LONDON
Kocha wa klabu ya Arsenal Arsen Wenger |
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema uwezekano wao wa kutofuzu kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya
kwanza katika Miaka 19 ni jambo la kutia wasiwasi.
Jumapili Arsenal walikosa nafasi ya
kukamata Nafasi ya 3 kutoka ya 4 ya BPL, Ligi Kuu England baada ya kutoka 0-0
na Sunderland huko Stadium of Light.
Wenger ameeleza: "Tunajali na
tuna wasiwasi kwa sababu sasa ni mapigano. Inakatisha tamaa kwani tulipigania
Ubingwa na ukweli ni kuwa hatuwezi kuutwaa, inahuzunisha!"
Arsenal, ambao hawajamaliza nje ya 4
Bora tangu Msimu wa 1995/96, wapo Pointi 12 nyuma ya Vinara Leicester City huku
Gemu 3 zimebaki.
Pia wako Pointi 5 mbele ya Timu ya 5
Man United ambao wana Mechi 1 mkononi na ni Timu 4 za juu ndizo zitacheza UEFA
CHAMPIONZ LIGI.
MECHI ZILIZOBAKI:
Arsenal
-Norwich (H) Aprili 30
-Man City (A) Mei 8
-Aston Villa (H) Mei 15
Man United
-Leicester (H) Mei 1
-Norwich (A) Mei 7
-West Ham (A) Mei 10
-Bournemouth (H) Mei 15
================
Akielezea kuhusu Mechi za mwisho wa
Msimu, Wenger amedai zipo Klabu zenye Ratiba rahisi kwa kusema: "Kuna Ligi
mbili wakati huu. Kuna Timu zimelegeza, zile ambazo ziko salama na haziendi
Ulaya. Na unazo Timu za juu zinazogombea kitu naa zilizo chini zinazopigana
kutoshuka. Ni Gemu tofauti!"
No comments:
Post a Comment