Baadhi ya Waliojeruhiwa katika tukio hilo huko somalia, na hali halisi ilivyokuwa.http://kiswahili.irib.ir/habari/afrika/item/53624 |
Habari kutoka Somalia zinasema kuwa, takriban watu 10 wameuawa na
wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mapigano yaliyotokea katika mji wa
Beledweyne nchini Somalia
Habari zaidi zinasema kuwa, mapigano makali yameibuka kati ya
makundi mawili ya kikabila ambayo yametumia silaha nzito na kusababisha
uharibifu mkubwa. Mashuhuda wamesema watu wasiopungua 25 wamejeruhiwa
ambapo wengi wao ni raia wa kawaida
Duru za hospitali zinasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na baadhi ya majeruhi kuwa katika hali mahututi.
Ugas Adirahman Ugas Khalif, kiongozi wa kikabila katika eneo hilo amelaani mauaji hayo ya raia wasio na hatia na kuzitaka koo zinazozozana kutatua hitilafu zao kwa njia za amani.
Baadhi ya duru zinasema juhudi za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika za kuzitenganisha pande hasimu hazikufua dafu na kwamba mwanajeshi mmoja wa Djibouti kutoka kikosi hicho ameuawa wakati wa makabiliano hayo
SOURCE: radio Iran Swahili

No comments:
Post a Comment