Na.
Stewart Meena
Wakati na majira katika
kalenda yamegawanywa kwa utaratibu maalumu unaotambulisha, hali na matukio
fulani kumbukizi katika upeo, historia, geographia, na sayansi na teknolojia.
Vivyohivyo hili
linapelekea, hata binadamu na ustaarabu wake kulingana na majira aliyozaliwa
kupewa majina yanayosadifu maendeleo na hali ya wakati huo husika kutoka vizazi
hadi vizazi kufuata wakati waliozaliwa.
Twende kwa pamoja
tukaangalie vizazi hivyo na majina wanayotambulikana kwayo ikigawanywa kuanzia
miaka14 hadi 25"
1883 - 1900 Watu wote wale
waliozaliwa kati ya miaka hiyo hutambulika kwa jina la" Kizazi potevu au
kilichopotea (The Lost Generation) sababu teknolojia ilikua duni, uvumbuzi na
utandawazi haukuwepo.
1901 - 1924 Watu
waliozaliwa hapa kati ya miaka hiyo walijulikana kama kizazi vumbuzi (The
Greatest generation) wakati huu ufahamu wa binadamu uliongezeka, teknolojia na
uvumbuzi kuelekea utandawazi vilianzishwa. Hiyo ilipelekea kuanzishwa kwa vita
vya kwanza vya dunia "1918-19" kugombea maeneo yenye mali ghafi
"raw materials"
1925 - 1945 Wale
walizozaliwa hapa walitambulikana kana Kizazi tulivu (The Silent Generation)
wakati huu maendeleo yalikuwepo, ikawa ni vita vya ushindani kuonyeshana nani
mwenye nguvu zaidi ya mwingine, mataifa yaliingia katika vita (nchi na nchi)
hiyo ikapelekea vita vya pili vya dunia "1938-39"
1946 - 1964 Waliozaliwa
hapa wanatambulika kama kizazi-Deko au LiaLia au kizazi-vivu (The Baby boomers
generation) hawa bhana walikuwa wabishi, wajuaji na zaidi wanaokimbia matatizo
wanayoyaanzisha wenyewe.
1965 - 1980 Watu
waliozaliwa hapa, wanajulikana kama kizazi-janja (Generation X / baby Buster)
hawa bhana wameishi utandawazi, maendeleo ya sayansi na teknolojia yalikuwepo,
na ongezeko la wasomi walikuwepo kwa kiasi kikubwa sana kulinganisha na vizazi
vilivyopita.
1981 - 1996 Waliozaliwa
hapa wanajulikanankama kizazi-milenia (The Generation Y / gen-mi
"Millennial")
1997 - 2012 Watu wote
waliozalika kati ya miaka hiyo wanajulikana kama kizazi-tukutu au Jeuri (Gen-Z
"Generation Z) hawa sina haja ya kuwaongelea sana nadhani mmejionea (Tanzania,
Kenya kule walichofanya kupeleka shinikizo kwa serikali kuhusu ukosefu wa ajira
na maisha magumu)
2013 - 2025 Watu
waliozaliwa kati ya miaka hii hutambulikana kama kizazi #Alfa au kizazi taarifa
(Generation Alpha) Alfa inamaanisha #mwanzo. Hii ni kuanza kwa jambo jipya,
tumaini jipya, maisha mpya, teknolojia mpya, uvumbuzi mpya maarifa mapya nk.
Walioko hapa ni kizazi taarifa (Information Society) kwa sababu karibu asilimia
90 ya maisha yao hutegemea taarifa inayorahisishwa na utandawazi, ambao huu
umeleta kitu kinaitwa Cyber space (online interaction). Hawa wako radhi wakose
kula ila #wasikose bando "internet" ya kuperuzi.
2026 - 2039 Hii hapa
itaanza mwakani, na watoto wote watakaozaliwa hapa watajulikana kama
kizazi-shirikishi, #GenBeta (Generation Beta) hawa inatarajiwa wataiishi
teknolojia yote iliyofikiwa hadi sasa, na kuendena na matokeo yake yaliyo
mazuri au mabaya. Hawa hawatahitaji kufundishwa ilhali wamezaliwa nayo.
Zaidi Hapa:
Tafadhali LikePage, share taarifa
hii iwafikie wengi zaidi, Pia ‘Follow page’ ukurasa huu, ili usipitwe na
taarifa nyinginezo zenye kuelimisha na kukuhabarisha kama hizi.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni