USHIRIKIANO WA
AJABU WA MKUNDEKUNDE KATIKA KURUTUBISHA UDONGO
Katika
udongo, kuna ushirikiano wa ajabu unaoendeleza uhai kati ya mimea fulani kama
mkundekunde (Pichani) na bakteria wapatikanao kwenye Ardhi ili kuendeleza uhai
na kuifanya ardhi husika kujitengenezea rutuba yake.
Fikiria
hili: Nitrojeni ni muhimu
ili mimea ikue na kuzaa, Lakini lazima gesi hiyo igeuzwe kuwa mchanganyiko wa
aina fulani kama vile amonia kabla ya kutumiwa na mimea.
Mikundekunde hufanya hilo liwezekane kwa kushirikiana kwa njia yenye
kunufaisha na bakteria inayoitwa rhizobia
ambapo Kupitia kemikali ya pekee, mikundekunde huvutia bakteria waiingie
katika mizizi yake.
Ingawa
bakteria na mmea huo si za jamii moja, gazeti Natural
History linasema,
hizo hufanya kazi pamoja “ili kutokeza kiungo kipya: mzizi wenye kifundo cha
kugeuza nitrojeni.” Bakteria huishi na kufanya kazi ndani ya kifundo hicho”.
“Ulimwenguni
pote kiwango cha nitrogenase
. . . kinaweza kutoshea ndani ya ndoo moja kubwa ya maji,”
linasema gazeti Natural
History.
Kwa
hiyo, kila molekuli ni muhimu! Lakini kuna tatizo kwenye kukamilisha umuhimu huo,
Katika mikunde Kimeng’enyaji hicho huharibiwa na oksijeni, lakini je! Suluhisho
la tatizo kama hili ni nini?
Mikundekunde
hutokeza kemikali fulani ya pekee ambayo huondoa oksijeni inayoweza kudhuru
mmea husika, kutengeneza mazingira salama ya bakteria-ardhi kuendelea kuishi,
kuhifadhi uhalisia wa mmea husika (kama una sukari kadiri unaendelea kukua ndivyo
unavyozidi kutengeneza sukari yake)
Mfano
dhahiri ni katika mabadilko ya mimea ya kupandikiza (yaani katika mche wa Limao, unaweza
kupandikiza mchungwa kwenye shina lake na pindi mmea unapokuwa unapata
machungwa yenye ladha tofauti iliyozoeleka kwa machungwa ya kawaida
yasiyopandikizwa )
Lakini kwa mikundekunde, Utando unaozunguka kifundo
hudhibiti kazi ya kugeuzwa kwa amonia, sukari, na virutubisho vingine kati ya
bakteria na mmea, Kama tu mimea mingine, mikundekunde nayo hufa kwanza ndio
ichipue, na Inapokufa, amonia hubaki katika udongo.
Hivyo, kwa kufaa kwake katika kurutubisha udongo,
mikundekunde imeitwa “mbolea ya kijani.” Na wakulima wanashauriwa
kitaaalamu kutumia mikunde kama njia asilia ya kurutubisha ardhi, punde tu
wanapovuna mazao mengine kwenye shamba husika “mfano mahindi” kama njia
mojawapo ya kupumzisha shamba husika.
Kwani tafiti zinasema kama misimu 3 iliyomalizika umelima
mahindi katika shamba lako, msimu huu yafaa upumzishe shamba lako pasipo kulima
ili walau ardhi hiyo irejeshe rutuba yake iliyokuwa nayo, au sivyo basi jenga
tabia ya kuchanganya mazao ndani ya msimu mmoja.
SOURCE:
Natural History Magazine & Amkeni-JW (watchtower)! & Wikipedia For further reading, click for underlined words above,
No comments:
Post a Comment