Leo ni siku mpya ya historia nchini Zimbabwe, ambapo rais
mpya Mh. Emmerson Mnangagwa aliyekuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo chini ya
uongozi wa Rais Robert Mugabe aliyeliongoza taifa hilo kwa kuda mrefu zaidi
tokea mwaka 1980 nchi hiyo ya Zimbabwe ilipojipatia uhuru wake anatarajiwa
kuapishwa rasmi kuwa Rais wa mpito wa taifa hilo hadi pale uchaguzi
utakapofanyika upya.
Mtambue zaidi hapa:
Lakini je! Robert Mugabe naye ni nani.!?,
Msome hapa:
Mugabe ni Rais wa muda mrefu zaidi kuliongoza taifa hilo
tokea lilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni 1980, na yeye kuwa ndie rais
wa kwanza mweusi kuiongoza nnchi hiyo baada ya kutumikia kifungo gerezani
kisichopungua miaka-10 wakati wa utawala wa Wakoloni nchini humo kabla ya uhuru.
Ni juhudi za raisi huyu kupigana kufa na kupona pamoja na
wazalendo na Askari wachache watiifu waliopata mafunzo nchini Korea ya
kaskazini, kushirikiana pamoja kupigana vita na Wakoloni na hatimaye kujipatia
uhuru wao kamili kama taifa huru.
Upo usemi unaosema “ubaya mmoja huficha 100mazuri” ni
kweli, Binafsi namwona Mh. Mugabe kama mzalendo wa
kweli kama ilivyokuwa kwa Wazalendo wengine waBara hilli, Mfano J.k Nyerere wa Tanzania, Nkurumah-Ghana, Mzee
Jomo-Kenya, Ghadafi-Libya, na wengineo....
Kwa hatua hii, ya kuapishwa rais mpya wa mpito Emmerson
hadi uchaguzi utakapofanyika, umesubiriwa kwa hamu kubwa na Wazimbabwe walio
wengi kutokana na ukata wa maisha ulioikumba Zimbabwe kwa siku hizi za usoni,
ikiwemo kushuka kwa sarafu ya nnchi hiyo, kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwa
hatua yake ya kuwanyanyang’anya haki ya umiliki wa Mashamba raia wake wenye
asili ya kizungu ikiwemo kuwaondosha wazungu wote nchini humo.
Mugabe sio kiongozi mbaya, labda ubaya alioufanya ni kung’ang’ania
madaraka kwa muda mrefu, na hatua yake ya hivi majuma kadhaa yaliyopita
kumfukuza kazi makamu wake mkuu Emmerson, ambaye sasa ndio anategemea kuapishwa
leo kuwa rais wa mpito wa Zimbabwe.
Hatua hiyo ilipingwa vikali na wabunge wa nchi hiyo,
pamoja na wananchi kuandamana na mabango mtaani kushinikiza Rais huyo kujiuzulu,
kabla ya kutaka kumpatia nafasi yake ya Urais mkewe Bi.
Grace Mugabe hatua iliyoshinikiza jeshi la nchi hiyo kuingilia kati na
kumweka rais huyo kizuizini:
Baada ya mazungumzo , nakupitia katiba ya nchi hiyo
Mugabe alikubali kuachia madaraka yake, ili kupisha uchaguzi au rais mwingine
wa mpito anayependekezwa na wabunge wa nchi hiyo:
LAKINI HISTORIA NYINGINE ZINASEMAJE:
Source: BBC
Mwaka 1982 aliushutumu
upinzani kwa kujaribu kupindua serikali
Maelfu ya watu waliuawa
alipolituma jeshi lake lililopata mafunzo Korea Kaskizini, kuwakandamiza maadui
zake
Mwaka 1987,alibadilisha
katiba ili imruhusu kuwa rais na kuongeza mamlaka yake
Uchumi ulidororeka
baada ya mwaka 2000…
Wakati Mugabe aliagiza
kunyakua mashamba yaliomilikiwa na watu weupe yaliyokuwa kinara ya uchumi
Mfumuko wa bei
ulipelekea sarufi ya taifa kuwa bila thamani na hali nchini humo ikazidi
kudororeka
Baada ya uchaguzi wa
mwaka 2008, Mugabe alilazimika kugawanya mamlaka na kiongozi wa upinzani Morgan
Tsvangirai
Japo kulikuwa na ghasia
dhidi ya wafuasi wa Bw Tsvangirai katika kampeni za uchaguzi
Ndoa yake na Grace
Mugabe ,anayemzidi kwa maika 40, yaweza kuwa iliyomponza
Wengi walikasirishwa na
Grace kuandaliwa kuwa mrithi wake.
Jeshi limeonesha
kumtaka Emmerson Mnangagwa aliyefutwa kazi kama makamu wa Rais na Mugabe mwezi
Novemba
KUJIUZULU
Awali kabla ya hatua ya kuwekwa kuwekwa
kizuizini na jeshi, Spika wa bunge la Zimbabwe alitangaza kuwa rais Robert
Mugabe amejiuzulu .
Spika wa bunge Jacob Mudenda alisema
kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa
mabadiliko ya amani ya mamlaka kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati
za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.
Awali bwana Mugabe alikuwa amekataa
kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na
maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.
Amekuwa mamlakani tangu taifa hilo
lijipatie uhuru wake 1980.
Bwana Mugabe ameshinda uchaguzi wa
urais mara kadhaa lakini katika kipindi cha miaka 15 iliopita shughuli hiyo
imekumbwa na ghasia dhidi ya wapinzani wake
Ameongoza kipindi cha uchumi ulioanguka ambapo raia
wamezidi kuwa masiki zaidi ya walivyokuwa 1980
Hatua iliosababisha yeye kuanza
kung'atuliwa madarakani ni ile alipomfuta kazi makamu wake wa rais Emmerson
Mnangagwa wiki mbili zilizopita.
Hatua hiyo ilionekana na wengi kama ya
kutaka mkewe kumrithi
Iliwaudhi viongozi wa jeshi ambao
waliingilia kati na kumweka rais Mugabe katika kizuizi cha nyumbani.
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
amesema kuwa kujiuzulu kwa Mugabe kunaipatia Zimbabwe fursa ya kuwa na mwanzo
mpya kufuatia ukandamizaji uliotawala uongozi wa Mugabe.
Amesema kuwa Uingereza ambaye ni rafiki
wa zamani wa Zimbabwe atafanya kila awezalo kusaidia kufanyika kwa uchaguzi
ulio huru na haki na kujenga uchumi wa Zimbabwe.
Ubalozi wa Marekani mjini Harare umesema kuwa ni hatua ya
kihistoria na kuwapongeza raia wa Zimbabwe kwa kutoa sauti zao na kusema kwa
njia ya amani kwamba ni wakati wa mabadiliko.
Utawala
wa rais Mugabe umekuwa ukikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi, ikiwa ni
pamoja na kushuka kwa sarafu ya nchi hiyo.
Hali
mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira vilisababisha maandamano makubwa kote
nchini humo, wanaharakati na raia kwa ujumla wakimtaka rais Mugabe aachie
mamlaka.
Hata
hivyo Mugabe amekuwa akiyazima maandamano hayo na kuwatia nguvuni wapinzani
wake anaosema kuwa wanachochewa na mataifa ya kigeni. kutokana na vikwazo
kutoka mataifa ya magharibi.
Mugabe
amekuwa akikosolewa kwa kukandamiza upinzani.
Lakini
amejiuzulu rasmi tayari, je! Ninini kitajiri tena zimbabwe chini ya utawala wa
mpito wa Rais anayeapishwa leo Mh.Emmerson!? huku hofu ikizidi kutanda kwa
wachambuzi wa siasa kwa uthibitisho dhahiri uliotukia nchini Libya baada ya kupinduliwa
kwa ghadafi.
No comments:
Post a Comment