Thursday, 30 November 2017

USIYOYAJUA KUHUSU NDEGE WAHAMAO KUTOKA MABARA MENGINE KUJA AFRIKA AINA YA KORONGO.

Kila mwaka ifikapo tarehe 10/11 MEI ni siku ya (Destination Flyways; Migratory Birds) “maadhimisho ya ndege wahamao” Tanzania na duniani kiujumla, Yaliyoanza kuadhimishwa tokea mwaka2006. ambapo (TANAPA Tanzania) imekuwa ikiwataka wananchi wa tanzania kuendelea kutunza na kulinda maeneo yote ambayo ni mapitio ya ndege hao wahamao (Ardhi-Oevu-Ramsar), ambapo kama zilivyo nchi nyingine Tanzania ilisaini mkataba wa kuhifadhi maeneo yote ya Ardi-oevu mwaka2000.
 
Wapo aina nyingi sana za ndege wahamao (Aquatic birds) kutoka mabara mengine mbalimbali (Hasa Ulaya na Asia, kuja Afrika) na Miongoni mwa ndege hao ni pamoja na Heroe wadogo na Wakubwa (Flamingo-eng), pamoja na Korongo (Crane & Stock-Pichani) nk.
 
Uhamaji uho wa ndege hawa huweza kukabiliwa na vifo vya takribani robo ya ndege wote kufa, lakini kutokana na kuzaliana kwao kwa wingi hutoshea kuirudisha idadi yao baada ya muda mfupi.
Ambapo kuhamahama kwao huchagizwa na kutafuta malisho yao ambayo hupatikana zaidi maeneo ya mito (Yanapopatikana maji baridi) pamoja na kwenye eneo lenye umajimaji asilia ya Magadi (Ardhi-oevu), ambapo ndipo chakula chao na kirutubisho chao kikuu kwa ndege hawa kinakopatikana.
 
Kwa mfano wa sehemu hizo ni pamoja na Ziwa Natron lililoko Arusha, ambapo asilimia karibu (80%) ya ndege heroe (Lesser Flamingo) ndipo mazalia yao makuu duniani, huku wale wakubwa (Greater Flamingo) wakipatikana kwa wingi zaidi eneo la Ziwa Ndutu, Manyara nk. Huku ndege aina ya Korongo, wakifikilia maeneo hayohayo ikiwemo eneo la hifadhi ya Kilimanjaro.
 
SASA TUMWANGAZIE KORONGO:
 
 
Kuhusu manyoya yake:
 
KORONGO anapiga mabawa yake chini na kuruka juu. Kisha yeye huanza kujipinda-pinda akipaa bila juhudi yoyote kwa kusukumwa na upepo, Akibadili kidogo mwelekeo wa mabawa na mkia, ndege huyo huelea bila kupiga-piga mabawa yake.
 
Ni nini humwezesha kufanya hivyo kwa uwezo wa ajabu na kwa njia yenye kuvutia? Kinachomwezesha kufanya hivyo hasa ni manyoya yake.
 
Hakuna mnyama mwingine leo aliye na manyoya kama ya ndege. Ndege wengi wana manyoya ya aina tofauti-tofauti. Manyoya yanayoonekana kwa urahisi ni yale ya nje ambayo humfanya ndege awe na umbo laini linalomwezesha kupaa. Manyoya hayo yanatia ndani yale ya mabawa na ya mkia, yanayomwezesha ndege kuruka na kukatisha kona hewani.
 
Ndege mvumaji anaweza kuwa na manyoya ya nje 1,000 hivi, naye bata-maji zaidi ya 25,000.
 
Manyoya yamebuniwa kwa njia ya ajabu. Mhimili wa kati wa manyoya ambao unaitwa rachis unaweza kupindwa lakini ni imara sana. Vishina vya manyoya huota pande zote mbili za mhimili navyo kwa ujumla hutengeneza unyoya laini. Vishina hivyo huunganishwa kwa vitu vidogo vinavyoitwa barbule, na kufanyiza kitu kama zipu.
 
Ndege huunganisha sehemu hizo ndogo za manyoya yao wanapojisafisha. Wewe unaweza kufanya hivyo pia kwa kuvuta unyoya kati ya vidole vyako.
 
Pande mbili za manyoya ambayo hasa hutumiwa kwa kuruka hazilingani, yaani, upande wa mbele wa unyoya ni mwembamba kuliko upande wa nyuma. Muundo huo wa ajabu unafanya kila unyoya uwe kama bawa dogo. Pia ukiangalia chini ya mhimili utaona mfereji, ambapo Mfereji huo unasaidia mhimili uweze kujipinda bila kuvunjika.
 
ENDELEA HAPA: https://wol.jw.org/sw/wol/d/r13/lp-sw/102007250
 
UWEZO WA KUONA WA NDEGE
 


Rangi za manyoya ya ndege huwapendeza sana wanadamu, Lakini inawezekana kwamba manyoya yanawapendeza ndege wenyewe hata zaidi ya wanadamu.
 
Ndege wengine wana aina nne za chembe za kuwawezesha kutambuana rangi, huku wanadamu wana aina tatu tu, Uwezo huo wa ziada huwasaidia ndege hao kuona miale ambayo wanadamu hawawezi kuiona.
 
Wanadamu huona kwamba ndege wa kiume na wa kike wa jamii fulani wanafanana, lakini manyoya ya ndege wa kiume hutokeza miale hiyo kwa njia tofauti na ya ndege wa kike, hivyo kuchagiza Ndege wenyewe kutambuana jamii yao na familia yao kiujumla kwa kupitia utofauti huo, na hilo limeelezwa kitaalamu kuwasaidia ndege hao kutambua wenzi wao au hata watoto.
 
NDEGE WAHAMAO:


 
Korongo akiwa ni miongoni mwa ndege wengine wahamao (Migratory birds), hupendelea kuishi zaidi sehemu zenye umajimaji au unyevunyevu msimu wote wa mwaka, na pia maeneo hayo pekee ndipo wapatapo vitoweo vyao, na hiyo ndio sababu kubwa inayowafanya kuhamahama mara kwa mara sehemu waliyopo kunapotokea mabadiliko ya hali ya hewa tofauti na waliyoizoea.

Ndege wengine wahamao ni pamoja na Penguins, Auks, Puffins, Ducks, Geese, Swans, Loons, Grebes, Herons, Egrets.
(Kwa kubofya kwenye Majina ya ndege hao, Mfano: “Penguins” utapelekwa kwenye picha ya ndege husika)
Mguu wa Korongo
 
Korongo haitaji viatu na wala hagandi hata akiwa amesimama miguu mitupu juu ya barafu au maji, swali ni kuwa je! Ndege huyu hudumishaje kiwango cha joto mwilini mwake?
Njia moja kuu ni kupitia mfumo wa kudumisha joto ulio miilini mwao, ambapo Mfumo huo wa kudumisha joto una mrija ulio na umajimaji wenye joto na mwingine ulio karibu na huo wenye umajimaji ya baridi.
Umajimaji kwenye mirija hiyo ukielekea upande mmoja ni nusu ya kiwango cha joto kitakachopitishwa, Lakini umajimaji ukielekea pande tofauti kiwango chote cha joto kitapitishwa.
Mfumo huo tata wa kudumisha joto mwilini mwa Ndege Korongo, unapunguza kiwango cha joto cha damu inayoelekea miguuni hadi karibu igande na kisha huipasha joto damu hiyo inaporudi katika mzunguko wake.
Mtaalamu wa ndege, Gary Ritchison, anaandika hivi kuhusu ndege wanaoishi katika maeneo yenye baridi: “Mfumo huo wa kudumisha joto hufanya kazi vizuri sana hivi kwamba wanadamu wameuiga katika ujenzi ili kuzuia kupoteza nishati.”
Je, mfumo huo wa kudumisha joto katika miguu ya korongo ulijitokeza wenyewe? Kama wanasayansi wanavyoamini kila kitu kilijifanyiza chenyewe (Theory) Au ni kwamba, ulibuniwa na aliyewaumba!?
 

Sunday, 26 November 2017

FAHAMU JAPO KWA UCHACHE KUHUSU UGONJWA WA PUMU!


Ulishawahi kujiuliza Pumu ni nini.! na husababishwa na nini.?
 
Pumu ni ugonjwa ambao unashambulia watu wa pande zote za dunia, na inakadiriwa kuwa karibu watu milioni 300 wanaishi au kusumbuliwa na ugonjwa huu duniani pote.
Pumu ni ugonjwa ambao hushambulia watu wa jinsia zote na rika zote lakini mara nyingi zaidi watu hupata ugonjwa huu tokea wakiwa utotoni, (mara nyingi watu huhusisha na magonjwa ya kurithi).
Watoto wengi huanza kupata dalili za ugonjwa huu wanapofikia umri wa miaka mitano, huku Watoto walio kwenye hatari kubwa zaidi ya kupatwa na maradhi haya ni wale wanaozaliwa wakiwa na uzito mdogo, wale wanaolelewa kwenye mazingira yenye moshi wa sigara na wale wanaozaliwa kwenye familia zenye kipato kidogo.
Mambo mengine yanayochangia ni mtoto kuwa na mzio (allergy) wa kitu Fulani au kkurithi kwa kuzaliwa na wazazi wenye asili ya kuwa na maradhi hayo, (Follow history of one of parent)
Kulingana na tofauti za kijinsia, imeelezwa Watoto wa kiume ndio hupatwa ugonjwa huu zaidi ya watoto wa kike lakini hali huweza kubadilika kadiri wanapokuwa wakubwa, huku mabinti wakikumbwa na ugonjwa huu wakiwa katika umri wa kujiambua kuanzia (miaka8 na kuendelea)

Chanzo cha Pumu ni nini?
Mzio (Allergy): Karibu watu wote wenye pumu wana mzio (allergy) ambayo ni hali ya miili yao kutopenda vitu fulani pale vinapovutwa na hewa mtu anapopumua, vikiliwa, vikiingizwa mwilini kwa kudungwa sindano au vikigusa ngozi zao.
Lo lote likitokea katika hayo mtu mwenye mzio anaweza akawashwa macho, akatokwa na kamasi, akapumua akitoa sauti ya vifilimbi, akatokwa na vjipele juu ya ngozi au akapata tumbo la kuharisha.
Baadhi ya vitu vinavyosababisha hali hiyo ni aleji (allergens) ikichagizwa na protini za wanyama, poleni ya mimea, nyasi, vumbi, mende na baadhi ya madawa tuyatumiayo.
Katika kujilinda, kinga za miili yetu zilizopo ndani ya damu mara nyingi husababisha njia za kupitisha hewa kutoka na kwenda mapafuni kuvimba ambako kunahusishwa na pumu.
Uchafuzi Wa Mazingira: Dalili nyingi za pumu zinatokana na uchafuzi wa mazingira na hasa wa majumbani kutokana na mvuke unaotokana na vifaa vya kusafishia nyumba na rangi za kutani. Majiko ya kupikia yanayotumia gesi yanayotoa hewa aina ya nitrogen oxide ambayo pia huhusishwa na tatizo la pumu, na Watu wanaopika kwa kutumia gesi huweza kupatwa pia na matatizo haya yanayoambatana na pumu kama kupumua kwa shida na kubanwa na pumu. Vitu vingine kwenye mazingira vinavyoaminika kusababisha pumu ni sulfur dioxide, nitrogen oxide, ozone, hali ya hewa ya baridi na hali ya kuwa na unyevunyevu mwingi katika hewa (high humidity).
Kula Kupita Kiasi: Watu wazima wenye uzito mkubwa sana wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata pumu ukilinganisha na wale wenye uzito wa kawaida. Utafiti unaonyesha kuwa hatari ya kupata pumu isiyotokana na mzio (nonallergic asthma ) ni kubwa
zaidi kuliko ile inayotokana na mzio (allergic asthma).
Ujauzito Na Uzazi: Jinsi uliovyoingia katika dunia hii ina uhusiano na uwezekano wa kupata pumu baadaye, ambapo Watoto waliozaliwa kwa
operesheni wana asilimia 20 zaidi ya uwezekano wa kupata pumu baadaye kwenye maisha yao. Inawezekana kuwa maambukizi yanayoathiri
kinga za mwili kutokana na uwepo wa bacteria wakati wa operesheni yanahusika na tofauti hii.
Uvutaji uliokithiri wa sigara (kwa wazazi)
 

Haswa Akinamama wanaovuta sigara wakati wa ujauzito ndio hatarishi zaidi, kwani uvutaji huo wa sigara husababisha watoto wao walioko matumboni kuwa na uwezo mdogo wa kupumua na kuongeza hatari ya watoto wao watakaozaliwa kupata ugonjwa huu wa pumu. Utafiti umeonyesha kuwa watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao (njiti)
wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuja kupata pumu baadaye.
Msongo Wa Mawazo: Kupatwa na msongo wa mawazo mara kwa mara kunaongeza uwezekano wa kupata pumu, moja ya sababu ni tabia za mtu anapokuwa na msongo wa mawazo kama vile kuvuta sigara kunakochochewa na msongo wa mawazo. Maelezo ya hapa karibuni yanaonyesha kuwa mfumo wa kinga za mwili hubadilika mtu anapokuwa na msongo wa mawazo.
Urithi: Wazazi wanahusika katika kumfanya mtoto awe na pumu, inakadiriwa kuwa katika watoto watano wenye pumu, watatu huwa
ni pumu za kurithi kutoka kwa wazazi wao.
NAMNA YA KUKABILIANA NA TATIZO HILI AU KUWASAIDIA WALIOKUMBWA NA TATIZO HILI
Kutibu Pumu
Pumu ni ugonjwa wa kudumu ambao haujapatiwa dawa ya kuuondoa moja kwa moja, na Tunapozungumzia tiba ya pumu tunamaanisha ushirikiano wa pamoja wa daktari na mgonjwa au na (mzazi wa mtoto mgonjwa) katika kuudhibiti ugonjwa huu ili:
-      Kuzuia mgonjwa asirudiwe na matatizo ya mara kwa mara ya kukohoa, kubanwa pumzi na mengineyo yanayoambatana na
ugonjwa huu
-      Kupunguza uwezekano wa kuzidiwa na kuhitaji huduma ya dharura.
-      Kuyaweka mapafu katika hali nzuri wakati wote.
-      Kumwezesha mgonjwa kushiriki katika shughuli za kawaida za kimaisha na kupata usingizi mzuri,
-      Kuzuia mgonjwa asibanwe na pumu na kusabibisha tiba za dharura,
Mgonjwa anahitaji kuwa na mpango mzuri unaoelekeza namna ya kutumia dawa ipasavyo, namna ya kuzuia mgonjwa asikumbane na vitu vinavyochochea pumu hiyo (asthma triggers), namna ya kufuatilia jinsi mgonjwa alivyoweza kuudhibiti ugonjwa huu na namna ambavyo mgonjwa atakavyoweza kupata huduma ya dharura endapo atazidiwa.
Tiba ya pumu huwa inagawanywa kwenye makundi mawili; tiba ya kutoa msaada wa haraka na tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu.
Tiba ya kutoa msaada wa haraka ni ile inayotolewa pale mgonjwa anapoona dalili za kubanwa pumu na tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu inalenga kupunguza athari zinazotokea kwenye njia za hewa na hivyo kuzuia kutokea kwa kubanwa na pumu.
Dawa za pumu huweza kutolewa kama vidonge, lakini nyingi huwa kama unga au mvuke ambavyo mgonjwa atavitumia kupitia kinywani mwake kwa kutumia kifaa kinachoitwa Inhaler (Pichani Chini).
Inhaler ni kifaa kinavyosaidia dawa kupita kirahisi katika njia za hewa kuelekea kwenye mapafu.
TIBA YA PUMU YA KUTOA MSAADA WA HARAKA
Mgonjwa yeyote wa pumu lazima awe na njia ya kupata msaada wa haraka ili kuzuia tatizo lisiwe kubwa pale anapohisi dalili za kubanwa na pumu.
Chaguo la kwanza kwa mgonjwa wa pumu la kupata msaada pale anapoanza kujihisi vibaya ni (Inhaled short-acting beta2-agonists) Hizi ni dawa ambazo mtumiaji atazipata kupitia kifaa kinachoitwa Inhaler.
Dawa hizi hufanya kazi haraka sana na kulegeza misuli ya njia ya hewa iliyokaza pale mgonjwa anapobanwa na pumu na hivyo kufungua njia ya hewa.
Vifaa hiivi vipo vya aina tofauti, yafaa kumwuliza daktari wako kuhusu njia nzuri ya kukitumia kifaa ulicho nacho.



Mgonjwa anatakiwa kutumia inhaler mara tu anapoanza kusikia dalili za kubanwa na pumu, hivyo basi mgonjwa anashauriwa kuwa na kifaa chake po pote alipo.
Kifaa hiki kinashauriwa kisitumike zaidi ya mara mbili kwa wiki, endapo matumizi yanaanza kuzidi idadi hiyo ni vizuri mgonjwa amwambie daktari wake kuhusu hali yake ili aweze kubadilishiwa mpango wake wa kuudhibiti ugonjwa wa pumu.
Kifaa hiki hata hivyo hakipunguzi tatizo la kuathirika kwa njia za hewa kama tutakavyoona katika tiba ya muda mrefu ya kudhibiti pumu.
Tiba Ya Muda Mrefu Ya Kudhibiti Pumu
Watu wengi wenye pumu hutumia njia za muda mrefu za kudhibiti pumu kila siku ili kuzuia uwezekano wa kutokea matatizo yanayoambatana na ugonjwa huo. Njia hizi za muda mrefu hupunguza kuathirika kwa njia za hewa (kuvimba kwa ndani na kuwa sikivu kuzidi kiwango) na hivyo kuondoa uwezekano wa kutokea kwa kubanwa na pumu. Njia hizi hazisaidii kutoa msaada wa haraka kwa mgonjwa.
Watu wengi wenye pumu hutumia corticosteroids (inhaled corticosteroids) kila siku ili kudhibiti ugonjwa wa pumu walio nao.
Corticosteroids ni kundi la kemikali ambazo hutengenezwa na figo au kwenye maabara ambazo hufanya kazi nyingi mwilini ikiwa ni pamoja na kupunguza vimbe katika mwili.
Matumizi ya dawa hii yameonyesha kuwa bora katika kuzuia kutokea kwa uvimbe na athari nyingine kwenye njia za hewa zinazotokana na mtu kuvuta hewa yenye vitu visivyopendwa na mwili wa muathirika.
Dawa hii hutumiwa kwa kuvutwa kwa mdomo kutoka kwenye kifaa maalumu.
 
Matumizi ya inhaled corticosteroids yana athari zake zikiwa ni pamoja na maambukizi ya mdomoni (thrush) yanayosabababishwa na matone ya dawa hiyo kuangukia kwenye mdomo au kooni.
Dawa hiyo pia huweza kuathiri mboni za macho na kupunguza uimara wa mifupa endapo itatumika kwa muda mrefu, pia Dawa nyingine zinazotumika katika udhibiti wa pumu wa muda mrefu ni pamoja na:
-Cromolyn
-Omalizumab
-Inhaled long-acting beta2-agonists
-Leukotriene modifiers
-Theophylline
Peak Flow Meter
Hiki ni kifaa kidogo cha kushikwa mkononi ambacho kinaonyesha jinsi hewa inavyotoka kutoka katika mapafu ya mtumiaji.
Mtumiaji anapuliza kwa mdomo kwenye kifaa hicho na ataonyeshwa alama alizopata ( peak flow number) ambazo ni ishara ya ubora wa kiafya wa mapafu yake kwa wakati huo alipopuliza kwenye kifaa hicho.
Mtumiaji anakitumia kifaa hicho kwa namna na muda alioshauriwa na daktari wake, kwa mfano, daktari anaweza kumshauri mgonjwa kukitumia kifaa hichio kila siku asubuhi na kunukuu alama anazopata kisha kumpelekea baada ya kipindi fulani ili aweze kushauriwa dawa za kuendelea kuzitumia.
Matumizi ya kifaa hiki yanaweza kukupa taarifa mapema ya hali ya kubanwa na pumu inayotegemea kukupata, ukajihami kwa kutumia dawa za kutoa msaada wa haraka na baadaye kujipima tena baadaye ili kuona msaada uliopewa na dawa ulizozitumia.
Katika mada ya leo tumeona ni nini chanzo cha ugonjwa huu wa pumu, njia zinazotumika kutoa msaada wa haraka mtu anapobanwa na pumu na njia za muda mrefu za kudhibiti ugonjwa huu wa pumu.
Kama hujasoma jinsi pumu inavyotokea na aina mbalimbali za pumu, rejea au tembelea Chanzo hiki: Ujue Ugonjwa Wa Pumu.
Maswali kuhusu ugonjwa huu, na namna ya kukabiliana nao wasiliana na wataalamu wake kwa kupiga namba hizi: 0655 858027 au 0756 181651
source: