Picha Na. Mtandao |
Utafiti mpya umebainisha Wanawake
wanaochelewa kuzaa wanaweza kukabiliwa
na tisho la kupata matatizo ya afya ya uzazi, kupata watoto wenye mtindio wa
ubongo pamoja na kuhatarisha maisha ya mama au mtoto mwenyewe.
Huu sio utafititi tu bali ni maoni ya madaktari mbalimbali ikiwemo daktari mmoja mkuu mjini
Nairobi Kenya.
Athari za mwanamke kuchelewa kupata mtoto wa kwanza
mapema ni pamoja na kukumbwa na utasa, tisho la kupata Saratani ya kizazi na
matiti pamoja na matatizo kadhaa wakati wa kujifungua mtoto wake wa kwanza
kwenye umri uliopitiliza.
Swali ni kuwa je! Ni upi umri sahihi kwa binti kupata
mtoto wa kwanza bila kuwepo na matatizo hayo?
Umri sahihi ulioshauriwa kitaalamu na watafiti na
madaktari bingwa wa maswala ya uzazi, umependekeza kuwa binti anatakiwa angalau
kujifungua mtoto wake wa kwanza anapofikisha umri kuanzia miaka 21-28, zaidi ya
hapo hutegemea bahati tu na mazingira aliyokulia muhusika.
Imebainika kuwa Wanawake wengi wanaofanya kazi maofisini,
huchelewa kuzaa mtoto wao wa kwanza hadi wanapofikisha umri kati ya miaka 35 na
kuendelea, badala ya kuzaa wakiwa na
umri unaoshauriwa kitaalamu wa miaka kuanzia 24-28.
Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya afya ya uzazi
kulingana na tofauti za kimaumbile, ikihusisha
mfumo mzima wa uzazi pamoja na historia ya matatizo ya tumbo la uzazi kwa wanawake.
Mfano:
KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BBC SWAHILI, kuhusiana na mada hii na mahojiano yao na
mtaalamu wa maswala ya afya ya uzazi Jijni Nairobi.....,
Mtaalamu
wa afya ya uzazi mjini Nairobi, Daktari John Ong'ech aliyehojiwa kuhusu hoja hii na BBC alinukuliwa akisema kuwa ''wanawake
kwanza wanataka kusoma masomo ambayo hayaishi, daima wako madarasani na ofisini na kuahirisha kuzaa
mtoto wao wa kwanza hii ni hatari
kubwa.''
Bwana
Ong'ech alisema kuwa wanaochelewesha kuzaa, wanaweza kupata Fibriods au uvimbe katika kizazi, na hata kupata magonjwa kama Saratani ya kizazi au HIV.
Fibroids
zinasababishwa na kuzagaa kwa homoni mwilini, kutokana na kutumia mbinu moja ya
kupanga uzazi kwa mda mrefu, ambayo ndiyo humletea muhusika madhara katika
mfumo wake wa uzazi.
Na ukichunguza kwa kina wengi wanaochelewa kujifungua, pia ndio wanaokabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hiyo ni kwa uchache tu, lakini hatari ni nyingi zaidi ya hapa, sasa chaguo ni kwako wewe binti unayesema bado upo-upo sana.
Lakini bado kuna utata mwingi na matarajio tofauti na mabinti au wanawake wenyewe watarajiwa kuhusiana na umri sahihi wa kubeba ujauzito na kujifungua mtoto wao wa kwanza, kwani kadiri siku zinavyozidi kwenda na mambo yanazidi kubadilika, lakini pia mitazamo tofauti miongoni mwao pia huzidi kushamiri.
Sio ajabu wazazi wakikwambia “mwanangu nataka mjukuu” au ukiwa na ujauzito wa kwanza wengine wasema “kuwa muangalifu zaidi mwanangu kwa kuwa uzao huu wa kwanza huenda ukakupelekesha sana” na nikweli mabinti wengi sana hupoteza uzao wa kwanza kwa kuzembea tu maneno ya wakuu, wakisahau “asiyesikia la mkuu....”
Nisiseme mengi kwa kuwa mimi sio mtaalamu sana wa mambo hayo, ila huu ni ushauri, na pia unaambiwa mwenye masikio na asikie, aonaye pia aone, lakini kubwa zaidi utafiti huu na tafiti nyinginezo kuhusu maswala ya uzazi usipende kuzipuuzia.
Ila yote kwa yote, najua umeshawahi kusikia umri ambao mwanamke akifikisha sio vyema kwake kubeba ujauzito (ikishauriwa hivyo kitaalamu) kwa kwakuwa mfumo wa uzazi na utaratibu wake huenda kubadilika na hatimaye kufikia ukomo kabisa.
Au endapo mwanamke akijifungua mtoto katika umri mkubwa, huenda akapata mtoto mwenye matatizo ya kiakili (mtindio wa ubongo) pamoja na matatizo ya mama husika ya kiuzazi nk.
UMRI SAHIHI WA MWANAMKE KUPATA MTOTO (KUZAA), Waweza Kuendelea hapa pia:
LINK: http://www.fikrapevu.com/umri-mzuri-kwa-mwanamke-kupata-mtoto-kuzaa/ na dokta Dr. Joachim Mabula 22/01/2014
Pia kwa kuwa nawe wajiandaa kuwa na familia yako, au unafamilia yako basi sio mbaya kama utajenga tabia ya kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo maswala ya uzazi kwa kuwaona wataalamu na madaktari kwa ushauri, ikiwemo wanandoa namna ya kuwekeana uangalifu wakati wa ujauzito na baada ya ujauzito. Maana
hapa kuna wale wenzangu na mimi, mkewe akiwa na mimba mpaka anajifungua hamna
hata siku moja wamekwenda naye kliniki kujua maendeleo na afya ya mtoto.!?
Hayaaa: Hebu tumalizie hapa, kuhusu muda sahihi unaoshauriwa kwa wanandoa kushiriki tendo la ndoa baada ya mama kujifungua, Hili ni swali ambalo limekuwa na utata pia..
Swali ni kuwa je! Ni muda gani sahihi au unaotosha kwa wanandoa kushiriki tendo la ndoa baada ya mama kujifungua.?
Hili ni swali lingine ambalo wanawake wengi, na waume pia wamekuwa wakijiuliza kuwa: baada ya kujifungua, “tutaanza kushiriki lini tena?”
Lakini kitaalamu ni kwamba uwe umejifungua kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida hutakiwi kushiriki tendo la ndoa mpaka wiki sita au na ziada ziishe (miezi2 kasoro), na hiyo huweza kuamuliwa pia na mwanamke mwenyewe baada ya muda huo kupita, kwa kujitafakari kama yuko tayari (amepona) au bado!, ili kuwezesha tendo hilo kuwa na raha badala ya karaha, nah ii ni kwa sababu za kisaikolojia zaidi (yaani uchovu na msongo wa mawazo)
Je kwanini sio vizuri kushiriki tendo la ndoa kabla ya wiki ya sita na ziada?
ENDELEA KUELIMIKA HAPA:
Baada ya kujifungua mtoto ni muda gani wanandoa wanaweza kushiriki tena tendo la ndoa: http://www.eyopah.com/2016/12/jeni-lini-unatakiwa-uanze-kushiriki.html
Nikutakie BAHATI NJEMA: TUMA (share) kwa wenzako pia nao waweze kupata elimu hii ya bure.
Maoni / Ushauri: usisite kuniandikia “inbox” kupitia:
E-mail: stewartmeena6@gmail.com
Facebook Page: https://www.facebook.com/stewart.meena Asante!
Na ukichunguza kwa kina wengi wanaochelewa kujifungua, pia ndio wanaokabiliwa na tisho la kuzaa kwa njia ya upasuaji au Caesarean .
Hiyo ni kwa uchache tu, lakini hatari ni nyingi zaidi ya hapa, sasa chaguo ni kwako wewe binti unayesema bado upo-upo sana.
Lakini bado kuna utata mwingi na matarajio tofauti na mabinti au wanawake wenyewe watarajiwa kuhusiana na umri sahihi wa kubeba ujauzito na kujifungua mtoto wao wa kwanza, kwani kadiri siku zinavyozidi kwenda na mambo yanazidi kubadilika, lakini pia mitazamo tofauti miongoni mwao pia huzidi kushamiri.
Sio ajabu wazazi wakikwambia “mwanangu nataka mjukuu” au ukiwa na ujauzito wa kwanza wengine wasema “kuwa muangalifu zaidi mwanangu kwa kuwa uzao huu wa kwanza huenda ukakupelekesha sana” na nikweli mabinti wengi sana hupoteza uzao wa kwanza kwa kuzembea tu maneno ya wakuu, wakisahau “asiyesikia la mkuu....”
Nisiseme mengi kwa kuwa mimi sio mtaalamu sana wa mambo hayo, ila huu ni ushauri, na pia unaambiwa mwenye masikio na asikie, aonaye pia aone, lakini kubwa zaidi utafiti huu na tafiti nyinginezo kuhusu maswala ya uzazi usipende kuzipuuzia.
Ila yote kwa yote, najua umeshawahi kusikia umri ambao mwanamke akifikisha sio vyema kwake kubeba ujauzito (ikishauriwa hivyo kitaalamu) kwa kwakuwa mfumo wa uzazi na utaratibu wake huenda kubadilika na hatimaye kufikia ukomo kabisa.
Au endapo mwanamke akijifungua mtoto katika umri mkubwa, huenda akapata mtoto mwenye matatizo ya kiakili (mtindio wa ubongo) pamoja na matatizo ya mama husika ya kiuzazi nk.
UMRI SAHIHI WA MWANAMKE KUPATA MTOTO (KUZAA), Waweza Kuendelea hapa pia:
LINK: http://www.fikrapevu.com/umri-mzuri-kwa-mwanamke-kupata-mtoto-kuzaa/ na dokta Dr. Joachim Mabula 22/01/2014
Pia kwa kuwa nawe wajiandaa kuwa na familia yako, au unafamilia yako basi sio mbaya kama utajenga tabia ya kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo maswala ya uzazi kwa kuwaona wataalamu na madaktari kwa ushauri, ikiwemo wanandoa namna ya kuwekeana uangalifu wakati wa ujauzito na baada ya ujauzito.
Hayaaa: Hebu tumalizie hapa, kuhusu muda sahihi unaoshauriwa kwa wanandoa kushiriki tendo la ndoa baada ya mama kujifungua, Hili ni swali ambalo limekuwa na utata pia..
Swali ni kuwa je! Ni muda gani sahihi au unaotosha kwa wanandoa kushiriki tendo la ndoa baada ya mama kujifungua.?
Hili ni swali lingine ambalo wanawake wengi, na waume pia wamekuwa wakijiuliza kuwa: baada ya kujifungua, “tutaanza kushiriki lini tena?”
Lakini kitaalamu ni kwamba uwe umejifungua kwa upasuaji au kwa njia ya kawaida hutakiwi kushiriki tendo la ndoa mpaka wiki sita au na ziada ziishe (miezi2 kasoro), na hiyo huweza kuamuliwa pia na mwanamke mwenyewe baada ya muda huo kupita, kwa kujitafakari kama yuko tayari (amepona) au bado!, ili kuwezesha tendo hilo kuwa na raha badala ya karaha, nah ii ni kwa sababu za kisaikolojia zaidi (yaani uchovu na msongo wa mawazo)
Je kwanini sio vizuri kushiriki tendo la ndoa kabla ya wiki ya sita na ziada?
ENDELEA KUELIMIKA HAPA:
Baada ya kujifungua mtoto ni muda gani wanandoa wanaweza kushiriki tena tendo la ndoa: http://www.eyopah.com/2016/12/jeni-lini-unatakiwa-uanze-kushiriki.html
Nikutakie BAHATI NJEMA: TUMA (share) kwa wenzako pia nao waweze kupata elimu hii ya bure.
Maoni / Ushauri: usisite kuniandikia “inbox” kupitia:
E-mail: stewartmeena6@gmail.com
Facebook Page: https://www.facebook.com/stewart.meena Asante!
No comments:
Post a Comment