku eneo analotoka akionekana kupata kura nyingi zaidi.
Ujumbe uliokuwa ukiwakilisha upinzani katika Tume ya Uchaguzi ulitoka nje na kukataa kusaini karatasi, zinazompa ushindi Rais Bongo.
Mwangalizi wa Uchaguzi huo, kutoka Jumuia ya Ulaya, Sara Crozier ameelezea hali ilivyo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville, kuwa ni ya wasiwasi.
Familia ya Bongo imekuwa madarakani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati kwa takriban miongo mitano.
SOURCE: BBC swahili
Labels:
HABARI KIMATAIFA
Thursday, 23 June 2016
FAHAMU KUHUSU HISTORIA MPIRA WA MIGUU (Soka)
LEO TUANGAZIE KUHUSU HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU (Soka)
Makalla na Stewart Meena.
https://www.facebook.com/stewart.meena
UTANGULIZI
MAANA YA SOKA.
Mpira wa miguu (pia soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya
wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili husika, kila timu ikiwa na wachezaji
kumi na mmoja.
Lengo hasa la
mchezo huu ni wachezaji kuonyesha uwezo wao wa kuumiliki mpira kwa kutumia
miguu na kuuingiza mpira katika wavu wa timu pinzani mara nyingi zaidi.
Matumizi ya mikono
ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango (golikipa) katika eneo maalumu na
wakati wa kurudisha mpira baada ya ya kutoka nje ya uwanja.
HISTORIA
YA MPIRA WA MIGUU
![]() |
|
Mfano
wa Mchoro unaoonyesha Mchezaji wa mpira wa miguu, Ugiriki Ya Kale.(karne ya 18-19)
|
Michezo mbalimbali ya
kuchezea mpira inaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia, Wachina,
Wajapani, Wakorea na Waitalia wote walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya
enzi zetu.
Wagriki
na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata
hivyo, ni nchini Uingereza pekee ambapo umbo la soka la kisasa lilianza kuibuka.
Kuibuliwa
kwake kulilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu na
Mpira wa Ragbi) yalitawanyika, ambapo Shirikisho la kwanza la soka lilibakia
nchini Uingereza.
Mnamo
Oktoba-1963, Vilabu-11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa (Freemason)
ili kujadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati
yao. Mkutano huo ulipelekea kuanzishwa kwa Shirikisho la Kandanda lililoitwa
‘Football Association’
Miongoni
mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na
kunyanganya kwa nguvu kama ilivyo kwa mchezo wa ragbi. Hapo ndio mwanzo wa Ragbi
kugawanyika na mchezo wa soka.
Miaka
minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA) lilikuwa na wanachama
50. Shindano la kwanza la kandanda lilianza mwaka huo. Kombe la FA- ambalo
lilifuatiwa na lile la Ligi ya Ubingwa miaka 17 baadaye.
Wachezaji
wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dove na Fergus Suter walikuwa wa kwanza
kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya kulipwa iliyohalalishwa
mnamo mwaka wa 1885.
Mwamko
huu ulipelekea kuanzishwa kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great
Britain). Baada ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho
yaliyofuatia ni ya Uskoti (1873), Wales (1875) na Eire (1880).
Kutokana
na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya Dunia, Soka ilizambaa kote
duniani. Mataifa mengine yalianzisha Mashirikisho ya Kandanda kufikia 1904
wakati Shirikisho la Soka Duniani
(FIFA) lilipoanzishwa.
Tokea
hapo mwanzo, kandanda ya kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali.
Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka
na kufikia 36 kwa mwaka 1925.
Mnamo mwaka1930,
kwa mara ya kwanza katika historia ya soka yalifanyika mashindano ya Kombe La
Dunia (FIFA) ambapo ilikuwa na wanachama wapatao-41. Na mshindi wa jumla kwa
mwaka huo wa kwanza alikuwa ni (URUGUAY) baada ya fainali
kufanyikia nchini humo, na nchi ya Uruguay iliifunga timu ya Argentina mabao
4-2. (pichani chini)
![]() |
| URUGUAY VS ARGENTINA -1930 |
SHIRIKISHO LA
KANDANDA DUNIANI (FIFA).
Shirikisho la
kandanda Duniani (FIFA) ndilo shirikisho kuu linalosimamia Kandanda duniani
(kwa nchi wanachama). Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi
mbalimbali, ambapo hadi kufikia mwaka wa 2000, FIFA ilikuwa na wanachama wapatao
204 kutoka pembe zote za dunia.
Shirikisho hili huandaa mashindano yote makuu duniani
yahusuyo soka la kimataifa. (michuano mikuu hufanyika kila baada ya miaka-4)
![]() |
| Uwanja wa Cape-Town Stadium uliotumika kwa Fainali za FIFA Barani Afrika kwa mara ya kwanza (Nchini Afrika Kusini-2010) |
HISTORIA ya
kombe la dunia iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1928 wakati Rais wa FIFA
wakati huo, Jules Rimet alipoamua kuandaa michuano mikubwa zaidi duniani
iliyohusisha mataifa mbalimbali, na Ufunguzi
wa michuano hiyo ukafanyika miaka miwili baadaye mnamo mwaka-1930 nchini
Uruguay na timu-13 zilialikwa kushiriki michuano hiyo.
Kuanzia hapo, FIFA ilifanikiwa kubadilisha miundo na
mifumo mbalimbali ya michuano tofauti, ambayo imepelekea kuanzishwa kwa soka la
kisasa zaidi.
Timu 32 zinapatikana baada ya mchakato wa mechi zakufuzu ambazo zinashirikisha timu kutoka mataifa 200 duniani kote.
Kabla ya kombe la dunia Mechi ya kwanza ya kimataifa
ya soka duniani ilichezwa mwaka 1872 kati ya England dhidi ya Scotland ingawa
katika kipindi hicho ilikuwa ni mara chache kwa mchezo wa soka kuchezwa nje ya Uingereza.
Hata hivyo, kuanzia mwaka 1900 mchezo wa soka ulipata umaarufu duniani kote na vyama vingi vya soka vikaanzishwa. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa kuchezwa nje ya Uingereza ilikuwa kati ya Ufaransa na Ubelgiji ambayo ilichezwa Paris,Mei 1904.
Mchezo huo ulisababisha kuanzishwa kwa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Mei 22, 1904.
Labels:
MAKALA / UCHAMBUZI
Subscribe to:
Posts (Atom)







