Thursday, 27 August 2026

MWANAMKE: KWANINI TALAKA HAIPASWI KUWA SULUHISHO LA MGOGORO JUU YA USALITI!

 

FIKIRIA: Mwanamke, unamuacha mumeo (Mwanaume wako) kwasababu ya usaliti, alioufanya kuwa na mwanamke mwingine, (Aah!)

Mna familia pamoja, mtoto mmoja" au wawili. (Ok!)

Hivyo, ukaomba talaka na mkatalikiana kwa sababu umeumizwa sana na usaliti wake na huwezi kuuvumilia! Na baada ya mchakato wa talaka kukamilika, ukaondoka na watoto wako! (Ooh!)

Ukaanza kufanya kazi kwa bidii ili ujipatie mahitaji yako na uwalelee watoto wako mweyewe bila kuonyesha kuhitaji msaada wa baba yao na kuzimudu gharama za maisha mwenyewe. (Good)

Ili kuendana na kuongezeka gharama za maisha, unaangukia kwa mwanaume mwengine ‘Labda tajiri) Hujali chochote maana unahitaji kulipa ada za watoto kama mwanamke unayejiamini na unajitegemea unahitaji kuuthibitishia ulimwengu unajiweza mwenyewe kwa yote ndio maana ukakubali kuwa na mwanaume huyo tajiri katika penzi la siri ingawa unafahamu ni mume wa mtu. (Unajikuta umerudia kosa lilelile lililofanya nyie kutengana kwa talaka)

Hatimaye sasa na wewe umekua mchepuko kwa mume wa mtu, tena mwenye familia yake na watoto pia (side chick to cheating situation)

Ndipo unakumbuka na unaanza kufikiria kuhusu mwanamke wa pembeni aliyekua naye mumeo, na kwa nini alikua naye! “Umechelewa’ Nda yako haipo tena!

Ulichofanya, ndicho alichokifanya mwanamke uliyemfuma na mume wako, hukufikiria kuhusu maadili, na unaanza kumuelewa taratibu: Pengine alikuwa na mume wako kwasababu ya ugumu wa maisha, wingi wa majukumu, watoto aliotelekezewa wa kuwalea! Na zaidi tumbo linalohitaji chakula kila siku.

NA SASA: Kama yule tu, unatamani hata kumpigia mwanaume wa sasa uliye naye, lakini huwezi sababu unatambua yupo na mke wake na familia yake nyumbani, na wewe unalinda nafasi yako kwake maana mkewe akigundua hawezi kukimbilia kuachana zaidi wewe ndio utaachika. “Mateso yanarudia tena upya”

Hivyo amekupa masharti yake ambayo utake usitake lazima uyafuate, na unapaswa kuheshimu faragha yao kuwa sasa yupo nyumbani na familia yake na wewe utaendelea kuwa option-tu, Linapokuja swala la Kupunguza mawazo na tamaa zake.


Unafikiria tu kuhusu maumivu yako!

Unafikiria tu kuhusu faraja (Consolation) yako!

Ila walau awali ulikuwa na mume wako pekee yako’ Ndio alikusaliti lakini bado aliendelea kuwa wako!

Hatimaye unajaribu kutafuta tena kufahamu juu ya yanayoendelea kwenye maisha yake baada ya kutalikiana na kila mmoja kushika maisha yake, unang’amua sasa ame ‘move-on’, na tayari anaishi na mwanamke mwingine pengine mdogo kiumri au mrembo kukuliko wewe.

Unakaza roho, kwakua mawasiliano yake bado unayo unaamua kupigia na kumuomba miadi ya kukutana sehemu kuongea kwa kigezo cha watoto wame-mmisi wanataka aje kuwatembelea, kweli anafika na kuwaletea vizawadi watoto na kukuachia pesa kidogo ya matumizi ya watoto, lakini haitoshelezi kama ilivyokuwa zamani. (Mke mpya ameshikilia matumizi yake yote)

Mnapanga kutoka matembezi kidogo, mnakumbushiana wakati mzuri mliokuwa nao zamani na hamadi-bila kutarajia, na ngono mnashiriki! Kwa muda mchache unasahau taabu na dhiki na upweke uliokuwa nao wote!

Punde, mmemaliza kila kitu anakuaga kurudi kwa mkewe anapiga simu, ghafla unagundua sio wako tena na dhiki, taabu na upweke unarudi kama ulivyokuwa siku zote!

NDIPO: Unagundua sasa unahusiana ‘dating’ na wanaume wawili tofauti, ambapo wote wawili wamewasaliti wake zao na wewe ndio sababu!

Ghafla unaikumbuka ndoa yako, uhuru uliokuwa nao ukiwa na mume wako wa ndoa, kisha unagundua ni kama dunia nzima imekugeukia na maisha hayako sawa kwako!


Unaweza kudhani hii ni stori tu, lakini kuna wanawake wanaoiishi kiuhalisia, na ninge’ au ningalijua huja baada ya kuwa tukio lishatokea. Siungi usaliti ndoani, Lakini pia siungi vitendo vya ukatili ndoani" Mninukuu vizuri!

Mbali ya tofauti zetu, familia ni baba na mama na sio mzazi mmoja, licha ya changamoto zilizoko ndani ya familia hizo.

Asilimia kubwa ya ndoa zinawaka moto, na sio salama kwa asilimia mia, (Ni kusameheana na kuvumiliana) Tafakari chukua hatua!

#MwalimuMeena (0778291375) Kwa Maoni, au Unahitaji ushauri wa ndoa nipo hapa kukushauri!

Unaweza kusambaza elimu hii: (Share) iwafikie wengi zaidi, lakini (usi-copy na ku-paste) na kufanya kama ni chanzo cha mawazo na Sanaa yako) ukifanya hivyo nipe credit yangu katika chapisho lako. Asante!

 LINK INTO ENGLISH VERSION: ReadMore

No comments:

Post a Comment