Saturday, 22 August 2026

MFAHAMU NDEGE KORONGO AINA YA MARABOU, 'THE UNDERTAKER'

 

Picha: Wikipedia

Na.

Stewart Meena

Kutana na ndege wasio na sauti au "mlio", wenye miguu mirefu na wenye kuweza kuhimili ongezeko kali la joto" ikilinganishwa na ndege wengine warukao, na hiyo ikampatia sifa ya upekee na majina mbalimbali kama: 

"Undertaker, na Marabou storks" Kiswahili wakijulikana kama ‘KORONGO MARABOU

Ndege hawa, ni waviziaji na vyakula vyao vikuu ni pamoja na mabaki ya mizoga ya wanyama tofauti, mabaki ya vyakula vitumiwavyo na wanadamu, samaki pamoja na vyakula vingine kama, mijusi, nyoka, vyura, wadudu, panya na ndege wengine wadogowadogo.

Makazi makuu ya ndege hawa ni maeneo yote karibu na mito, maziwa, milimani ndani ya miamba, na kwenye hifadhi za wanyamapori, tambarare zilizo na miti mirefu, ambapo licha ya urefu na ukubwa wao, wanaweza kuruka katika eneo kubwa la anga na kupaa umbali mrefu.

Kuruka kwao, huweza kuruka hewani umbali wa futi-13,000 (feet) toka usawa wa bahari, na inapokuja swala la mwendokasi katika jamii yao ya ndege, Korongo huwenda hawa wakawa wana kiwango kidogo cha mwendokasi huo.

UKWELI USIOUJUA KUHUSU NDEGE HAWA.

Picha: Rubega Safari

Marabou stork, ni miongoni mwa ndege wasiovutia (ugliest bird on the world) kwa kuwatazama, kwa mwonekano wao (wakiwa na Miguu mirefu, shingo ndefu na eneo kama tumbo la kuhifadhia chakula linaloning’inia karibu na shingo yao likiwa na rangi ya pinki (Eng: a pink gular sac).

Ndege korongo huyu, hutambulikana pia kama ndege muuwaji kwa muonekano wake kwa nyuma ukiwa unamtazama, wazungu wakimuita “Nature’s eyesore / the undertaker bird” na ndiye ndege jamii ya tai mwenye miguu mirefu katika jamii hiyo centimita karibu 50, huku mbawazao zikiwa na urefu wa futi11 na kuwafanya ndege hawa kuwa na upekee tofauti na ndege wengine.

Sambamba na ndege wote kuwa au kutambulikana pia kwa milio yao, ndege hawa hawana milio hiyo, ingawa huweza kuwasikia wakitoa milio Fulani inayotokana na kugongesha midomo yao au mbawa zao.

Hadi kufikia umri wa ukomavu ndege hawa, huchukua karibu miaka mine ‘4’ na kuwafanya miongoni mwa ndegw wanaokua taratibu-taratibu Zaidi ikilinganishwa na ndege wengine wanapoanguliwa kwenye mayai yao.

Korongo hawa wa marabou, hupatikana pekee yake barani Afrika (Ukiacha waliohifadhiwa katika zoo za wanyama) kwenye maeneo ya kitropiki kwenye nchi kama, Senegal, Eritrea, Ethiopia, Somalia, Tanzania, Kenya, Uganda, Namibia, Congo, Afrika ya Kusini nk.

(Unaweza kusoma pia hapa)

Kwa nchi ya Tanzania: Ndege hawa ni maarufu Zaidi kwenye ukaanda wa ziwa Victoria na Tanganyika, na huweza kuwaona Zaidi kwenye hifadhi ya taifa ya Serengeti, Manyara, Nyerere, Tarangire nk. Ambapo wenyeji wa mikoa ya Manyara, Mara, Mwanza, Geita ndege hawa huingia hadi maeneo ya masoko na mijini.

Picha: Natalie Carberi
Marabou (Korongo) ni ndege anayependa kuchangamana Zaidi na binadamu ndani ya makazi yao na hii ni kwa ajili ya urahisi wa kupata vitoweo vyao, huku wale kwenye hifadhi ya wanayama hupendelea Zaidi kuwa karibu na wanyama wawindaji kama Fisi, Chui, Duma, Simba na Mbweha ikiwa ni sehemu rahisi kwao kuvizia mawindo yao na kuyaiba. (Marabou stork are known to be scavenger bird) Kimsingi ndege hawa korongo sio wawindaji hodari, ila ni waviziaji hodari.

Wanawezaje Kuhimili Joto Kali La Uwanda Wa Savana?



Ili kupunguza ongezeko la joto na jua kali linalowatesa ndege wengi, kwa ndege Korongo ni tofauti kidogo, ambapo miili yao inauwezo wa asili wa kubadili kanijoto mwili wao kuendana na ukali wa jua au joto la maeneo waliyopo, kuficha uso wao ndani ya mabawa na kutanua mfuko wao wa pinki uliopo chini ya shingo huwawezesha kuendana na mabadiliko hayo ya joto.

Na endapo kutakua na baridi kali na wanahitaji joto, basi hutanua mabawa yao (mbawa) na hiyo huwawezesha kurudisha kwa haraka ongezeko lao hilo la joto ndani ya miili yao.

Kimazingira kwenye jamii yao, huwenda hawa ndio ndege wavivu zaidi na wasiopenda kuhangaika kutafuta vitoweo, isipokua kusimama karibu na wanaotafuta (kuwinda) na wakishapata kitoweo chao wao ndio huenda eneo hilo na kuwafurusha kwa ajili ya kuiba kitoweo hicho. Mfano: Kanda ya ziwa huiba samaki zilizovuliwa na wavuvi.

Mazaliano yao hupendelea zaidi majira ja kiangazi wakati kina cha maji maeneo mengi yakiwa yameshuka au kukauka, kwani ndio urahisi zaidi wa wao kupata vitoweo vyao kwa urahisi zaidi.

Ni msimu huu huweza kuwaona ndege hawa wakiwa karibu-karibu zaidi, na madume wakipambana kwa midomo yao ili kuwania haki ya kumiliki korogo jike kwa ajili ya mwanzo wa mazalia yao, ambapo atakayeshinda ndio kuanzia hapo ataambatana na jike husika kwa muda wote wa kujenga kiota, kurutubisha mayai, kutaga na kuyaatamia, kisha watoto watakao anguliwa kushirikiana kuwatafutia chakula kwa pamoja hadi watakapoweza kujitegemea wenyewe.

Angalia

Ndege hawa wakishaungana, huishi hivyo wawili pekee kifamilia hadi mwisho wa maisha yao, na ajabu nyingine ni kuwa hawachanganyi mwenza na ikitokea mmoja kati yao amekufa mwingine huakia hivyo hivyo na huelezwa, sababu ya upweke na yeye hachukui muda mrefu kabla ya kufa, ambapo baadhi ya tafiti husema ndege mwenza aliyesalia huweza kujinyima chakula kama njia ya yeye kufa.

Waweza pia kusoma HAPA

MWISHO: Kwa sababu ya urefu wa miguu yao, mbawa zao na midomo yao hii huwafanya kuwa na uwiano sawa wenye kupungua uzito hivyo kumuwezesha kuruka kwa urahisi zaidi wanapopaa angani, ikilinganishwa na jamii nyingine za ndege walio na urefu na uzito kama wa kwake.

Pia eneo la pinki karibu na shingo yake, hutumia hapo kama akiba ya kuhifadhi chakula chake akiwa ameshiba, kisha kula kwa wakati mwingine hususani anapokuwa ana njaa.

Tafadhali unaposasisha (Kushare taarifa hii), hakikisha unatambulisha chanzo cha taarifa hii kwa kutupa ‘credit’ Asante! StewartMeena

No comments:

Post a Comment