Friday, 10 November 2017

NYANYA NI KIUNGO/ TUNDA AU MBOGA? ONGEZA UFAHAMU HAPA KUHUSIANA NA MNYANYA!

Miche ya Minyanya iliyopandwa kwa kufuata contua. Picha na iStock
 Ikiwa ungeulizwa kutaja tunda bora zaidi duniani , labda nyanya haitakuwa akilini mwako, Lakini unalolihitaji kulifahamu ni kuwa nyanya ni tunda na huzalishwa kwa wingi zaidi duniani kuliko tunda jingine lolote.

Baadhi ya watu hudai kuwa tunda la embe ndilo maarufu zaidi duniani kwa misingi kuwa linaliwa kwenye nchi nyingi zaidi kuliko matunda mengine!.

Lakini ikiwa utapima umaarufu kwa uzalishaji kote duniani, na uhitajio mkubwa zaidi kwa matumizi ya binadamu, utagundua kuwa nyanya zinaongoza (kama kiungo muhimu cha mboga/chakula) na na matunda mengine kama Embe, ndizi na mengineyo yapo nyuma ya tufaa kwa nyanya.
 
Tunda la nyanya huwa na muonekano wa rangi mbili (njano na Nyekundu) zikiwa zimeiva tayari kwa matumizi

Nchi inayoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa tunda la ndizi duniani ni India, ambapo Kuna zaidi ya tani 100 za ndizi ambazo huzalishwa kila mwaka.

Lakini kuhusu Nyanya, ambayo huweza kuliwa bila kupikwa (kama kwenye kachumbari) au kwa kupikwa (kwenye mboga/chakula), Uzalishaji wake duniani kote ikiwa ni tani 170 za nyanya, ambazo huzalishwa kila mwaka, na hivyo tunda hili kupita hata uzalishaji wa ndizi.

Wengi huchukulia nyanya kama mboga, lakini ukweli ni kwamba nyaya ni tunda kama nlivyokwambia kwa kuwa, kama ilivyo kwa matunda mengine Nyanya nayo ina mbegu hali ambayo huiweka katika familia ya kundi (mimea jamii) la matunda.

Kwa utofauti wa nyanya Kuna zaidi ya aina 20,000 ya nyanya duniani kote, kwa kujumuisha hata zile ziotazo maporini.

HISTORIA NA CHIMBUKO LA MCHE (Mmea) WA MNYANYA:

Muonekano wa Nyanya Nyekundu.

CHIMBUKO / Chanzo Wikipedia,

Mnyanya ni mmea, ambao daima huota na kukua kwa kutambaa, na hukuzwa kwa makusudi ya kutumiwa na watu, Matunda yake yanaitwa nyanya.

Miongoni mwa aina zaidi ya (makumi elfu) ya nyanya zinazozalishwa, kati ya hizo, nyingi sana huwa na rangi nyekundu haswaa pindi inapoiva, huku nyingine zikiwa na rangi ya manjano au machungwa.

Mnyanya huwa na urefu wa mita 1-3 na huwa na shina laini ambalo mara nyingi hujibebelesha kwenye mmea mwingine, au huitaji kushikishwa mimea mingine au miti kwa ajili iweze kutambaa na kuzaa matunda mengi zaidi.
 
Mche wa mnyanya ukiwa umetokeleza maua, ambayo huonekana kwa rangi ya njano. Picha na iStock
Majani yake huwa na urefu wa sentimeta 1-25, na petali zake hufikia 5-9, huku Majani ya shina la nyanya huwa na vinyweleo au (vimwiba vidogovidogo), Maua yake huwa na upana wa sentimita (sm-1-2), na huonekana kwa rangi ya manjano, na majani yake yakigawanyika sehemu tano (5leaf branches) na huvunwa kuanzia miezi3, 6 hadi mwaka mmoja.

Historia

Nyanya zikiwa zimevunwa shambani na kuwekwa kwenye matenka tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda viwandani vya kusindika nyanya hizo.

Asili ya mnyanya ni Amerika ya Kusini. Na historia yake huonesha kuwa mimea hii ilianzia nchini Peru, na Mimea hiyo ya mwanzo ya Peru ndiyo imekuja kuwa na aina hizi nyingi za nyanya tulizonazo duniani hivi wa leo.

Spishi moja ilisafirishwa kutoka Peru mpaka Meksiko (Mexico)  kwa ajili ya matumizi ya binadamu, na Ushahidi unaonyesha kuwa hapo awali mmea wake ulikuwa tunda dogo lenye rangi ya njano (kama zile ziotazo maporini).

Neno la Kiingereza ‘tomato’, lenye maana ya nyanya, limetoka ana Nsha ya Manati ‘lomatl’.

Mtaalamu wa mmea wa kifaransa, Joseph Pitton de Tournefort, alitoa jina la kisayansi ’Lycopersion esculum’ kwa nyanya, na wakati huo nyanya ilifikiriwa kuwa ina sumu ndiyo maana ilipewa jina la mito lenye maana ya tunda la mbwa mwitu.

Watu wa Acret na wengine wanaanza kutumia nyanya kwenye mapishi yao, wakti huo ikilimwa huko Peru, mnamo mwaka 500 K.K, Baadaye nyanya zilizobadilika na kuwa laini, kubwa kutoka kwenye mboga laini, na kuanza kushamiri huko Amerika ya Mwanzo, na inaaminika hii ndiyo asili ya nyanya tunazotumia sasa.
 
 
Kulingana na Andrew Smith, aliyeandika kitabu cha ‘The Tomato in America’, (Pichani juu) Nyanya zilianza sehemu za miinuko ya magharibi ya kusini mwa Amerika, Hata hivyo anasema hakuna ushahidi wa kuonesha kuwa nyanya zilikuwepo na hata kuliwa huko Peru kabla ya Wahispania hawajavamia na kuitawala nchi hiyo.

Baada ya utawala wa wahispania huko Amerika, Wahispania walisambaza nyanya kwenye makoloni yake yote mpaka Kusini mwa Asia na baadaye Asia yote, na baadaye walipieleka nyanya hiyohiyo Ulaya pia kwa biashara.

Nyanya zilizozalishwa wakati huo zilikuwa nzuri sana na bora, ndipo kilimo chake kilianza rasmi mnamo 1540 sehemu mbalimbali duniani ikiwemo eneo la miditeraniani.

Nyanya zilianza kuliwa rasmi huko Hispania mnamo 1600, baada ya kufuta uvumi wa kwanza wa kuwa nyanya ni sumu, ndipo Mwaka 1692, kilipatikana kitabu kinachoaminika kuwa kilichapishwa huko Naples, kilichokuwa kikielezea mapishi yaliyohusika zaidi na nyanya kama kiungo.

Uingereza
Kwa Kiswahili cha kienyeji, "Matomanti" ni miongoni mwa jamii maelfu za tunda la nyanya, zikipatikana sehemu zote, lakini kwa barani afrika Tanzania ikiwemo nyanya hizi hujiotea zenyewe maporini.
Nyanya zilikuwa hazizalishwi huko Uingereza mpaka 1590, kulingana na Smith, na Miongoni kati ya wakulima wa mwanzo alikuwa ni John Geral, daktari-Kinyozi.

Kitabu cha “Kitotou Geralds’s Iteneal’, kilichochapishwa mapema 1597, kilizua mjadala wa kwanza kuhusu nyanya huko uingereza, ambapo Gerald alijua kuwa nyanya zinaliwa huko Hispania na Italia.

Lakini aliamini majani yake yana sumu na tunda lake (nyanya) ni salama, Na hadi kufikia miaka ya 1200, watu wengi walikuwa tayari wanakula sana nyanya.

Afrika ya Kati

Nyanya ziliingia huko katika kilimo cha Mashariki ya kati kupitia John Barker, mnamo 1799-1825, na Mnamo karne ya 19, matumizi yake makubwa yalikuwa bado ni kama kiungo, na ndio iliyokuwa pekee ikitumika katika maeneo yale.

Nyanya ziliingia Mashariki ya kati kutumia njia mbili, Njia ya kwanza ni kupitia uturuki na Armenia na njia ya pili ni kupitia familia ya Mfalme wa Qatar, iliyokuwa mara kadhaa ikisafiri kuelekea ufaransa.

Na hivyo kuzidi kusambaa, kusambaa na kutapakaa sehemu zote barani Afrika ikiwemo Tanzania, wa hivi leo hakuna sehemu yoyote afrika hawazalishi mmea au tunda hili la nyanya.

KUMBUKA: Kwa Amerika Nzima

Utambuzi wa kwanza wa nyanya huko Amerika uliripotiwa na William Salmon, mnamo 1710, aliyesoma nyanya zilikuwa huko ambako leo kunajulikana zaidi kama South Carolina, na Inawezekana nyanya hizo zikawa zililetwa kutoka Karibeani, na mpaka sasa watu kadhaa huko wanaona au hudhani kuwa nyanya bado huwa zina sumu, na ni hatari kwa kuliwa, na hutumika sana kama mmea wa bustani na mapambo tu.

UMAARUFU USIOUDHANIA WA MATUMIZI YA NYANYA HIVI SASA DUNIANI:

Licha ya kuwa tunda hili, (ambalo hutumika kama kiungo maalumu cha chakula) kutumiwa sana na watu mbalimbali duniani, pamoja na kujizolea umaarufu wake kwa sifa hizo za mapishi.

Lakini, kwa baadhi ya nchi kama vile ilivyo Hispania nyanya hizi zimejipatia umaarufu wa tofauti sana kwa kuwa zimewekwa katika sherehe na mila za utamaduni za waHispania, ambapo hutumiwa kama kikolezeo cha sherehe husika.
 
 

Sherehe hizo za kijadi hujulikana kama “La tomatina” ambapo watu huadhimisha kwa kurushiana (kulengana) nyanya pamoja na kujitandaza miilini mwao.

“La Tomatina” ni sherehe ambazo huandaliwa kila mwaka hasa zaidi kwenye mji mdogo wa Uhispania uitwao (Bunol) ambapo katika sherehe hizo huweza kuwakusanya kwa pamoja wakaazi karibu elfu arobaini (40.000) ambao hurushiana nyanya zilizokwiva vyema.
 
 
kuendelea Zaidi kuhusu sherehe hizi za "La tomatina" Bofya hapa:
 
ASANTE KUENDELEA KUTUFUATILIA, TUNAKUAHIDI KUTOKUKUANGUSHA KATIKA KUKUHABARISHA: Maoni ushauri tutembelee kwenye ukurasa wetu wa Facebook kwa linki hii:
 

No comments:

Post a Comment