PHOTO BY: INTERNET |
UNAPOSIKIA NENO ROBOTI, huleta wazo gani akilini mwako?
Watu fulani huona roboti kuwa zenye faida na vitu
vinavyoweza kusaidia kazi. Wengine huziona kuwa tisho, yaani, mashine zenye
uwezo mkubwa wa akili ambazo siku moja zitachukua kazi zinazofanywa na
wanadamu. Hata hivyo, wengine huziona kuwa ni kazi za ubunifu tu wa kisayansi.
Vipi kwa siku hizi za leo? Kulingana na kadirio la
uchunguzi mmoja lililotolewa 2006 na Shirikisho la Kimataifa la Utengenezaji wa
Roboti, kuna roboti karibu milioni moja zinazofanya kazi viwandani ulimwenguni
pote, na karibu nusu ziko barani Asia.
Sasa swali Kubwa ni kuwa je! Kwa nini kuna uhitajio
mkubwa hivyo wa roboti hizo?
(Binadamu wamekuwa wavivu, Kupunguza
vitengo vya kazi zifanywazo na binadamu na zisizo za lazima, kuongeza ufanisi
zaidi wa kazi, kuvutia utalii, kufanya mapinduzi zaidi ya sayansi na teknolojia
au Wanasayansi kutaka kukosoa uumbaji na kutengeneza binadamu wao!?)
TUANGALIE KAZI ZINAZOFANYWA NA
ROBOTI
Ukweli ni kuwa, Roboti ni mfanyakazi ambaye haachi
kufanya kazi zake alizoamriwa kuzifanya muda wote, halalamiki, na anafanya kazi bila
kuchoka kwa saa 24 kila siku, siku saba kwa juma, Je! Binadamu ataweza.!?
Hivyo kazi inayofanywa na roboti katika viwanda vya kutokeza
bidhaa mbalimbali kama vile magari, vifaa vya umeme, na vifaa vya nyumbani, na
kwa Jina lao, (Roboti), linawafaa sana kwa kuwa linatokana na neno la Kicheki, (Robota),
linalomaanisha “kazi ya kulazimishwa.” Na Inakadiriwa kwamba
katika mwaka wa 2005, kulikuwa na roboti mmoja kwa kila wafanyakazi 10 katika
viwanda vya kutengeneza magari.!
Hata hivyo, siku hizi roboti hazitumiki kwenye viwanda
peke yake, bali pia Roboti za kisasa zina vifaa vya kutambua sauti, zinaweza
kutembea, zina mfumo wa mawasiliano usiounganishwa kwa nyaya, zina Mfumo wa
Kupokea Habari Kutoka kwa Satelaiti (GPS), na vifaa vya kupima joto, nguvu,
sauti zisizoweza kusikiwa na wanadamu, kemikali, na mnururisho.
Kwa kuwa sasa roboti zina nguvu zaidi na uwezo mwingi
kuliko zamani, zinafanya kazi ambazo miaka michache iliyopita ilionekana kwamba
haziwezi kufanya kutokana na zilivyofanyizwa.
KWA
MFANO:
Huduma MBALIMBALI. Katika
hospitali moja huko Uingereza, roboti inayofanya kazi katika chumba cha dawa,
inapokea na kuwapa wagonjwa dawa kwa sekunde chache. Shirika la Posta la
Marekani lina roboti ambazo zinatumiwa kukagua, kuinua na kupanga masanduku
yenye barua. Roboti nyingine pia hutumiwa kufikia maeneo yenye nafasi ndogo,
kama vile ndani ya mbawa za ndege, ili kufanya uchunguzi au marekebisho.
Mwandamani. Katika
makao ya kuwatunzia wazee huko Japani, wagonjwa waliozeeka kwa zamu wanapapasa
roboti ndogo yenye umbo la siri (Nyeti) iliyo na nywele, Roboti hiyo inaweza
kutambua na kuitikia inapoguswa, kunapokuwa na mwangaza, inaposikia sauti, joto
linapobadilika, na kulingana na inavyoshikwa.
Inaweza
kuiga tabia za mnyama kwa kupiga kelele kwa uchangamfu, kufumba na kufumbua
macho, na kuchezesha mapezi yake. Inasemekana kwamba roboti hiyo inatimiza
uhitaji wa msingi wa mwanadamu wa kuwa na mwandani na inatumiwa katika matibabu
pia.
Matibabu. Roboti yenye mikono
mitatu husimama kando ya mgonjwa, na Daktari husimama kando yake na kuangalia
kupitia kiwambo kikubwa kinachoonyesha moyo wa mgonjwa (Computer), kisha Daktari
huyo anaongoza mikono ya roboti hiyo inapofanya upasuaji wa kurekebisha mshipa
wa moyo.
Njia
hiyo huwezesha kufanya upasuaji bila kugusa viungo vingine vya mwili kwa sababu
roboti inaweza kuzifikia sehemu pekee zinazokusudiwa kupitia mtambo husika
uliokadiriwa (setting), na hilo hufanyika upesi sana na kwa ufanisi, na linapunguza
mshtuko wa mwili, uvujaji wa damu, na kumsaidia mgonjwa kupona haraka.
Majumbani. Unahitaji
tu kubonyeza swichi kwenye roboti yenye umbo la mviringo ili kufyonza uchafu
kwenye sakafu., Roboti hiyo huondoa uchafu kwenye maeneo yasiyo na vifaa
ikizunguka na kusonga kandokando ya ukuta, na hivyo kutambua mpangilio wa
nyumba ulivyo na inaweza kutambua mahali ngazi zilipo na kuziepuka.
Roboti
hiyo huacha kusafisha inapomaliza na kurudi mahali inapoongezwa
nguvu. Kuna roboti zaidi ya milioni mbili kama hizo zinazotumika kwa sasa
sehemu tofauti barani ulaya na Asia.
Angani. Roboti yenye
magurudumu sita inayoitwa Spirit inachunguza sayari Mihiri (Mars), Ikiwa na
vifaa vya kisayansi kwenye mikono yake, roboti hiyo kwasasa inachunguza udongo
na mawe.
Kwa
kutumia kamera iliyopandikizwa, roboti hiyo imepiga picha zaidi ya 88,500
kwenye sayari hiyo, zikitia ndani mchanga, mabonde, mawingu, dhoruba za
mchanga, mawio na machweo, na Ni mojawapo ya roboti mbili zenye magurudumu
zinazotumika kwenye sayari hiyo ya Mihiri.
Roboti kwenye sayari ya nne (Mihiri) umbali kutoka jua. Roboti hii ilitumwa na NASA inayohusika na sayansi na uchunguzi nnje ya dunia (Robot in the 4th Planet -Mars). Picha na NASA. |
Kazi ya Kutafuta na Kuokoa Watu. Chini ya vifusi vya chuma moto zilizopindika na zege za majengo
yaliyoanguka ya World Trade Towers, roboti 17 zinazotoshana na mpira wa
vikapu zilitumiwa kutafuta watu waliokwama kwenye majengo hayo, na Tangu wakati
huo, roboti za hali ya juu zaidi zimetengenezwa.
Chini ya Maji. Roboti
zinazojiendesha chini ya maji zinatumiwa na wanasayansi kuchunguza eneo la
dunia ambalo halijavumbuliwa, yaani, bahari, Roboti hizo hazina dereva, na Matumizi
yake mengine roboti hiyo chini ya maji ni pamoja na kutafuta na kuokoa watu,
kukagua nyaya za mawasiliano, kufuata nyangumi, na kuondoa mabomu yaliyotegwa
baharini.
ROBOTI ZINAFANANA NA WANADAMU KADIRI GANI?
Kwa karne nyingi zilizopita, Mwanadamu (Mwanasayansi) ametamani
kujenga roboti zinazofanana na kutenda kama mwanadamu, Lakini hilo limekuwa
jambo gumu sana kufanyika kwani kutokana na sayansi duni ya wakati huo
majaribio kadhaa yalishindikana.
“Ni
jambo rahisi zaidi kujenga kompyuta za hali ya juu, majengo marefu sana, au
hata kuchora ramani ya majiji mazima kuliko kuiwezesha mashine iwe na uwezo wa
kusonga kama mwanadamu, kuona, kunusa, kusikia, na kugusa, pia uwezo wa akili
unaokaribia ule wa mwanadamu,” nukuu kutoka jarida Business Week.
LAKINI: Baada ya miaka 11 ya utafiti wenye kina na
kutumia mamilioni ya dola, wataalamu kutoka Japani walitimiza jambo hilo la kustaajabisha
mnamo Septemba 1997, Kwa kufanikiwa kutengeneza roboti ya kwanza inayoweza
kutembea.
Tangu wakati huo, wataalamu wameendelea kutengeneza
roboti zinazoweza kupanda ngazi, kukimbia, kucheza dansi, kubeba vitu kwenye sinia,
kusukuma mkokotena, na hata kujiinua baada ya kuanguka chini!
WAKATI UJAO WA ROBOTI
Roboti zitatumiwaje wakati ujao? Kwa sasa, shirika la
NASA la Marekani linabuni roboti inayoweza kufanya kazi hatari angani. Bill
Gates alisema inawezekana kwamba “roboti zitatimiza fungu muhimu katika kuwasaidia
watu na zitakuwa waandamani (Wenza) kwa wazee.”
Vivyo
hivyo, katika ripoti iliyotolewa na serikali ya Japani, inatarajiwa kwamba
kufikia 2025 roboti zitashirikiana na wanadamu kutunza wagonjwa, kulea watoto,
na kufanya kazi za nyumbani.
Kufikia
2050, watafiti wanatarajia kwamba kutakuwa na timu ya mpira ya roboti itakayoshinda
timu ya wanadamu, Pia inatarajiwa kwamba baada ya makumi ya miaka, mashine
zenye uwezo wa akili unaopita ule wa wanadamu zitatokezwa.
UKWELI
NI KUWA: Ingawa watu fulani wana
matarajio hayo mazuri, si kila mtu anayekubaliana nao, kutokana na kwamba ni
Wanasayansi, lakini pia zitabakia kuwa tu ni mashine zilizofanyizwa na
Mwanadamu na huweza kupata hitilafu (kama ilivyo vyombo vingine vya moto kama
magari) muda au wakati wowote.
Pia hatuwezi kujua roboti hizo zitafanyiwa maendeleo kwa
mafanikio yapi mapya, itakapofika wakati huo ujao, Hata hivyo, ukweli utabaki
kuwa ukweli kuwa: Ni wanadamu tu ambao sikuzote watakuwa na uwezo wa kuonyesha upendo, kutenda kwa hekima, haki, na nguvu. Kwa nini? Biblia
inasema wazi kwamba tofauti na viumbe wengine, ni mwanadamu peke yake
aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu.
CHANZO MAKALA: JARIDA LA AMKENI LINALOTOLEWA NA MASHAHIDI WA JEHOVA KUPITIA
(MNARA WA MLINZI)
https://wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102008326#h=23
LAKINI PIA HIVI
KARIBUNI MWEZI WA OKTOBA 24-2017 SAUDI ILITOA URAIA KWA ROBOTI ILIYOKUWA NA
UWEZO MKUBWA ZAIDI:
ROBOTI SOFIA-Mwenye Urai wa Saudia Kwasasa |
Kwenye mkutano wa
mapendekezo ya uwezekaji katika siku zijazo uliofanyika kuanzia tarehe 24 hadi
tarehe 26 Oktoba mjini Riyadh, Saudi Arabia, roboti iitwayo Sophia (Pichani
Juu) imepewa uraia wa nchi hiyo rasmi. CHANZO-Redio China.
Lakini Saudi Arabia
haijaeleza maana kamili ya uraia wa roboti hiyo na itapewa uhuru kiasi gani wa
kuishi na kuchangamana na raia wengine nchini humo.
Lakini Roboti-Sofia yenyewe
ilipozungumzia uraia wake, imesema, "Naona fahari kubwa kupata hadhi hii ya kipekee, nimekuwa
roboti ya kwanza kupata uraia katika historia."
Hivi sasa kuzifanya roboti
kufanya kazi badala ya binadamu kunakabiliwa na vizuizi vingi vya kisheria,
lakini roboti zikipata uraia, baadhi ya vizuizi huweza kuondolewa.
Wakati ilipoulizwa kama
roboti inayofanana sana na binadamu itasababisha hofu ya binadamu au la, roboti
Sofia ilijibu, "Nilisanifiwa kwa
mujibu wa maadili ya binadamu, ikiwemo busara, wema na rehema, Nitajaribu kuwa
roboti inayoweza kuhisi hisia ya binadamu, na kuwasaidia binadamu kupata maisha
bora."
Sofia yenye sura ya
mwanamke ilisainifiwa na kampuni ya roboti ya Hanson ya Marekani, ina ngozi ya
mpira, inaweza kuiga ishara 62 za usoni, inaweza kutambua sura za binadamu,
kuelewa lugha, na kukumbuka mawasiliano na binadamu. Watu wengi wamesema
wanaiogopa sana Roboti hiyo kwa sababu hufanana sana na binadamu.
SWALI NI KUWA JE: Kama
ilivyo hulka na wasifu wa Wanadamu, je! Roboti nazo zitaweza kufikia wasifu huo
wa wanadamu kwa Asilimia 100%.?
MAONI YAKO YANAHITAJIKA: Waweza tembelea pia Hapa:
No comments:
Post a Comment