Maziwa hayo mawili makuu yanatajwa kuwa na aina mbalimbali za samaki wa mapambo, ambapo miongoni mwao wamo baadhi wenye sifa ya kutoa umeme (Electricity).
Ziwa Tanganyika lina urefu wa kilometa 673 na ni la pili duniani kwa kuwa na kina kirefu. Nafasi ya kwanza inachukuliwa na ziwa Baikar ambalo lipo katika nchi ya Urusi. Kina cha Ziwa Tanganyika ni kilometa 1.47 au meta 1470 na lina kilometa za ukubwa 18,900 na linachukua asilimia 17 ya maji yote baridi duniani.
Ziwa Tanganyika lina utajiri wa viumbe wa majini wa aina mbalimbali wakiwemo samaki, mamba, viboko na viumbe wengineo tofauti waishio majini.
Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Samaki katika maziwa (TAFIRI) unaonesha kuwa ziwa Tanganyika lina aina za samaki zaidi ya 400 ambazo zimekuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi kwa watu wanaoishi mwambao mwa ziwa hilo.
Kulingana
na sensa ya samaki ya mwaka 1999 iliyofanyika katika ziwa Tanganyika inaonesha
kuwa ziwa hilo linakadiriwa kuzalisha samaki kati ya tani laki1 na 65 elfu
(1.65.000) hadi Laki2 (200,000) zenye thamani ya dola za Marekani kiasi cha milioni
80 hadi milioni 100.
Kwa
upande wa Ziwa Nyasa, limezungukwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania, Malawi na Msumbiji.
Ziwa
hilo lipo kwenye usawa wa meta 500 kutoka usawa wa bahari ambapo kina cha ziwa
hilo ni karibu meta 750 na urefu wake ni karibu kilometa 1000.
Kulingana
na utafiti ambao ulifanywa katika ziwa hilo na Jumuiya ya Nchi zilizo kusini
mwa Afrika (SADC) kwa kushirikiana na nchi ya Uingereza kati ya mwaka 1991 hadi
1994 na mwaka 1996 hadi 2000, ziwa hilo lina kiasi cha tani 165,000 za samaki.
Kati
ya tani hizo za samaki, tani 35,000 za samaki ni jamii ya samaki wa maji ya juu
ambao wanaweza kuvuliwa bila kuathiri uvuvi kila mwaka. Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Nyasa, Oscar Mbyuzi anasema utafiti umebaini ziwa Nyasa lina
aina 503 ya samaki wa mapambo ambao hawapatikani sehemu nyingine duniani.
Hata
hivyo kati ya aina hizo, kama ilivyo katika ziwa Tanganyika, kuna aina ya
samaki adimu ambao wana uwezo wa kutoa umeme ambao pia ni samaki wa mapambo
wanaofahamika kwa jina la (Electric Fish)
Mhifadhi
wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma, Noelia Mnyonga
anawafahamu vyema samaki wanaotoa umeme waliopo katika ziwa Tanganyika na ziwa
Nyasa.
Mnyonga
anasema samaki hao ni kivutio adimu na cha kipekee duniani na kwamba wanaweza
kuwa chanzo muhimu cha mapato kwenye sekta ya utalii ambayo ni miongoni mwa
sekta zinazoongoza kwa kuchangia uchumi wa taifa.
“Samaki
wanaotoa umeme wakitangazwa kikamilifu ndani na nje ya nchi watalii wengi
watamiminika hapa nchini ili kufika kuwaona samaki hao wa ajabu na taifa kupata
fedha nyingi za kigeni,’’ anasema Bw. Mnyonga.
Anasema
utafiti unatakiwa kufanyika zaidi kuhusu samaki hao kuwa watalii na watafiti
wengi wanapenda kujifunza maisha ya viumbe adimu vya nchi kavu na majini wakiwemo
samaki hao wanaotoa umeme.
Bila
shaka watafiti wakipata fursa ya kufika katika maziwa haya mawili wangependa
kufanya utafiti wa kina kufahamu idadi ya samaki hao na tabia yao ya kutoa
umeme wanaposogelewa na adui.
Utafiti
wa awali ambao ulifanywa katika ziwa Tanganyika na mwanasayansi, Erick Fortune kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha nchini Marekani, unaonesha kuwa
samaki-umeme wana uwezo wa kutoa umeme kwa kutumia ogani umeme iliyopo kwenye
mikia ya samaki hao.
Utafiti huo unaonesha kuwa samaki huyo anaweza kutumia umeme unaozalishwa mwilini mwake kwenye mawindo yake, hata hivyo umeme unaozalishwa na samaki huyo ni kidogo na hauwezi kuleta madhara makubwa.
Hata
hivyo utafiti uliofanywa Februari mwaka huu na mtaalamu wa kimataifa, John Sullivan umebaini kuwepo kwa aina mbili za
samaki umeme katika nchi ya Gabon.
Sullivan
anazitaja aina hizo mbili za samaki umeme ambazo amezigundua kwenye Mto Ogooue uliopo katikati ya nchi ya Gabon kuwa
ni Cryptomyrus jina lenye maana ya samaki
aliyejificha na Ogoouensis jina lenye maana
ya mto ambao samaki huyo ametoka.
Mtafiti
huyo wa kimataifa anabainisha kuwa umeme unaotolewa na samaki umeme ni dhaifu
na hauwezi kuleta madhara kwa binadamu na kwamba samaki hao wana seli
zilizojificha juu ya ngozi zao ambazo zinawawezesha kutambua maadui na kuhisi
hatari hivyo huzalisha umeme kukabiliana na maadui zao na kwamba hutumia umeme
huo pia kwa mawasiliano na samaki wenzao.
Kulingana
na Sullivan, tangu mwaka 1977 hadi sasa, kuna zaidi ya aina 200 za samaki umeme
waliogundulika kwenye maji ya maziwa na mito katika Afrika, na Ni wajibu wa
serikali na wadau wengine wa utalii hususani Bodi ya Utalii Tanzania
kuhakikisha kuwa samaki huyu adimu duniani anatangazwa kwa kasi ndani na nje ya
nchi ili kuwavutia watalii na watafiti.
Vikta
Komba ambaye ni mkazi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma anasema wengi hawajui
kuhusu samaki umeme katika maziwa ya Tanzania lakini Anaamini vyombo vya habari
vikitangaza aina hii ya kivutio cha utalii wasomi na watalii wataingia kwa
wingi, na hivyo watu watakuwa na uelewa zaidi kuhusu samaki-umeme hao.
WITO WANGU KWA SERIKALI
Idara
ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na viongozi wa serikali katika mikoa
inayozunguka maziwa makuu hayo wanatakiwa kuwahamasisha wananchi kutumia fursa
hiyo ya utalii kwa kuongeza vipato vyao.
Ambapo
Wakazi wa maeneo hayo wanaweza kuanzisha utalii wa utamaduni ambao utawaongezea
kipato maradufu kutoka kwa watalii ambao watafika kuona utalii wa ikolojia kwa
kuwa watauza bidhaa za utalii wa kiutamaduni zikiwemo, ngoma za jadi, vifaa vya
jadi na vyakula vya asili.
Kwa
kuwa Nchi ya Tanzania imebahatika kuwa na maziwa makuu mengi kuliko nchi yeyote katika bara la Afrika, Maziwa hayo ni Tanganyika, Victoria, Nyasa, Rukwa, pamoja nay ale
madogo-madogo ya Manyara, Jipe, Ndutu, Ziwa Duluti, na mengineyo.
Maziwa
yote hayo, Yana rasilimali nyingi ambazo zinaweza kuiondoa nchi katika umaskini
uliokithiri, na mfano mzuri ni pamoja na gesi iliyogundulika kwenye ziwa nyasa,
lakini sio nyasa tu vipi tafiti mbalimbali zikielekezwa zaidi kwenye hayo
maziwa mengine.?
Tanzania
ilipigiwa kura na kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa kuwa na mazingira
rafiki katika sekta ya utalii huku Afrika Kusini ikishika nafasi ya tano.
Utafiti
uliofanywa na Shirika la Habari la CNN la nchini Marekani unaonesha kuwa
Tanzania inashika nafasi ya pili duniani, kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii
huku nchi ya Afrika ya Kusini ikishika nafasi ya 14.
Hata
hivyo, kulingana na utafiti huo, Tanzania katika mapato na miundombinu
yanayotokana na sekta ya utalii inashika nafasi ya 110 kati ya nchi 133
duniani, Aibu kubwa hii, sasa ni wasaa wa
serikali yetu sikivu kuamka na kuvitangaza vivutio vilivyopo kwa manufaa ya
taifa pamoja na wananchi wake.
MAONI YAKO MUHIMU: ukipendezwa tuachie hapa.
https://www.facebook.com/stewart.meena/
No comments:
Post a Comment