Baadhi ya Wachezaji wa timu ya Azam FC ambao wapo kambini kujiwinda na Michuano ya Mapinduzi Cup yanayotarajiwa kuanza kurindima Visiwani Zanzibar Mapema Mwezi wa januari. |
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka
visiwani Zanzibar Kassim Haji Salum amesema Klabu za Gor Mahia ya kenya ,
KCCA ya Uganda , Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa sugar kutoka Tanzania
Bara na Mafunzo na JKU kutoka visiwani Zanzibar ndio Timu
zitakazoshiriki Mashindano ya Mapinduzi Cup Mashindano ambayo
yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2 visiwani Humo.
Michuano hiyo ya Mapinduzi
Cup itazisaidia Timu za Yanga, Azam FC, JKU na Mafunzo kujiandaa na
Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika.Kikosi cha timu ya Yanga SC ambacho kitashiriki Michuano hiyo, na Huku kikijiwinda na Mazoezi ya Kushiriki Mashindano ya CAF ya Klabu bingwa Barani Afrika. |
Mafunzo ya zanzibar wao watacheza na klabu ya AS Vita ya Congo DR kwenye CAF Champion Ligi na Timu ya JKU itashiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Gaborone United ya Botswana.
No comments:
Post a Comment