Ulishawahi kujiuliza Pumu
ni nini.! na husababishwa na nini.?
Pumu ni ugonjwa ambao unashambulia watu wa pande zote za dunia, na inakadiriwa kuwa
karibu watu milioni 300 wanaishi au kusumbuliwa na ugonjwa huu duniani
pote.
Pumu
ni ugonjwa ambao hushambulia watu wa jinsia zote na rika zote lakini mara
nyingi zaidi watu hupata ugonjwa huu tokea wakiwa utotoni, (mara nyingi watu
huhusisha na magonjwa ya kurithi).
Watoto
wengi huanza kupata dalili za ugonjwa huu wanapofikia umri wa miaka mitano,
huku Watoto walio kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na maradhi haya ni wale
wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, wale wanaolelewa kwenye mazingira yenye
moshi wa sigara na wale wanaozaliwa kwenye familia zenye kipato kidogo.
Mambo
mengine yanayochangia ni mtoto kuwa na mzio (allergy) wa kitu Fulani au
kkurithi kwa kuzaliwa na wazazi wenye asili ya kuwa na maradhi hayo, (Follow history of one of parent)
Kulingana
na tofauti za kijinsia, imeelezwa Watoto wa kiume ndio hupatwa ugonjwa huu zaidi ya watoto wa
kike lakini hali huweza kubadilika kadiri wanapokuwa wakubwa, huku mabinti
wakikumbwa na ugonjwa huu wakiwa katika umri wa kujiambua kuanzia (miaka8 na kuendelea)
Chanzo cha Pumu ni nini?
Mzio
(Allergy): Karibu watu wote wenye pumu wana
mzio (allergy) ambayo ni hali ya miili yao kutopenda vitu fulani pale
vinapovutwa na hewa mtu anapopumua, vikiliwa, vikiingizwa mwilini kwa kudungwa
sindano au vikigusa ngozi zao.
Lo
lote likitokea katika hayo mtu mwenye mzio anaweza akawashwa macho, akatokwa na
kamasi, akapumua akitoa sauti ya vifilimbi, akatokwa na vjipele juu ya ngozi au
akapata tumbo la kuharisha.
Baadhi
ya vitu vinavyosababisha hali hiyo ni aleji (allergens) ikichagizwa na protini
za wanyama, poleni ya mimea, nyasi, vumbi, mende na baadhi ya madawa
tuyatumiayo.
Katika
kujilinda, kinga za miili yetu zilizopo ndani ya damu mara nyingi husababisha
njia za kupitisha hewa kutoka na kwenda mapafuni kuvimba ambako kunahusishwa na
pumu.
Uchafuzi
Wa Mazingira: Dalili nyingi za pumu zinatokana na
uchafuzi wa mazingira na hasa wa majumbani kutokana na mvuke unaotokana na
vifaa vya kusafishia nyumba na rangi za kutani. Majiko ya kupikia yanayotumia
gesi yanayotoa hewa aina ya nitrogen oxide ambayo pia huhusishwa na tatizo la
pumu, na Watu wanaopika kwa kutumia gesi huweza kupatwa pia na matatizo haya
yanayoambatana na pumu kama kupumua kwa shida na kubanwa na pumu. Vitu vingine
kwenye mazingira vinavyoaminika kusababisha pumu ni sulfur dioxide, nitrogen
oxide, ozone, hali ya hewa ya baridi na hali ya kuwa na unyevunyevu mwingi
katika hewa (high humidity).
Kula
Kupita Kiasi: Watu wazima wenye uzito mkubwa
sana wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata pumu ukilinganisha na wale
wenye uzito wa kawaida. Utafiti unaonyesha kuwa hatari ya kupata pumu
isiyotokana na mzio (nonallergic asthma ) ni kubwa
zaidi kuliko ile inayotokana na mzio (allergic asthma).
zaidi kuliko ile inayotokana na mzio (allergic asthma).
Ujauzito
Na Uzazi: Jinsi uliovyoingia katika dunia hii ina
uhusiano na uwezekano wa kupata pumu baadaye, ambapo Watoto waliozaliwa kwa
operesheni wana asilimia 20 zaidi ya uwezekano wa kupata pumu baadaye kwenye maisha yao. Inawezekana kuwa maambukizi yanayoathiri
kinga za mwili kutokana na uwepo wa bacteria wakati wa operesheni yanahusika na tofauti hii.
operesheni wana asilimia 20 zaidi ya uwezekano wa kupata pumu baadaye kwenye maisha yao. Inawezekana kuwa maambukizi yanayoathiri
kinga za mwili kutokana na uwepo wa bacteria wakati wa operesheni yanahusika na tofauti hii.
Uvutaji
uliokithiri wa sigara (kwa wazazi)
Haswa Akinamama
wanaovuta sigara wakati wa ujauzito ndio hatarishi zaidi, kwani uvutaji huo wa
sigara husababisha watoto wao walioko matumboni kuwa na uwezo mdogo wa kupumua
na kuongeza hatari ya watoto wao watakaozaliwa kupata ugonjwa huu wa pumu. Utafiti umeonyesha kuwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda
wao (njiti)
wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuja kupata pumu baadaye.
wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuja kupata pumu baadaye.
Msongo Wa Mawazo: Kupatwa na msongo
wa mawazo
mara kwa mara kunaongeza uwezekano wa kupata pumu, moja ya sababu ni tabia za
mtu anapokuwa na msongo wa mawazo kama vile kuvuta sigara kunakochochewa na
msongo wa mawazo. Maelezo ya hapa karibuni yanaonyesha kuwa mfumo wa kinga za
mwili hubadilika mtu anapokuwa na msongo wa mawazo.
Urithi: Wazazi wanahusika
katika kumfanya mtoto awe na pumu, inakadiriwa kuwa katika watoto watano wenye
pumu, watatu huwa
ni pumu za kurithi kutoka kwa wazazi wao.
ni pumu za kurithi kutoka kwa wazazi wao.
NAMNA
YA KUKABILIANA NA TATIZO HILI AU KUWASAIDIA WALIOKUMBWA NA TATIZO HILI
Kutibu Pumu
Pumu ni ugonjwa wa
kudumu ambao haujapatiwa dawa ya kuuondoa moja kwa moja, na Tunapozungumzia
tiba ya pumu tunamaanisha ushirikiano wa pamoja wa daktari na mgonjwa au na (mzazi
wa mtoto mgonjwa) katika kuudhibiti ugonjwa huu ili:
-
Kuzuia
mgonjwa asirudiwe na matatizo ya mara kwa mara ya kukohoa, kubanwa pumzi na
mengineyo yanayoambatana na
ugonjwa huu
ugonjwa huu
-
Kupunguza
uwezekano wa kuzidiwa na kuhitaji huduma ya dharura.
-
Kuyaweka
mapafu katika hali nzuri wakati wote.
-
Kumwezesha
mgonjwa kushiriki katika shughuli za kawaida za kimaisha na kupata usingizi
mzuri,
-
Kuzuia
mgonjwa asibanwe na pumu na kusabibisha tiba za dharura,
Mgonjwa anahitaji
kuwa na mpango mzuri unaoelekeza namna ya kutumia dawa ipasavyo, namna ya kuzuia
mgonjwa asikumbane na vitu vinavyochochea pumu hiyo (asthma triggers), namna ya
kufuatilia jinsi mgonjwa alivyoweza kuudhibiti ugonjwa huu na namna ambavyo
mgonjwa atakavyoweza kupata huduma ya dharura endapo atazidiwa.
Tiba ya pumu huwa
inagawanywa kwenye makundi mawili; tiba ya kutoa msaada wa haraka na tiba ya
muda mrefu ya kudhibiti pumu.
Tiba ya kutoa msaada
wa haraka ni ile inayotolewa pale mgonjwa anapoona dalili za kubanwa pumu na
tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu inalenga kupunguza athari zinazotokea
kwenye njia za hewa na hivyo kuzuia kutokea kwa kubanwa na pumu.
Dawa za pumu huweza kutolewa
kama vidonge, lakini nyingi huwa kama unga au mvuke ambavyo mgonjwa atavitumia
kupitia kinywani mwake kwa kutumia kifaa kinachoitwa Inhaler (Pichani Chini).
Inhaler ni kifaa
kinavyosaidia dawa kupita kirahisi katika njia za hewa kuelekea kwenye mapafu.
TIBA YA PUMU YA KUTOA MSAADA WA HARAKA
Mgonjwa yeyote wa
pumu lazima awe na njia ya kupata msaada wa haraka ili kuzuia tatizo lisiwe
kubwa pale anapohisi dalili za kubanwa na pumu.
Chaguo la kwanza kwa
mgonjwa wa pumu la kupata msaada pale anapoanza kujihisi vibaya ni (Inhaled
short-acting beta2-agonists) Hizi ni dawa ambazo mtumiaji atazipata kupitia
kifaa kinachoitwa Inhaler.
Dawa hizi hufanya
kazi haraka sana na kulegeza misuli ya njia ya hewa iliyokaza pale mgonjwa
anapobanwa na pumu na hivyo kufungua njia ya hewa.
Vifaa hiivi vipo vya
aina tofauti, yafaa kumwuliza daktari wako kuhusu njia nzuri ya kukitumia kifaa
ulicho nacho.
Mgonjwa anatakiwa
kutumia inhaler mara tu anapoanza kusikia dalili za kubanwa na pumu, hivyo basi
mgonjwa anashauriwa kuwa na kifaa chake po pote alipo.
Kifaa hiki
kinashauriwa kisitumike zaidi ya mara mbili kwa wiki, endapo matumizi yanaanza
kuzidi idadi hiyo ni vizuri mgonjwa amwambie daktari wake kuhusu hali yake ili
aweze kubadilishiwa mpango wake wa kuudhibiti ugonjwa wa pumu.
Kifaa hiki hata
hivyo hakipunguzi tatizo la kuathirika kwa njia za hewa kama tutakavyoona
katika tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu.
Tiba Ya Muda Mrefu Ya Kudhibiti Pumu
Watu wengi wenye
pumu hutumia njia za muda mrefu za kudhibiti pumu kila siku ili kuzuia
uwezekano wa kutokea matatizo yanayoambatana na ugonjwa huo. Njia hizi za muda
mrefu hupunguza kuathirika kwa njia za hewa (kuvimba kwa ndani na kuwa sikivu
kuzidi kiwango) na hivyo kuondoa uwezekano wa kutokea kwa kubanwa na pumu. Njia
hizi hazisaidii kutoa msaada wa haraka kwa mgonjwa.
Watu wengi wenye
pumu hutumia corticosteroids (inhaled corticosteroids) kila siku ili kudhibiti
ugonjwa wa pumu walio nao.
Corticosteroids ni
kundi la kemikali ambazo hutengenezwa na figo au kwenye maabara ambazo hufanya
kazi nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kupunguza vimbe katika mwili.
Matumizi ya dawa hii
yameonyesha kuwa bora katika kuzuia kutokea kwa uvimbe na athari nyingine
kwenye njia za hewa zinazotokana na mtu kuvuta hewa yenye vitu visivyopendwa na
mwili wa muathirika.
Dawa hii hutumiwa
kwa kuvutwa kwa mdomo kutoka kwenye kifaa maalumu.
Matumizi ya inhaled
corticosteroids yana athari zake zikiwa ni pamoja na maambukizi ya mdomoni
(thrush) yanayosabababishwa na matone ya dawa hiyo kuangukia kwenye mdomo au
kooni.
Dawa hiyo pia huweza
kuathiri mboni za macho na kupunguza uimara wa mifupa endapo itatumika kwa muda
mrefu, pia Dawa nyingine zinazotumika katika udhibiti wa pumu wa muda mrefu ni
pamoja na:
-Cromolyn
-Omalizumab
-Inhaled long-acting beta2-agonists
-Leukotriene modifiers
-Theophylline
-Omalizumab
-Inhaled long-acting beta2-agonists
-Leukotriene modifiers
-Theophylline
Peak
Flow Meter
Hiki ni kifaa kidogo
cha kushikwa mkononi ambacho kinaonyesha jinsi hewa inavyotoka kutoka katika
mapafu ya mtumiaji.
Mtumiaji anapuliza
kwa mdomo kwenye kifaa hicho na ataonyeshwa alama alizopata ( peak flow number)
ambazo ni ishara ya ubora wa kiafya wa mapafu yake kwa wakati huo alipopuliza
kwenye kifaa hicho.
Mtumiaji anakitumia
kifaa hicho kwa namna na muda alioshauriwa na daktari wake, kwa mfano, daktari
anaweza kumshauri mgonjwa kukitumia kifaa hichio kila siku asubuhi na kunukuu
alama anazopata kisha kumpelekea baada ya kipindi fulani ili aweze kushauriwa
dawa za kuendelea kuzitumia.
Matumizi ya kifaa
hiki yanaweza kukupa taarifa mapema ya hali ya kubanwa na pumu inayotegemea
kukupata, ukajihami kwa kutumia dawa za kutoa msaada wa haraka na baadaye
kujipima tena baadaye ili kuona msaada uliopewa na dawa ulizozitumia.
Katika mada ya leo
tumeona ni nini chanzo cha ugonjwa huu wa pumu, njia zinazotumika kutoa msaada
wa haraka mtu anapobanwa na pumu na njia za muda mrefu za kudhibiti ugonjwa huu
wa pumu.
Kama hujasoma jinsi
pumu inavyotokea na aina mbalimbali za pumu, rejea au tembelea Chanzo hiki: “Ujue
Ugonjwa Wa Pumu.”
Maswali
kuhusu ugonjwa huu, na namna ya kukabiliana nao wasiliana na wataalamu wake kwa
kupiga namba hizi:
0655 858027
au 0756 181651
source:
No comments:
Post a Comment