Jumapili, 25 Oktoba 2026

FAHAMU: ULAJI WA KARANGA, CHANZO CHA JOTO MWILINI NA MAFUA/FLU!?

 


Writer: Stewart Meena

Karanga, ni nafaka ambayo ni mashuhuri sana Tanzania na Duniani kwa walaji na watumiaji wa bidhaa hii adhimu, ambapo hupatikana ndani ya ardhi baada ya kuchimbuliwa au kuvunwa katika mmea wake.

Kama ilivyo nafaka nyinginezo, karanga pia huwa na chanzo cha kuupatia mwili nishati ya joto, ambapo mara nyingi mwili wa binadamu hupata joto kupitia madini mwili mbalimbali pamoja na ulaji wa Vyakula vya wanga.

Ili mwili ujijenge vizuri unahitaji virutubisho kamili, ambavyo hupatikana kwenye ulaji wa mlo kamili unaojumuisha "Vitamini, Protini pamoja na Wanga"

Vitamini: hupatikana zaidi katika matunda ya aina tofauti-tofauti; Wanga: hupatikana zaidi katika nafaka, na Protini: hupatikana zaidi kwenye Nyama na baadhi ya nafaka kama vile Maharagwe, karanga nk.

Je!?

Karanga ni chanzo cha joto mwilini, lakini pia imekuwa ikihusianishwa na chanzo cha mafua makali "Flu" Je ni kweli?



KARANGA: Peke yake hazileti mafua ‘Flu’ kwa mafua yenyewe husababishwa na Virusi na sio chakula, na mtu huweza kupata ‘Flu’ kwa kuambukizwa na mtu mwingine aliyeambukizwa au unaposhika sehemu ye virusi au bakteria hao wa ‘Flu’

Walaji wengi wa karanga hula kwa sababu ya kuupatia mwili joto sababu karanga zina wingi wa mafuta na protini ambayo ndio chanzo kikuu cha nishati ya joto mwilini.

Swali: Kwanini watu hupiga chafya baada ya kula karanga na kunywa na vimiminika kama maji baridi?

Jibu: Hii mara nyingi ni mzio (allergy) ndogo, ambapo karanga ni miongoni mwa vyakula vinavyoongoza kwa kuwapatia watumiaji wake mzio Duniani. Ambapo dalili zake ni pamoja na:

  • ·       Kuwashwa kooni
  • ·       Kukohoa au kupiga chafya
  • ·       Macho kutoa machozi
  • ·      Ngozi kuwashwa na kutoka vijipele vidogovidogo nk.

Ambapo dalili hizo mara nyingine huweza kuleta flu kali ya ghafla kwa muhusika lakini kwa muda mfupi kulingana na uimara wa kinga-mwili ya muhusika, kwani mwili na kinga zako ‘reaction’ yake ndio inapambana na mzio wa karanga kama adui aliyeingia kwa wakati huo.

Mwili wa Binadamu huwa na Nyuzijoto 37c., na huweza kupungua au kuongezeka katika nyakati tofauti, kama vile mtu kuwa na homa (mgonjwa) au kupitia kipindi cha baridi au joto kali, ambapo mwili hujaribu kubadili jotoridi lake kuendana na huo wakati husika.

VYANZO VYA MAFUA:



Mafua (Flu) huchagizwa na Bacteria (Virus) ambao huweza husambaa kutoka mtu mmoja na mtu mwingine endapo kutakuwa na kukaribiana.

Mtu huweza kupata mafua pia kutokana na vumbi kuingia katika chemba ya pua na kusababisha usumbufu kwenye mfumo wa upumuaji ndani ya tundu za pua ndani ya kinywa kutokea nje.

Maganda ya karanga pia huwa na viambata-bacteria ambavyo huweza kusababisha mafua miongoni mwa watumiaji kwa kuzingatia kinga yao ya mwili na kundi la damu alilonalo muhusika.

Mfano: wengine husema, nimepata aleji ya mafua, kutika damu puani nk. (kambaku) baada ya kula vyakula fulani, labda dagaa, uono, karanga mbichi, uji, ndizi za kuchemsha nyama za kondoo na mbuzi nk)

·       Baridi kali pia huweza kusababisha mafua mepesi, msimu na nyakati za baridi pia watu hushuhudia kupata mafua (Mf. Asubuhi pindi uamkapo mapema huweza kupata una mafua mepesi, ambayo huweza kuisha ukisha-koga na kuuchangamsha mwili kwa mazoezi:

KIMSINGI: Ulaji wa karanga mbichi pamoja na maganda yake mepesi kwa baadhi ya watu huwasababishia mafua, na hiyo ni kawaida sababu nilizozieleza hapo juu (Mzio au allergy) na reaction ya mwili kutengeneza kinga ya kuambana na mzio huo:

Hivyo karanga nazo huweza kuleta mafua "Endapo mlaji akiwa na kinga mwili dhaifu na kundi lake la damu likiwa dhaifu lakini pia kwa kula karanga zilizokaangwa na maganda yake, haswa baada ya kuziacha zilale na wakati wa kuzila ukaambatanisha na maji (kuzilowesha)

Makundi ya damu (Blood groups) ni kama vile: Group O "positive & negative"; Group A; Group B; na Group AB.

KINGA MWILI:

Mwili wa mwanadamu una kinga-mwili kuu mbili ambazo hupambana na magonjwa ambukizi na zipo kwenye damu nazo ni seli hai nyekundu na nyeupe (White cell and red cells)

ZINGATIA: Kuacha tabia ya kula karanga na maganda yake (haswa zilizokaangwa) zimenye, pia ukila karanga mbichi hakikisha usinywe na maji baridi wakati unapozila, labda unawezakula karanga mbichi na chai haina tatizo.

KARANGA KAMA BOOST-NGUVU ZA KIUME



Usile karanga pamoja na vinywaji vyenye "Caffeine" kama Chai ya kahawa, baadhi ya soda kama "energy drink" nk sababu vinywaji hivyo huwa na kawaida ya kuongeza msukumo wa damu, hivyo ni hatari kutumia na karanga maana nazo sina sifa sawia mbili au tatu zaidi tofauti.

Mfn. Baadhi vya wanaume hutumia karanga mbichi, energy au wine, mchuzi wa pweza au samaki, muhogo au nazi kuongeza nguvu za kiume"

ni kweli unaweza kuongeza, ila madhara huweza kuja kupatikana baadae taratibu bila muhusika kung'amua ameshakua mraibu (kuathirika) Hadi a-boost ndio awe imara.

Kila kitu hutumiwa kwa kiasi, usiwe unatumia karanga nyingi kila siku kupita kiasi, ila unashauriwa utumie kiasi kidogo tu inatosha, maana virutubisho mwili sio lazima utumie sinia nzima ndio uvipate, HAPANA: hata kiasi kidogo tu inatosha.

USHAURI:

Ugonjwa wa Mafua "Flu" unaweza kuepukika kwa kutokukaa karibu sana na watu wenye dalili za mafua makali (na kupiga chafya) maana Flu, husambaa kwa virusi (Bacteria)

Usikae sana maeneo yenye vumbi, na ikibidi kukaa (hakikisha umevaa barakoa "mask") ili kujikinga na na vumbi hilo ili kutokupata mafua.

Pima kundi lako la damu" litambue, fahamu vyakula vinavyoweza kuchochea na kukuza kinga mwili-damu yako, na pia zingatia kila siku unakula matunda ambayo yatakupatia vitamini, maana Vitamins huusaidia mwili kutengeneza kinga yake na kupambana na magonjwa.

Hakikisha unakula mbogamboga zenye uchachu, "Mnafu, mchunga nk: na pia kila mlo wako uwe na mboga za majani.

MWISHO:

Vyakula, matunda, Mbogamboga, mimea, mazingira ndio uhai wetu, tunaweza kutokuugua mara kwa mara tukijitambua, kuzingatia na kutafuta maarifa zaidi (elimu) kuhusu ulaji sahihi, miti na mimea dawa pamoja na kuyatawala na kuyatunza mazingira yetu".

Kwa MAONI, MASWALI na KUFAHAMU ZAIDI: WASILIANA NASI KUPITIA.

E-mail: stewartmeena6@gmail.com ; WhatsApp.0778291375

Facebook: Elia Stewart Jr.

Fb Page: www.facebook.com/stewart.meena

Tafadhali, (Follow us) Like page na share ujumbe unaokuvutia kuelimisha wengine pia nao wapate kujifunza na kuelimika.

Facebook #EliaStewartJr. #Special4fans #HistoryAndAmazingThings

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni