kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014. |
Shirikisho
la kandanda la nchini Ujerumani (DFB) limesema licha ya kinyang'anyiro cha
mwaka huu kuwa na timu nyingi, na kuongezwa kwa hatua za mechi za mchujo,
viwango vya bahashishi vitakuwa sawa na vya michuano ya Euro-2012 ambapo
Ujerumani iliondolewa katika hatua nne za mwisho.
Meneja
wa timu hiyo Oliver Bierhoff amesema wamekubaliana na DFB pamoja na wachezaji
kuwa “kabla ya kuanza kwa Mchezo wao wa kwanza dhidi ya Ukraine mwezi juni-12
Fedha hizo watakuwanazo mkononi, na endapo watinga hatua ya robo fainali
watalipwa euro elfu-50 kila mchezaji, euro laki-1 kwa nusu fainali na Euro laki
1 na kwa kutinga hatua ya fainali.
Ikiwa
watashindwa katika hatua ya 16 bora za mwisho, au washindwe kufuzu katika Kundi
lao wataambulia patupu, lakini Washindi hao wa Kombe la Dunia mwaka-2014 nchini
Brazil, ni miongoni mwa timu 24 zinazopigiwa upatu wa kufanya vyema katika mashindano
hayo.
Michuano
hii inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mnamo tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu,
ambapo Ujerumani ipo katika Kundi C pamoja na timu za Ukraine, Poland na
Ireland ya Kaskazini.
Wakati huo huo: Kiungo wa Borussia
Dortmund Ilkay Guendogan mwenye umri wa miaka 25 atakosa dimba la Kombe la
Mataifa ya Ulaya Euro 2016 baada ya kuumia goti wakati akifanya mazoezi na
anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa
kipindi chote cha msimu.
Habari
hii ni pigo kwa kocha wa timu ya Ujerumani Joachim Loew na pia bahati mbaya
mchezaji huyo aliyekosa tena Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kutokana na
maumivu ya mgongo yaliyomweka nje kwa miezi 14 kuanzia Agosti 2013.
No comments:
Post a Comment