Msongo wa mawazo mara nyingi huwapata mabinti wadogo kuanzia
umri wa miaka 13-22, ambapo wakati huu kwa motto wa kike huwa ni kipindi cha
Kuvunja Ungo (Balehe) na hivyo huanza kushuhudia mabadiliko kadha wa kadha
katika miili yao.
KWA NINI
HILI HUTUKIA
Mabadiliko
ya kimwili. Kukua kwa haraka kunakotokea wakati
wa kubalehe kunaweza kumfanya msichana awe na mkazo sana, hasa ikiwa amechelewa
kukua au amewatangulia wasichana wenzake.
Marry * ambaye
sasa ana umri wa miaka 20 anasema hivi: “Nilikuwa kati ya wasichana wa kwanza
kuvaa sidiria, na niliona haya sana. Nilipojilinganisha na wasichana wengine,
nilijiona kana kwamba nina kasoro fulani.”
Mabadiliko ya kihisia. Jackline, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, anakumbuka hivi:
“Nilichanganyikiwa, sikuelewa kwa nini nilikuwa na furaha mchana na usiku
ulipofika nililia sana. Sikujua nilikuwa na tatizo gani. Nilishindwa kabisa
kudhibiti hisia zangu.”
Kuanza kupata hedhi. Msichana anayeitwa Vivian anasema: “Nilipopata hedhi kwa
mara ya kwanza nilishtuka sana ingawa mama yangu alikuwa ameniambia mengi
kuhusu kipindi hicho. Nilioga mara nyingi kwa siku kwa sababu nilijihisi mchafu
wakati wote. Na pia, kaka zangu watatu walinitania sana bila huruma. Walidhani
kwamba kupata hedhi ni jambo la kuchekesha.”
Kushinikizwa na marafiki. Debora, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, anakumbuka hivi:
“Nilipokuwa na umri wa kati ya miaka 12 na 14, marafiki wangu walinishinikiza
sana. Wanafunzi wenzangu walimchokoza yeyote aliyekuwa tofauti nao.”
MAMBO
UNAYOWEZA KUFANYA
Mtie moyo binti yako azungumzie
mkazo anaokabili. Mwanzoni,
anaweza kusita kuzungumzia jambo hilo. Lakini uwe mvumilivu na ujaribu
kuzungumza naye kwa Upole zaidi naamini atakuelewa na kuweza kuikabili hali
yake mujaraba.
.
Usipuuze mkazo anaopata binti yako. Kumbuka, hana uzoefu kama wewe kwa kuwa hajapitia mikazo
maishani, hivyo hana ujuzi wa kumwezesha kushughulika nayo na pia isitoshe ni
mabadiliko yanayotokea katika mwili wake ghafla tu.
Usimpangie binti yako mambo mengi ya kufanya. Vijana ambao wana mambo mengi sana ya kufanya “mara nyingi
huonyesha dalili za mkazo, kama vile maumivu ya kichwa na tumbo. Na hii hutokea
wakati Familia nyingi za kiAfrika na tamaduni zao humpangia zaidi mtoto wa kike
majukumu mengi kuliko Mtoto wa Kiume.
Hakikisha binti yako anapumzika vya
kutosha. Mara nyingi vijana hawalali vya
kutosha. Binti yako asipolala vya kutosha, uwezo wake wa kufikiri utapungua na
hivyo hataweza kukabiliana na mikazo wake unaomkabili.
Msaidie binti yako ajue jinsi ya
kukabiliana na mkazo. Kwa
wasichana wengi, mazoezi hupunguza mkazo.
Mfano: Wasichana wengi huona kwamba
wanapoandika hisia zao kwenye kitabu, (Diary) huweza kuwiasaidia kukabiliana na mkazo katika
fikra zao. Hivyo nawe Mzazi pia unaweza kumjengea Binti yako utamaduni huu wa
kujitunzia kumbukumbu zake mara kwa mara na hiyo inaweza kumfanya akaifahamu
hali yake vyema na impasavyo.
4HISTORY UP-DATES GO HERE ALSO: www.facebook.com/stewart.meena
No comments:
Post a Comment