![]() |
| Picha na: Ahli Hospital |
FIGO ni miongoni mwa viungo muhimu sana katika mfumo wa utendaji
kazi wa mwili wa binadamu. Wiki iliyopita nilieleza jinsi kiungo hiki
kinavyopata mawe na jinsi ya kujikinga na tatizo hili.
Chanzo: Global
Nashukuru wengi wamepiga siku kushukuru kwa elimu ile. Kwa
kawaida, mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo yanayofanana kama yale
ya maharage, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo
ya mbavu za chini.
Kazi kuu za figo ni kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu
katika damu na hivyo kusaidia katika kuhifadhi na kuthibiti kiwango cha maji na
madini (electrolytes) mwilini.
Katika kutekeleza hayo, figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji
yaliyo mwilini na kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini
huku yakinyonya madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu
na kutoa nje uchafu usiohitajika.
Kazi nyingine za figo ni kurekebisha na kuthibiti kiasi cha vitu
mbalimbali katika damu pamoja na kiasi cha maji katika mwili, husaidia
kutengeneza kiasili cha erythropoietin ambacho ni muhimu sana katika
utengenezaji wa chembe nyekundu za damu, husaidia uzalishaji wa vitamini D na
husaidia pia katika kuthibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).
Kwa kawaida damu inayozunguka mwilini hatimaye huingia kwenye
figo kwa ajili ya kuchujwa, kutoa uchafu pamoja na sumu nyingine zisizohitajika
mwilini.
Kitendo hiki cha utengenezaji mkojo hufanyika katika hatua kuu
zifuatazo;
Hatua ya kwanza ni UCHUJAJI.
Damu kutoka nje huingia ndani ya mafigo na kupita kwenye
glomeruli, lenye umbo kama chekeche/chujio ambalo limeundwa na mishipa mingi
midogo ya damu iliyojizungusha pamoja.
Vitu mbali mbali, maji pamoja na sumu zilizo katika damu
inayopita kwenye vimishipa hivi na kisha kuingia katika mirija mingine mikubwa
kwa ajili ya uchujaji zaidi.
Mirija inayofuata huendelea kuchuja damu na kunyonya baadhi ya
vitu vilivyo chujwa kimakosa kuvirudisha mwilini, mpaka kiasi sahihi cha uchafu
kinachotakiwa kuchujwa kinapokuwa kimefikiwa.
Mara baada ya mkojo kutengenezwa na kutolewa kwenye figo,
husafiri kuingia kwenye kibofu cha mkojo kwa kupita kwenye mirija ijulikanayo
kama ureta.
Kutoka kwenye kibofu, mkojo hutolewa nje ya mwili kupitia kwenye
mrija wa urethra.
Kushindwa kufanya kazi kwa figo hutokea iwapo sehemu ya figo au
figo lote litapoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kutoka katika damu na
kutengeneza mkojo.
Kitendo hiki husababisha kusanyiko la uchafu pamoja na sumu
kadhaa katika damu ambazo ni hatari kwa afya ya mhusika.
Figo kushindwa kufanya kazi kumeganyika katika makundi
yafuatayo, Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure (ARF),
Figo kushindwa kufanya kazi kwa kiasi (Mild renal/kidney insufficiency) na
tatizo sugu la figo kushindwa kufanya kazi (Chronic renal failure).
Figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla (Acute Renal Failure
(ARF) Hii ni hali inayotokea kwa ghafla, na kudumu kwa saa chache mpaka siku
chini ya 14, na kusababisha ongezeko la kiwango cha creatinine na urea katika
damu.
Hali hii huwapata karibu asilimia 5 ya wagonjwa waliolazwa
hospitali kwa sababu ya matatizo mbalimbali. Aidha hali hii hutokea zaidi kwa
wagonjwa mahututi na wale wanaohitaji uangalizi wa kipekee, yaani waliolazwa
ICU.
SABABU ZAKE
Visababishi (au aina) vya ARF vinaweza kugawanywa katika makundi
makuu matatu: Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika
figo (Prerenal causes/failure), matatizo ndani ya figo lenyewe yanayozuia na
kuathiri uchujaji wa damu au uzalishaji wa mkojo (Renal causes/failure),
matatizo yanayoathiri mtiririko wa mkojo nje ya figo (Postrenal causes/
failure)
Matatizo yanayoathiri mtiririko wa damu kabla ya kuingia katika
figo (Prerenal causes/failure) Aina hii hutokea kwa takribani asilimia 60 mpaka
70 ya ARF zote. Katika kundi hili, figo hukosa damu ya kutosha kwa ajili ya
kuchuja na hatimaye hushindwa kufanya kazi yake ipasavyo. Mambo
yanayoweza kusababisha pre-renal failure ni pamoja na:
Upungufu wa maji mwili unaosababishwa na kutapika kupita kiasi,
kuharisha, au kupoteza damu kupita kiasi (kwa sababu ya ajali au kuumia),
kuvurugika kwa mtiririko wa damu inayoingia kwenye figo kwa sababu ya: Kushuka
kwa ghafla kwa shinikizo la damu kwa sababu ya kupoteza damu nyingi wakati wa
upasuaji mkubwa, kuumia au kuungua sehemu kubwa ya mwili, au maambukizi katika
mfumo wa damu (sepsis) yanayoweza kufanya mishipa ya damu kutanuka na kushusha
shinikizo la damu, kuziba au kusinyaa kwa mishipa inayopeleka damu kwenye figo.
Figo inaweza kufeli pia kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi
(heart failure) au shambulio la moyo (heart attack) linalosababisha kushuka kwa
shinikizo la damu na ini kushindwa kufanya kazi (liver failure) kunakoweza
kusababisha mabadiliko katika mfumo wa homoni zinazoathiri shinikizo la damu
pamoja na mtiririko wa damu kwenda kwenye figo.
Mwanzoni kabisa mwa pre-renal failure huwa hakuna athari yoyote
inayotokea kwenye figo, na mara nyingi, figo laweza kurudi katika hali yake ya
kawaida iwapo chanzo cha tatizo kitagunduliwa na kushughulikiwa ipasavyo.
Mambo yanayosababisha madhara katika figo husababaisha karibu
asilimia 25 mpaka 40 ya vyanzo vyote vya ARF. Visababishi vilivyo katika kundi
hili hujumuisha vile vinavyoathiri uchujaji, mtiririko wa damu ndani ya figo na
seli za figo zinazoshughulika na uchujaji na ufyonzaji wa chumvi na maji.
Visababishi hivyo ni pamoja na: Magonjwa katika mishipa ya damu,
kuwepo kwa damu iliyoganda ndani ya mishipa ya damu inayopita katika figo,
ajali/ Kuharibika kwa tishu na seli za figo, magonjwa ya mzio katika glomeruli
na figo kwa ujumla (glomerulonephritis).
Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na maambukizi
(infection) ya bakteria jamii ya streptococci.
(More: Here Endelea kusoma hapa)

No comments:
Post a Comment