Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Friday, 27 October 2017

ITAMBUE BETRI MPYA YA MAGARI INAYOHITAJI KUCHAJIWA KWA DAKIKA 6 TU.


IMAGE: By Internet


Kampuni ya Toshiba ya Japan imesanifu betri mpya ya magari yenye ukubwa wa mkono ambayo inahitaji kuchajiwa kwa dakika 6 tu tofauti na zile nyingine za Oxide zinazohitaji masaa8-10.

Tofauti na betri nyingine za Li-ion ambazo ncha hasi zilitengenezwa na grafati, betri mpya imetengenezwa na Niobium Titanium Oxide, ambayo inaleta nishati nyingine na inaweza kuchajiwa kwa muda mfupi sana.

Betri za kawaida za magari zikichajiwa kwa nusu saa umeme utafikia asilimia 80, lakini betri mpya ikichaji kwa dakika 6, umeme utafikia asilimia 90. Magari ya majaribio ya kampuni hiyo yalikwenda kilomita 320 baada ya kuchajiwa kwa dakika 6 tu.

Aidha, betri mpya ikichajiwa na kutumiwa kwa mara 5000, bado ina zaidi ya asilimia 90 ya ujazo wa betri mpya, na inaweza kuchajiwa katika mazingira baridi yenye joto la nyuzi 10 chini ya sifuri sentigredi.

Kampuni ya Toshiba itaendelea kuboresha betri hiyo, na kujaribu kuuza bidhaa rasmi ifikapo mwaka 2019.

HABARI KAMILI ENDELEA HAPA CHINI KWENYE LINK:

source:
https://www.greencarreports.com/news/1113332_toshiba-claims-6-minute-recharge-for-new-electric-car-battery-cell

Thursday, 24 December 2015

WIKI YA X-MASS MTOTO HATUMWI DUKANI, LIGI NNCHINI UINGEREZA.

King Power Stadium Uwanja wa nyumbani wa Timu Wababe wa Msimamo wa Ligi kuu Nchini uingereza (Leicester City).

Ligi kuu soka Nchini Uingereza maharufu kama EPL kuendelea tena wikendi hii hapa Jumamosi Siku ya Wiki ya X-mass ambapo takribani Wiwanja tisa kuwaka moto.

Michezo ambayo itakayochezwa siku hiyo ya tarehe 26 Decemba ni pamoja na:

Stoke city VS Man U - 12:45
Aston Villa VS West Ham - 15:00
Bournemouth VS Crystal Palace - 15:00
Chelsea VS Wartford - 15:00
Liverpool VS Leicester City - 15:00
Man City VS Sunderland - 15:00
Spurs VS Norwich City - 15:00
Swansea VS WestBromwich - 15:00
New Castle VS Everton - 17:30
Southampton VS Arsenal -19:45

Msimamo wa ligi hiyo ya EPL Unashikiliwa na Leisester City ikiwa na Pointi 38 imecheza michezo 17 na ina faida ya magoli 13, Nafasi ya pili, tatu hadi tano, zinashikiliwa naArsenal ikiwa na pointi 36, Man City pointi 32, Spurs pointi 29 na Manchester United inakamilisha nafasi hizo tano za juu ikiwa na pointi 29 sawa na Spurs yenye ziada ya tofauti ya magoli 6 na timu zote zikiwa zimecheza michezo 17.

Timu za Swansea, Sunderland na Aston Villa ziko kwenye hali mbaya ya chati ya kushuka daraja, ambapo "The Villans" wanakamata mkia wakiwa na pinti 7 tu baada ya kushakucheza michezo 17 ya ligi kuu.

Wednesday, 23 December 2015

TIMU 16 KUCHUANA CHAN 2016 NCHINI RWANDA.

  • 23 Disemba 2015
    Huu ndio Uwanja wa Taifa wa Amahoro nchini Rwanda ndio Uwanja mkubwa kuliko wote, Ambapo unaweza kubeba takribani Watazamaji 25,000
Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) na Mkuu wa Kamati ya Ndani ya Maandalizi (LOC) ya Michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN), Vincent Nzamwita amesema kwamba viwanja vyote vinne vitakavyotumika kwa mashindano hayo, vipo katika hali nzuri tayari kwa mechi.
Michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee, inatarajiwa kuanza Januari 16 hadi Februari 7.
Nzamwita amesema kazi za ukarabati katika viwanja vya Amahoro na Nyamirambo mjini Kigali tayari imekamilika.
Viwanja hivyo ni pamoja na Huye na Umuganda (Rubavu) vitatumika kwa michuano hiyo ya pili kwa ukubwa barani Afrika ambayo itashirikisha timu 16 za Afrika.
Mara ya mwisho Rwanda kuandaa mashindano makubwa ya Afrika ilikuwa ni mwaka 2011 ilipokuwa mwenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Afrika, ambayo mwishoni timu nne ikiwemo Amavubi, ziliiwakilisha Afrika katika fainali za dunia nchini Mexico mwaka huo.

 

Makandarasi wakiendelea na ukarabati wa baadhi ya Viwanja Nchini Rwanda kwa ajili ya Michuano ya CHAN. Rwanda imepangwa Kundi A pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gabon.

Uwanja wa taifa wa Amahoro ndiyo mkubwa zaidi Rwanda ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 25,000, ukifuatiwa na Huye (mashabiki 10,000), Nyamirambo (mashabiki 7,000) na Umuganda (mashabiki 5,200).
Rwanda imepangwa Kundi A pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gabon, wakati Kundi B lina timu za DRC, Ethiopia, Cameroon na Angola, Kundi C kuna Tunisia, Guinea, Niger na Nigeria na Kundi D kuna Zimbabwe, Zambia, Uganda na Mali.

Source: BBC-Link http://www.bbc.com/swahili/michezo/2015/12/151222_chan_rwandaready