Friday, 3 June 2016

WAJUA? MTUNZI WA HADITHI ZA KUSISIMUA ATABIRI AJALI YA MELI NA KWELI IKATOKEA.!


Je wajua?
 
RSM Titanic


Hebu tafakari mwandishi wa hadithi za kwenye vitabu anaandika kuhusu tukio la kufikirika, anatoa kitabu na watunwanafurahianhadithi yake. Miaka michache baadaye, tukio kama hilo aliloliandika kutoka kichwani mwake linatukia vilevile!


HAKIKA ITS AMAZING…..!

Kwa taarifa yako tukio kama hilo limewahi kutokea likihusisha meli kubwa ya
Titanic. Je wajua ilikuwaje.!?

(Twende sawia)

Mnamo mwaka 1898, Mwandishi wa mahiri wa vitabu kipindi hicho aitwaye Morgan Robertson alitoa kitabu cha Hadithi alichokipa jina la Furtility (The wreck of The Titan).
 
Simulizi za Morgan zilizogeuka kuwa ajali ya ukweli kwa asilimia 99%

Ndani ya kitabu hicho Morgan alikuwa anaelezea Meli ya Kufikirika aliyoipa jina la Titan ambayo ilikuwa na uwezo wa kubeba watu wengi na Mizigo mizito kuliko meli nyingine zote kuwahi kutokea.

Katika Hadithi hiyo Morgan alielezea jinsi Meli hiyo ya TITAN ilivyogonga Mwamba katika  Bahari ya Atlantic na kusababisha izame. Ndani yake kulikuwa na afisa Mstaafu wa Jeshi, John Rowland aliyekuwa ametopea kwenye ulevi wa kupindukia na kusababisha maisha yake yapoteze mwelekeo.

Katika ajali hiyo Rowland anageuka na kuwa shujaa baada ya kufanikiwa kumuokoa mtoto wa Mwanamke aliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano ya kimapenzi, akamkimbia kwasababu ya ulevi.

Baada ya kunusurika kwenye ajali hiyo Rowland anaanza ukurasa mpya wa maisha yake, anajirekebisha na kuachana na tabia zote mbaya zilizosababisha maisha yake yakakosa mwelekeo.

Miaka 14 baadaye, katika Maisha halisi (achana na hadithi) kunatokea tukio Halisi ambalo linafanana kwa kiasi kikubwa na kile kilichoandikwa na Morgan.
Meli kubwa ya RSM TITANIC iliyokuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi na Mizigo kuliko Meli nyingine yoyote inazama kwenye bahari ya Atlantic baada ya kugonga mwamba.
Kuzama kwa Meli ya RSM Titanic katika bahari ya Atlantic, tarehe 14/04/1912, tukio lililo la kweli lililotabiriwa na Morgan, mwandishi wa riwaya.


Katika Hadithi Morgan alieleza kwamba meli ya Titan ilizama Aprili na ndani yake hakukuwa na maboya ya kutosha kuokoa abiria waliokuwemo ndani yake.
Katika tukio halisi, Meli ya Titanic Ilizama usiku wa Aprili-14, 1912 ikiwa na Maboya-16 tu kati ya abiria zaidi ya elfu-3 iliyobeba.

Na katika Hadithi Morgan alieleza kuwa meli hiyo ilikuwa na urefu wa mita-244, Meli halisi ya Titanic ilikuwa na urefu unaokaribiana sana na huo.
Hata kwa upande wa majina pia yanafanana, Meli ya kwenye kitabu ilikuwa ikiitwa Titan, na Meli halisi ilikuwa ikiitwa Titanic.

Katika ajali ya kwenye hadithi, zaidi ya watu-2500 waliokuwa kwenye meli waipoteza maisha. Katika tukio halisi, zaidi ya watu-2200 walipoteza maisha.
Baadhi ya watu walianza kumshutumu Morgan kwamba ndiye aliyetengeneza ajali hiyo.

 
Hata hivyo, Ilipotimu mwaka 1997 Star wa Muvi kutoka Hollywood, #Leornado akatumia wazo hilo kuigiza filamu aliyoipa jina hilo la TITANIC…..

MAKALA KAMA HIZI PIA TEMBELEA HAPA: www.facebook,com/stewart.meena

Thursday, 26 May 2016

HAKIKA HII NI ZAIDI YA MUUJIZA KATIKA SOKA, TIMU ECUADOR YALIMWA GOLI 44-1!


Timu ya Polileo ambayo ndio ilifanya mauwaji hayo. (goli 44-1)


Klabu moja ya soka nchini Ecuador imepata ushindi mkubwa ambao ukiidhinishwa basi itakuwa rekodi mpya ya ufungaji mabao duniani.

Klabu hiyo ya Pelileo Sporting Club ilicharaza Indi Native mabao 44-1 katika mechi ya ligi ya daraja la tatu nchini humo mbele ya mashabiki 200, ambapo Mshambuliaji wa Pelileo Ronny Medina pekee alifunga mabao 18.
 
Rais wa Indi Native Diego Culequi amesema matokeo hayo hayakutarajiwa na wachezaji hawakuwa wamezoea joto kali ambalo anasema lilichangia kushindwa kwao.

Mwandishi wa habari Mwingereza Tim Vickery, ambaye amekuwa Brazil kwa miaka 20, amesema Bon Accord kwa sasa wamejadiliwa sana katika vyombo vya habari Ecuador.

Anasema ligi ya daraja la tatu ya Ecuador huwa na ushindani mkubwa.
Rekodi ya sasa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36-0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopita.

Mwenyekiti wa Arbroath FC John Christison amesema ana wasiwasi kiasi kwamba rekodi yao waliyoiweka 1885 huenda ikavunjwa.
Amesema klabu hiyo itasubiri uamuzi wa Guinness World Records.

Tuesday, 24 May 2016

BAADA YA UBINGWA FA VAN GAAL SASA IMEKWISHA



 
Meneja wa Man U aliyemaliza muda wake, Lois Van Gaal akisalimiana na meneja mpya Jose Mourinho.
Meneja wa timu ya Manchester United ya Nchini Uingereza Louis van Gaal amenukuliwa akisema sasa imekwisha wakati akitarajiwa kumaliza kandarasi yake ya miaka miwili ya kuifundisha klabu hiyo.

Kuondoka kwa LVG kunafungua fursa ya kocha mpya wa timu hiyo Jose Mourinho ambaye sasa tayari ameshafunga mkataba wa kuinoa klabu hiyo ya Man united ambayo haijafanya vizuri tokea kustaafu kwa kocha wake wa muda mrefu (Ferguson) ambaye alikabidhi kandarasi kwa David Moyes kabla ya kutimulliwa na timu kukabidhiwa kwa Van gaal.

Mourinho amekubali kutia saini ya miaka mitatu ya kuinoa Man United na anatarajiwa kutangazwa mbele ya waandishi wa habari mapema wiki hii, ingawa kumekuwa na minongono kutoka kwa wachezaji wa zamani kuwa meneja huyo mpya hawezi kuipatia timu hiyo mafanikio yaliyokosekana kwa muda mrefu.

Van Gaal aliyechaguliwa kuinoa Man united tokea msimu wa 2014 ameiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja pekee la FA CUP kwa kuichapa Crystal Palace mabao 2-1 fainali wikendi ya jana jumamosi, na amefanikiwa kumaliza nafasi ya tano msimu huu na hivyo timu hiyo ya Manchester itakosa kushiriki UEFA lakini  itashiriki michuano ya Uropa msimu huu unaofuata.

Mourinho, kocha mpya wa Manchester United alifukuzwa kutoka klabu ya Chelsea mwezi desemba mwaka jana baada ya mwenendo mbovu wa uchezaji wa timu hiyo.

KUELEKEA FIFA-2016 , TIMU YA TAIFA UJERUMANI YAAHIDIWA DONGE NONO


kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.

Wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda ya Ujerumani maarufu kama (Die Mannschaft) watapokea bahashishi ya euro laki-3 kila mchezaji ikiwa watashinda Kombe la Mataifa ya Ulaya (Euro 2016).
 
Shirikisho la kandanda la nchini Ujerumani (DFB) limesema licha ya kinyang'anyiro cha mwaka huu kuwa na timu nyingi, na kuongezwa kwa hatua za mechi za mchujo, viwango vya bahashishi vitakuwa sawa na vya michuano ya Euro-2012 ambapo Ujerumani iliondolewa katika hatua nne za mwisho.

Meneja wa timu hiyo Oliver Bierhoff amesema wamekubaliana na DFB pamoja na wachezaji kuwa “kabla ya kuanza kwa Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ukraine mwezi juni-12 Fedha hizo watakuwanazo mkononi, na endapo watinga hatua ya robo fainali watalipwa euro elfu-50 kila mchezaji, euro laki-1 kwa nusu fainali na Euro laki 1 na kwa kutinga hatua ya fainali.

Ikiwa watashindwa katika hatua ya 16 bora za mwisho, au washindwe kufuzu katika Kundi lao wataambulia patupu, lakini Washindi hao wa Kombe la Dunia mwaka-2014 nchini Brazil, ni miongoni mwa timu 24 zinazopigiwa upatu wa kufanya vyema katika mashindano hayo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu, ambapo Ujerumani ipo katika Kundi C pamoja na timu za Ukraine, Poland na Ireland ya Kaskazini.

Wakati huo huo: Kiungo wa Borussia Dortmund Ilkay Guendogan mwenye umri wa miaka 25 atakosa dimba la Kombe la Mataifa ya Ulaya Euro 2016 baada ya kuumia goti wakati akifanya mazoezi na anatarajiwa  kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu.

Habari hii ni pigo kwa kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew na pia bahati mbaya mchezaji huyo aliyekosa tena Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na maumivu ya mgongo yaliyomweka nje kwa miezi 14 kuanzia Agosti 2013.

FIFA SASA KIMENUKA, WAANZA TIMUATIMUA


Jerome Valke, naibu katibu wa Shirikisho la Soka duniani FIFA

 Shirikisho la soka duniani Fifa limemtimua naibu katibu wake Markus Kattner kwa kujihusisha na ukiukwaji wa matumizi ya siri ya mamilioni ya dola.
Kattnet raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 45 alikua akiitumikia nafasi hiyo baada ya aliyekua katibu Jerome Valcke kutimuliwa kazi kutokana na kashfa za rushwa.
Kufutwa kazi kwa kiongozi huyu kulikuja mara moja baada ya bodi ya uchuguzi ya ndani ya Fifa kugundua kulikua na ukiukwaji na uvunjaji wa majukumu yake.
Kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha mapungufu katika majukumu yake kwa kutumia pesa za ziada ambazo waliamua kiasi gani rais, katibu mkuu na naibu katibu mkuu walipwe.

Monday, 23 May 2016

SOKA MATAIFA YA EURO-2016 NCHINI UFARANSA ZIMEBAKI WIKI MBILI TU.



Moja ya Kiwanja cha mpira wa Miguu nchini ufaransa (kati ya Viwanja 10) kitakachotumika kwa michuano ya mataifa ya ulaya (Euro-2016)

 Ikiwa zimebaki wiki mbili pekee kuanza kwa michuano ya UEFA-Euro 2016, hali ya usalama nchini Ufaransa Inakofanyika Michuano hiyo bado imeelezwa kuwa tete, ambapo Wanausalama nchini Ujerumani wameonya kuwa Mtanange huo huenda ukakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi.


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault anasema "Kila kitu kimefanywa kuimarisha usalama wa raia wa Ufaransa pamoja na wageni wote wataokuja kushiriki katika Euro 2016”


Mapema wiki hii Bunge la nchini Ufaransa limeidhinisha mswada wa kurefushwa kwa miezi miwili zaidi, kutangazwa kwa hali ya hatari ambayo iliyowekwa tangu mashambulizi ya kigaidi ya Novemba mwaka jana.


UEFA inapanga kuwaajiri maafisa usalama wa kibinafsi takribani elfu-10, wakati wa kinyang'anyiro hicho na kila uwanja kati ya viwanja-10 vitakavyotumika kutakuwa na maafisa 900 wa usalama watakaoweka ulinzi kwa kila mchuano.