Tuesday, 21 March 2017

FAIDA ZA MISITU HUKUTEGEMEA WEWE KUZILINDA

Moja ya miti iliyopandwa na Binadamu kwa ajili ya kurejesha halimisitu iliyopotea katika eneo hili. Picha Na Stewart Meena

Msitu ni mkusanyiko wa uoto asilia unaojumuisha miti ya aina mbalimbali, mimea na nyasi ambazo huweza kuwa fupi au ndefu. lakini pia ipo misitu mingine ya Kupandikizwa na binadamu katika mazingira yaliyomzunguka na kwa muundo anaoutaka yeye mwenyewe (Artificial)

 https://sw.wikipedia.org/wiki/Msitu

Kila mwaka ifikapo Tarehe 21/03 ni siku ya Misitu duniani ambapo sambamba na maadhimisho hayo pia elimu hutolewa kuhusiana na utunzaji wa misitu asilia pamoja na ile ya kupandwa na Binadamu ili kurejesha Muingiliano mzuri kati ya binadamu na Mimea (Frora & Fauna)
Mtiririko wa Maji katika chemchem zitokazo ardhini kwenye misitu ya asilia. Na Stewart Meena
Hivyo basi palipo na utunzaji mzuri wa  Uoto wa Asili, hua ndio chanzo kizuri zaidi cha maji safi na salama pamoja na hewa safi kwa ajili ya kuendeleza maisha ya mwanadamu ambaye hutegemea mimea hiyo kujipatia hewa ya (oxigen) ambayo huibadilisha na ile waitoayo ya (Cabondioxide) ambayo hufyonzwa na Mimea.

Pasipo mimea hakuna mvua, kutokana na mzunguko mzima wa kuvukiza Maji kwenda angani, na kisha tena kurejea Ardhini, hutegemea sana misitu hii kuvuta mvua hiyo.
Kuanza kufunga kwa mawingu ikiwa kama ishara ya kutaka kunyesha kwa Mvua. Na Stewart Meena
Misitu hii huzua pia uharibifu wa Upepo mkali, mvua nyingi kwa kutunza mmomonyoko wa udongo unaoweza kupelekea majanga makubwa zaidi kama ukame, pamoja na vifo viwezavyo kutokana na mabaa ya njaa kwa ukosefu wa chakula.

TUNZA MISITU IKUTUNZE

Sunday, 29 January 2017

KUMWEPUSHA MTOTO NA UDUMAVU INAWEZEKANA:



  Tanzania ni miongoni mwa nchi 10 zinazokabiliwana changamoto ya kuwa na watoto wenye udumavu, ugonjwa ambao unachangiwa kwa kiwango kikubwa na lishe duni wanazozipata watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mashirika mbalimbali ya ndani ya nchi na nje ya nchi yamekuwa yakihangaika kuhakikisha kuwa changamoto hii inapungua kama si kutoweka kabisa hapa nchini.
   Kwa nyakati tofauti, jitihada zimekuwa zikichukuliwa katika kuhakikisha kuwa afya inaimarishwa kwa kila mtu, ambapo zimekuwa zikiungwa mkono na taasisi mbalimbali za dini.
 Lakini bado hali ni tete kwa watoto ambao ndio wanaokumbana na tatizo hili la udumavu na ukondefu unaosababishwa na kukosa lishe bora.

   Takwimu za shirika la afya duniani (WHO) zinaonyesha kuwa kila siku zaidi ya watoto 270 waliochini ya umri wa miaka 5 nchini Tanzania hupoteza maisha yao kwa lishe duni, huku zaidi ya watoto milioni 2 na Laki 7 wakikabiliwa na aina ya udumavu unaotokana na utapiamlo.
    Takwimu hizo zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo hivyo hutokea katika mwezi wa kwanza wa maisha ya watoto hao.
    Huku takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani UNICEF, zinaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto wote wa Tanzania waliochini ya umri wa miaka mitano wamedumaa kutokana na kukosa lishe bora.
    Chanzo cha ugonjwa huu wa udumavu kinaelezwa kuwa ni utapiamlo unaosabibishwa na lishe duni kwa mtoto ambapo huchangia mtoto kuwa na kimo au urefu mfupi usioendana na umri wake.
   Japo kumekuwapo na dalili za kupungua kwa kiwango cha udumavu nchini kwa asilimia 30, kati ya mwaka 1994 hadi 2014 japo idadi ya watoto waliodumaa ikiwa imeongezeka kutoka milioni 2.4 hadi 2.7 katika kipindi hicho.
    Sababu nyingine ya udumavu ni kutokana na kuugua mara kwa mara katika miaka mitatu ya mwanzo ya makuzi yake.
   sababu nyingine ni Afya na Lishe duni kwa wanawake kabla ya Ujauzito, wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua, pia kutokupangilia uzazi, yaani kuzaa watoto kwa karibu karibu pamoja na tatizo la wasichana kubeba mimba wakiwa katika umri mdogo.
   Taratibu duni za ulishaji Watoto, ikiwamo kutonyonyeshwa maziwa ya mama pekee katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo baada ya kuzaliwa na kupewa chakula cha nyongeza kisichokidhi mahitaji yao ya lishe pale wanapotimiza umri wa miezi sita.
   Watoto kupewa kiasi kidogo cha chakula au kisichokuwa na ubora au mchanganyiko wa Makundi mbalimbali ya chakula pia ni sababu nyingine zinazodumaza watoto.

ATHARI:

   Mtoto kuwa na Udumavu, huchangia kupata athari zisizoweza kurekebishika katika maisha yake hata kama kwa hapo baadaye atapewa lishe bora, mwili wake tayari utakuwa umedumaa na hivyo kushindwa kupokea Marekebisho.
   Kushuka kwa maendeleo ya akili kwa mtoto pia ni moja ya Athari za udumavu, hatua hii humfanya mtoto kushindwa kufanya vizuri hata kwenye masomo yake.
   kuwa na uzito mkubwa kuliko umbo na umri wake "KIRIBA TUMBO" na kukumbwa na magonjwa yasiyoambukiza kama moyo, Kiharusi, Shinikizo la damu na hata Kisukari katika umri mdogo.

NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU.

   Ni wazi kuwa mpango wa (WHO) kwa Tanzania ifikapo mwaka 2025 walau idadi ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano waliodumaa iwe imepungua kwa walau asilimia 40.
   Hata hivyo malengo haya yatafanikiwa tu iwapo Watanzania watazingatia lishe bora kwa watoto na Mama wajawazito kulinda afya zao katika kipindi chote cha ujauzito na kuzingatia unyonyeshaji pindi anapojifungua.
   Ni muhimu kwa Akina mama kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama hadi watakapofikisha umri wa "MIAKA 2" Hapa wanawake wajitahidi kutowaachisha watoto wao nyonyo mapema.

"Mama anashauriwa kumnyonyesha mwanaye ziwa lake kwa kipindi cha miaka miwili"



 VISIT ALSO: http://www.facebook.com/stewart.meena
                    FOR AMAZING UPDATES...............
 

Saturday, 31 December 2016

FAHAMU KUHUSU ORODHA YA WACHEZAJI 48 BORA DUNIANI WA MUDA WOTE, AFRIKA WAMO 7.

Ripoti mpya za Shirikisho la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu (IFFHS) zimeonesha list yenye majina ya mastaa 48 bora wa soka duniani wa muda wote ambao ni wakongwe, zaidi wakitamba na timu zao za taifa ambapo kwa bara la Afrika limefanikiwa kuingiza majina ya wachezaji 7 waliofanya vizuri kwenye listi hiyo.

Mwanko Kanu miongoni mwa Wachezaji bora wa muda wote kwenye orodha hiyo, Akitokea nchini Nigeria

Wachezaji kutoka Afrika waliotajwa kwenye Orodha hiyo ni pamoja na Nwanko Kanu (Nigeria), George Weah (Liberia), Lucas Radebe (Afrika Kusini), Mahmoud El-Khatib na Mohamed Aboutrika (Misri), Mustapha Rabah (Algeria) na Roger Milla (Cameroon).
George Weah, enzi zake akiwika zaidi na timu ya Liberia. kwasasa Weah ameachana na maswala ya soka na kujikita zaidi kwenye Maswala ya siasa
Roger Miller (mwenye bukta nyekundu) enzi zake akiwika zaidi na timu yake ya Cameroon

Fahamu zaidi, tunakuletea majina mengine ya wachezaji mashuhuri ambao waliweka rekodi kwenye timu zao za taifa, na Klabu mbalimbali waliowahi zichezea.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na kiungo mshambuliaji aliyewahi kutamba na timu ya taifa ya Brazil, huyu anaitwa (Edson Arantes Do Nascimento (PELE) huyu alitamba nyakati zile za kina Maradona na Goli lake la mkono alilolibatiza (Goli la mkono wa mungu).
Katika nafasi ya kiungo wa kati kwa timu hiyo ya Brazil, aliyewahi kutamba na kushika nafasi hiyo ni pamoja na ‘Arthur (Antunes Coimbra) almaharufu akijulikana kama (Zico), Manuel Francisco dos Santos (Garrincha)

Wachezaji wengine bora wa muda wote kwa dunia ni pamoja na ‘Ronaldo Luís Nazário De Lima’ (Ronaldo) akitokea timu ya taifa ya BrazilBrazil, na ngazi ya klabu akiwika na Real De Madrid ya nchini Hispania.

Nchini ujerumani wapo, viungo wa kupanda na kushuka, kama vile Sweeper au Franz Anton Beckenbauer almaharufu kama (Becken-bauer) mshambuliaji ‘GERD MÜLLER akijulikana zaidi kama (Gerd) pamoja na kiungo mkabaji ‘Lothar Matthäus’
Nchini Uholanzi wamo Hendrik Johannes Cruijff maarufu zaidi kwa jina la (Johan Cruyff) Germanyakicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji. Wengine ni ‘Marco Van Basten alwatan zaidi (Marco) pamoja na Ruud Gullit-OON / Netherlands.
Netherlands

Uingereza, wamo viungo washambuliaji, Bobby Charlton akiichezea timu man united wakati huo, akijulikana zaidi kama (Bobby) lakini pia kiungo wa katikati ‘United KingdomDavid Robert Joseph Beckham’ akijulikana kama (David Beckham) naye ni miongoni mwa wachezaji hao wa misimu yote naye akitokea uingereza na kuichezea man united pia.

United Kingdom

David Beckam,( manchester united legendary) Akiwika zaidi na timu yake ya taifa ya Uingereza
  • Forward / STANLEY MATTHEWS LATE / United Kingdom United Kingdom
  • Midfielder / Diego Armando Maradona Franco (Maradona) / Argentina Argentina
  • Forward / Alfredo Stéfano Di Stéfano Laulhé LATE / Argentina Argentina
  • Forward / HAO HAIDONG / China China
  • Defender / Sun Jihai / China China
  • Forward / Mahmoud El-Khatib (Bibo) / Egypt Egypt
  • Midfielder / Mohamed Aboutrika / Egypt Egypt
  • Midfielder / Michel Platini / France France
  • Midfielder / Zinedine Yazid Zidane (Zizou) / France France
  • Goalkeeper / Antonio Carbajal (Tota) / Mexico Mexico
  • Forward / Hugo Sánchez Márquez (Sánchez) / Mexico Mexico
  • Forward / Eusébio da Silva Ferreira (Eusébio) / Portugal Portugal
  • Midfielder / Luís Filipe Madeira Caeiro Figo (Luis Figo) / Portugal Portugal
  • Goalkeeper / Dino Zoff / Italy Italy
  • Forward, Midfielder / Roberto Baggio / Italy Italy
  • Striker / Mustapha Rabah Madjer (Rabah Madjer) / Algeria Algeria
  • Forward / Albert Roger Mooh Miller (Roger Milla) / Cameroon Cameroon
  • Forward / Ferenc Puskás LATE / Hungary Hungary
  • Forward / Baichung Bhutia (Bhutia) / India India
  • Forward / Ali Daei / Iran Iran, Islamic Republic of
  • Midfielder / Hidetoshi Nakata / Japan Japan
  • Striker / Cha Bum-kun (Tscha Bum) / South Korea Korea, Republic of
  • Striker / Jasem Yaqoub Sultan Al-Besara / Kuwait Kuwait
  • Forward / George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah (George Weah) / Liberia Liberia
  • Forward / Wynton Alan Whai Rufer / New Zealand New Zealand
  • Forward / Nwankwo Kanu / Nigeria Nigeria
  • Goalkeeper /José Luis Félix Chilavert González (José Luis Chilavert) / Paraguay Paraguay
  • Goalkeeper / Lev Ivanovich Yashin (Lev Yashin) LATE / Russia Russian Federation
  • Forward / Majed Ahmed Abdullah Al-Mohammed (Majed Abdullah) / Saudi Arabia Saudi Arabia
  • Forward / Francisco Gento Lopez (Paco) / Spain Spain
  • Striker / Tanju Çolak / Turkey Turkey
  • Forward / Oleh Volodymyrovych Blokhin / Ukraine Ukraine
  • Inside forward / Juan Alberto Schiaffino Villano (Pepe) LATE / Uruguay Uruguay
  • Forward, Midfielder / Landon Timothy Donovan / USA United States
  • Defender / Lucas Valeriu Ntuba Radebe (Lucas Radebe) / South Africa South Africa
  • Midfielder / Ryan Joseph Giggs (Ryan Giggs) / Wales Wales