Monday, 23 May 2016

SOKA MATAIFA YA EURO-2016 NCHINI UFARANSA ZIMEBAKI WIKI MBILI TU.



Moja ya Kiwanja cha mpira wa Miguu nchini ufaransa (kati ya Viwanja 10) kitakachotumika kwa michuano ya mataifa ya ulaya (Euro-2016)

 Ikiwa zimebaki wiki mbili pekee kuanza kwa michuano ya UEFA-Euro 2016, hali ya usalama nchini Ufaransa Inakofanyika Michuano hiyo bado imeelezwa kuwa tete, ambapo Wanausalama nchini Ujerumani wameonya kuwa Mtanange huo huenda ukakabiliwa na mashambulizi ya kigaidi.


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault anasema "Kila kitu kimefanywa kuimarisha usalama wa raia wa Ufaransa pamoja na wageni wote wataokuja kushiriki katika Euro 2016”


Mapema wiki hii Bunge la nchini Ufaransa limeidhinisha mswada wa kurefushwa kwa miezi miwili zaidi, kutangazwa kwa hali ya hatari ambayo iliyowekwa tangu mashambulizi ya kigaidi ya Novemba mwaka jana.


UEFA inapanga kuwaajiri maafisa usalama wa kibinafsi takribani elfu-10, wakati wa kinyang'anyiro hicho na kila uwanja kati ya viwanja-10 vitakavyotumika kutakuwa na maafisa 900 wa usalama watakaoweka ulinzi kwa kila mchuano.

No comments:

Post a Comment