Wednesday, 22 November 2017

MIMEA YA MIKUNDEKUNDE NA SIFA YA MAAJABU KUGEUZA NAITROJENI KUENDELEZA UHAI WA VIUMBE-ARDHI NA MIMEA


 
 
USHIRIKIANO WA AJABU WA MKUNDEKUNDE KATIKA KURUTUBISHA UDONGO

Katika udongo, kuna ushirikiano wa ajabu unaoendeleza uhai kati ya mimea fulani kama mkundekunde (Pichani) na bakteria wapatikanao kwenye Ardhi ili kuendeleza uhai na kuifanya ardhi husika kujitengenezea rutuba yake.

Fikiria hili: Nitrojeni  ni muhimu ili mimea ikue na kuzaa, Lakini lazima gesi hiyo igeuzwe kuwa mchanganyiko wa aina fulani kama vile amonia kabla ya kutumiwa na mimea.

Mikundekunde hufanya hilo liwezekane kwa kushirikiana kwa njia yenye kunufaisha na bakteria inayoitwa rhizobia ambapo Kupitia kemikali ya pekee, mikundekunde huvutia bakteria waiingie katika mizizi yake.

Ingawa bakteria na mmea huo si za jamii moja, gazeti Natural History  linasema, hizo hufanya kazi pamoja “ili kutokeza kiungo kipya: mzizi wenye kifundo cha kugeuza nitrojeni.” Bakteria huishi na kufanya kazi ndani ya kifundo hicho”.
 
 
 Bakteria hao hutumia hasa kimeng’enyaji cha pekee, yaani, aina fulani ya protini inayoitwa Nitrogenase, inayotumiwa kugeuza nitrojeni inayopatikana katika hewa na ile ambayo hupatikana katika udongo.

“Ulimwenguni pote kiwango cha nitrogenase . . . kinaweza kutoshea ndani ya ndoo moja kubwa ya maji,” linasema gazeti Natural History.

Kwa hiyo, kila molekuli ni muhimu! Lakini kuna tatizo kwenye kukamilisha umuhimu huo, Katika mikunde Kimeng’enyaji hicho huharibiwa na oksijeni, lakini je! Suluhisho la tatizo kama hili ni nini?

Mikundekunde hutokeza kemikali fulani ya pekee ambayo huondoa oksijeni inayoweza kudhuru mmea husika, kutengeneza mazingira salama ya bakteria-ardhi kuendelea kuishi, kuhifadhi uhalisia wa mmea husika (kama una sukari kadiri unaendelea kukua ndivyo unavyozidi kutengeneza sukari yake)

Mfano dhahiri ni katika mabadilko ya mimea ya kupandikiza (yaani katika mche wa Limao, unaweza kupandikiza mchungwa kwenye shina lake na pindi mmea unapokuwa unapata machungwa yenye ladha tofauti iliyozoeleka kwa machungwa ya kawaida yasiyopandikizwa )


Lakini kwa mikundekunde, Utando unaozunguka kifundo hudhibiti kazi ya kugeuzwa kwa amonia, sukari, na virutubisho vingine kati ya bakteria na mmea, Kama tu mimea mingine, mikundekunde nayo hufa kwanza ndio ichipue, na Inapokufa, amonia hubaki katika udongo.

Hivyo, kwa kufaa kwake katika kurutubisha udongo, mikundekunde imeitwa “mbolea ya kijani.” Na wakulima wanashauriwa kitaaalamu kutumia mikunde kama njia asilia ya kurutubisha ardhi, punde tu wanapovuna mazao mengine kwenye shamba husika “mfano mahindi” kama njia mojawapo ya kupumzisha shamba husika.

Kwani tafiti zinasema kama misimu 3 iliyomalizika umelima mahindi katika shamba lako, msimu huu yafaa upumzishe shamba lako pasipo kulima ili walau ardhi hiyo irejeshe rutuba yake iliyokuwa nayo, au sivyo basi jenga tabia ya kuchanganya mazao ndani ya msimu mmoja.
 
 
Una maoni gani? Je, bakteria na mimea inaweza “kubuni” mfumo huo tata wenye kustaajabisha unaotegemeza uhai, au je!, huo ni uthibitisho mwingine wa kazi ya ubuni? Umbaaji wa ajabu, ama! kwanini mimea ya kupandikiza hutokelezea ladha tofauti na ya awali iliyozoeleka? Au pengine! Unadhani tofauti na mikunde, ni mimea gani mingine inayoweza kuleta rutuba katika udongo!?


SOURCE:
Natural History Magazine & Amkeni-JW (watchtower)! & Wikipedia For further reading, click for underlined words above,

No comments:

Post a Comment